MSAMAHA WA KWELI?
JINA LA HADITHI FUPI: MSAMAHA WA KWELI ? MWANDISHI: SAID KAITA FACEBOOK PAGE: Saidikaitastories.com BLOG: Saidikaitastories MAWASILIANO: 0783372139 E-MAIL: Saidikaita7@gmail.com Usilolijua ni sawa na usiku wa giza nene. Ni msemo ambao mara chache hutumika katika ndimi za watu ila huwatokea tu muda ambao jambo husika limeshatendeka pia kuwa na uhakika nalo. Usiku ulioambatana na sauti za mbu zililizunguka eneo alilokuwa amelala Ahata. Sauti zilizojawa hasira kila mmoja wao akiwa anatafuta kitoweo. Kwa ukali wa sauti zile ulisikika kama mtu akiwa anapiga kinanda kwa utaalamu na hakuna ambaye angeweza kulala kwa sauti zile. Sauti ya makofi ilikuwa ikisikika kila mahali “Paaa... Paaa” kila mtu alikuwa akijihami asing'atwe. Ahata alikuwa amelala chini ya kalavati akiwa amejifunika na mfuko wa kubebea uchafu. Mbalamwezi iliyokuwa iking'aa angani kwa namna yake iliweza kutoa nuru na kufanya watu wengi waliokuwa wamelala pale ku...