SIRI
HADITHI FUPI
JINA LA HADITHI: SIRI
MWANDISHI: SAID KAITA
MAWASILIANO: 0783372139
E-mail: Saidikaita7@gmail.com
FACEBOOK PAGE: Saidikaitastories.com
Nyota njema huonekana alfajiri. Ni fikra ilojaa kwa kila mwanadamu aliyepevuka akili. Lakini Jose kwake sidhani kama atakuwa ameiona hiyo nyota njema. Jose akiwa amesimama huku anasikiliza usia kutoka kwa baba yake anayeonekana yuko kitandani akiwa amelala na afya yake ikiwa imedhoofika sana. “Jose… mwanangu… ni muda mrefu nikiwa nai… angalia …. dunia kwa ma…ma… chungu kwa ugonjwa niliokuwa nikisu… sumbuliwa. Mmejaribu kunitibu kwa njia yoyote ile lakini juhudi zenu zote naona kama zinaenda kugonga ukuta”. Jose akawa ameshtuka na kumuuliza baba yake. “Baba mbona kama unanitisha? …”. Ilikuwa ni vigumu sana kwa Jose kuweza kuelewa nini hasa kilichokuwa kikiendelea kwa baba yake ambaye kwa hali halisi ni kwamba alikuwa akienda kuaga maisha yake ya dunia ya tatu ili kwenda kuonana na maisha ya dunia nyingine. Baba Jose alizungumza huku machozi yakiwa yanambubujika. “Mwanangu Jose kwasasa wewe umeshakuwa mkubwa. Jambo la kumshukuru sana Mungu kwa kuwa wewe umeshakuwa na mimi nimeshazeeka narudi nilipokuwa nimetokea kama wewe unavyotakiwa kwenda, kwa ujumla ni kila mwanadamu lazima aende kama ilivyopangwa. Jose… hadi mimi ninakaribia kuondoka nitakiwapo kuondoka… kuna mengi sana yananiuma ninavyokuacha. Umaskini …. Umaskini jambo kubwa sana limetukumba katika familia yetu. Mama yako amefariki na huu umaskini, wakubwa zako wamefariki kwasababu ya huu umasikini, na mimi pia ninakufa na huu umasikini. Kwasababu sidhani hata kama nifanyeje kama kuna mabadiliko yoyote yanaweza yakajatokea kwa muda niliobakia nao hapo. Mimi kufa maskini isikufanye na wewe kufa maskini. Ninachokuomba mwanangu tumia mbinu zozote zile usije ukafa na umaskini. Nasema mwanangu tumia njia yoyote ile hadi ufanikiwe kimaisha. Acha nikufuru … nasema hivi hata kama ni kwa namna nyingine chamsingi ujue utapata utajiri. Pesa nimezitafuta tangu nikiwa na miaka kumi na tano hadi leo hii ninakufa na miaka sabini sijaona chochote kwa pesa za ki halali nilizozitafuta”. Jose alimkatisha baba yake maongezi na kusema hivi “Sawa baba nimekuelewa ila unajua ni kazi ngumu iliyoje katika baadhi ya maneno au mahitaji kwangu kuweza kukamilisha”. Baba anamuangalia Jose kwa jicho la upande na jicho lake likionesha kabisa muda si mrefu linaenda kuzima. “Ninakwambia hivi mwanangu … embu nielewe mwanangu… yaani mimi nakuomba na hapo hapo… hapo hapo ninakulazimisha kuwa ufanye juu chini hadi uweze kufanikisha maisha yako yawe ni mazuri … hata kama ni kwa uchawi… ukiangalia umebaki wewe tu katika hii familia…. Mimi ninamalizikia sasa hivi. Sina namna kabisa na hayo ndiyo maneno yangu”.
