PESA ILIVYO


HADITHI: PESA ILIVYO

MWANDISHI: SAID KAITA

MAWASILIANO: 0783372139

E-MAIL: Saidikaita7@gmail.com

FB Page: Saidikaitastories.com


SURA YA KWANZA
          Ni katika jumba la kifahari lililojaa kila aina ya urembo uhitajikao katika nyumba. Jumba hilo kwa nje kuna ulinzi mkali sana. Moja ya ulinzi ulioko hapo nje ni nyaya za umeme zimepitishwa juu ya kuta zilizozunguka nyumba. Pia hapo getini kuna mlinzi maalumu yuko hapo kwa kulinda na kuweza kufungua geti hilo japokuwa geti hilo hufungwa na kufunguliwa kwa kitenzambali maalumu. Pia pembezoni mwa geti hilo panaonekana kuna kamera zikiwa zimengaa macho huku na kule kama mlinzi wa rais ili kurekodi yote yanayoendelea katika maeneo yale. Hapo ndani pamejaa kila aina ya urembo wa nyumba kwa ndani. Runinga iliyokuwa kubwa kufikia nusu ubao. Kwa upande wa ndani kwa juu palikuwa pamezungukwa na kila aina ya taa ambayo ni kirembo cha ndani ya nyumba. Palikuwa na rangi katika jumba hilo kwa muonekano wake wa ndani tu. Kwenye ukuta palionekana kuna picha ya watu wawili wamechorwa kwa umahiri na kuonesha kabisa yule mchoraji alikuwa na kipaji kabisa cha kuchora bali si kwamba amesomea kuchora kama ilivyo karne ya 21. Picha hiyo ilionesha mwanamke na mwanamume wakiwa wamekumbatiana na kuonesha ni enzi zao wakiwa katika wakati wao. Mwanamume akiwa amevaa kofia la kifahari mithili ya watu wa kinaijeria. Alivaa kanzu iliyokuwa ni ya rangi fulani ikiwa ya rangi ya bluu bahari. Miguuni alivaa sendo. Kwa ujumla mavazi yake yalidhihirisha kabisa hadhi ya maisha ya mtu huyo. Kwa mwanamke huyo alikuwa amevaa gauni kubwa ambalo lililoonekana kabisa gauni hilo limeshapanda ndege kabisa. Kwa gharama yake kwakweli yawezafikia kodi ya mwaka mzima kwa wale wanetu wa elfu thelathini. Pia kwa pembeni palikuwa na picha iliyokuwa imebandikwa ya msichana ambaye alionekana ndiyo mwanao aliyejaaliwa umbo lake kama malaika wa uzuri.
            Kwa upande wa nje kwa hapo uwanjani tu palionekana kuna magari matano. BMW, NOAH, na mengine yakiwa yamefunikwa na mwamvuli maalumu wa kufunikia magari ili yasiweze kukutana na mwanga wa jua kali. Ukuta uliokuwa umezunguka jumba lile la kifahari ulikuwa ni kama ukuta uliojengwa enzi hizo za kipindi cha ujamaa. Ukuta huo japokuwa ulikuwa ni mrefu sana lakini bado tu tena palipitishiwa nyaya za umeme kwa ajili ya kuzidisha ulinzi zaidi.
         Saa ya ukutani ilikuwa ikizungumza mishale yake na kuonesha kuwa ilikuwa ni saa tano asubuhi tayari jua limeshaanza kukasirika na kujiandaa kuvaa sura ya mchana. Hapo ndani palikuwa na mazungumzo matamu kati ya wawili wapendano. Nuru na Nura kwenye kochi wanaonekana wakiwa katika bahari ya mazungumzo. Siku hiyo basi walikuwa na mazungumzo kidogo ambapo ni Nuru ndiye aliyekuja kumtembelea Nura nyumbani kwao. Nura akiwa amekaa karibu na Nuru. Nguo aliyovaa ni miniskirt ambayo ilikuwa imemkaa vizuri ikiwa ni ya rangi nyekundu hivi. Midomo yake muda wowote kwakweli huvutia sana na kuonekana kama anataka kuchumu. Mdomo wake ulio mwekundu kama amekula ubuyu muda si mrefu. Kifua chake kilichokuwa kimevimba kwa machungwa ambayo mungu kamjaalia na kumfanya hata Nuru kubaki kuyaangalia tu huku akitilia hamu kwenye ulimi na kutaka kuangusha mate kama mbwa aliyeona nyama buchani. Nura alikuwa akasema. Aaaa Nuru. Nuru akiwa amevaa suruali nyeusi na tisheti nyekundu huku akiwa amevaa pia kapero ya rangi nyeusi. Nuru Alisema hivi. “Nhaaam Nura kipenzi changu. Aaaaaaa mambo yaliyojitokeza kuhusiana na wewe ambayo ni ya kufeli mtihani wako wa kidato cha nne kama mwanzo nilivyokutaarifu kwamba jambo hili lisikuvunje moyo sana katika kuweza kuyafanikisha maisha yako. Nura alinena hayo kisha Nuru akasema. “Lakini Nura ni sawa kweli haina haja ya mimi kuweza kulalamika kutokana na mambo yaliyojitokeza. Ila tatizo liko hapa ni namna gani mimi nitaweza kuwakwamua wazazi wangu katika hali hii ya umaskini waliyonayo?. “Aaaaa Nuru jaribu kuweka chini hasira za maisha ulizonazo. Kila mtu ana hasira na maisha lakini si kama za kwako kabisa. “Hapana Nura mimi ni mwanaume ukumbuke.” “Nalijua hilo Nuru ndiyo maana nakuita mume wangu nikijua kuna mwanaume hapa. “Kwahiyo unanishaurije Nura?. Nurub aliomba ushauri. Aaaaa ndiyo maana nimekuita Nuru uje hapa. Madhumuni ya kukuita hapa ni ili tuweze kuzungumza kuhusiana na namna gani ya wewe kuweza kufanya kazi na kuweza kuingiza hela nzuri tu. Nura alimueleza Nuru kisha Nuru akasema. Sawasawa kwa hapo nimekuelewa. Kwasababu mimi ndiyo hivyo imebaki kama wiki moja tu na ninaenda shule. Nuru aliuliza. Hapa hapa Arusha?. Hapana ni huko Dar es salaam. Nuru alimuuliza Nura swali kwakushangaa. Kabisaaa Dar es salaam? .
“Ndiyo”.
“Kwahiyo wewe ndiyo umeamua kwenda Dar es salaam au vipi?.
“Hapana”.
“Bali kama siyo hapana?.
Ni baba na mama ndiyo wamekubaliana kwamba wanipeleke Dar es salaam.
Basi sawa.
“Ok basi tuongee yaliyotukalisha hapa
“Sawasawa”.
“Aaaaaaa kwa mimi kama huwa navyokwambia na kukuonesha maduka yangu ambayo mzee wangu kanifungulia. Nahisi unayajua?. Nuru alikubali. Ndiyo nayajua vizuri. Moja wapo ni lile ambalo liko pale makao mapya pale. Lile ndilo kubwa kabisa. Nuru alikubali Ndiyo hata lile ninalijua. Nura alimuuliza swali Nuru. Unaonaje ukawa unauza pale?.
Kweli?
“Kwani Nuru kwamba unahisi tunafanya utani hapa?.
“Hapana ni kama swali tu. Kwasababu ni kama vile siamini kwa unachokiongea.
Ndiyo uamini sasa.
Sawasawa
Ninataka pale kwa duka lile uwe ndiyo kama msimamizi pale. Kwasababu kwasasa nataka nipunguze wafanyakazi pale. Alikubali. Sawasawa. Kisha Nura akasema Kwasababu ni mzee ndiyo aliyenishauri kuhusiana na hili jambo. Nuru akasema. Itakuwa ni vizuri sana Nura. Kwasababu kwakweli sina mbele wala nyuma. Kwasababu hata ukiangalia hiyo form four yenyewe nimemaliza kigumugumu tu. Nura akampa faraja kwakusema. Haina shida nahisi tumeshakubaliana kuhusiana na hilo suala la wewe kuuza hapo dukani. Ndiyo Nura tumekubaliana. Haya basi kwa mimi kama nilivyokwambia wiki ijayo hivi naenda shule. Kwasababu mzee atanipeleka na gari yake. Amesema ijumaa ndiyo nitaondoka naye. Pia nitamjuza vizuri mzee wangu kuhusiana na wewe kuuza kwenye lile duka langu pale na kuanza kusimamia maeneo mbalimbali. Sawasawa Nura. Haya basi itabidi tutoke sasa hivi kwasababu kuna mzigo hivi mzee amenituma pale kwa Benson.
Ahaaa
Walitoka pale na Nura akawa ameelekea kufungua gari lililokuwa limepaki ambayo ni Noah. Basi na Nuru naye akawa ameingia kwenye gari huku mlinzi hapo getini akiwa anafungua geti ni baada ya honi iliyopigwa na Nura ikiashiria kwamba Nura anataka kutoka.


Ni mishale ya saa Moja jioni hivi kwa siku hiyo hiyo. Ambapo muda huo wazazi wake Nura walikuwa wamesharudi kutoka katika matembenzi yao ya siku nzima. Muda huo mama na baba Nura wakiwa wamekaa kwenye sofa moja. Baba Nura akiwa bado amevaa nguo zake ambazo alikuwa nazo matembezini na mama pia. Basi Nura akawa na maneno na wazazi wake kwa muda huo akisema.
“Baba nimempata mtu wa kuweza kusimamia pale dukani kwangu. Baba Nura aliuliza kwa sauti iliyojaa furaha. Ohoo  vizuri sana. Umempata wapi?. Mama naye akauliza swali kabla swali la baba halijajibiwa. Aliuliza. Ni wa kike au kiume?. Alicheka na kusema. Nianze kujibu swali lipi? Wote walicheka kisha baba akasema. Aaaaa kama ilivyo tu Lads the First. Anza na swali la Mama tu. Nura alifurahi kwa kuona ni namna gani baba yake anavyompenda mke wake. OK. Swali lako la kusema ni wa kike au wa kiume si ndiyo hivyo?.
Ndiyo
Aaaaaa ni wa kiume
“Umefanya vizuri Sana kwa hapo nakupa hongera”.
Asante
“Aaaaa kwa baba hapa umeniuliza kwamba anaishi wapi
“Ndiyo Ndiyo mwanangu”.
Anaishi hapa hapa Arusha maeneo ya mtaani kwetu Njiro
“Ahaaaa ana uaminifu kabisa kwa namna ulivyomuona?
Ndiyo.
Kwa vigezo vipi?.
“Aaaa ninamjua vizuri. Kwa ujumla tulikuwa tukisoma naye hadi tunamaliza kidato cha nne. Baba akauliza. Aaaa hadi kidato cha nne kabisa. Kwanini Yeye haendi shule?. Alimjibu. Hajafaulu. Baba akasema. Ahaaaaa basi itakuwa ni vyema kesho au Kesho kutwa akaja hapa ili tumuone vizuri inawezekana sisi tukawa tunamjua kiundani Zaidi. Nuru alipokelea na kusema Sawasawa  haina shida.
Kwa pale nyumbani akiwa mama wala baba hakuna anayejua kuwa kama Nura ana mpenzi. Hakuwahi kuonesha viashiria kabisa mbele ya wazazi wake. Labda jambo hili anayelijua ni mlinzi tu na mlinzi mwenyewe hana uaminifu juu ya suala hili.
Kwa ujumla Nura ni mtoto aliyezaliwa katika familia ya kitajiri na yeye ndiye wa kwanza na wa mwisho katika familia yao. Nikimaanisha kwamba katika familia yao Nura yuko peke yake tu. Yote hii ni kutokana na kipindi baada ya kuzaliwa kwa Nura alipofikia umri wa miaka mitano wazazi wake walipata ajali mbaya sana iliyokaribia kuchukua roho za wazazi wake. Katika ajali hiyo kama ni kuumia waliumia sana na wote yaani Mama na Baba Nura baada ya kwenda hospitali walifanyiwa matibabu ya hali ya juu hadi wakawa wamepona. Lakini vipimo vilikuja kuonesha kuwa baba aliumia sana katika sehemu zake za siri ya Mbele haswa haswa kwa ndani kitu ambacho madaktari walimwambia kwamba hatoweza kuzalisha tena. Pia hata Mama Nura tatizo hilo naye lilimkumba. Kwahiyo kuanzia hapo Mama Nura na Baba Nura hawakuwahi kupata mtoto tena zaidi ya huyo mmoja tu waliye naye. Ni huyo Nura ndiye kipenzi chao pekee.


Ikiwa ni mishale ya saa tano asubuhi ya siku iliyofuatia. Muda huo Nuru alikuwa ameshawasili katika jumba la kifahari la baba yake Nura. Ambapo baba yake kwa jina lake kabisa anaitwa Kerima Isambe. Kerima Isambe ni mzee aliyekuwa akijulikana sana katika jiji la Arusha kwa utajiri. Jiji la Arusha lilimtambua sana kwa namna ya utajiri wake aliokuwa nao. Si mtoto si mzee wote walimjua kuwa Isambe ni tajiri. Wakiwa wanaonekana wamekaa katika sebule nzuri yenye utulivu hewa inayotoka hapo kwakweli inaashiria kabisa hadhi ya jumba hilo la kifahari. Basi muda huo wakiwa Mama Nura na Mzee Kerima wakiwa wamekaa sehemu moja. Nuru akiwa naye amekaa kwenye kochi pekee yake na Nura hivyo hivyo. Mada iliyokuwa mezani ni kuhusiana na suala la Nura kuja kumtambulisha kijana atakayekuwa anasimamia duka lake. Mzee Kerima alimuita Nura.
“Mmmmh Nura.
Beee baba
“Naona huyu ndiyo yule uijana uliyesema?.
“Ndiyo ndiyo Baba hujakosea kabisaa. Baada ya Nura kumpa majibu mzee Kerima alimkaribisha Nuru. Aaaaaaa kijana karibu sana. Nuru aliitikia kwa adabu. Asante sana Baba
Hivi jina nani vile?
“Naitwa Nuru.
Ahaaaaa Nuru
Ndiyo ndiyo
 Mama Nura naye akasema hivi. Karibu sana Nuru”. Nuru akapokelea kwa furaha Asante”.
Mzee Kerima akasema hivi. Nuru kama mwanetu alivyokwambia kuhusiana na pale dukani kwake. Kwahiyo katutaarifu sisi kama wazazi wake ila tukasema ni vyema sana kama tukimuona mapema sana na kuanza kujuana vizuri”. Nuru alijibu. Ni Kweli baba ndiyo mimi hapa. Kwasababu Nura katuambia kwamba anajuana na wewe vizuri”.
Ni kweli baba.
“Kwahiyo kijana Nuru ninachokuomba tu kutoka kwangu ni kuhusiana na ukarimu na pia utu uwe nao pale dukani. Kama ni mshahara utakuwa unapewa mshahara mzuri tu.”
Sawasawa baba nimekuelewa. Mama Nura naye aliongea jambo. Unajua Baba Nura ni kwa nini mimi nilimuuliza Nura lile swali la kusema kwamba huyo mtu ni wa jinsia gani?
Ndiyo ndiyo nilisikia hilo swali ukiwa unamuuliza Nura.
Ndiyo.
Alafu sikukuuliza ulikuwa unamaanisha nini pale?.
“Aaaaaa unajua baba Nura kwa ujumla wanawake wanapenda wavae vizuri yaani kwa kifupi tu wanawake wanapenda sana kwamba wawe wanaenda na fashion. Kwahiyo Nura ungemleta msichana hapa kwakweli nisingekupa tick kabisaaaa. Kwasababu wanawake mimi nawajua. Alieleza mama Nura. Sawasawa mama japokuwa nilikuwa silijui hilo jambo ila nakushukuru kwa kuniambia jambo hilo nikiwa nimelifaulu vizuri sana. Sawasawa. Mzee Kerima akasema hivi. Nahisi kijana umesikia kura za mama Nura hapa.
“Ndiyo nimezisikia”.
“Haya. Kwahiyo kazi hii utaanza jumatatu ya wiki inayofuatia. Kwasababu itakuwa ndiyo tarehe ya moja na tutaweza kwenda na mahesabu vizuri. Baba Nura aliongea. Mama Nura akauliza swali kwakusema. Nura umeshamuonesha hilo duka?. Nura alijibu kwa heshima. Ndiyo nimeshamuonesha na analijua vizuri sana. Mzee Kerima naye aliuliza. Ni Kweli kijana unalijua hilo duka?”.
Ndiyo nalijua Kabisa.
Basi vyema kwa hivyo. Kwasababu kikubwa hapa tulichokuwa tumekuita hapa ni kuweza tu kukujua vizuri sura yako ili hata lolote likitokea tujue nini cha kufanya. Nuru alikubali. Sawasawa. Haya basi acha mimi nirudi nyumbani. Mzee Kerima na mama Nura waliitikia kwa pamoja kwakusema hivi. Haya siku njema”.  Basi Nura aliwezakuinuka na kuanza kumsindikiza Nuru hadi alipofikia pale getini na wakawa wamefanya maongezi kidogo. Nuru alipigia simu dereva bodaboda ilia je kumchukua Nuru na kumpeleka nyumbani.
Ilikuwa ni furaha sana kwa wazazi wa Nura kwa kupata kijana ambaye sura yake ilionekana kabisa ni sura isiyo ya kutatanisha katika masuala ya kazi. Baada ya Nuru kuondoka huko nyuma wakaanza kumjadili. Baba Nuru akasema. Lakini mbona huyu kijana anaonekana ni mpole Sana?. Nura akajibu. Hapana baba. Ni kawaida mtu akifika nyumbani kwa watu huwa anapaheshimu na kujikuta mdomo anaufunga haoneshi makucha yake. Mzee Kerima akasema. Basi sawa inaweza ikawa kweli. Mama Nura akasema. Kwa mimi sijaona kasoro yoyote kwa huyu kijana. hivi umesema anaitwa?. Aliuliza swali uchokozi tu.
Anaitwa Nuru.
Ahaaaa alafu mnapishana irabu tu kwenye majina yenu. Nura aliongea kwa kufurahi. Haya bana mama na wewe una mambo. “Hapana Nura labda panaweza kuwa na jambo hapo. Haya Bana. Mama akasema. Haya bana.. siku za mwizi arobaini.
Ni siku hiyo hiyo ikiwa ni mishale ya saa nane mchana. Nuru alikuwa na rafiki yake wakiwa na maongezi ya hapa na pale kuhusiana na mipangilio ya kimaisha. Rafiki yake Nuru anaitwa Kambi walikuwa wamekaa eneo fulani hivi la kupumzikia. Basi maongezi yao yalikuwa hivi.
Eee bwana Kambi kuna kazari naona kamejitokeza. Kambi alifurahi kusikia vile. Wapi tena brother?. “Siunajua yule demu wangu anaenda maschool wiki ijayo. Ahaaaa Nura siyo?. Ndiyo ndiyo. Imekuwaje tena?
“Ameniambia nisimamie kwenye lile duka lake la maeneo ya pale makao mapya. Kambi akasema. Ahaaaa basi ni vizuri hapo brother. Ila yule demu bado kabisa mna uhusiano naye?. Kambi aliuliza swali kisha Nuru akajibu akiwa anafurahi. Ndiyo jibu lake bwana Kambi. Kwanini umeniuliza hivyo?. Aaaaaa unajua yule ni mwanamke wa familia ya kitajiri. Kwahiyo kuna muda anaweza akaamua kuwanunua tu vijana kama nyiye kwa ajili ya kumuweka tu yaani kumburudisha tu.
Duuu unanitisha ndugu. Nuru alinena kisha Kambi akasema. Hapana ila ndivyo ilivyo tu hivyo ndiyo maana nimekwambia mapema hili jambo. Basi sawa nimekuelewa mwanangu. Pamoja sana.
Basi mida mida tutasomana.
“Poapoa.
Nuru alitoka pale baada ya kumaliza stori mbili tatu na Kambi kisha akawa ameelekea nyumbani.


