SARA- Hadithi ya watoto
MWANDISHI: SAID KAITA HADITHI: SARA NAMBA: +255783372139 E-MAIL: saidikaita7@gmail.com Fb Page: Saidikaitastories.com Blog: Saidikaitastories.blogspot.com Sara ni mtoto mwenye miaka mitano. Anampenda sana mama yake, hupenda kukaa nyumbani na kujishughulisha na michezo mbalimbali kama vile kupika kwa kutumia matope. Ambapo, huchota maji, kisha hutafuta mahali ambapo pana mchanga mzuri na kujipikilisha mwenyewe. Ila, michezo yote hiyo hupenda kufanyia nyumbani kwao tu. Huwa hapendi kabisa kwenda kucheza kwa majirani, kwani huhofia sana mama yake akirejea asijemgombeza. Pia, huogopa kupigwa na wenzake kwa kuwa yeye ni mpole sana. Aonapo amechoka hutafuta sehemu nzuri na kutandika kwa vipande vya kanga ambavyo mama yake amempatia kama vya kuchezea. Michezo hiyo hufanya baada ya kumaliza shughuli zake ndogo ndogo ambazo mama yake humuachia pale nyumbani kama vile kufagia uwanja wao, kuosha vyombo kama vile sahani, bakuli na vijiko. Kabla mama yake hajatoka huwa amemwandalia viz...