“Sawa baba nitakusikiliza… sababu asiyesikia la mkuu huvunjika mguu na kuvunjika mguu sitaki kabisa. Nitakuwa kilema wakujitakia. Baba nitatekeleza maneno yangu”. Kwa baba alianza kabisa kumuona malaika wa roho akiwa anazunguka karibu naye “Mwanagu… mimi ninaenda kwetu … sitarudi bali na wewe utakuja…. Kwa muda nitakaokuacha hapa duniani hadi uje huko niliko… jaribu sana kuishi na watu vizuri”.
Jose akiwa anamuangalia baba yake kwakweli ilimbidi akaze moyo tu kwasababu aliona kabisa hata kama akilia ni kama hamna chochote tu. Kwasababu kama ni yeye kufiwa alishafiwa sana na alishatoa machozi sana. Basi hana budi kwa leo kuweza kuyakazia machozi yake yabaki ndani tu. Baada ya kufariki Jose hakuwa na namna aliamua kumzima macho na kumfunga mdomo baba yake huku akiwa anasema hivi “Kwaheri baba… kwaheri baba… kwaheri baba … tutakutana tena Mungu akitukutanisha… nenda salama… kwaheri”.
Jose alichukua shuka alilokuwa amejifunika baba yake na kumfunika gubi gubi baba yake baada ya kumzima macho. Jose alitoka nje na kuamua kusimama mlangoni huku akiwa anayatafakari mambo yanayoenda kutokea mbeleni mwake baada ya yeye kubaki pekee yake katika familia yao. Muda huo tayari kulikuwa kumeshaanza kukucha kabisa. Hali ya hewa ilikuwa imeshaanza kubadilika kwa namna yake kabisa. Alianza kuzungumza pekee yake.
“Baba na ndugu zangu wawili mliotangulia huko kwenda kutuandalia makazi… basi makazi mliyoyaandaa haya baba huyo anakuja. Mama mume wako ambaye ulimpenda na mliadhimiana kuwa kutenganishwa kwenu ni kifo basi anakuja huko kwa uwezo wa Mungu atawakutanisha huko. Ndugu zangu baba yuko anakuja… anakuja. Mimi ndiyo nimebaki katika kaya hii. Najua mumeniachia mzigo mkubwa sana ila sina namna kwa mimi kulifanyia kazi jambo hili. Kwasababu kukimbia tatizo si kwamba ndiyo kutatua tatizo bali kutatua tatizo ni kutafuta namna ya kuweza kuondokana na tatizo. Nitalisimamisha jina la mzee Ndee. Mtakuwa mnalisikia huko mliko. Sijatoa kabisa machozi ni kwasababu nimeona hata kama nikilia ni sawa na kilio cha samaki tu baba atakuja huko mliko”. Kwakweli ilikuwa ni dhoruba kubwa sana kwa Jose. Aliamua kutoka pale na kuamua kuanza kwenda kuwataarifu majirani kuhusu taarifa hizo za msiba. Kwa kipindi hicho kilikuwa ni kipindi cha kiangazi kwahiyo hata hapakuwa na mazao. Njia ilikuwa ni kupita popote. Alipita moja kwa moja hadi kwa jirani yake. Alipofika ndipo aliwakuta watu ndiyo kama wanaanza kujiandaa na shuguli za asubuhi. Lakini wengine walikuwaa hata hawajanawa uso. Mama wa kaya ile alimkaribisha Jose. Mama huyo akiwa amevaa gauni lake refu jeusi tiii.
“Karibu Jose”.
“Ahsante mama Johari… shikamo”
“Maarhaba Jose. Karibu kiti”.
“Ahsante mama Johari”.Anaamua kuketi huku sura yake ikiwa inawakilisha jambo lililotokea muda si mrefu.
“Jose ehee vipi hali? ”.
“Hivyo hivyo tu mama Johari kazi ya Mungu haina makosa”.
“Kwanini?”.
“Baba amefariki!”
“Atiiii nini?”
“Baba amefariki”.