Ikiwa ni mishale ya saa mbili usiku. Mezani palionekana kuna matunda embe, ndizi, parachichi, nanasi lililokuwa limechongwa vizuri na kukatwa katika vipande viwili na kipande kimoja wakawa wamekata katika vipande vingine vidogo vidogo na kuviweka katika sahani iliyokuwa ikimeremeta kama lulu. Mama Nuru na baba Nuru wakiwa wamekaa pamoja na Nuru akiwa amekaa kwenye kochi pekee yake huku akiwa anaendelea kupata matundaa pole pole ili kuzidi kujenga afya yake kama ilivyo ada kuwa mwili haujengwi kwa matofali bali ni kwa kula tena mlo kamili. Kulikuwa na maongezi maalumu kati ya mzee Kerima, mama Nura na Nura mwenyewe. Basi muda huo mzee Kerima alikuwa akisema.
Nura mwanetu.
Beee Baba. Baba akasema. Natumai unajua na kutambua kwamba wewe ndiye mwanetu pekee katika familia hii ya mzee Kerima na Bibiye Hadhila ambaye ni mama yako?. Nura alijibu kwa heshima. Ndiyo wazazi wangu nalitambua jambo hili. Aaaaa kilichotufanya hadi kuweza kukalishana hapa mda huu ni kuweza tu kuwekeana ahadi na mikataba baina yetu sisi na wewe ambaye ni mwanetu.
Sawa.
“Nakumbuka kipindi sisi tulipokuwa tumepata ajali kipindi hicho wewe ulikuwa na miaka kama mitano hivi. Kwakweli roho iliniuma sana kwa kusema kwamba je ningekufa au tungekufa ni nani haswaa angerithi mali zote hizi. Jambo hili kwa kweli lilikuja kunikereketa sana roho. Nilichukulia mfano ndiyo tumekufa ni wapi leo wewe ungekuwa kwa hali ya dunia ya leo namna ilivyo?. Hakuna cha ndugu wala nani angekuwa upande wako kila mtu angeanza kuangali chake kilichompendeza na kuchukua kisha anaondoka zake na hadi ungeambiwa uondoke kabisa na nyumba hii si yako. Ndugu hawa hawa unaowaona leo wanakuchekea na unacheka nao vizuri tu lakini kesho na kesho kutwa ndiyo wanakuja kuchoma kiatu chako ili utembee peku. Kwahiyo siku moja nikiwa bafuni kwa kweli machozi yalinitoka sana nikiwaza tu juu ya suala hili. Sidhani kama ungepona mwanagu. Nawajua hawa ndugu namna walivyo. Hata mimi nisingekuwa na nguvu za watu wa juu sidhani kama ningeweza kufanikisha mali za mzee Isambe. Mzee Isambe alikuwa na magari si ya mengi sana. Aliamua kuwaweka ndugu katika kila gari ili waweze kumsaidia katika suala la kiulinzi. Ndugu zake walipata hela sana kupitia mgongo wa mzee Isambe. Katika jumba lake watu kuja na kutoka hapakuwa panaisha pale. Si wageni si wenyeji waliingia muda wowote katika kaya ya mzee Isambe. Kila aliyeleta shida yake kwa mzee Isambe aliweza kusaidiwa. Lakini mwisho wa siku mzee Isambe anakuja kufariki nakuambia kulikuja kutokea mvurugano mkubwa sana. Ndugu zake walikuwa wakichukua mali za mzee Isambe kipindi hicho mimi nikiwa bado kijana kijana kwahiyo kwa baadhi ya watu wa juu ambao walikuwa ni marafiki wa baba yangu nilikuwa ninawajua na wenyewe walikuwa wakinijua fika. Baada ya mali nyingi kuchukuliwa na watu wakaanza kujimilikisha ndipo nikakutana na kiongozi mmoja hivi alikuwa anakaa jirani na sisi na alikuwa ni rafiki wa baba damu damu. Niliamua kumuelezea situation nzima ya tukio hilo kwasababu na yeye kwenye msiba alikuwepo so siku ile mazishi yalivyoisha tu aliamua kuondoka. Kwasababu alikuwa ni mtumishi wa serikali kwahiyo masuala ya kusafiri alikuwa akisafiri mara kwa mara sana. Ndipo akawa amelivalia njuga suala hili na mali zote zikafanikishwa kurudishwa na kuanzia pale tayari nikawa nimeshakua kiakili kabisa. Hakuna aliyekuja kuleta mdomo kwangu sijui aseme hivi na afanye vile. Kwahiyo kwasasa niseme tu umeshakuwa ni mkubwa wa umri, wa mwili na akili pia na kuweza kujua kwamba hiki kitakuwa changu hiki kitakuwa chake. Natumai kwasasa ni miaka kama ishirini na kitu umefika kabisa. Wakiwa wamekaa kwa makini wakiwa wanamsikiliza mzee Kerima Nura akasema. Ndiyo nimefikisha. Baba akasema. Sawasawa. Kwahiyo niseme tu hiyo siku unapoenda huko shule uwe unajua Kabisa kwamba hata kama tukifa leo au kesho yake ujue kabisa mali zote hizo ni zako. Maduka yote yaliyoandikwa Kerima shop ni yako. Pia na maduka yaliyoandikwa Hadhila shop ni yako si ndiyo hivyo mke wangu?. Mama Nura alijibu kwa heshima. Ndiyo ndiyo mume wangu.
Umesikia?.
Ndiyo Baba.
Hatuna mtoto mwingine zaidi ya wewe tu. Wewe ndiyo mwanetu wa kipekee ambaye tunamtegemea. Kwasababu nimeamua kuongea jambo hili mapema kabisa. Kwasababu hamna anayejua kwamba kati ya mimi, mama yako hapa au wewe nani atakayefariki wa kwanza. “Sawasawa Baba”
“Kwahiyo mimi ni hayo tu niliyokuwa nilitaka kukujuza mapema kabisaa ili usije ukaanza kuumiza kichwa kipindi hicho. Yaani katika maduka yote na mali yoyote ile niliyowahi kukuonesha hamna share na mtu kabisa. Isije ikaanza kutokea eti mimi nilikuwa na share na mzee Kerima. Hamna hamna hamna kabisa. Mama Nura akasema. Aaaaa Nura mimi kama mama yako niseme tu haya mambo baba yako aliyekuambia hapa ni mambo ya msingi sana katika maisha yako. Kwahiyo kuwa makini sana. Kuna watu wanatamani sana wangeambiwa maneno kama haya lakini ndiyo hivyo too late.
Sawa mama. Kumbuka kuishi na watu vizuri. Usije ukajiona kwamba mali zote hizi kwamba eti kufilisika ni vigumu. Hapana kufilisika ni kitu ambacho chanzo chake unaweza usione kabisa bali mwisho wa siku utajikuta hauna chochote tu. Mheshimu kila anaye kuheshimu.  Nura akajibu. Sawasawa nimekuelewa. OK fanya ukalale ili kesho tuwahi maeneo fulani hivi kwaajili ya kufuatilia karatasi fulani za kukuwezesha wewe kuweka saini ili kuwa na rekodi mapema sana. Sawasawa Baba. Nura alitoka pale na Kisha akawa ameelekea kitandani kwa ajili ya Kulala.





























SURA YA PILI
Ilipofika siku ya ijumaa Nura kwake ilikuwa ndiyo siku ya kuweza kusafiri ili kuelekea huko shule. Amabapo shule aliyokuwa amefanikisha iko huko Jijini Dar es salaam. Ambapo msafara huo ukiongozwa na Mzee Kerima ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari huku Nura akiwa ametulia tuli kwenye gari akiwa anawaza kwamba ameshayazoea maisha ya Arusha sijui kama ya huko Dar es salaam atayazoea kwa muda mfupi. Shule aliyokuwa amepangiwa inaitwa Jitegemee.
Muda huo wakiwa njiani Nura alizama katika bahari kubwa sana ya mawazo. Basi alikuwa akijiuliza maswali na kujijibu. Akiwa amekaa pembeni hapo na mzee Kerima akiwa ameshikilia vizuri sukano yake na kuonesha umahiri wake wa barabarani akiwa na gari. Nura alikuwa akiwaza. “Hivi haya maisha ya Dar nitayaweza kweli?. Duuu miaka miwili si ya utani. Yaani naona itanipotezea muda sana huku. Ila nitafanyaje sasa wakati ndiyo nimeshayavulia maji nguo kwahiyo shariti niyaoge tu sina lingine tena. Shule yenyewe ni ya jeshi yaani hapa sijui itakuwaje. Muda huo akiwa anaendelea kuwaza na kuwazua mzee Kerima alimshtukia Nura akiwa katika mawazo ikabidi mzee Kerima amuite Nura kwa kusema.
Nura  Nura. Nura aliitika kwa kushtuka fulani hivi. Beeee baba. Baba akasema. Haupo kabisaa hapa. Yaani nakuona haupo kabisa hapa. Nura akakataa kwa kujiamini kabisa. Hapana baba niko hapa Kwenye gari.
Simaanishi hivyo.
Bali.
Haupo hapa kimawazo.
Bali nipo hapa kinini.
“Kimwili tu. Nini tena kinakusumbua kichwani mwanangu?.  Inaonekana mshale wa speed ukiwa unazidi kupungua yaani mzee Kerima akawa amepunguza kidogo mwendo wa gari. Kwasababu ya maongezi yale ya ghafla. Nura alimjibu baba yake. “Hapana baba sina mawazo. Naangalia tu huko nje tunavyoiacha miti nyuma na sisi tunazidi kwenda mbele. Yaani hapo ndipo ninapofikia mahali naanza kuamini kwakweli sometimes hakuna ukweli katika hii dunia. kwasababu sisi tunaenda mbele miti inarudi nyuma. Huoni huo ni uongo kabisa?.
Mzee kerima alicheka sana kwakuona kwamba Nura anamdanganya kisha mzee Kerima akasema. Nura wewe comedy sana. Mzee Kerima akacheka kicheko kilichofanya hadi meno yake ya mwisho kuweza kuonekana.
Comedy tena?. Aliuliza Nura.
“Ndiyo. Yaani wataka kuniambia kuangalia kote huko nje ndiyo suala hilo tu?.
Ndiyo.
“Hapana kabisa”.
“Unajua baba kwakweli Dar sijawahi kuishi kabisa. Alimuueleza ukweli.
Kwahiyo unatakaje?. Baba aliuliza huku akiwa anamuangalia Nura.
Naona sijui yaani hadi nije nizoee siyo leo. Alimjibu baba yake huku akiwa anaonesha sura ya furaha.
“Haina shida utazoea tu kadri muda na siku zitakavyozidi kwenda. Kwani hakuna aliyezaliwa akiwa ana mazoea na hii dunia. Bali kila mtu alizaliwa akiwa ana mazoea ya tumboni tu. Hakusita kutoka tumboni kwasababu kwamba hajazoea mazingira ya duniani. lahasha. Kila jambo jipya huwa la baada ya muda fulani ukiamua tu. Huko njiani akiwa anapishana na mabasi yaendayo Dar es laam na magari ya mizigo.
Sawasawa
“Kwa ujumla maisha kwa mwanadamu ni kama vile upepo tu namna ulivyo. Yaani kuna sehemu upepo utakuwa na nguvu sana na sehemu nyingine kidogo hautakuwa na nguvu. Akiongea huku akiwa ameshika sukano kwa mkono mmoja na mwingine ambao ni wa kushoto akiwa anaonesha kwa ishara katika maongezi yake.
         Basi maongezi yaliendelea pale ndani ya gari baina ya mzee Kerima na Nura hadi ilipofikia Nura kupitiwa na usingizi. Safari kwa kweli ilikuwa shwari sana kwa kuwa ni usafiri wa binafsi basi hakukuwa na kusema utasimama kituo hiki wala utashusha kituo hile. Safari ilinoga hadi wakawa wamefika katika jiji la Dar es salaam.
Maneno ya baba kama kichwa cha familia kuyatanguliza katika maisha ni jambo zuri sana katika familia yake. Kwasababu yeye ndiye kichwa cha familia hivyo angali akiwa hai asipoacha maneno yoyote katika kaya yake ya mungu mengi na siku zote mungu si athumani aijue ratiba yake ni yeye mweyewe. Siku zote mipango ya mungu haina makosa. Basi nisemapo hivyo kidogo ugumu upo. Ila ni kwamba ukikumbuka maneno ya mzee Kerima alivyokuwa akimwambia mwanaye wakati wakiwa katika kikao kwa ajili ya kumrithisha mali zote ninatumai maneo yangu utayaelewa. Kwahiyo ni jambo jema sana alilifanya kwa yeye kuweza kumpa maneno yale.
Katika maisha kila mtu huhitaji matarajio mazuri kwa kila mipango yake. Lakini siku zote hakuna aijuae leo wa kesho bali unajua tu baada ya kupita hiyo siku ndipo utasema kwamba jana palikuwa hivi bali hutasema leo patakwa hivi kiimani.
Ni baada ya miaka mitatu. Nura akiwa katika masomo yake ya elimu ya juu katika chuo kikuu cha Dar es salaam wazazi wake yaani mzee Kerima na Bibiye Hadhila waliweza kupata ajali mbaya sana ambayo ilikuwa tofauti na ajali ya mara ya kwanza kipindi Nura akiwa na umri wa miaka mitano. Kwa kipindi ajali inawakuta wazazi wa Nura ndiyo Nura alikuwa mwaka wa kwanza hapo katika chuo Kikuu cha Dar es salaama. Kwakweli baada ya kupata taarifa ile aliumia sana. Nura alikuwa ni mtu wa kulia tu kwanzia safari ilipoanza kutoka Dar es salaam hadi kuja kufika Arusha. Taarifa ya kifo cha matajiri wale wakiwa ni mke na mume kwa kweli zilisambaa sana katika vyombo vya habari vya ndani na nje. Kila kijana ambaye alikuwa akitegemea chakula kutoka kwa mzee Kerima aliweza kushtushwa sana na kifo kile.
Kwa ujumla ajali ile iliweza kupoteza maisha ya wazazi wote wa Nura. Yaani mzee Kerima na Bibiye Hadhila waliweza kupoteza uhai wao kwa ajali ambayo waliipata. Ajali hiyo ilitokea ni baada ya kuanguka na gari pindi walipokuwa wakielekea huko mkoani Dodoma kwa ajili ya kwenda katika mazishi ya ndugu yao. Kwenye gari walikuwa wawili tu na dereva alikuwa ni mzee Kerima. Lakini mwisho wa siku ndiyo hivyo ajali ikawakuta na tayari nao wakawa ni watu wa kusema si kwenda kuzika bali ni kurudishwa kuzikwa tu.
Kwakweli jambo lile liliweza kumuwazisha sana Nura kwa wazazi wake kuweza kufa kwa siku moja na kisababishi kimoja ambacho ni ajali ya gari. Wazazi wa Nura haswa haswa mzee Kerima ni mtu aliyekuwa akijulikana sana. Yote hiyo ilikuwa ni kutokana na Mzee Kerima alikuwa ni mfanya biashara mkubwa katika jiji la Arusha kwa miaka hiyo. Siku hiyo ya mazishi Kwakweli watu wengi waliweza kuwasili katika mazishi yale. Ndugu jamaa na marafiki  walitoa machozi sana kwa kuondokewa na mtu ambaye alikuwa ni maarufu sana tena wa faida kwa watu wengi sana. Nuru alikuwa ndiyo wa kumfuta machozi kila Nura alipolia. Hakuwa na namna kwasababu japokuwa Nuru ameajiriwa kwa akina Nura lakini kwa upande wa pili Nuru ni mpenzi wa Nura. Kwahiyo ilikuwa ni jukumu lake kumfanya Nura asijihisi mpweke kabisa.
Kwahiyo kwa siku hiyo ya mazishi ilikuwa ni siku nzito sana kwaajili ya kuweza kupokea pole nyingi sana za majonzi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki kutoka maeneo mbalimbali. Kifo kile cha wazazi wa Nura kilimuweka Nura katika hali ya mkanganyiko kwa muda mrefu sana ambapo kwanza ndiyo yuko mwaka wake wa kwanza huko Chuo. Basi siku ya maziko maandalizi ya maziko yaliweza kufanyika. Wakati wa kusafirisha miili kwa jili ya maziko kwa kweli palikuwa na magari ya kifahari ya kila aina. Wengine wakiwa ni waarabu kutoka huko uarabuni, wengine ni watu kutoka mataifa ya ulaya na wengine kutoka huko mataifa ya Amerika.  Msafara wa kusafirisha miili yao kwakweli ulikuwa ni kama msafara wa kiongozi mkubwa kabisa. Mwisho wa siku mama na baba Nura walizikwa katika eneo moja ikiwa ni maeneo ya makaburi ya mkoa yalipo. Wakati wanazika Nura hakuwa anaamini kama ni kweli kuwa wazazi wake wamefariki kwa mkupuo na hata baada ya kumaliza kuzika na ndugu walimshika na kumrudisha kwenye gari lakini bado tu hakuwa anaamini kuwa mzee Kerima na Bibiye Hadhila wameaga duni na ndiyo hatoweza kuwaona tena hadi naye kifo kitakapomkuta na parapanda kupulizwa.
Baada ya mazishi kumalizika sasa ikawa ni mda kwa mwanadada Nura kuumiza kichwa ili kuweza kutekeleza maneno ya baba na mama ambayo aliweza kupatiwa wakati wazazi wake wakiwa hai. Ni katika tu suala la kuweza kumiliki mali zote ambazo zilikuwa ziko chini ya mzee Kerima na Bibiye Hadhila. Kufanya hivyo haikuwa rahisi sana kwa yeye kama yeye kuweza kukamilisha kila kitu bali aliamua kupata msaada mkubwa kutoka katika mahakama za juu kwaajili ya kuweza kumiliki mali zote hizo. Pia huku Kijana Nuru alikuwa bado yuko katika duka la Nura lililopo hapo makao mapya.

