KIJIJI CHA UPEPO
KIJIJI CHA UPEPO MWANDISHI: SAID KAITA SIMU: +255 783 372 139 BARUA PEPE: saidikaita7@gmail.com ONESHO LA KWANZA ( Jua limewaka. Mriri anatembea hatua tatu kisha anasimama anatega masikio. Kuna kitu anakisikia kwa mbali, anatega masikio vyema. Inasikika kwa mbali sauti ya ngoma ) Ngit Ngit Ngit ( Sauti ya mwimbaji anayesikika inaonesha dhahiri mwimbaji huyo ana ujuzi wa uimbaji. Wanakaribia kutokea eneo alikokuwa amesimama Mriri. Anaongea pekee yake ) MRIRI : Mbona hizi ngoma kama vile hivi si … nahisi kama kuna jambo hapa. Wanakuja… nahisi kama wanakuja na njia hii hii ninakoelekea mimi. Embu nifanye mpango nijifiche sababu huwa nasikia hizi ni kama ngoma za heshima japokuwa siujui uheshima wake. ( Harakaharaka Mriri anajificha kwenye kichaka ili wasimuone. Muda si mchache wanafika karibu na alipojificha Mriri. Wanasimama huku wakiwa wanaimba na kucheza. Wanaonekana wasich...