Alishtuka sana kwa taarifa ile. Mzee Ndee alikuwa ni jirani mwema sana. “Kweli mzee Ndee umeamua kutukimbia kabisa? Mzee Ndee kweli umeamua kumuacha kabisa Jose abaki pekee yake?”. machozi yalianza kumbubujika mama Johari kama bahari ya Hindi. Ndipo wana wa mama Johari wakaanza kumnyamazisha Mama na kumnyanyua pia Jose akawa anatoa msaada. Jose akawa anawaambia wana wa mama Johari hivi.
“Sasa Johari na mdogo wako nawaombeni mkawajulishe watu kuwa Mzee Ndee amefariki.”
Wote wanapokelea. “Sawa kaka”.
“Wakiwauliza amefariki saa ngapi wambieni kuwa amefariki alfajifi ya leo”.
Wote wanajibu “Sawa kaka”.
Basi ilibidi mama Johari na Jose wakakae pale nyumbani kwenye msiba ili kuwe na uangalivu juu ya mambo yanayotakiwa kuendelea kwa siku ile. Baada ya mama Johari kwenda kumuangalia mzee Ndee ndipo mama Johari akaamua kutoka nje na kuanza kuweka mazingira ya watu kuja katika msiba huo. Harakati za mazishi zilianza kufanyika. Watu waliwasili pale wakiwa ni majirani ili kuja kumpa pole Jose.
Mazishi kumalizika sasa ikawa ni kazi kwa Jose kuanza kuyasaka maisha na maisha yenyewe kuna mbinu mbalimbali ambazo Mzee Ndee alimpatia akiwa anakaribia kukata kamba. Ni wiki moja kupita baada ya msiba na maziko ya Mzee Ndee. Pale nyumbani hapakubakiwa na hata ndugu yeyote kutoka upande wa mama au wa baba bali Jose alibaki pekee yake kaya akiwa anaiangalia mwenyewe. Hakuwa na namna kwasababu yeye ndiye kidume aliyebaki basi si muda mrefu wa yeye kuanza kulalamika bali ni muda wa yeye kuanza kuangalia ni namna gani ya kusimamisha maisha na kuleta heshima katika kaya ya marehemu mzee Ndee. Asubuhi ikiwa ni mishale kama ya saa nne hivi tayari watu wote walikuwa wamerejea majumbani mwao. Wale wa safari za mbali basi nao walianzisha safari mapema sana. Jose alisimama kwenye mti ambao mzee Ndee alikuwa akipenda sana kujiegemeza wakati akiwa hai. Alikuwa akifanya tafakuri iliyokuwa ndefu sana. Aliweza kuingia katika msitu wa mawazo. Maneneo ya pole pole akiwa anayaongea kimoyomoyo.
“Nilizaliwa nikiwaa nimewakuta baba na mama wakiwa na wakubwa zangu wawili. Wakafariki wakubwa zangu na mama yangu, tukabaki wapweke mimi na baba yangu Mzee Ndee. Nimeishi na mzee Ndee kwa muda mrefu lakini ndiyo hivyo aliye juu kampenda Zaidi kuliko walimwengu akiwemo ni mimi. Baada ya kufariki mzee Ndee watu wakakaa kuanzia siku waliposikia kuwa mzee Ndee amefariki. Ndugu kutoka kaskazini na kusini waliwasili, kutoka mashariki na magharibi waliwasili. Kuwasili kwa watu hawa ni kwa vile tu baba yangu alivyokuwa maarufu lakini umaarufu wake ulikuwa ni umaarufu wa jina tu ambao haukuwa na msaada wowote kabisa katika maisha yake na maisha aliyoniachia mwanaye. Mazishi wamefanya baada ya kumaliza wachache walibaki na wengine wakaondoka. Kila mtu amekuwa akizungumza yake kuhusu mazishi ya baba yangu. Mzee Ndee amezikwa na watu wengi inaonesha anajulikana sana. Tatizo kubwa ni kwamba hana mali… kujulikana kwake ni kama vile tu upepo unavyosifika wakati wa upepo tu bali wakati wake ukishapita utakuwa hauna maana