 Mzee Kerima katika mkoa wa Arusha alikuwa na maeneo mengi sana ambayo yalikuwa chini yake. Yakiwa ni maduka, gereji, timu za mpira zikiwa ni mbili yaani timu ya wasichana na wavulana. Vijana wenye vipaji waliweza kusajiliwa katika timu hiyo iliyokuwa ikijulikana kwa jina la KFC yaani Kerima FootBall Club. Timu hiyo iliweza kutamba sana na ilikuwa ikichukua ushindi sana katika ligi mbalimbali zilizokuwa zikichezwa. Kwahiyo vijana mbalimbali waliokuwa na vipaji haswa waliweza kujipatia ajira. Katika masuala ya usafiri mzee Kerima alikuwa na mabasi kumi yaliyokuwa yakisafiri katika mikoa mbalimbali ambayo ilikuwa ni mikoa mikubwa. Magari yake yaliitwa Kerima Trans. Watu walijipatia fedha sana kuptitia tu mabasi hayo. Huko kwenye maduka yake ya mavazi kwakweli nako watu waliajiriwa sana. Kwahiyo ni kama sehemu karibia zote alikuwa ameweka vitega uchumi ili tu kuweza kusaidia pia vijana kuweza kujipatia fedha na kujikwamua kimaisha.


Siku zote wawili wapendanao wanapoishia maeneo ya mbali kijiografia yani huyo yuko kule na yule yuko sehemu nyingine kwakweli kuna mengi sana huweza kujitokeza. Nura akiwa chuo alianza mahusiano ya kimapenzi bila Nuru kutambua lolote. Mtu huyo waliyekuwa wameanza naye mapenzi alikuwa naye akiwa katika chuo hicho ambacho alikuwa akisomea Nura. Utofauti ulikuwa ni kwamba kijana ambaye alianza naye uhusiano wa kimapenzi ambaye alikuwa akiitwa Mpundu alikuwa akisomea kitivo cha uanasheria na kwa Nura yeye alikuwa akisomea uandishi wa habari. Kwahiyo Mpundu naye ni mzaliwa wa huko huko Arusha. Baba yake Mpundu naye ni mwanasheria mkubwa sana. Kwahiyo ilibidi sasa Nura aweze kuwa sanjari na huyo Mpundu ili kuweza kupata mali zote za wazazi wake kuwa chini yake. Kwahiyo kwa msaada ule mkubwa ambao Nura alipatiwa na Mpundu hapo sasa Nura ndipo alipozidisha mahusiano ya kimapenzi na huyo Mpundu na kuanza kumsahau Nuru ambaye wametoka naye mbali. Mwisho wa siku Nuru akawa amebaki kama mfanyakazi tu wa Nura.
Mambo yote yalipoweza kukamilika ndipo Nura na Mpundu wakawa wamerejea chuo. Basi siku hiyo ilibidi Nuru ampigie simu Nura. Ambapo ilikuwa ni mishale ya saa nane mchana Nuru anaonekana yuko dukani. Nura akiwa anaonekana yuko katika maeneo fulani hivi ya chuo. Muda huo nguo aliyovaa ni miniskirt na juu akiwa amevaa kinguo ambacho kiliweza kuonesha namna alivyojaaliwa mgongo wake. Mazungumzo yao yalikuwa hivi.
Mambo vipi Nura. Nura akiwa anaongea kwa bashasha kwakuwa anaongeana mwandani wake.
Safi. Nura alijibu kama vile hataki.
Pole na masomo.
Asante. Pole na wewe na kazi. Aliongea kama boss.
Asante sana mpenzi wangu.
“Mbona kama maneno yamekuteleza hivi Nuru?. Aliongea kama akiwa amekasirika hivi.
Yameniteleza?. Alimuuliza kwa mshangao sana.
“Ndiyo maana Yake.
Nura... Kuna kitu kilimwijia moyoni mwake na kuhisi kama moyo unamuuma hivi ila akaamua kupiga moyo konde tu kisha akasema. Unamaanisha nini unaposema hivyo?.
“Hapana nimesema tu kama ulivyosema. Alimjibu kirahisi.
Sijakuelewa vizuri. Ila unajua Nura tangu baada ya kufariki kwa wazazi wako kwakweli mbona kama naona mabadiliko makubwa sana katika uhusiano wetu?.
Uhusiano gani?.
Unauliza uhusiano gani kabisaaaa?. Kwakweli Nuru hakuamini majibu aliyokuwa akipatiwa na Nura. Alikata simu baada ya kuona kwamba Nuru anaanza kuleta mambo mengine. Ambapo mda huo kwa pembeni alikuwepo Mpundu. Mda huo Mpundu akamuuliza Nura.
Nani huyo anakusumbua?. Aliuliza kwa sauti yakle iliyokuwa ya nzito kama dufu la tatu.
Aaaaaa si huyu mfanyakazi bana.
Mfanyakazi wa wapi?
“Wa lile duka la kule makao mapya. Yule siku ile ya msiba nilikuwa nae.
“Ahaaaaa… kama anazingua mteme bana. Aliongea kwa sauti ya juu angali hata hajui chanzo ni nini kabisa.
Tulia dawa yake iko motoni. Nura alitoa jibu hilo huku akiwa amesahau fadhila zote za Nuru kwake Nura.
Jambo lile la Nura kukata simu Nuru alishtushwa. Hakamini kabisaa kama ni huyo Nura ndiyo anaongea hivyo na anaamua kumfanyia vile.
Kwakweli wanadamu ni watu ambao tumeumbiwa na shida. Hakuna ajuae shida yake itafumbuliwa na nani japokuwa wote huwa tunanyoosha mikono juu na kumshukuru mungu ila hatukumbuki mungu kakusaidia kupitia nani. Mwanadamu unaweza kumtoa katika shimo lililokuwa na maji lakini bado akaja kukukojolea kwa maji aliyokunywa sehemu nyingine yakiwa katika aina nyingine. Hapo ndipo utakapoamini kuwa shukurani ya punda mateke na siku zote tenda wema nenda zako usisubirie shukrani.
Nuru alijikuta akiwa ameingia kwenye msitu wa mawazo sana kwa jambo ambalo Nura amemfanyia. Nuru alijikuta kama dunia imemuelemea kabisa. Kwasababu siku zote hakuna kitu kibaya kama unampenda mtu alafu mtu huyo naye kakuaminisha kuwa anakupenda lakini baada ya mtu huyo anaanza kukuonesha dalili za usaliti. Kwakweli roho huwa inauma sana jambo kama hilo litokeapo. Moyo huwasha na kutamani hata utoke tu sema ndiyo hivyo ukitoka nawe utakosa uhai na utakufa mwisho wa siku utajikosea na mengine mazuri ya dunia. Muda Nuru akiwa amekaa kwenye kiti alianza pekee yake kimoyomoyo akiwa anajiuliza maswali na kujipatia majibu ambayo nayo aliyakata. Muda huo kuna wateja wanachagua nguo hapo dukani.
“Hivi huyu ni Nura au ni nani?. Yaani unajua siamini au huyu amechanganyikiwa kwasababu ya wazazi wake kufariki kwa mkupuo?. Lakini hata kama ni kufiwa jamani haya miezi imeshapita mingi tu. Yaani tuseme hadi leo hajayasahau tu hayo mambo?. Ila mimi nahisi kuna kamchezo kapo hapa lakini sielewi chochote hapa. Kwani mimi ni nani kwa Nura?. Aaaaaa nahisi nipo mara mbili kwa Nura. Upande wa kwanza kwa Nura mimi ni mpenzi wa Nura na upande wa pili wa Nura mimi ni mfanyakazi wa Nura. Sasa hapa ni kama mtu mwenye jinsia mbili yaani moja ikiwa inafanya kazi sana ndiyo itajulikana jinsia ya huyo mtu. Duuuuuu mbona sasa kwa mimi hapa sijielewi kabisaa. Nahisi niko njia panda kabisa sijui niko kulia au kushoto. Akiwa anaendelea kuwaza na kuwazua japokuwa mawazuo hayakuwa na hitimisho alishtushwa na sauti ya mteja ambaye aliita takribani mara tatu huku Nuru akiwa mbali kimawazo. Mteja yule alikuwa ni msichana mrembo alojaaliwa uzuri.
Wewe kaka. Akiwa amesogelea na alipo Nuru na kumgusa kichwani.
Nuru alishtuka na kusema.  Nhaam Nhaam. Dada.
 Mbona nakuita hata hauitiki?. Nini tatizo.
Dada samahani nilikuwa mbali sana kimawazo. Ninuie radhi dada. Alimuomba msamaha.
Sawa. Pole sana kaka kwasababu si kwa mawazo hayo. Una shida gani angali una kazi nzuri tu na wateja wanakuja muda wowote wanajichagulia nguo za kutosha tu alafu unakuwa na mawazo hivyo ya nini?.
 Unajua dada unaweza ukawa na pesa hata ukajaza hili duka lakini kuna jambo moja tu japokuwa ni dogo likakukosesha raha sana katika haya maisha. Alimjibu kwa sauti ya upole.
Ahaa hapo nimekuelewa. Haya basi shika fedha yako hii hapa. Naona mzigo ulioenda kuchukua awamu hii mzuri sana ndiyo maana watu wanajaa sana. Aliongea huku akiwa na tabasambu lililojaa.
Alipokea fedha kisha akawa anasema. Nashukuru sana dada. Ni kweli ila ndiyo hivyo. Akawa anaweka fedha zile sehemu maalum kwaajili ya ulinzi zaidi.
 Haya basi mimi naenda kaka.
Sawa. Karibu sana dada.  Aliongea huku macho yake yakiwa yamevutiwa sana na umbo la msichana yule lilivyokuwa zuri.
Sawa upunguze mawazo. Aliongea huku akiwa anamalizikia mlangoni.
“Sawa dada. Kisha akasema kimoyomoyo. Natumai atakuja tu tena hapa. Hapo sitofanya kosa.
Kuwepo kwa mteja yule kulimfanya Nuru aweze kurudisha furaha yake katika moyo wake. Kwasababu msichana yule alionekana akiwa na umbo zuri kumzidi Nura. Kwahiyo kuondoka kwa msichana yule kulirudisha tena simanzi katika moyo wa Nuru.



