ZUCHU
MUSTAKABALI WA MSANII ZUCHU (ZUHURA OTHUMANI) BAADA YA MIAKA MITANO IJAYO MWANDISHI NA MCHAMBUZI: SAID H. KAITA MAKALA NAMBA MoJA (2020) +255783372139 1.0 UTANGULIZI Uchambuzi katika makala hii utazungumzia historia fupi ya ZUCHU na hatua hadi kufikia katika muziki, maisha yake ya muziki baada ya kuingia katika lebo kubwa ya muziki barani Afrika iliyopo nchini Tanzania chini ya msanii Diamond Platinumz, Wasafi Classic Baby (WCB Wasafi). Katika uchambuzi huo mfupi ndipo tutakapotoa mustakabali wa ZUCHU baada ya miaka mitano katika muziki atakuwa katika hatua gani? Uchambuzi huu hautajikita katika kutetea upande fulani kwa hisia bali ni kuangalia mambo ya hakika ya msanii ZUCHU na kumpatia mustakabali wake. Mwisho, makala itatoa maoni na ushauri kwa ZUCHU. 2.0 HISTORIA FUPI YA ZUHURA OTHUMANI (ZUCHU) Zuhura Othman (ZUCHU) ni mtoto wa mwisho katika familia yao. Mama yake akiwa ni moja ya wasanii wakubwa wa muziki wa taarabu na mduara ambaye ...