yoyote kabisa. Wiki kupita hapa nimeachwa pekee yangu … ila baba yangu angekuwa na mali ungeshangaa watu hadi leo wako hapo wakiwa wanasubiria siku ya kugawa mali za marehemu. Nashukuruu baba kwakuwa hivyo… sababu ungekuwa namali na nilivyo pekee yangu basi ningehangaika sana. Hao mashangazi, wajomba sijui akina nani wangenikaba sana hadi mambo ya uchawi yangeanza kabisa. Najua nitasimama… nitasimama na kweli nitasimama. Ninaamka kwaajili ya kusimama kisimamo cha mafanikio.” Mawazo yale kwakweli yalimpeleka mbali sana. Alianza kutembea huku akiwa anatafakari sana kuhusu ardhi ndogo ambayo baba yake alikuwa nayo. Lakini alijipa moyo na kusema kuwa “Ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi.” Akiangalia mifugo iliyoko zizini ni mifugo michache sana lakini alibaki na msemo wake wa kujipa moyo kuwa kisicho chako siku zote hakikusitiri. Alizidi kuzunguka zizi lile na kuelekea mlangoni mwa zizi lile na kuwafungulia ng’ombe wake. Walikuwa watatu tu dume mmoja na majike wawili. Ng’ombe walianza kutoka huku Jose akiwa amesimama kwa pembeni na kuwaruhusu wapite huku akiwa anasema hivi “Natumai hawa hawa wachache watanifaidisha… nitahangaika nao hadi malengo yangu yatatimia. Sina budi kuwalinda kama mboni yangu niilindavyo. Kwasababu kingine cha kutegemea hamna kabisa.” Basi aliwafuata ng’ombe wake akiwa anawaswaga kuelekea mbugani kwenda kuwapatia malisho huku nyumbani akiwa amepaacha kama vile watu wamehama kwamba kurudi kwao hamna kabisa.
Siku zilizidi kwenda na Jose kwa hali ile ya upweke akawa ameshaizoea tu. Kwahiyo pale nyumbani akawa yuko pekee yake na kuonekana kama vile ndiyo ameanzisha makazi mapya kabisa kumbe hiyo kaya ilishakuwepo tangu enzi hizo kabisa. Baadhi ya marafiki zake walikuwa wakimfariji kwa namna yake kwa kuja pale nyumbani kwa mida ya mchana ambapo mida hiyo anakuwa amesharudi kutoka machungajini. Hubonga hadithi za hapa na pale cha msingi ifike saa kumi tena wakufungulia ng’ombe na kwenda kuwalisha ili kukamilisha malisho yao ya siku.
Kipindi cha kiangazi watu walikuwa wameshaanza kuandaa mashamba yao kwaajili ya kusubiria kujiandaa na kilimo. Basi naye Jose hakuwa nyuma katika kufanya hivyo. Nusu heka iliyokuweko pale nyumbani kwao alianza kuiandaa na kuchoma mabuwa baada ya kutoa mbaazi na shamba likawa limebaki jeupee pee likiwa linasubiria tu jembe la ng’ombe lipite na mbegu kufukiwa. Baada ya kumaliza kuandaa shamba lae basi ilimbidi aongee na jirani yake ambaye ni baba Johari waone ni namna gani ya kusaidiana katika kilimo. Siku hiyo alimfuata baba Johari nyumbani kwake kabisa. Ikiwa ni mishale ya saa kumi na moja jioni wakiwa wanaonekana wamekaa chini ya mti uliokuwa na kimvuli kilichokuwa kimejitandaza vizuri sana.
“Baba Johari bana mimi shamba langu nimeshaliandaa.”
Alikubali kwa kichwa huku akiwa anavuta sigari yake ya kusokota “Vizuri sana Jose.”
“Ahsante baba Johari… ”
“Hatua inayofuatia sasa ni kusubiri mvua inyeshe ili tuanze kulima”
“Ndiyo… sasa hapo kwenye kulima hapo ndiyo jambo kubwa lililonileta hapa.”