SURA YA TATU
Siku nyingine ilo kheri kwa watu wengine bali iso kheri kwa Nuru. Ikiwa ni mishle ya saa kumi jioni anaonekana Nuru akiwa dukani kwa Nuru. Muda huo anaonekana mavazi yake aliyovaa ni mavazi ya kawaida tu huku akiwa amekaa zake tu kwenye kiti cha CELLO. Akiwa amezama kwenye mawazo akiwaza na kuwazua hivi na vile huku akiwa ameshika tama kama mtu aliyefiwa na wazazi wake wote na kubaki pekee yake katika ulimwengu ghafla simu iliita. Mwito wa simu ya NOKIA uliita na kumfanya ashtuke sana na kuikikmbilia simu iliko. Ambapo simu hiyo ilikuwa ikichajishwa kwa muda huo. Alipoangalia jina ili ajue ni nani anapiga muda huu wa kuweza kumponesha donda ambalo limejitokeza tangu siku iliyopita. Alipoangalia vizuri aliona jina likiwa limekuja ni MPENZI NURA likiwa limeandikwa kwa herufi kubwa. Aliganda kama sekunde tano akiwa kama hajielewi yaani apokee simu au asipokee simu huku akiwa anajiuliza maswali kuwa huyu Nura amempigia simu muda huu kwasababu gani. kwasababu ni mazoea ya Nura kupiga simu mishale ya saa mbili usiku ili kujua mapato kwa siku. Hiyo ndiyo kawaida ya Nura. Basi Nuru akiwa bado ana uzito wa kupokea simu alijikuta tu tayari dole gumba limeshaminya kwenye kibonyezeo cha kupokea simu ile na kusema.
 Haloo Mambo vipi Nura?.
Safi.
Za tangu siku hiyo?.
“Natumai nzuri tu labda kama kwako huko Arusha ni mbaya. Aliongea Nuru kwa sauti ya kutokutaka.
Nahisi ni mbaya.
Ahaaaaa unahisi siyo basi inaweza ikawa siyo
Basi ni kweli ni mbaya.
Ubaya wake uko wapi?.
“Siku ile ulinikatia simu na nilikuwa nina maongezi mazuri sana na wewe. Nura akasema. Kama yapi?. Kwani kwanza unajua mimi nimekupigia kwaajili ya nini?.
“Si kama kawaida wewe ni mpenzi wangu. Alijibu Nuru. Nura alimkata Nuru kauli na kusema hivi. Angalia muda mwingine hayo maneno unayoyaongea.
Samahani kama nimekosea.
“Kumbe unajua umekosea alafu wazidi kuboroja tu”.
Ukimaanisha nini?
Ndiyo ukweli huo. Iko hivi mimi hapa nimekupigia ili nikujuze kuhusu kwamba kesho kuna mizigo nataka uipokee hapo stendi.
Kwa gari gani?.
Sai Baba.
“Ahaaaaa Sawa”.
“Natumai unajua namna ninavyoandikaga majina ya mizigo yangu ikiwa inatoka mikoani?
Ndiyo.
Sawasawa. Basi ndiyo nilikuwa nataka tu nikutaarifu kuhusiana na suala hilo ili usije ukasema hiyo kesho nimekushitukiza sana.
“Sawasawa Nura haina shida nitakuwa makini kwa hilo.
Natumai kwakesho hiyo Sai Baba hadi mida ya saa kumi litakuwa limeshaingia labda tu itokee la kutokea huko njiani.
“Sawasawa. Ila Nura embu ni vyema ukanielewesha.
“Nini tena unataka nikueleweshe?.
Mimi sielewi unajua. Mbona nashangaa nikikuuliza au nikiongelea kuhusiana na suala la mahusiano yetu unakuwa unabadilika ghafla sana au nimekukosea nini Nura?.
Hapana  amna chochote.
Sasa tatizo ni nini?.
“Kwani wewe Nuru ni kipi kabisaa unakosa?. Kama ni mshahara nakupatia na hela nyingine pia tu nakupatia. Sasa nini unataka?.
“Nataka moyo wangu ufurahishwe na mpenzi wangu.
Ambaye ndiyo nani?
Wewe hapo.
Nuru
“Nhaamu.
Ujue Nuru ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Nuru, I am the boss and I am your boss wako na siyo mpenzi wako. Jaribu kuliweka hilo kichwani kabisa. Kwakweli maneno yale yalimshitua sana Nuru kisha akawa anasema hivi. Hivi Nura haya maneno mimi nayasikia kwa masikio yangu au vipi?.
“Sijui ndiyo nikuulize wewe hapo. Labda una masikio ya jirani hapo.
Nura.
“Ndiyo jina langu hilo ukipenda malizia kabisa Nura Kerima Isambe familia ya kitajiri. Nikwambie kitu Nuru fanya kazi. Mwisho wa siku utakuja kukosa vyote hapa. Kuwa makini siko hapa mjini kijinga kijinga tu.
Duuu yamefikia hapo tena jamani?
“Ndiyo maana nimekupa onyo. Japokuwa Wanasema mavi ya kale hayanuki ila kwako nahisi yananukia machozi. Kwahiyo kuwa makini sana na mimi.
Yananukia machozi?
Ndiyo
Tangu lini machozi yakanuka?
Ndiyo ujiulize sasa.
“Nura ndiyo hivyo kabisaaaaaaa?
“Nakwambia fanya kazi uokoe familia yenu katika janga la umasikini kama hilo
“Atiiiiii unasema nini Nura alimuuliza kwa sauti ya juu. Natumai umesikia kabisa ndiyo maana umeuliza ulichokisikia. Huo haukuwa muhtasari wa habari bali ndiyo taarifa kamili iliyosomwa na Nura Kerima.
“Kwahiyo mimi kwa wewe ni kama nani na nani.
“I am your Boss and you is my Servant.
Sijakuelewa. Maneno yale yalimuuma na kumfanya hajayaelewa ikambidi aulize.
Ni vigumu kunielewa.
“Ndiyo maana nimekuuliza
“Mimi siyo mwalimu.
Sawasawa Nura.
“Tumeongea mengi ila la msingi natumai unalikumbuka. Nura alikata simu na kumfanya Nuru kuumia sana lakini huku akiwa hana namna yoyote ya kulitua jambo hilo na kubaki akiwa kaduwaa tu mithili ya sanamu.
Basi ikiwa ni mishale ya saa mbili usiku hivi Nuru ilibidi taarifa zile ampelekee rafiki yake huyo Kambi ambaye ndiye mshauri wake Mara kwa Mara katika mambo mbalimbali. Kwahiyo alienda hadi sehemu alikopangisha huyo Kambi. Basi mazungumzo yao yalikuwa hivi.
Bana Kambi mimi kwangu nahisi maji ya moto yamekuwa baridi kabisaa.
“Nini tena brother Wakati kwasasa ndiyo uko kwenye Boom yaani Kwenye kilele kabisa cha pesa na huyo demu wako. Nini unalialia tena?.
Ayaaaa hapo hapo sasa kwa huyo demu.
Pamekuwaje tena.
“Brother unajua hata simuelewi Nura kwasasa sijui ni kapata jamaa mwingine huko chuo hata sielewi kabisa .
“Brother mbona kama hauna memory nzuri kabisa.
Memory tena.
Ndiyo.
Ya kufanya nini?
“Kwani wewe mbona nilishawahi kukuambia kitambo sana natumai ni kama miaka kadhaa imepita hivi. Nilikuambia kwamba hawa watoto wa kike wa kitajiri huwa wana tabia ya kununua wanaume. Kisha Nuru akamwambia. Lakini mbona Nura tumetoka nae mbali sana.Yaani tangu kidato cha kwanza. Kambi akasema. Ohooooo. Nikwambie tu ukweli Nura alikuwa anakupenda kwasababu tu wewe kwa darasani ulikuwa uko vizuri kimasomo na ulikuwa ukipata alama nzuri kabisa. Lakini ndiyo hivyo mungu si Athuman na kazi ya mungu haina makosa siku zote ndiyo hivyo ukawa umefeli. Kwa hapo sidhani kama kweli angeendelea tena na wewe katika mahusiano yale yale. Huko chuo nako kuna masharobaro zaidi ya wewe. Mbona hawa wadada tunawajua vizuri sana brother embu changamka wewe chukua chako pita hivi. Yule ashakufanya wewe kama vile kijakazi tu. Kwasababu huwezi kumhudumia zaidi kama level yake. Maneno yale kwakweli yalizidi tena kumuuma Nuru kwakuwa yalikuwa ni maneno ya ukweli kabisa. Siku zote mtu umwambiapo ukweli wa kitu ambacho ana udhaifu kwake ni vigumu sana huyo mtu kuweza kukuelewa kwa haraka na ndivyo ilivyo kwa Nuru. Sababu tayari ameshafia kwa Nura mrembo kutoka katika familia ya kitajiri. Nuru akasema. “Duuuuu Kambi nahisi ndiyo umenifungulia akili zangu kabisa. Yaani ni kama zilikuwa zimefanywaje sijui. Kambi akasema. Ila nikwambie kitu Nuru wewe pale Nura hata akusaliti vipi ng'ang'ania pale pale dukani wewe acha akusaliti lakini upate hela. Mbona wanawake wako wengi sana dunia hii wewe tena wazuri zaidi ya Nura kabisa. Wasichana wazuri kila siku wanazaliwa kwanini wewe uanze kungangania kwenye penzi la Nura kama kupe wakati mwenyewe unajionea kabisa huwezi kuhudumia pale?. Embu acha hivyo bana wewe kuna watu wanatamani wapate nafasi kama hizo lakini wapi hadi wanaenda kwa mashekhe lakini bado tu wanaishia kugonga ukuta na kuzidi kuvimba manundu tu.
Duuuu ni kazi hapo.
“Hapana ila ni maamuzi yako ili usije ukaanza kusema kwamba mimi nataka kukuvunjia kabisa uhusiano wako na Nura ambao ni wa tangu zamani kabisa. Hapana mimi ni kama ndugu yako tu nakushauri tu haya mambo. Kwasababu naona mwisho wa siku itajakuwa undugu lawama kabisa. Mimi hawa mademu nawajua sana washenzi sana wakishika hela. Kambi alimpa tahadhari. “Hapana Kambi siwezi kufikia huko. Yaani nianze kukulaumu wakati wewe ndiyo mchizi wangu.
“Siwezijua katika akili zako unauchukuliaje huu ushauri
Wala usiwe na hofu Kambi. Kwa hapo nimekuelewa kabisa wewe ni rafiki yangu na tumetoka mbali. Ila ndiyo hivyo tu Nuru wewe ng'ang'ania tu pale yule demu ana hela chafu. Wewe angalia mali zote zile zilizokuwa za wazazi wake ni yeye anazimiliki. Tumia nafasi hiyo mchizi Wangu. Hapo Hapo ndipo pakutokea. Kwa ujumla Pesa kwanza mapenzi Baadaye. Walipomaliza maongezi yale waliweza kuagana na kila mtu akashika njia yake.


Siku iliyofuatia mishale ya saa kumi jioni. Nuru alienda kuipokea mizigo ambao aliagizwa na Nura tangu siku iliyopita. Basi aliichukua mizigo ile na kwa muda huo alikuwa tayari ameshamuandaa jamaa mwenye toroli ili aweze kupeleka mizigo ile moja kwa moja hadi dukani huko maeneo ya makao mapya. Baada ya kuifikisha ile mizigo basi Nuru aliweza kumjuza Nura kuwa ameshapokea ile mizigo.
Kwa ujumla duka ambalo Nuru anauza ni duka la nguo za watoto wa kike na wakiume, pia za watu wakubwa yaani kuanzia umri wa miaka kumi na tano na kuendelea. Kwa Arusha nzima hilo lilikuwa ndilo duka ambalo lilikuwa na jina lenye kujulikana sana kwa kipindi hicho. Mara kwa Mara wateja huja sana katika duka hilo. Muda mwingi wateja huingia na kutoka kama mchwa wakiwa wanajenga kichuguu harakati zao huwa haziishi kamwe.
Baada ya kupita muda mrefu hivi Nura aliweza kuwasili jijini Arusha bila hata kumjulisha Nuru. Alipowasili nyumbani kwakwe siku hiyo Nuru alishangaa tu akiwa ametumiwa ujumbe wa simu ukisema “funga duka muda huu. Mimi niko nyumbani Nijiro”. Nuru alishangazwa sana na ujumbe ule ndipo akawa amejibu. Sawa. Kwasababu alishindwa hata namna ya kuuliza kwamba kwanini hajamtaarifu kama alikuwa anakuja. Nuru hakuwa na namna basi akawa amefunga duka na kuweza kupanda usafiri wa boda boda kuelekea huko Njiro. Basi muda huo wakiwa nyumbani ambapo Nuru yuko pale pale katika jumba la kifahari la marehemu mzee Kerima ambapo kwasasa anayeishi hapo na kulimiliki jumba hilo ni huyo Nura. Pia Nura akisafiri huwa kunakuwa na wafanyakazi wa kike na wa kiume. Kwa muda ule wafanyakazi wale walionekana wakiwa wanajishughulisha kila mtu na kazi wake na kuwaacha Nura na Nuru wakiwa katika maongezi mazito.
Nura najua aaaaaa au basi tu. Nuru alikatisha maongezi baada ya mate kumjaa mdomoni. Ongea kilichopo moyoni mwako. Nura alinena. Unajua Nura kwasasa kama sielewi kabisa. Nuru aliongea huku akiwa akiwa anonesha sauti ya upole kisha Nura akamuuliza. Huelewi nini?.
“Unajua Nura mapenzi yangu mimi na wewe ni ya toka mbali sana
Nalijua hilo.
“Sidhani kama unalijua hilo.
“Nalijua. Wewe jua tu hivyo kwamba nalijua.
Lakini mbona mimi sioni dalili za kusema unalijua hilo?.
“Mmmmh pole sana Nuru mbona mawazo yako yanakutuma mbali sana?.
“Lazima yanitume mbali. Mimi ni mtu mzima kwasasa.
“Kwahiyo kwakesho utakuwa siyo mzima.
Sijamaanisha hivyo Nura.
Ila ni nini?
“Mimi ni mtu kwasasa nimekuwa na akili za uelewa kwamba huyu mtu hachezi fair play kabisaaa.
Hofu yako tu
Au tatizo ni nini
“Sijui wewe kwani waona tatizo ni nini?
Nahisi hapa natumai sijui ni pesa”
“Yaweze ikawa hivyo
“Yaani kama leo unakuja bila hata kunitaarifu na unajua kabisa Arusha una mpenzi wako ambaye ni mimi alafu unakuja utafikiri sijui nini vile yaani jamani. Aliongea kwa sauti ya kuonesha jambo lile limemkasirish sana. Unajua Nuru sikuelewi kabisa unacholalamika ni nini haswa?. Nura alimuuliza swali mithili ya mtu asiyejua kabisa ni mada gani iliyoko mezani kwa muda huo. Kisha Nuru akasema hivi. Huwezijua kwasababu kwasasa tayari wewe umeshakuwa ni wa matawi ya juu kabisa na siyo level zangu kabisa. Nura alicheka kicheko cha dharau kilichoweza kuenea pale ndani na sauti ile kusikika kama inajirudi hivi. Kisha akawa amesema hivi. Unajua Nuru unachekesha sana tena sana. Ndiyo naweza nikawa nachekesha sawa ila ndiyo hivyo acha niyaongee yangu ya moyoni tu. Aliongea Nuru kwa sauti ya masikitiko. Nura fanya kazi wewe. Wewe cha msingi fanya kazi uokoe maisha ya familia yenu. Familia yenu ndiyo kama ile alafu unaanza kulilia mapenzi na mtu kama mimi siunataka kuumia tu Nuru?. Embu fanya kazi. Aliongea huku akiwa anamuangalia Nuru kwa makini. Haya bana amakweli pesa inarun dunia na siyo mapenzi tena. Alinena Nuru kwa moyo msononeki. Kawaida  ndivyo dunia inavyobadilika hivyo.
Siku iliyofuatia Nura aliweza kuzungukia maeneo mbalimbali ambapo kuna vitega uchumi vyake. Kila alipokuwa akienda alifanya ushitukizi na sehemu aliyokuta kuna uvivu wa kikazi basi watu waliadhibiwa sana. Adhabu hiyo ilikuwa ni kutokulipwa mshahara kwa mwezi mmoja. Wafanyakazi walishangaa sana namna ujaji wa Nura ulivyokuwa ni wa kushtukiza.
Kwakweli jambo lile lilibaki kuwa kikwazo sana katika akili ya Nuru kwa muda mrefu sana. Basi Nura alikaa Arusha kwa siku tatu tu kisha amerejea jijini Dar es laam. Wakati wa kurudi Dar es salaam alipanda ndege kupitia uwanja wa ndege wa KIA. Ambapo aliondoka na ndege ya saa mbili kamili asubuhi ili aweze kuwahi kwenda kufanya mambo mengine yanayomhusu huko Jijini Dar es salaam.
Wakiwa wanaonekana marafiki wa karibu sana ambao ni Nuru na Kambi wakiwa maeneo ya kijiweni ambapo siku hiyo ilikuwa ni siku ya jumapili. Ikiwa ni mishale ya saa Kumi jioni. Nuru kama yake ilivyo aliweza kwenda kumwelezea Kambi stori nzima ya kuja kwa Nura. Lakini Kambi katika ushauri wake ule ule.









































SURA YA NNE
Siku nazo zilizidi huku Nuru akiendelea kuyaweka vizuri maisha yake na ya nyumbani kwao kwa ujumla. Alianza kutafuta maeneo ya kununua viwanja kwa ajili ya kuanza kujiandaa kujenga nyumba. Huku wazazi wake nao akiwa anawandalia makazi mazuri.
Siku zote Nuru alikuwa akijipa tu moyo kwamba maisha na vikwazo anavyokutana navyo vyote hivyo ndiyo vitakuwa kama ufunguzi wa maisha yake. Kwasababu kwenye maisha changamoto ni kitu ambacho hakiepukiki kabisa. Pindi changamoto fulani ikukutapo si kwamba uikimbie changamoto ile bali inatakikana tu namna nzuri ya kuitatua changamoto hiyo. Ndivyo ilivyo katika maisha ya mwanadamu yeyote yule. Nuru alizidi kujibana hapo hapo huku akiwa anavumilia kwamba mpenzi wake kwasasa anamuita Boss na siyo Boss tu anamuita pia shemeji. Ndipo utakapotambua kwamba haya Maisha ni kama vile gwaride tu yaani ukisikia tu nyuma geuka hapo wa kwanza atakuwa wa mwisho na wa mwisho atakuwa wa kwanza hivyo basi hata majina yao hubadilika.
Basi ni baada ya kupita mwaka mmoja na miezi kadhaa. Siku hiyo Nuru na Kambi wako nyumbani kwa Kambi. Kambi naye ni mtu wa kibaharia sana yaani na yeye kama ni fedha kazishika kweli kweli. Kwasababu kazi yake ambayo alikuwa akijishughulisha nayo ni kazi ya kununua madini kwa maeneo ya pale Arusha na kwenda kuuza maeneo ya nchi za nje. Kazi ile ilimfanya ajulikane na matajiri wengi sana kwa maeneo mbalimbali akiwa bado ni kijana mdogo tu. Kambi wazazi wake walishafariki zamani sana ambapo walifariki kipindi akiwa na umri wa  miaka saba hivi. Hivyo basi katika makuzi yake alilelewa na mjomba wake ambaye naye  alikuwa akijishughulisha na ununuzi wa madini. Kwahiyo Kambi akawa amefuata nyayo za mjomba wake na kuweza kuzishikilia ipasavyo.
Ikiwa ni mishale ya saa saba mchana Nuru na Kambi Walikuwa wana maongezi hapo. Nuru akiwa amevaa suruali ya jinsi ya rangi nyeusi na tisheti nyeusi na Kambi naye akiwa amevaa tisheti nyekundu na suruali nyeusi. Mezani hapo panaonekana kuna vinywaji vipo hapo ikiwa ni Fanta Passion ambayo Nuru ndiyo anakunywa na Kambi yeye anakunywa coca-cola. Jumba hilo nalo lilionekana kweli anayeishi hapo ndani ni kijana ambaye ameshika fedha akiwa na umri mdogo. Sauti ya muziki wa HipHop ilikuwa ikisikika ndani hapo. Jumba hilo kwa juu limerembwa kwa hali ya juu sana kuwekwa taa ambazo zilionekana kama majumba ya Sinema ya huko HollyWood.  Ukutani palibandikwa picha za wasanii mbalimbali wa HipHop wakiwa ni wa nje na ndani ya nchi. Picha zilizokuwa zimejaa pale zilikuwa ni picha za wasanii wa HipHop kutoka marekani akiwemo RICKROSE, 5OCENT, NICKMINAJ na wengineo. Wasanii wa kitanzani ambao walionekana pale ukutani walikuwa ni kama vile JCB, vikundi kama vile weusi na watengwa, KCK. Hilo kundi la KCK ambao wao walikuwa vizuri sana katika uimbaji wa nyimbo kwa haraka haraka mithili ya cherehani za umeme. Basi waliongea kwa kina wakiwa wanaenda mashariki na magharibi kupanda na kushuka katika maongezi yao. Kuna jambo Nuru alisema.
“Kwahiyo bana mimi lengo la mimi kuja hadi hapa ni ili uweze kunipa ushauri kwa namna yake.
Sawasawa.
Kwani kwa muda wote huo kuna hela pia nilikuwa nikiihifadhi mahali. Ila kwasasa naona imefikia mahala pakuanza kutumika ili kuweza kuendelea kuleta faida.
“Ahaaa ni vizuri sana.
Ni kama milioni kumi hivi inawezafika.
“Ayaaaa mbona hiyo kubwa tu. Yaani hapo  tena ndiyo ukiamua kuanzisha Chegani mahala fulani hivi mbona fresh sana hiyo.
Chegani ndiyo nini hicho?.
Ni Salon
Ahaaaaa Kumbe nacho kiswahili kipana na kina uwezo wa kuringa kabisa.
“Ndiyo maana yake. Mbona Kiswahili kipana tu sema ndiyo hivyo sisi hatujaamua tu. Kwahiyo ukifungua Chegani tena ya kike itakuwa ni vizuri sana. Kwasababu hizo zina faida sana kuliko Chegani za wavulana.
Basi itakuwa ni jambo zuri sana. Kwasababu kwa huyu mwanadada bana mimi nimeamua kupotezea tu na kuona kwamba ni kama mapito tu.
“Ndiyo maana yake”.
Kwahiyo kwa namna ninavyojionea ni bora tu nianze kuanzisha vimiradi vyangu vidogo vidogo tu kama hivi.
“Ni vyema sana. Kwasababu kumbuka Nuru wewe tayari leo unaposema unasherehekea sherehe yako ya kuzaliwa ni kwamba unasherekea kuzeeka. Sijui kama umenielewa hapo?
Nimekuelewa kabisa.
“Kwahiyo nitakuwa nakuona wa maana sana kama kweli utakuwa unajiongeza hivyo. Kwasababu yule mtoto tayari keshokutwa tu hapa anaweza kuingizwa mjini na wajanja wa mjini ukashangaa hela zote hizo zinapuputika. Yaani kuna watu hawatakagi kuchezea nafasi. Yaani kwanza wewe una roho ya huruma sana. Kwasababu ingekuwa ni mwingine hapa angeshasepa na kila kitu. Yaani mwanamke anaenda huko karibia mwaka mzima na wewe unamlindia tu mali yake weeee kuna watu wana akili mbaya sana wewe.
Haya banadaaaaa sidhani kama zinawezakupuputika kirahisi hivyo.
Ahaaaaa. Nuru unasema nini wewe. Ohooooo nikuambie sasa wahuni walivyosema kwamba pesa makaratasi basi subiri iko siku utanipa majibu yake. Ukistaajibu ya Musa utashangaa ya Firaghuni. Ukumbuke siku za mwizi ni arobaini ndipo utakapokuja kuniambia kwamba bwana Kambi eee maneno yako yametimia. Kambi aliongea huku akiwa anaambatanisha na vitendo kwa mikono. Daaaaa haya bana. Nuru alikubaliana na hoja ya Kambi.
“Unajua Nuru kwa mwanadamu kutajirika inaweza kuchukua muda mrefu sana hadi aje kuitwa bilionea. Unawaona hawa kina Biligeti sijui nani huko wote hawa hawakulala na kuinuka tayari wakiwa matajiri. Walisota sana katika chanzo cha kutajirika kwao. Ila sasa kufilisika ni kitu kidogo sana yaani cha dakika tu ambacho kufumba na kufumbua hutoamini kutokea kwake chanzo chake hujulikana ni baada ya tukio hilo kutokea. Kama ukirudi katika masuala ya kitaaluma huko kwenye somo la historia hivi ninakumbuka kuna mada inaitwa anguko kubwa la kiuchumi kwa kimombo wanasema The Great Economic Depression ambalo lilianza kutokea huko Marekani na kuanza kusambaa maeneo mbalimbali ambalo lilianza mnamo tarehe 29.10.1929 hadi kuja kufikia mwaka 1933. Dunia ilishangaa sana kwa hali ile iliyojitokeza. Marekani iliyumba sana kwa kipindi hicho ndipo akaja Franklini Delano RouseVolt kuanzia 1933 na sera zake zile. Ni baada ya kuanguka kwa soko la hisa lililokuweko mtaa uliokuwa ukiitwa Wall Street kwa kimombo. Watu hawakutajaria kama janga lile lingewezatokea kabisa. Kambi alimuelezea mithili ya mwalimu akiwa anamfundisha mwanafunzi. Nuru alicheka kisha akasema. Daaaaa kumbe bado uko vizuri kwenye mambo ya historia. Ahaaaaa niko vizuri. Huo ni kama mfano tu ambao kweli utakupa majibu sahihi ya kusema kwamba kufilisika ni jambo la namna gani. “Sawasawa Kambi nimekuelewa sana. Walipoamaliza maongezi yao basi Kambi aliweza kumsindikiza Nuru kisha Kambi akawa amerudi katika himaya yake.