“Ahaaa… embu nieleze kwa undani.”
“Ni kwamba baba Johari kwa pale nyumbani kama unavyojionea mimi sina mtu wa kulima naye… sasa nikawa nimefikiria namna ya kuweza kupata msaada wa kutoka kwako… yaani tuwe tunasaidiana tukianza kulima… yaani leo mimi nije kwako kukusaidia na kesho wewe unakuja kwangu kunisaidia. Kwasababu nimeona sina namna kabisa.” Alizima sigara yake na kuiweka kwenye mfuko wa shati.“ Ni wazo zuri sana hilo. Kwasababu hata mimi nilikuwa nafikiria ni namna gani kukusaidia katika suala hili… kwahiyo kwa hilo ondoa shaka kabisa. Vijana wapo hapo… watakusaidia vizuri.” Jose alimshukuru sana baba Johari. “Nashukuru sana baba Johari… ” alimjibu kwa kumpa mkono “Ondoa shaka Jose… ” tayari akiwa ameinuka. Basi adhima ile waliweza kuitekeleza kama walivyokuwa wameahidiana hadi wakawa wameshamaliza suala la kilimo.
Kwa mwaka huo kwakweli mavuno yalikuwa katika hali nzuri sana. Watuu walivuna mazao mengi sana. Kwakweli ilikuwa ni furaha kubwa sana katika kijiji chao kwa neema waliyokuwa wameipata. Ni muda mrefu sana haikuwa imetokea katika kijiji chao. Wanakijiji nao hawakuwa na matumizi mabaya ya mali zao bali waliamua kuhifadhi mazao yale katika sehemu ambayo ilikuwa ni nzuri sana. Jose naye kwa nusu heka yake tu ile ambayo alilima mbaazi na mahindi alipata magunia mengi tu ya mahindi na mbaazi. Hakuyachezea magunia yale bali aliamua kuyahifadhi sehemu nzuri ili tu isije ikawa ni hatari kwake kama akija kuyatumia vibaya.
Ni mwaka mmoja na nusu kupita tangu baba yake kufariki. Kwa kipindi hicho Jose hisia kuhusu kifo cha baba yake tayari zilikuwa zimeshafutika kabisa na kubaki tu kuwa akiona tu kaburi la baba yake ndipo mawazo humjia sana. Kwa siku hiyo kuna binti alikuja nyumbani kwa Jose. Binti yule alionekana sura yake ya upole iliyojaaliwa weupe mithili ya malaika wa huruma. Muda huo ilikuwa ni mishale ya saa nane mchana ambapo tayari Jose alikuwa ameshatoka machungajini na g’ombe wake wakiwa wamepumzika huko kwenye zizi. Mwanadada huyo alijigubika gauni refu huku nywele zake akiwa hajazifunika zilionekana zikiwa nyeusi mithili ya oil. Jose alikuwa amevalia nguo zake za kazi zikiwa ni chafu chafu tu. Shati lake lilikuwa limechanika na suruali yake ikionesha ikiwa ina matopetope yakiwa yamekaukia kwenye suruali hiyo. Walikuwa wamekaa kwenye mti uliokuwa na kimvuli kizuri sana. Mazungumzo yao yalianza kwa kutakiana hali.
“Marry hujambo?”
Akijibu kwa tabasamu. “Sijambo…”
“Nipe habari”
“Habari ni kwamba mguu huu ni wako… ”
“Ahaaa sawa…”
“ Unakumbuka kuna siku uliniambia kuwa nikiwa na nafasi nije kwako kukusalimia?”
“ Ahaaa… Ni kweli… nakumbuka…. Aaaaaa Marry kama unavyoniona mimi hapa nimebaki kama mimi katika kaya yetu hii. Mimi ndiyo baba na mimi ndiyo mama. Kila jukumu nalibeba mimi… basi kwangu kweli kuna muda huwa natamani sana kupata msaada kwa baadhi ya kazi”. Muda huo Marry alikuwa ametega sikio sana akiwa anamsikiliza kwa makini Jose. “Lakini ikafikia mahali nikawa nasema bana sisi tu binadaamu na binadamu kusaidiana ni mapenzi mazuri sana. Basi muda wote huo nilikuwa nikikaa na kutafakari ni namna gani ya kuja kukueleza Marry kuwa mwenza wangu wakuweza kuanzisha nawe maisha.” Moyo ulimshtuka sana kimoyomoyo Marry akawa anasema hivi “Kumbe naye alikuwa na hisia na mimi” aliendelea kumsikiliza Jose “Ndiyo maana siku ile nikakujulisha kuwa nakuomba sana siku ukiwa na nafasi unitembelee nyumbani kwangu. Dhumuni kubwa ni kukueleza kuwa Marry nakuomba uwe mwandani wangu… tufunge ndoa tuanzishe maisha katika kaya hii ya mzee Ndee.” Kimya kilitawala kama sekunde chache kama shetani akiwa amepita. Marry akiwa ameinamisha kichwa chini kisha akanena. “Jose… Jose…”. Jose aliitika kwa moyo mlaini.
“Nhaam Marry.”
“Unachonieleza ni kweli kinatoka moyoni mwako?”
Alimjibu kwa ukakamavu huku akiwa anamuaangalia Marry. “ Ndiyo Marry. Tangu muda mrefu sana nafasi hii nilitamani nikueleze bali natumai ilikuwa si muda wake… haikuwa muda wake… bado nilikuwa na mambo mengi tu kichwani. Kwahiyo ni jambo kutoka moyoni.” Marry alimjibu kwa moyo wa ukarimu “Sawa Jose ila…” Moyo wa Jose ulishtuka baada ya kusikia ilaa huku akiwa anasubiria ila nini? “Ilaaa acha nikamwambie kwanza maana natumai jibu kamili nitakupa.” “Sawa… Ila kwa wewe umelipokeaje?”
“Nimelipokea vizuri.”
“Nashukuru sana Marry”
“Sawa ”
Basi baada ya maongezi kumalizika Jose aliamuaa kumsindikiza Marry. Hakumpeleka hadi nyumbani bali aliishia njiani na kugeuza zake ili kwenda kuangalia ni namna gani ya kuhudumia mifugo wake. Jose alifurahi sana kwa hitaji lake la moyoni kupokelewa kwa mtu mwafaka aliyetakiwa alipokee hitaji lake. Alichokuwa anakisubiri ni jibu tu kutoka kwa wazazi wake haswaa mama ndiyo mwenye ushawishi mkubwa sana kwa mtoto kuweza kuolewa na mtu Fulani au laa.
Ikiwa ni mishale ya saa kumi na moja jioni mama Marry wakiwa wamekaa kwenye kimvuli huku wakiwa wanaandaa mboga za jioni. Hadithi za hapa na pale hazikukosekana. Mama aliongea hili likaisha na Marry aliongea hili likaisha. Kila mtu alionekana kama ameishiwa hadithi. Kunakitu kilikuwa moyoni mwa Marry. Kama dakika moja hivi kupita baada ya ukimya uliojitokeza Marry akasema.
“Mama.”
“Beee mwanangu.”
“Mama kuna jambo nataka nikueleze…sijui nianzie wapi?”
“Kuwa huru… nieleze mwanagu”
“Aaaa… mama… unamjua Jose?”
“Ndiyo… Jose wa marehemu mzee Ndee?”
“Ndiyo… huyo huyo.”
“Mhhh… kunani mwanangu? Sababu na wewe si haba”
“Anasema anataka anioe!”
Mama Marry alifurahi na kusema hivi. “Hongera mwanangu… tena hongera”
“Kweli mama?”
“Ndiyo mwanangu… unajua ni kwanini nimefurahi mwanangu?”