Ikiwa ni siku nyingine mishale ya saa mbili usiku ambapo Nuru alikuwa tayari amesharudi kutoka kazini. Muda huo Nuru alikuwa yuko chumbani kwake. Chumbani hapo akiwa anaonekana yuko anaandika kitu fulani kwenye Diary yake ambaye aliinunua siku chache hivi kwaajili ya kuweza kuweka kumbuka za matukio yake yaliyomtokea katika maisha yake. Matukio hayo yakiwa ni mazuri au mabaya. Stori ile aliiandika kama ifuatavyo.
“Nakumbuka kabisa ilikuwa ni asubuhi na mapema sana kipindi tukiwa kidato cha kwanza. Ilikuwa ni mwezi wa sita tulipokuwa tukigawiwa mitihani yetu ya middle term. Mwalimu Namkumbuka kabisa aliyekuwa akifundisha fizikia mwalimu Biyuni. Alikuwa akigawa mitihani akiwa ameanzia na mtihani wa mtu aliyepata namba kubwa na kushuka hadi namba iliyokuwa ya mwisho kabisa. Jina la mwanafunzi aliyepata alama ya juu sana lilitajwa ambalo jina hilo kwa pale darasani kwetu hapakuwa na mtu mwingine aliyekuwa akiitwa jina hilo. Mtu huyo ni Nuru. Niliinuka na kwenda kuchukua mtihani wangu wa somo la fizikia huku mwalimu Biyuni akiwa ananipa maneno ya kunipongeza huku akifurahi. Nuru umepata tisini. Ulitakiwa upate zote kabisa ila ni kwa vile tu usijeukaonekana kama ulikuwa na mwalimu nilipokuwa nikitunga mtihani. Wewe ndiye uliyeshika nafasi ya kwanza kati ya wanafunzi wa darasa hili. Nazidi kukupa hongera sana Nuru. Natumai miaka ijayo hivi tutakuwa na mainjinia wakubwa sana katika Taifa letu la Tanzania. Moja wapo ni wewe hapa. Nilifurahi sana kwa maneno yale ambayo mwalimu Biyuni aliyoniambia. Nilichukua mtihani wangu na kurudi kukaa kwenye kiti. Mwalimu Biyuni aliendelea kugawa mitihani ile na hadi kufikia jina mwisho ambalo kwa masikio yangu mawili yaliyo mazima yalisikia jina likiitwa Nura Kerima Isambe. Mwalimu hakusita kusema kuwa huyu ndiyo mtu wa mwisho na amepata kumi ya mia moja. Kusikia vile kwakweli kwangu kuna kitu kilinijia hapa moyoni na kuhisi kama moyo wangu unaungua hivi. Nilitamani sana kutoa machozi lakini nikawa nimekaza moyo tu. Nilijiuliza ni kwanini mtoto mzuri hivi anafeli mtihani?. Majibu sikupata kabisa juu ya swali langu nililojiuliza. Ilipofika wakati wa mapumziko ulinifuata na kuanza kuniomba jambo. Maneno yako nayakumbuka kabisa na mandhari ya sehemu hiyo nayakumbuka kabisa ambayo yalikuwa ni mandhari ya uwanjani. Nakumbuka kabisa ni wewe ndiye uliyenifuata nilipokuwa nimepumzika hapo uwanjani. Kwa mimi kwa siku ile kwa wakati wa mapumziko sikuweza kula chochote kwa sababu ya hali yangu tu kiuchumi haikuwa vizuri. Basi ndipo nakumbuka mrembo ulinijia hadi hapo na kukaa pembeni yangu huku ukiwa umeniletea Biskuti iliyokuwa kubwa na hata sikuimaliza kuila kabisa na sikuwahi kununua kabisa biskuti kama hiyo. Wote tulikuwa tumevaa mashati meupe ya tomato na sweta la bluu huku kila mtu tai yake ikiwa inaonekana kidogo tu. Kwa suruali yangu ilikuwa ni nyeusi kama sketi yako. Maneno yako nayakumbuka ambapo uliongea kwa sauti ya mtelezo iliyonifanya kuyeyuka mwili wangu na kujikuta naanza kutega masikio vizuri kama vile antena za jongoo. Ninakumbuka kabisa ulinieleza mkanda mzima kuhusu maendeleo yako kitaaluma. Nilikujibu huku nikiwa nimekuangalia kwenye paji lako la uso huku nikishusha kwenye macho yako yakiwa kama yanatoa machozi. Ikabidi nikujibu kwa uzuri kabisa nikisema. Nura usilie. Nitakusaidia kwa namna yoyote hadi uwe unafaulu vizuri kama mimi. Ninatamani sana na wewe uje ufikie hatua hii. Nura nilikufuta machozi na kitambaa chako kilichokuwa cheupe pee sura. Bubujiko la machozi yale lilikuwa kama bahari ya Hindi. Ndipo ikazidi kuniuma sana na kuchukua kitambaa chako na kuanza kukufuta machozi. Natumai moyoni ulifarijika sana kwa kitendo nilichokufanyia. Ulishukuru sana kwa kwa maneno yangu matamu ambayo yalikuangia moyoni mwako na kujipa faraja kubwa zaidi na kuona kuwa tayari kila kitu kimeshafanikiwa kwako. Ulinijibu kwa sauti iliyokuwa imeambatano na mshituko wa mlio fulani hivi ukisema.
“Nuru nashukuru sana kwa kukubali ombi langu la kuwa pamoja katika masomo. Itakuwa ni njia kubwa sana ya kuweza kunisaidia mimi katika janga hili la kupata alama mbaya kama hii. Nakushukuru sana roho inaniuma sana pindi wewe unapopata tisini na mimi napata alama ndogo vileee wakati tuko darasa moja umri sawa tofauti jinsia tu. Nuru sina budi kukung'ang'ania wewe kwa ajili ya kuweza kunielekeza kwenye haya masomo na mimi niwe napata alama kama ya leo uliyoipata. Mrembo wangu nakumbuka kabisa maneno niliyokupa baada ya kukujibu vile ndiyo nahisi kama yalikaribisha hisia zako za upande wa pili kwangu. Nilijikuta nimekujibu kwa huruma sana nikisema.
“Nura usikate tamaa katika haya mambo ya kitaaluma. Kama kweli unasoma utafaulu labda tu kama hujui style za kusoma. Nura hata mimi hapa roho yaniuma sana pindi msichana mrembo kama wewe ambaye nyumbani kwenu mmejaaliwa kila kitu kama ni hela zipo, maduka yapo, sijui nyumba nzuri zipo lakini cha kushangaza bado mtu huyu anashindwa na mtoto ambaye kwao hawana hata nyenzo za kuweza kumfanya mwanao kuweza kusoma kwa raha. Nyumbani kwenu kuna mfanyakazi kabisa ambapo wewe uamkapo tu unaenda bafuni na kupata maji ya moto. Lakini kwa mimi mtoto wa kitanda cha teremka tukaze muda huo wewe unaoga na maji ya moto mimi nipo huko kwa majirani nikiwa ninahangaika kuyasaka maji ya foleni tukiwa tumeipanga mithili ya watu tunaoenda kupatiwa rudhuku. Nura si kama nakupondea hapana bali nakuonesha tu ni namna gani una faida kubwa na uwezekano mkubwa wa kufaulu. Mrembo wangu nakumbuka kabisa ulinijibu kabisa huku machozi ukiwa unayatoa. Basi matumaini yangu ya kusema kwamba nimepata rafiki yangu ambaye tutakuwa tunasoma naye vizuri tena ni mtoto ambaye amezaliwa katika familia ya kitajiri sana basi mambo mengi atanisaidia sana.
“Nakumbuka tayari kipindi hicho Nura tukiwa kidato cha pili mapema sana ikiwa ni mwezi wa pili tarehe ya kumi na tano. Siku hiyo ndipo ulipoamua kuvunja ukimya kabisa kwamba mimi na wewe si kwamba ni marafiki tu bali pia tuanze kuitana wapenzi. Hisia zako wewe mrembo ambazo ulikaa nazo moyoni mwako kwa muda wa miezi nane kabisa na kutokujaribu kuniambia lolote zaidi na kubaki kusema tu kwamba utakuwa rafiki yangu hadi tumalize kusoma na tutaendelea pia kuwa marafiki milele daima. Siku hiyo nakumbuka kabisaa uliamua kunikaribisha nyumbani kwenu kwa mazungumzo maalumu na kwa siku hiyo marehemu mzee Kerima na marehemu Bibiye Hadhila hawakuwepo. Ni mara yangu ya kwanza kuingia katika jumba kubwa ambalo kwa namna tu nilivyoliona nilifananisha kabisa na mandhari ya peponi. Harufu iliyokuwa nzuri ya kuvutia ilikuwemo ndani mule. Neno kubwa uliloniambia kwa siku hiyo ambalo kwakweli sitolisahau milele daima. Neno hilo moja ulilokuwa umeniambia kwa muda huo lilifanya kuzaliwa kwa maneno mengine kemukemu. Ulikuwa umekaa kwenye sofa hapo yaani karibu na mimi. Kwanza siku hiyo nikashangaa hadi uvaaji wa mrembo wangu ambaye ni Nura ulikuwa tofauti. Neno hilo uliniambia kupitia sikio langu la kulia huku likiwa limeingia katika ngome ya sikio langu kuja nje shikio langu likiwa linaweka ulinzi wa kwamba neno hilo lisijelikatoka. Uliniambia. Nakupenda.  Kwa sekunde chache baada kuniambia hivyo ukimya ulitawala pale kila mtu akiwa anaangalia chini kama akiwa anasali. Kisha ukarudia kusema kwa ufasaha ukisema. Nuru nakupenda sana. Nilitaamaki tu tayari unaniwekea mikono yako juu ya kifua changu ila kwa mimi sikuwa najua nini haswa kifuatacho katika Jumba lile la kifahari la marahemu Mzee Kerima. Hadi muda huo sikuweza kukujibu lolote bali mdomo wangu ulibaki kuwa mzito kama vile umejaa maji na kuyatema nashindwa. Lakini mrembo wangu hapo ndipo ulipozidi kukomelea msumari wa nchi kama saba kabisa ukiwa unasema.
“Nuru ni muda mrefu sana nimevumilia sijawahi kukuambia yaliyoko moyoni mwangu ila leo ndiyo nimeamua kumwaga mboga kwenye bakuli kubwa na wewe uweze kufaidika na mboga hii kutoka kwangu. Nakuomba pokea ombi langu kwa mikono yako miwili na moyo ukiwa unaiongoza mikono hiyo. Ni juhudi nyingi sana nimezifanya ili kuweza kufikisha ombi langu kwako. Najua kabisa haukuwa na hisia yoyote ya kimapenzi na mimi bali ulikuwa na hisia za kusema kwamba huyu ni mwanafunzi mwenzangu tu basi tuishi kama wanafunzi tu. Hapana. Kwasasa tutakuwa katika sehemu mbili. Nuru nimeongea sana yaani hadi kama vile ulimi unataka kuishiwa na girisi nasubiri ombi langu kwako kukubaliwa ukiwa kama wewe ndiyo kama mahakama ya juu kabisa. Nakuomba Nuru. Kwakweli sikuwa na namna yoyote ile kwa mrembo Nura ilibidi tu nimkubalie japokuwa sikuwa najua nini kilichopo nyuma ya pazia. Sauti niliyoitoa kwa kweli hata awe mtu na vipimo vya kusikia sauti kwa kweli asingesikia. Nilisema hivi. Nura Nakupenda pia. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Nura kusikia sauti yangu kutoka kwenye kinywa changu ikipitia mdomoni mwangu huku akiwa anaangalia mdomo wangu ulivyo na macho yake yalikuwa ni kama ya paka yaliyokuwa na kimduara chekundu hapo kati.
Lakini baada ya dakika moja tu tayari nilikuona tu Nura ukiwa unashika shati langu na kunivuta huku ukiwa tayari unajirusha kwenye sofa lile la kifahari huku tayari kifua chako umeshakifunua nje nje. Kwakweli nilichokuwa nimekiona pale ni kitu ambacho huwa nilikuwa nikikiona kikiwa kimefichwa tu na nguo ila kwa pale kwa mrembo wangu Nura niliona moja kwa moja hadi nikafumba macho kama sekunde chache hivi ndipo nikafungua macho. Kwasababu ilikuwa ndiyo kama mara yangu ya kwanza kuweza kutaka kufanya jambo hilo. Kwa muda huo tayari na Nura nakuona macho yako yamelegea hadi nikawa naogopa nikijua kwamba umezimia. Ilibidi nikuulize swali la kizushi japokuwa lilikuwa lina faida kubwa sana kwangu na kwako mrembo wangu ambapo kwa mda huu nahisi uko kifuani kwa mtu mwingine ulaaaniwe wewe.
Nura kwani hapa kwenu si kuna kamera?
Nimestopisha.
“Lakini kule getini si kuna mlinzi?
“Hana shida”.
Baba na mama wakitukuta?
Hawaji sasa hivi
Nilizidi kushangaa sana kwa muda ule pindi Nura ukawa unaona ni maswali mengi nakuuliza kwahiyo ndipo ukaamua kuzitoa mwenyewe nguo zako ambazo zilikuwa ni chache tu mwilini mwako tayari na mimi Ali kichwa wazi akawa ameondoa uoga kabisa na huku akiwa ana hamu kweli ya kutema mate meupe tena mazito mengine. Nilipoangalia shimo la nyoka lilivyorembwa hapo nje hamna majani yoyote bali ni kazi tu kwangu kutelezesha Ali kichwa wazi. Ni mara ya kwanza kwangu tangu kubalehe bali nilichokutana nacho ni kitu cha utu ukubwa. Nilipokuwa nateleza alikuwa akitoa sauti mithili filimbi aina ya nai. Basi kuanzia hapo tayari mimi na Nura tukawa tunaishi kwa kila mtu na hisia za mwenzake. Sikuwahi kufikiria kama kweli Nura atakuwa mpenzi wangu bali kwa namna tu siku hiyo ilivyokuwa katika sofa lile ilibidi tu nikubaliane na matokeo tu ya kusema kwamba Nura ni mpenzi wangu. Basi mrembo wangu sijui huko uliko ukoje. Najua kuanzia siku hiyo ndipo uliponionjesha ladha ya asali. Kwahiyo sikuwa na haja yoyote ya mimi kuweza kwenda kulowea kwa warina asali wengine.
Basi ikawa ni tabia tumejijengea kabisa kwamba mimi na wewe kila siku ya jumapili ni mwendo wa kupeana utamu tu huo utamu wa asali amabayo ni asilia. Kuanzia hapo ndipo nilipozidisha ukaribu kwako. Mashuleni wanafunzi wa darasa letu karibia wote tu walijua tuko katika uhusiano wa kimapenzi na hata baadhi ya walimu walikuwa wakijua kabisa mahusiano yetu ya kimapenzi. Nilikuwa nikifurahi sana pindi ulipokuwa ukiniambia ukweli kwamba kuna mwalimu pia naye anakutongoza ila ukamkatalia ukijua kabisa kuwa yule siyo NECTA kama ilivyo maisha ya chuo ninavyoyasikia kwa watu. Hapo niliamini kweli Nura unanipenda kutoka moyoni kabisa. Nakumbuka siku hiyo tukiwa mapumziko tulikuwa tukinywa chai na mihogo ya mama Fatuma ambaye alikuwa ni mkarangishi mzuri sana kwa pale shuleni kwetu. Tulikuwa tukipenda sana kukaa maeneo ya uwanjani. Nilipofurahi zaidi ni pale ulipomkataa mwalimu Futo kwa kuwa alikutongoza na kukuahidi kuwa akitunga mtihani atakuwa anakwambia lakini bado ukakataa. Majibu niliyokupa ni majibu yaliyokuwa mazuri sana na yakawa ni furaha kubwa sana kwako. “Nura mpenzi wangu  Nakuomba usidanganyike hata kidogo. Mimi nitafanya jitihada zote hadi tufaulu wote. Kwanza mimi kwasasa nimeshaanza kuona mabadiliko makubwa sana kwako. Siyo kama kipindi kile mtu ulikuwa ukipata namba za kiatu wakati kwasasa unapata sitini na kuendelea kabisa. Majibu ulonipa kwa kweli moyoni nilifurahi sana. Maneno yale yalipita masikioni mwangu huku yakiwa yanaenda pole pole kama mwendo wa kobe au konokono ili yaache alama yapitapo. Nura nakumbuka uliniambia Sawa mpenzi wangu sitokutenda, sitokuliza, sitokuumiza, sitokunyanyasa, sitokuwazisha, sitokushangaza macho yako na sitokufanya kichwa chako kikuume kwaajili ya kuongea maneno ya hasira kwangu badala ya kuumiza kichwa kwaajili ya masomo. Nakupenda sana Nuru. Nitakuwa wako milele daima. Nitasimama nawe na tujenge familia kubwa na kuwa ndefu kabisa kama mnara wa Baberi uliozungumziwa ndani ya bibilia takatifu ya agano jipya.
Kwakweli Nura kwa maneno hayo yaani hadi Nura anatolea mfano wa kwenye Bibilia japokuwa ni muislam ndipo nikasema kwamba kweli hapa nimepata mpenzi mwenye mapenzi kumbe nimepata mpenzi mwenye mapezi. Kwa hapo ndipo huwa ninajikuta ninafikiria sana na hadi ninasema kwamba hivi mapenzi yangu na Nura mbona yalikuwa ni kama ndoto tu. Yaani nimeamka tayari na ndoto ile imeshapotea. Ooo Mrembo wangu huko uliko nilikupenda sana. Maneno yako hayo ndiyo yalinifanya mimi kuzidi kuwa mjinga katika himaya ya mapenzi kwangu na wewe nilikupenda sana Nura. Usione hadi muda huu nimekesha hapa Dayari hii ni hata pia nikifa leo ndugu zangu na marafiki zangu wapate kujua ni namna gani maisha yangu yalikuwa kabla ya kifo changu. Ila nitazidi kukutumikia hadi nitajirikie hapa hapa wewe mwanakulaaniwa mkubwa.