“Hapana mama.”
“Unajua mwanangu hata mimi nilikuwa nafikiria sana kwamba ni lini utaolewa. Kwasababu nilichokuwa naogopa ni kwamba usije ukajifungulia ukiwa hapa nyumbani yaani huna hata mume alafu unajifungulia hapa nyumbani. Yaani ingekuwa ni aibu kubwa sana kwangu.” “Sawa mama nimekuelewa.” “Kwahiyo nitaenda kumueleza baba yako kuhusu suala hili. Yule kijana ana maono kuhusu maisha yake. Si kama vijana wengine tu hapa kijijini wanavyokunywa pombe tu hata asubuhi unakuta kijana mdogo tu amelewa. Kwahiyo mshukuru Mungu.” “Sawa mama.” Baba Marry alisikika akiliza kengele ya baiskeli yake kisha mama Marry akasema hivi “Sasa embu tangulia jikoni kaandae mboga tulia mimi niandae mambo mengine huku. Baada usiku ndiyo nitamjulisha baba yako kuhusu suala hili.” Marry aliinuka pale na kujikung’uta kisha akachukua zile mboga na kupitiliza moja kwa moja hadi jikoni.
Hapakuwa na ugumu wowote kwa mzee kukubali mwanaye aolewe na Jose. Kwanza baba Marry alikuwa ni rafiki sana wa Marehemu mzee Ndee kwahiyo ilikuwa ni furaha pia ya kuzidi kuunganisha udugu wa ukweli. Basi maandalizi yalianza na taarifa zilianza kutolewa kwa majirani na ndugu mbalimbali kwa upande wa Bibi arusi na bwana arusi. Kijiji kizima kilinusa harufu ya Jose. Kila mtu arusi ile aliweza kuizungumzia kwa namna yake. Baadhi walikuwa wakisema kuwa hatoyaweza maisha ya ndoa kwasababu bado hayuko vizuri kiuchumi lakini baadhi walisema kuwa raha ya moyo ni utimizie hitaji lake tu. Kwahiyo wamuache kwasababu ni muda wake. Baadhi ya vijana waliokuwa sawa na rika lake baadhi yao kimaisha kwakweli hawakuwa wanajielewa kabisa. Kwahiyo wale ambao walipotea kimaisha walikuwa wakimchukia sana Jose.
Na kweli siku ya arusi ilifika. Baadhi ya marafiki wa kweli wa Jose waliungana naye na kuweza kumsaidia Jose katika arusi yake. Arusi ile ilikuwa ni arusi ya namna yake kwakeli watu walifurahia sana wawili wale wapendanao namna walivyokuwa wamependeza sana kwa siku hiyo tofauti hata na siku nyingine kabisa. Ngoma za kikabila zilichezwa sana. Harusi hiyo iliyokuwa imeanza mishale ya saa nane iliweza kuisha saa kumi na mbili jioni. Watu walikula sana siku hiyo na kuzidi kufurahia Zaidi arusi ile.
Ni siku iliyofuatia baada ya tafrija kubwa iliyofanyika kwa siku iliyopita. Muda huo Jose na Marry walikuwa bado wamejifunika. Wakiwa wamelala kwenye kijumba chao cha nyasi. Palikuwa pameshapambazuka kwa nje kuna baadhi ya watu wanaongea huko. Jose na Marry wakiwa bado wamejifunika Jose alianzisha maongezi.
“Mke wangu.”
“Beee mume wangu.”
“Ni furaha yetu sana kwa malengo kuweza kukamilika. Natumai kwa baadhi ya vitu hapa nyumbani kwangu unaona ni kama bado sana… vitu kama vile nyumba bado sijajenga. Ila natumai kwangu haitakuwa shida kwa vile nimekupata wewe natumai kila kitu kitaweza kukamilika. Malengo yangu kuhusu hii kaya yatakamilika. Ila cha kwanza kabisa ambacho nilitarajia ni kukupata wewe.” Marry alimjibu Jose kwa sauti ilioyoonekana ni ya usingizini. “Sawa mume wangu nimekuelewa. Natamani sana watu katika hiki kijiji waje kukushangaa sana. Na mimi nasema nitakuwa na wewe bega kwa bega katika suala hili hadi kuisimamisha hii kaya. Tuwaandalie wanetu mazingira yaliyo mazuri.”
Siku zote maisha ni maamuzi tu. Kwa Jose na Marry walianza maisha yao pole pole. Usiku namchana walifanya kazi huku wakiwa wanaumiza kichwa Zaidi ni namna gani kwao maendeleo yatawafikia. Basi hawakulala kilalo cha fungate bali waliinuka na kushikana mikono kwa pamoja na kuanza kuyasimamisha maisha. Ndani ya miezi tisa tayari Marry alijifungua mtoto wa kiume. Ilikuwa ni furaha sana kwao. Kwasababu kwa pale nyumbani hapakuwa na mtoto wakusumbua kaya ambaye muda wowote angekuwa anapiga makelele pale nyumbani. Kwa kipindi hicho tayari Jose alikuwa ameshajenga nyumba yenye vyumba viwili na kuipaua kwa mabati kwa mfumo wa ulalo. Pole pole waliendelea hadi ilipotimia miaka miwili tangu ndoa yao tayari pale nyumbani akawa amejenga nyumba yenye vyumba sita. Nyumba ya kwanza waliyokuwa wameijenga yenye vyumba viwili waliamua kufungua duka. Kwakweli baada ya kufungua duka lile watu walianza kupazoea kwelikweli na pale kwa mzee Ndee ndipo pakawa kijiwe kikubwa katika kijiji kile. Kila bidhaa katika kijiji kile ilipatikana. Waliishi kwa Amani na utulivu. Ilipopita miaka kumi tangu ndoa yao na mafanikio yao Jose aliamua kugombea nafasi ya ubunge na kinyang’anyiro kile aliweza kukipata kwa alama ya juu Zaidi. Nyumbani kwake kwakweli palijengwa vizuri sana. Siku hiyo akiwa amesimama kwenye mti ambao mzee Ndee alikuwa akipenda kusimama huku akiwa anaongea pekee yake. “Baba nakushukuru kwa ushupavu ulionipa. Najua katikaa usia wako uliniambia nitafute mali hata kwa uchawi chamsingi nipate mali. Lakini sikufuata usia wako nikatumia njia nyingine tu. Ni kweli asiyesikia la mkuu huvunjika guu lakini nakuomba usinilaani kwakuwa sijafuata msemo wako bali cha msingi nimefanikisha maisha. Nimetambua kabisa siku zote siri ya maisha ni kuishi na watu vizuri. Sababu hakuna ajuae kesho” Nafasi ya ubunge aliitumia kwa muda wa miaka minne na Jose akawa amejulikana. Mafanikio yalimwijia sana na alizidi kuwaheshimu watu wote. Hata kama kuna waliokuwa wakimchukia kipindi hicho lakini hakuwalipa ubaya kwa ubaya.
MWISHO.
SAID KAITA

Napenda kuwakaribisha kuisoma hadithi fupi hii iitwayo SIRI. Maoni yako ni jambo la msingi sana kwangu .
ReplyDeleteKaribuni.

Shukran kaka! Tunajifunza kupitia umahiri wako.
ReplyDeleteNashukuru Sana
DeleteNice
DeleteThanks
DeleteImekaa vzri hadth nimeipenda
ReplyDeleteNashukuru sana kaka. GD
DeleteNashukuru sana kaka. GD
DeleteNashukuru sana kaka. GD
DeleteNashukuru sana kaka. GD
DeleteUnaweza Sana kakaa💪💪💪
ReplyDeleteNashukuru sana ndugu.
DeleteNashukuru sana ndugu.
DeleteNashukuru sana ndugu.
Delete