Kwakweli mambo ambayo aliyaandika katika dayari ile yalikuwa ni mengi sana karibia kujaa dayari nzima. Historia hiyo ilikuwa ni kwazia walipojuana na Nura tu hadi kuanza kuzozona. Ilichukua masaa mengi sana hadi kuja kumaliza ndipo alipopitiwa na usingizi hapo hapo na kujikuta malaika wa usingizi kamwijia na kumchukua polepole kitandani akajirusha. Huku kalamu ni kijitabu kile akiwa amevishikilia na kulala kwa upande wa kulia.


Basi siku hiyo ikiwa ni mishale ya saa mbili usiku. Muda huo Nura na Kambi wanaonekana wanatoka kwenye benk ya DTB kutoa fedha. Aliyekuwa akitoa fedha alikuwa ni Kambi. Basi walinyooka maoja kwa moja hadi kwenye gari na kwenda kupanda gari aina NOAH VOX. Dereva aliyekuwa akiendesha alikuwa ni Kambi. Wakiwa wanaelekea maeneo ya Njiro ndani ya gari walikuwa na mazungumzo ya hapa na pale.
Unajua Kambi kwasasa ninaishi pale kwenye lile jumba la kifahari. Nuru aliongea huku akiwa na furaha.
“Kwa marehemu mzee kerima?.
Ndiyo maana yake Kambi
Ayaa kivipi?.
“Si yeye.”
Nani huyo?.
Nura
“Kwahiyo Nura ndiyo amekwambia uishi pale?.
Ndiyo mbona kama imepita miezi kwasasa”.
Ayaaa ndugu yangu ng'ang'ania hapo hapo ninakwambia hadi utajirikie.
Haina shida.
“Wewe shangaashangaa hapa uje.......uje ujionee mwewe kachukua mnofu wako alafu hakuna mwingine uliobaki na wewe hujaonja chochote kabisa. Muda huo wakiwa wamefika maeneo ya Clocktower wakiwa wamesimama kwanza ili kuruhusu magari mengine kupita. Baada ya muda ndipo wakawa wameondoka.
“Haina shida Kambi. Kwasasa niko makini kama vile hiki cha kutolea pesa kinaitwaje kwa kiswahili vile?
ATM siyo?
Kwa kiswahili sasa.
Ahaaaaa kinaitwa Kiomotela.Haswahaswa ndiyo ninatoka niwe kama vile kiomotela ambacho hakizidishi wala hakipunguzi helaHaya bana kweli kwasasa umeshajitambua. Ndiyo maana yake
Yaani ndiyo maana mimi pale nilipokuwa nikiishi kwa mjomba wangu nilikuwa ninaishi kwa taimingi kweli kweli. Kutokana na zile issue zake za madini nikasema huyu mzee hata mimi nitakuja kuwajua vizuri hawa matajiri. Kwasababu duuu alikuwa anajuana nao na kama ni hela alikuwa anaishika yule ile kinyama. Yaani ukikaa naye pale nyumbani inaingia simu hii ikikata hii inaingia tena nyingine na hata akiwa anaongea simu utashangaa simu nyingine imeingia. Kwahiyo ishi kwa akili. Hapo sawa. Basi Kambi aliweza kumpeleka Nuru hadi nyumbani kwa mzee Kerima kisha Kambi akawa amepitiliza zake hadi nyumbani kwake.
Ni siku iliyofuatia Nura alimpigia simu Nuru ili aweze kupata taarifa vizuri kuhusiana na biashara zake za maduka ya Arusha. Muda huo Nuru alikuwa maeneo ya dukani hapo makao mapya. Ilikuwa ni mishale ya saa nne asubuhi pia ndiyo muda huo Nuru alikuwa akipata kifungua kinywa pale pale dukani. Muda huo wanaonekana wateja wakiwa wanaangalia angalia nguo ili waweze kupata wazipendazo na kuzinunua. Nura alimuuliza Nuru kuhusu maendeleo ya duka lake na maeneo mengine anayosimamia Nuru. Pia alimuulizia kuhusu kule nyumbani na Nuru akamuambia kuwa pako shari kabisa. Jambo la kushangaza ni kwama Nura alimwambia Nuru kuwa atakuja siku chache mbeleni akiwa na rafikiye.


SURA YA TANO
   Ni baada ya wiki moja hivi kupita tayari The Boss Lady ambaye ni huyo Nura alikuwa ameshawasili katika jumba lake la kifahari ambalo ameachiwa na wazazi wake kama urithi. Muda huo ikiwa ni mishale ya saa moja jioni ambapo Nuru alikuwa ameshawasili kutoka kazini. Hapo sebuleni wamekaa Nuru, Nura na pamoja na mgeni aliyekuja na Nura. Mgeni anaonekana ni dume lenye miraba minne kwa tisheti aliyoivaa kwa haraka inavyoonekana utasema kwamba inataka kuchanika kwa namna alivyo na unene wa mazoezi. Nura akiwa amevaa kama vile mwanadada wa kihindi huku na Nuru naye kama kawaida yake kavaa suruali nyeusi na tisheti nyekundu. Maongezi yao yalikuwa hivi.
Aaaaaa....  ninatumai Nuru kwa huyu unayemuona hapa hujawahi kufanya naye mazungumzo sana. Akiwa ananyoosha Mkono kwa mgeni ambapo alikuwa amekaa pembeni yake.
 “Ndiyo. Muda huo akiwa amejiegesha kwenye kochi lake.
“Okay  huyu ndiyo yule mgeni ambaye nilikwambia mapema kwamba nitakuja naye.
“Ahaa kwani anaitwa nani?.
“Aaaaa......nahisi ni vizuri akajitambulisha mwenyewe
Mgeni akasema. “Aaaaaa... naitwa Mpundu. Lafudhi yake ni ya kiarusha.
Ahaaaaakaribu sana Arusha jisikie huru kabisa kwamba hautapata bughuza yoyote ile”.
Aaaa Shukurani sana. Pia kwa maelezo mengine mimi nikimuangalia Nura ni kama mpenzi wangu”. Nuru kuna kitu Kwakweli kilimchoma sana moyoni mwake ila hakukionesha katika uso wake na wala hakukiongelea kwa maneno yoyote yale bali. Hongera kubwa Sana”.
“Aaaaa....Kwa ujumla huyu ndiye mume wangu. Nura alidakia maongezi kisha Nuru akasema. Kumbe na arusi mmeshafanya kabisa?
Bado ndiyo tuko mbioni. Nura alimjibu kwa ulaini.
Sawa nimeelewa kwa hapo na ndiyo maana nimempa hongera kubwa Sana”.
Maneno ya Mpundu kwa Nuru yalikuwa ni kama mwimba uliochoma kwenye roho yake ilikuwa laini kama sauti ya mtoto aliyezliwa muda huu. Ndipo alipoamini kuwa maji ya moto yamekuwa baridi.
Ikiwa imewadia mishale ya saa tatu usiku hivi muda huo Mpundu alikuwa ameingia bafuni ili aweze kuoga na apunguze uchovu wa safari ya kutoka Dar es salaam hadi Arusha japokuwa walikuja na ndege ila safari ni safari tu. Lakini kwa muda huo pia Nuru na Nura walikuwa wamekaa hapo sebuleni wakiendelea na maongezi sasa wao kama wao. Muda huo Nuru akiwa amesogea karibu na sehemu aliyokaa Nura. Basi Nuru akawa anaongea muda huo kwa malalamiko akimlalamikia Nura.
“Hivi Nura kweli mawazo yako ulishawahi kuyajaribu kuyarudisha nyuma na kucheki ni namna gani mapenzi yetu yalivyokuwa kwa kipindi hicho?. Yaani tulipendana kama jicho la kulia na kushoto. Jicho la kulia likilia na la kushoto linalia, jicho la kushoto likiblink nalo linablink. Lakini kwasasa imekuwa sijui nitolee mfano gani tu.
Alicheka kwa dharau kama sekunde chache hivi kisha akasema. Sidhani kama ni vyema kurudia kuosha uso na maji ambayo umeshapigia mswaki. Yaani inabidi yale uyamwage na utafute mengine. Nura aliongea kimadaha.
“Nura Nura Nura sauti yake akiwa anaibana ili Mpundu asisikie.
Yes it's ma name ex
Yaani mimi kabisa leo hii ninateseka kwaajili ya mapenzi kwako kabisa. Wakati wewe ndiye uliyenitongoza!... amakweli dunia shujaa ulimwengu adaa. Aliongea huku akionesha ana hasira sana.
Hhahhaha... aliyepiga kengele anaweza kuchelewa msitarini.
“Nura ni maneno gani kabisa haya unaniambia. I was your darling yaani kwasasa eti ninakuita Shemeji na Boss juudoest makes sense?
Yeah  it makes sensendivyo ilivyo. Hali ya mtu humponza awe katika hali fulani. Natumai umenielewa.
Nura
Nuru kama wewe ulivyoniita. Ndivyo maskini walivyo…Yaani hata wapigwe fimbo mia watabaki kusema tu asante sana. Masikini wanajifanya wanajua kupenda kumbe ni umasikini tu ndiyo unawafanya wasioneshe makucha yao. Wewe embu peleka umasikini wako kule. Nimekunja na mume wangu kwahiyo sitaki makelele mengi. Fanya kazi uokoe familia yako. Unaanza kulia mapenzi mapenzi ambaye haijulikani hata nani aliyatengeneza hayo mapenzi.
“Sawa…ila afadhali masikini waliojaaliwa sauti ya kusema shukurani na uvumilivu kwamba wakijua iko siku gwaride litasema yake na litaonekana ni la ukweli. Nuru aliongea maneno yale kwa hisia kisha Nura akasema. Kwani wewe Nuru kama ni mshahara si nakupatia au na huko nakutesa pia?
Hapana. Nuru alijibu.
“Ahaaaa basi nakushangaa sana utafikiri mwanamke ni mmoja kwa namna unavyonung'unika.
“Haina shida kwasababu siku zote mchawi hajui kwamba na yeye atakuja kupatwa na usingizi tu kwa namna anavyowasumbua watu katika majumba yao wakiwa wamelala. Nuru Nakumbuka kabisa wewe ndiye ambaye kwa kipindi kile ulinifuata na kuniambia mambo ya uhusiano mimi na wewe mwisho wa siku ndiyo hivyo. Amakweli nimeamini si kila akuambiae nakupenda si kweli anakupenda mwingine anataka kutimiza tu malengo yake.
Waliendelea kuzungumza hadi Mpundu alipotoka bafuni na Nura ikawa ni zamu yake kwenda kuoga. Kwahiyo akawa amemuacha Nuru akiwa peke yake pale sebuleni. Lakini baada ya dakika chache tu Mpundu naye akawa amekuja pale sebuleni na Kuanza kuzungumza na Nuru. Sasa Mpundu naye ikabidi amdodose vizuri huyo Nuru kuhusiana na Nura. Mazungumzo yao yalikuwa hivi. Unajua Mpundu nikwambie tu ukweli cha kwanza kabisaa sisi ni wanaume. Kwahiyo ni vyema tu kuwekana sawa mapema kabisa katika baadhi ya mambo. Ni Kweli. Kambi alijibu.
“Aaaaaa huyu Mwanadada huyu alikuwa ni mpenzi wangu. Yaani hadi anaondoka Arusha hii mimi najua ni mpenzi wangu. Lakini ndiyo hivyo mabadiliko yalikuja kutokea baada ya wazazi wake kufariki na kisha Nura akawa ameachiwa mali zote za wazazi wake. Kwasababu Yeye ndiye mtoto wa kipekee katika familia yao. Nakumbuka ulikuwepo kipindi kile.
Ndiyo ana bahati sana.
“Yaaani kubwa sana. Baada ya kupewa mali zote zile akawa tayari tabia ameshaanza kunibadilishia. Baadaye kuna rafiki yangu anakuja kuniambia ukweli kwamba mademu kama hawa wana tabia ya kununua wanaume. Nuru aliyatoa yote ya moyoni kisha Mpundu akasema. Ni vyema sana na nakushukuru sana Nuru kwa kunipa dondoo hii na wewe ukiwa ni kama mtu wa pili kuniambia hivi. Pia jambo hilo nilikuwa nimeshaanza kulifanyia mchakato na namna ulivyoniambia wewe ndiyo umezidi kuniweka katika njia ya mimi kulifanya jambo hili kwa haraka sana iwezekanavyo. Basi kila mtu aliweza kueleza yake huyu kanena hili na lile hadi Nura alipotoka bafuni. Hawakuchelewa sana pale sebuleni bali walielekea kulala.


Basi ikiwa ni siku iliyofuatia mishale ya saa tatu asubuhi ambapo muda huo Nura alikuwa ametoka ili kwenda kuangalia maduka yake yaliyoko huko mjini. Pia na huyo Nuru naye alielekea huko huko kazini. Kwahiyo nyumbani akawa amebaki Mpundu tu. Mpundu alikataa kwenda huko kwa kisingizio kwamba alikuwa bado ana uchovu wa msafara wa jana wa kutoka huko Dar es salaam hadi Arusha japokuwa walisafiri kwa ndege. Lakini kumbe naye kijana Mpundu ana marafiki zake wengi tu kwa pale katika jiji la Arusha wakiwa wanaishi katika mitaa tofautitofati. Basi Mpundu aliweza kuwaita rafiki zake ili waweze kujuliana hali vizuri na pia kufahamishana vizuri.
Kwa ujumla rafiki wale wa Mpundu walikuwa wanne. Wakionekana kabisa ni wadhoefu wa jiji la Arusha kushinda Mpundu japokuwa naye amezaliwa Arusha. Basi wakiwa wamekaa kwa kujipanga kwenye yale makochi na Mpundu alikuwa amekaa katikati yao kwa namna walivyokuwa wamekaa. Wawili upande wa kushoto wa Mpundu, ambapo wa kawanza alikuwa amevaa suruali nyeusi na shati aina ya dog dog  likiwa limemvaa na siyo kulivaa tena anaitwa Munaa, aliyekuwa anafuata alikuwa amevaa tisheti nyekundu na suruali nyeusi anaitwa Kibweni na wawili ambao walikuwa wamekaa upande wa kulia wa Mpundu wa kanza kutoka kulia anajiita Nyoka akiwa amevaa suruali nyekundu na tisheti ya bluu huku akiwa amevaa boshori jeusi, na aliyekuwa akifuatia alikuwa amevaa kama vile tu Kibweni ambaye anaitwa zaka. Basi Mpundu alikuwa ana mazungumzo nao kama ifuatavyo.
“Oyaa machali mnajua ni kitambo sana tangu niondoke Arusha. Hiyo kawaida tu, siunajua tena kwenye kuyasaka maisha lazima kambi popote kasoro kwenye kituo cha polisi tu. alijibu Kibweni. Wote walicheka kwa sekunde kama tano hivi. Kisha Mpundu akasema hivi.
“Hiyo kawaida tu. Eeee bwana mimi kitu nilichowaitia hapa bana mmh... mimi najua nyiye hapa mjini mshakuwa ni watoto wa mzinga mkali. Nyoka akawa amemjibu Mpundu kwakusema. Kama kawaida Nigga ndiyo njia mojawapo ya kuyasaka maisha kwa hapa mjini. wewe kama una issue lolote lile tuambie muda wowote kazi ifanyike”. Wala msihofu kwasababu kuna huyu demu niliyenaye nimepata stori zake kumbe ana mazoea ya kununua wanaume. Rafiki zake wote wakasema hivi. “Ayaaaaa wale wale.
Kwahiyo sasa mimi huyu demu kabla hajaenda kumnunua jamaa mwingine lazima nimchafulie ATM yake yote. Kwahiyo ndiyo maana nikawa nimewaita nyiye hapa. Kwasababu kuna stori pia kubwa sana nimepewa na huyo mfanyakazi wake ambaye alikuwa ni kama mpenzi wake kwa kweli hapo ndipo nimezidisha hasira na kuanza kutafuta njia kali sana ya kuweza kumshusha huyu demu. Mpundu aliongea kwa ujasiri mkubwa kisha Munaa akasema hivi. Hao sisi ndiyo tunawataka. Kwahiyo inakuwaje huo mchongo?. Aaaaa... kwa namna ninavyofikiri ni kwamba huyu kwanza nitaanza kumchukulia vihela vyake polepole bila yeye kujijua. Nitaanza na huko benki kwasababu hata nywila yake yaani password naijua vizuri sana. Sasa chakufanya hapa baada ya hapo hata chuo tayari tutakuwa tumeshamaliza. Kwahiyo hapa tutafute namna ya kuweza kuchukua kila kitu kilichopo hapa kwenye hili jumba na kuviweka kwenye gari na kwenda kuviuza. Tunaeda kuvipiga mnada kwa tajiri yeyote yule.
“Sasa wakati huo tunataka kufanya hivyo yeye atakuwa wapi? Kibweni aliuliza.
“Mimi nitatumia ujanja wa kumuacha huko huko Dar es salaam. Kwanza kuhusiana na hii nyumba mimi nitajua ni namna gani ya kuifanya hadi ije kupigwa mnada. Nikiamua hata maduka yake nitayafanyia kazi na maeneo yote anayomiliki. Hapa cha msingi tuandae matajiri wahuni tu.
Mnajua inabidi tujipange sana kuhusu hili jambo. Kwasababu tukumbukeni huyu demu mzee wake alikuwa anajulikana sana na watu wakubwa wakubwa hapa Arusha  na hata serikalini. Nyoka alitoa ushauri kisha Mpundu akawa amesema. Ayaaa hiyo tutaiendea kisomi zaidi brother. Mimi nakwambia tulia uone movie itakavyochezwa. Huyu mtoto pesa zinamsumbua tu. Afu ni mtoto mdogo kinyama  hawezi kusumbua watu akili kabisa. Ohooooo muda mwingine wasomi washenzi pia ayaaaa wewe jifanye hivyo alafu ndiyo hivyo ndege mjanja hudakwa kwenye tundu bovu tu. Inabidi tuwe makini sana. Kibweni alitoa ushauri kisha Mpundu akasema. Hapana Kibwenimimi nakwambia hapa hata akili ya ziada itatumika tu. Kwasababu hata mimi najua kabisa mtu tunataka kupambana naye ni mdogo bali ni mkubwa kwa kuwa anajuana na wakubwa kabisa. “Chamsingi ni umakini hatuangalii kwamba eti anajulikana na vigogo serikalini aya na sisi tunajulikana na nani mtaani?. Muna aliongea kwa kujiamini. Lakini mimi napenda nitoe tahadhari tu. Nyoka alitoa tahadhari. Kila mtu alitoa mawazo juu ya mpango wao wanaotaka kufanya. Mwisho wa siku walifikia maafikiano kuwa lazima wamfilisi Nura kwa namna yoyote ile.
Hiyo ni mipangilio ambaye Mpundu alikuwa akipanga na hao marafiki zake. Mpundu naye alijua naye ipo siku atakuja kufanywa kama Nuru ndipo akaona ni bora ajifunze kuogelewa mapema ili asijekufa kijerumani na tai shingoni. Ukiona mwezako ananyolewa zako tia maji japokuwa ni msemo uliopitwa na wakati.


Basi ikiwa ni mishale ya saa kumi jioni ambapo muda huo tayari Nura alikuwa ameshawasili kutoka huko kwenye kuangalia maduka yake. Alijonea hali halisi ya mali zake na akawa amesharejea. Muda aliokuwa amerejea alimkuta Mpundu akiwa pekee yake tu akiangalia movie ambapo hata wale rafiki zake walikuwa wameshaondoka. Basi kufika pale nyumbani pole za hapa na pale zilitoka kwa Mpundu. Mpundu akawa amemuahidi Nura kuwa siku inayofuatia wataenda wote kufanya mazunguko huko mjini. Mpundu alijaribu kumdodosa Nura kwa namna yake kuhusu uhusiano wake na Nuru nini chanzo kabisa cha kuachana. Majibu ambayo Nura alimpatia basi Mpundu alichanganya na mawazo yake tayari akawa ameshapata jibu kuwa hapa si mahali pa kuishi bali ni mahali pa kupita tu.
Katika matembezi ya huku na kule siku hiyo Kambi alikutana na Nura maeneo ya kwa BENSON. Muda huo ilikuwa ni mishale ya saa saba mchana jua likiwa limewaka sana. Ambapo muda huo kila mtu alikuwa amepaki gari lake na kutaka kuingia ndani kwaajili ya kwenda kufanya manunuzi ya vitu alivyokuwa amevitarajia. Kambi aliamua kumsimamisha Nura kabla hajaingia ndani. Kwasababu Kambi naye roho inamuuma sana namna anavyomfanyia Nuru. Kambi, Nura na Nuru kwa ujumla ni marafiki tangu kipindi hicho wakiwa sekondari. Kwahiyo ndiyo maana kujuana kwao si kama kwa kuambiwa bado kuna uchanga. Kujuana kwao kumekomaa sana. Nura alikuwa amevalia nguo kama mwingizaji mmoja hivi katika movie iitwayo Nikita. Nywele zake zilizoninginia hadi kiunoni zilikuwa zimejaa kama mkia wa farasi mweupe. Kambi alikuwa amevaa suruali ya jinsi na shati jeusi ambalo lilikuwa llimeandikwa WEUSI kwa mgongoni na kwa mbele ya shati yake palionekana picha za wana kundi la weusi wakiwemo Joah Makini na wengine.
Nura. Alimuita huku akiwa anaenda kumshika mkono.
Beee. Nura aligeuka na kutahamaki alikuwa ni Kambi rafiki yake sana.
Naomba tufanye mazungumzo kidogo kabla hujaingia. Kambi alimuomba.
Sawa.
Embu nakuomba tungeingia ndani ya gari kabisa ili tufanye maongezi vizuri. Sababu hapa nako jua limewaka sana.
Sawa. Waliingia moja kwa moja kwenye gari la Nura ambalo lilikuwa ni kampuni la BMW. Nura upande wa dereva na Kambi akawa amekaa pembeni. Nuranafurahi sana kukutana na wewe natumai tunaweza kufanya mazungumzo mazuri sana baina ya mimi na wewe.
Ni sawa pia nashukuru na wewe kuweza kuniita kwanza umenikumbuka vizuri sana... as I remember ulikuwa ni rafiki sana wa Nuru. Nura aliongea huku anaonesha tabasamu.
“Ndiyo ndiyo. Sasa hapo ndipo mada inatakiwa ianze.
Wapi?
Kwa Nuru
“Aaaaaaa.....kuna aaaa....kunaaa nini kuhusiana na Nuru tena? alikunja sura kidogo baada ya kutaja suala la Nuru.
“Aaaaaaa wala usihofu ni mazungumzo ya kawaida tu. Kwahiyo yasikutie presha tu
Sawa
“Unajua Nura japokuwa uyoga hutokea kwa kubahatisha tu yaani ni kwa kipindi hadi kipindi bali hata kipindi hicho ukija kutoka pia watu huukimbilia na kwenda kuuchuma. Hiyo basi inaonesha watu wanavyoupenda uyoga. Nahisi unaujua uyoga?.
“Ndiyo ndiyo. Ila kuna uhusiano gani kati ya mazungumzo yetu na uyoga?.
OK unajua Nura katika haya maisha kwa mwanamke kama wewe ambaye ndiyo  unakuwa lakini pesa imeshakuzoea mkononi mwako mapema sana yatakikana kuwa makini katika matumizi yako. Kwa umri wako yaani kushika hela sijui nisemeje. Tena afadhali hata kwa mwanamume na siyo mwanamke. Aliongea huku akiwa anaangalia kwenye kioo.
Kwanini waniambia hivyo?
“Safi sana wewe ni mwanafunzi mzuri sana.
Kwanini?
“Kwasababu unapenda kuuliza maswali na si kusikiliza maelekezo tu.
Haya bana
Kila mtu kwa muda ule kwa kweli alikuwa na yake ya kuongea. Nura aliongea hili na Kambi akaongea lile. Nura alianza kukatisha maongezi alipoona Kambi anaanza kuzungumzia kuhusu mapenzi yao yaani Nura na Nuru ambayo ni ya tangu zamani zama. Mapenzi kwa mwanzoni yalikuwa mazuri kama mapenzi yaliyokuwa katika movie mbalimbali za muimbaji wa Kihindi wa miaka hiyo. Maongezi yale yalichukua muda kidogo kutokana Kambi kuzidi kumuongelea Nura kwa mafumbo tu akizidi kumuachia maswali mengi ya kwenda kufikiria.  Baada ya kumaliza maongezi yao ndipo wakawa wameingia ndani kila mtu akiwa anaenda kununua chake alichokuwa amekipanga. Lakini hadi muda huo wanaingia ndani tayari kama kulishatokea msuguano kati ya Nura na Kambi. Kwasababu Kambi alikuwa akimzungumzia sana Nuru katika maongezi yao na wakati Nura hakuwa anapenda kabisa mazungumzo hayo.
Basi ikiwa imepita kama wiki moja hivi tayari ambapo Nura ameshaelekea Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kwenda Chuo. Lakini alimuacha Mpundu huko Arusha akiendelea kuishi katika jumba la kifahari la marehemu mzee Kerima ambalo kwasasa anayelimiki jumba hilo ni huyo Nura. Kumbe kubaki jijini Arusha alikuwa na madhumuni makubwa sana. Basi muda huo ikiwa ni mishale ya saa tatu asubuhi kwa jiji la Arusha baridi ikiwa kwenye kiwango cha kila siku. Mpundu anaonekana na rafiki yake katika ofisi ya taasisi moja hivi iliyo na tawi lake hapo Arusha. Ofisi hiyo inajishughulisha na utoaji wa mikopo. Mpundu yuko hapo akiwa amekaa kwenye viti vya wateja hapo kukiwa na foleni. Mpundu anaonekana amevaa kiafisa kabisa. Suti nyeusi chini akiwa amevaa kiatua cha bei kali sana.




























SURA YA SITA
Basi zamu ya Mpundu kuweza kuingia ofisini pale iliwadia baada ya mtu aliyekuwa akihudumiwa kutoka. Mpundu akiwa na bahasha yake ya kaki iliyokuwa ikionekana imesheheni makabrashi mengi sana aliingia moja kwa moja hadi ofisini hapo akiwa na rafiki yake. Rafiki yake Mpundu ambaye walikuwa naye pale anaitwa Jeshi. Basi waliingia hapo na kukaribishwa vizuri sana na muhudumu ambaye alikuwa hapo katika kitengo hicho cha kusikiliza watu wanaohitaji mikopo ya kibiashara. Basi mwanadada huyo aliwakaribisha Mpundu na Jeshi. Mpundu aliruhusiwa aketi kwenye kiti kilichokuwa kina mvuto wa hali ya juu sana. Naye Jeshi aliketi kwenye kiti kilichokuwa ni cha mneso kama mwendo wa twiga. Muhudumu aliyekuwa akiwakaribisha kwa kweli sura yake alikuwa amejaaliwa sana kwasababu kwa usoni tu na ule weupe alionekana kama vile sura ya mtoto wa malaika. Nywele zake alizokuwa amejaaliwa mithili ya malikia wa huko mbali na ule weupe wake ndiyo alionekana kabisa kama vile malaika wa warembo.
Alianza kufanya mazungumzo na Mpundu na Jeshi kuhusu taasisi hiyo ya kutoa mkopo. Alimuelezea faida za kuchuku mkopo katika taasisi ile kwasababu kwanza taasisi ile ilikuwa ikitoa mikopo kwa riba nafuu sana. Baada ya muhudumu kuwaelezea kwa ufupi ndipo sasa akawa amewaambia kuwa Mpundu aanze kuelezea madhumuni ya kuja pale. Mpundu alianza kwa kujitambulisha kuwa jina lake ni nani ambapo jina lake alijiita Mpundu Ahmed Omar na mwezake akawa amejitambulisha ambaye anaitwa Jeshi Mkwasi Msophe. Alikuja na Jeshi akiwa kama shahidi kwaajili ya mkopo ule. Mpundu alianza kuzungumza madhumuni makuu ya kumleta pale ambayo yalikuwa ni kwa ajili ya kuchukua mkopo katika taasisi ile. Basi kutokana na aina ya mkopo aliokuwa akiuhitaji kuna vigezo vyake vilikuwa vikihitajika kutokana na mkopo aliokuwa akiihitaji. Alitaja umri ambao amezaliwa huku muhudumu akiwa anaendelea kurekodi kwa makini zaidi katika kitabu cha taarifa maalumu. Pia kwa pembeni palikuwepo kifaa cha kunasa sauti ambacho ilikuwa ni vigumu kwa mtu kujua kama kifaa hicho ndicho kinahusika na jambo hilo. Muhudumu alikuwa makini sana katika kurekodi taarifa za Mpundu kwasababu kile ndicho kilikuwa kidhibiti chake kabisa. Muhudumu alipata nafasi ya kumuuliza maswali Mpundu na Mpundu akawa anajibu kwa ujasiri kabisa. Majibu ambayo Mpundu alikuwa akiyatoa alikuwa akijiigiza kama tajiri fulani ambaye ni mkubwa sana na anajulikana sana. Muhudumu alimuuliza kiasi cha fedha alichokuwa akihitaji na madhumuni ya fedha yale na pia kitu cha kuweka rehani kuhusu mkopo ule aliokuwa akiuchukua. Mpundu alimjibu yule dada kwa makini kiasi cha pesa alichokuwa akihitaji kutoka katika taasisi ile ili aweze kuanzisha jambo alilokuwa amelitaka kuanzisha. Basi akawa amesema kuwa anachukua mkopo ule kwaajili ya kwenda kuanzisha kilimo. Kilimo alichotarajia kwenda kuanzisha ilikuwa ni kilimo cha ufuta na ufugaji wa kuku wa kienyeji na kisasa. Alihitaji kufungua eneo kubwa sana kwa ajili ya kufuga kuku wa kienyeji na kisasa ambao kwake aliona ni faida kubwa sana. Pia aliuliza kwamba akishindwa kulipa mkopo ule ni nini kitamuokoa?. Kwa ujumla alichoweka rehani ni jumba la marehemu mzee Kerima. Ambapo alielezea vizuri kuhusu uhusiano wake na Nura. Ambapo kwa vithibitisho kabisa kumbe Mpundu aliweza kutengeneza hadi cheti feki cha ndoa na kuonekana kuwa Nura na Mpundu wameoana na hata baadhi ya mali za Nura zilianza kumilikiwa na Mpundu. Vyeti na hati alizokuwa nazo nyingi zilikuwa ni feki kabisa lakini kwa namna zilivyokuwa hakuna aliyeweza kutambua kabisa kama baadhi ya vitu ambavyo alikuwa anavyo vilikuwa ni feki. Aliweza kumuonesha muhudumu yule hati ya nyumba ya marehemu mzee Kerima na hati ile muhudumu akawa ameikubali na kupitisha kuwa ana uwezekano mkubwa wa kpata mkopo ambao anahitaji na zaidi ya hapo. Mpundu alipouliuzwa kuwa Nura ni mke wake kweli hakika Mpundu aliweza kujibu kwa ujasiri zaidi. Alipoulizwa kuwa yuko wapi aliweza kujibu kirahisi kuwa mke wake kwa muda huu yuko Uchina kwenye biashara zake huko. Kwahiyo imemuwia vigumu kuja hapo kwasababu tu yuko nje ya bara kabisa. Muhudumu alimuamini Mpundu kama malaika fulani ni kwa namna tu Mpundu alivyokuwa akiongea kwa ujasiri na ujasiri huo ukiwa umejaa ushwawishi wa hali ya juu. Pia muda wa kurudisha mkopo ule aliambia anatakiwa iwe ndani ya miezi sita awe tayari ameshakamilisha fedha zote ikijumuisha na riba ambayo alipatiwa ni riba ya asilimia thelathini. Mpundu alimjibu kiurahisi tu kwasababu yeye ndiyo alikuwa akijua kuwa huo mkopo anaenda kuufanyia nini.
Basi mazungumzo baina ya Mpundu na muhudumu yule yaliweza kwenda kwa kina sana na muhudumu yule akawa anampatia sana ushauri Mpundu kuhusu namna ya kwenda kuutumia mshahara mkubwa kama ule ili uweze kuleta faida kubwa zaidi. Lakini kwa hapo mengi aliyokuwa akimwambia Mpundu yaliingia sikio la kushoto na kutokea sikio la kulia bila hata moja kubakia katika kichwa chake. Baada ya kumaliza michakato yote pale ya kujaza fomu mbalimbali kama ilivyo tararibu za taasisi hizo. Alipiga passport na kuziacha pale zikiwa zinamtambulisha yeye. Pia Jeshi naye alipiga picha akiwa kama shahidi wake kwa ajili Mpundu apatiwe mkopo aliokuwa akiuhitaji. Ndipo hatua zote zilipokamilika Mpundu na Jeshi waliweza kuondoka huku Mpundu akitembea kwa kuiga kuwa yeye ni tajiri mkubwa sana katika mkoa wa Arusha na hata nje ya mkoa wa Arusha.
Basi ikiwa ni baada ya siku tatu hivi kupita muda huo ikiwa ni mishale ya saa mbili usiku. Walikuwa wakianagalia movie ambayo ilikuwa ikiendelea katika runinga hiyo.  Ambapo muda huo Mpundu na Nuru walikuwa wamekaa hapo sebuleni wakiwa wana mazungumzo ya hapa na pale. Mpundu alijaribu kumwambia ukweli wote na kila kitu alichokuwa amekipangilia kabisa kuhusu namna ya kumshusha Nura. Kwakweli Nuru alijiongelea kimoyomoyo akisema kuwa. Amakweli ukisikia farao asiyemjua Musa ndiyo huyu jamaa. Alimuelezea mipangilio yote kabisa. Mpundu alimuomba msamaha pia Nuru kwa baadhi ya makosa ambayo alimfanyia na mengine hakuwa anayajua chanzo chake kabisa. Kwa kuwa mafahari wawili wakikaa kwenye zizi moja lazima tu ugomvi unaweza kuzuka. Sasa ugomvi ule hauwezi ukasema iwe ndiyo chanzo cha wao kutokuongea moja kwa moja yaani hadi kufa. Hakuna ajuae leo wala kesho zaidi ya mungu tu. Yawezekana huyo uliyemnunia kesho ndiyo anakuwa msaada kwako kwa asilimia zote katika tatizo lako ambalo ulikuwa ukilihitaji litatuliwe kwa haraka. Kwahiyo ni vyema kuishi kwa amani na utulivu tu ndiyo suala la msamaha ni binadamu ndiyo wameumbiwa na si wanyama. Kwasababu wanyama hata kama wakipigana hapo muda huo huo tena utawaona wako tu hapo japokuwa hawajakaa kikao na kuombana msamaha. Kwahiyo ndiyo maana Mpundu aliona atakuwa hajafanya jambo la kheri sana kama hajamuomba msamaha Nuru kwa kuwa Nuru ndiyo kila kitu katika jumba lile. Kusimamia mali zote zile bila kudhorota si kitu cha utani. Ni jambo ambalo linahitajika umakini mkubwa sana. Wakiwa wanaendelea na mazungumzo pale simu ya Mpundu iliita na alipoangalia alikuta ni Nura ndiye alikuwa akimpigia. Alipokea kwa kujigamba kama mtu asiyekuwa ametenda lolote baya kwa Nura.
Mambo vipi Mume wang?
Fresh za huko?
Mimi niko poa kabisa.
Ok mume wangu unakuja lini huku? kwasababu time inaenda alafu still uko Arusha. Dont you Know kuwa nimekumiss sana mume wangu?
I know that my wife kesho niko safarini . So dont worry kesho mapema sana nitakuwa hapo Airport.
Sawa. Nitafurahi sana. Nura alipokata simu Mpundu na Nuru waliweza kuendelea na maongezi yao hadi pindi sasa ilipofikia ana usingizi ndipo walipoamua sasa kila mtu akaingie chumbani kwake na kulala.


Ni siku iliyofuatia mishale ya saa nne asubuhi tayari Mpundu alikuwa ameshawasili kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerer Terminal 2. Muda huo anaonekana akiwa katika sehemu ya wanaowasili huku akiwa na mabegi yake. Baada ya kujitokeza vyema Nura aliweza kumuona Mpundu. Nura alifurahi sana kumuona Mpundu ameshawasili pale akiwa salama japokuwa hajui huko alikotoka kama pako salama au laa. Muda huo hapo nje kuna watu wengi sana wakiwa wanawasubuiri ndugu zao ili wawapokee. Waliokuwa wamejaa sana pale walikuwa ni waarabu, wahindi na wazungu. Wabongo waliokuwa pale walikuwa ni wachache sana. Basi kwa muda huo Nura tayari akiwa na toroli cha kubebea mizigo aliweza kumsaidia Mpudu ni baada yaa kusalimiana kwa bashasha sana. Basi moja kwa moja wakawa wameelekea hadi alipokuwa amepaki gari. Gari alilokuwa ametembea nalo ni BMW ambayo Nura hupenda kutembea nayo sana akiwa anajitambulisha hakika yeye ni mtoto wa zimba japokuwa wazazi wake wote wamefariki ila yeye ndiyo yeye. Waliweka mizigo kwa umakini na tayari wakawa wanaanza kutafuta ni namna gani watatoka. Ambapo muda huo dereva alikuwa ni Nura. Basi Nura akiwa yuko makini katika uendeshaji wake tayari akawa ameshaingia vizuri kwenye barabara na kuanza safari ya kwenda kutokea pale. Ndipo alipnyooka kama anaenda kwenye ofisi za Swiss Pot ndipo akakuja kona na kuuanza mwendo. Alifika shemu ya kukagua gari alitokea askari mmoja aliyekuwa mweusi tii tii akiwa amevalia miwani iliyokuwa nyeusi kama Kiwi ya kangaroo. Baada ya askari yule kuridhika na ukaguzi wake ndipo gari likawa limeruhusiwa kupita. Moja kwa moja waliweza kutoka pale na kushika lami ya JET, vingunguti, TAZARA hadi walipoiona hiyo Mbezi ambako ndiko walipokuwa wakiishi huko.


Nura akiwa kama dereva alikuwa makini barabarani hadi kufika katika eneo walilokuwa wakiishi. Sehemu wanayoingia panaonekana kuna ulinzi mkali sana hapo ndipo wanapoishi yaani Nura na Mpundu. Basi geti lilifunguliwa na mlinzi aliyekuwa pale getini na Nura akwa yuko makini sana katika kuingiza gari lile na kuweza kwenda kupaki. Katika eneo hilo panaonekana ni majengo ya magorofa tu ndiyo yaliyotawala katika ameneo hayo ambapo panaonekana pako kimya sana ikiwa inamaanisha kuwa watu waishio maeneo hayo kwa muda wa mchana kila mtu yuko kivyake akiwa anasaka hela kwa namna mbalimbali ambayo ameona itamfanikishia yeye kupata hela. Maeneo hayo kwa ujumla huwa pana upepo mzuri sana utokao baharini hivyo ukiwa katika maeneo hayo kwa kweli furaha ya jiji utaipata sana. Nura alipaki gari lile kwa makini kisha katika sehemu ya kupaki magari na kulizima ndipo wakaanza kushuka. Mpundu alichukua mabegi machache na kutangulia ndani ndipo ikawa kazi kubwa ya Nura kuyachukua mabegi ya Mpundu. Nura alipomaliza kushusha mizigo ile ndipo wakawa wameenda kukaa sebuleni huku tayari Mpundu akiwa ameshabadilisha nguo na akawa amevaa bukta tu kwaajili ya kuepuka na joto lililokuwa likitambaa katika jiji la Dar es salaam. Nura akiwa amevaa nguo ambazo zilimuacha mabega juu na kuonesha uzuri wake vizuri aliokuwa amejaaliwa na mungu. Pia huku akiwa amevaa kisketi ambacho kilikuwa ni chepesi sana kwa ajili ya kuepuka kupata joto. Muda huo hapo mezani palionekana kuna chupa ya chai na vitafunwa vilikuwa katika sahani maalum. Vitafunwa hivyo vilikuwa ni chapati za mayai zilizokuwa zimepikwa kwa ustadi mzuri na mfanyakazi wao. Pia runinga kwa muda huo ilikuwa imewaka ikionesha kipindi maalumu. Mfanyakazi wao alikuja na kumsalimia Mpundu kisha akawa amerudi kwenda kuendelea na kazi nyingine za mchana na kuwaacha Nura na Mpundu wakiwa katika uwanja wa mazungumzo. Kwakweli Nura alikuwa na bashasha sana na Mpundu kwakuwa ni siku zimepita hajamuona Mpundu. Muda huo wanaonekana wote wamekaa katika sofa lililokuwa limejaaliwa nyama za kunesa kwelikweli ndipo maongezi walipoyaanzisha.
Mume wangu usafiri wa ndege uko faster sana unajua. Nura aliongea huku akiwa amemshika mkono Mpundu.
Ni kweli kabisa yaani chap utu tayari nimeshafika Dar yaani siamini kama leo nimeamkia Arusha lakini muda huu niko Dar. Aliongea huku akiwa anafurahi.
Ndiyo maana wafanyabiashara wakubwa huwa wanaamua kufanya hivyo tu. Yaani mtu anaona ni bora atumie hata laki mbili kwa saa moja lakini anajua anaenda kuingiza zaidi ya laki mbili huko aendako. Lakini kwa maskini yaani utakuta siku nzima mtu unasafiri kuanzia saa kumina mbili asubuhi unakuja kufika Dar saa kumi hadi kufika nyumbani kwako unajikuta saa kumi na mbili kabisa na midakika kutokana na hizi foleni.
Yeah ni kweli.
Endelea kupata chai mume wangu au umepata kifunguo kinywa kwenye ndege?. Nura alimuuliza Mpundu huku akiwa anafurahi.
Hata kama nimepata hapa nyumbani lazima ntakunywa tu ya nyumbani ni ya nyumbani tu. Basi mazungumzo yao yalipanda yakashuka hadi walipoanza kufika mazungumzo juu ya Nuru. Nura alimuuliza Mpundu kuhusu Nuru na Mpundu akawa anamjibu kama alivyokuwa akitaka. Kwasababu siku zote ukiishi Roma inabidi uigize kama waroma tu na ukishi Saudi Arabia inabidi uishi kama Wasaudia tu ndivyo alivyoamua kufanya Mpundu. Alimpamba vizuri sana kwa maneno mazuri juu ya maendeleo ya maduka yake na magari huko Arusha. Lakini Nura aliona ni vizuri akamuuliza Mpundu kuwa ni kwanini amechelewa kuja sana jijini Dar es salaam. Katika mazungumzo yao yalienda kama ifuatavyo.
Kwani Mpundu nini kilikufanya hadi ukaniambia mimi nitangulie kuja Dar na ukachelewa kuja hivyo?. Kwasababu siku ile hata sikutaka kukuuliza zaidi juu ya mipangilio yako hiyo. Japokuwa uliniambia siku ile kuhusiana na yule rafiki yako uliyekuwa ukimngojea.
Mpundu alinyanaza kwa sekunde chache akiwa anafikiria vyema majibu ya kumpa Nura akijua tu Nura ni bado mtoto kiakili kwahiyo kumdanganya ni kitu cha kawaida kwake. Aaaaaa yap nilimsubiri na akawa amewasili ndani ya siku zile nilizokuwa nimeahidiana naye. Tulifanya issue moja hivi japokuwa haikuwa katika ratiba. Kwahiyo ndiyo maana hata ukaona nimechelewa kuja huko kutokana na namna nilivyokuwa nimekuahdi.
Issue gani hiyo?. Nura alimuuliza Mpundu kwa umakini Zaidi.
Aaaaa issue ya kawaida ya kibiashara tu. Siunajua hapa mjini bana bila kuumiza kichwa huwezi kuishi vziuri.
“Haya bana ila muda mwingine inakuwa tatizo nyota pia.
Haya bana
“Lakini mambo hayo yote yalikwenda vizuri kabisa?.
“Ndiyo hapakuwa na challenge yoyote kabisa. Kwahiyo mambo yakawa yameenda kama tulivyokuwa tumepangilia kabisa.
“Masula ya kibiashara hayo au siyo Mpundu?. Mazungumzo yasiyokuwa na kikomo kwa siku ile ndiyo yaliyokuwa yametawala hapo ndani hadi muda wa chakula cha mchana ulipofikia. Walipata chakula na baada ya kumaliza kula ndipo sasa kila mtu alichukua nafasi ya kwenda kupumzika.
Ikiwa ni siku ya jumapili mishale ya saa kumi jioni marafiki wa karibu ambao ni Kambi na Nuru. Mda huo walikuwa maeneo ya nyumbani wakiwa katika maeneo ya kibarazani hivi hapo uani panaonekana kuna magari matatu ya kifahari yakionesha nafasi halisi ya kimaisha ya Kambi.  Kambi hakutaka kujificha maisha yake eti mtu asimjue kama yeye ni tajiri kama walivyo matajiri wengine wa kupuliza. Jumba lake lililozungushwa na ukuta mrefu kwelikweli. Kambi akiwa amevalia suruali ya jinsi ya rangi ya bluu na tisheti nyeusi akiwa amevalia na kofia ambayo kwa juu ilikuwa imeandikwa KING kwa herufi kubwa maandishi yale yakiwa ni meupe na sehemu nyingine ya kofia ikiwa ni nyeusi. Miguuni alivaa ndala za kupumzikia. Nuru naye alivaa hivyo hivyo utafikiri mapacha kasoro kichwani na miguuni. Ambapo kichwani hakuvaa chochote na miguuni alikuwa na sendo. Basi muda huo walikuwa wana mazungumzo kama ifuatavyo.
“Daaa Kambi nakuona umeng'aa kweli kweli kwasababu ya huko ughaibuni kwa miezi michache tu. Nuru alimsifia
Kambi alicheka kama sekunde chache ndipo akasema. Ahaaaa huko ndiko mbinguni yaani ninakwambia huko Brother nimekutana na matajiri hadi najiuliza hivi hawa watu tuseme wao wameumbwa na mungu kiuepekee?.
Naye Nuru alicheka na kusema. Yaani hao wafanyabiashara wa madini siyo?.
Ndiyo ndiyo yaani nakwambia kuna ambao kwanza nilikutana nao hapo Armstadium uwanja wa ndege hapo ni shida. Yaani hao ni wa kimataifa.
“Duuuu Armstadam kabisa?.
Ndiyo maana yake
“Yaani mimi nimezoea kukiona hicho kiwanja kwenye magazeti na video tu
“Ohooooo huko yaani nimepaona live bila chenga.
“Armstadam hapo
Ndiyo ndiyo yaani nilikuwa na Tanzanite za kutosha kinyama.
Tanzanite kabisa
“Ohooooo ndiyo maana yake.Yaani awamu hii nilikuwa na huo mzigo tu wa Tanzanite. Hapo uwanjani tu walikuja kunipokea yaani hao sasa mazimba si wa utani utani kabisa. Yaani nikawa nakumbuka zile movie za mtu akiwa ana mzigo mkubwa anavyonuswaga na majambazi. Kwahiyo nikawa niko makini sana muda huo.
“Daaa brother unanitamanisha sana.
Kwanini?.
Unavyosema hayo mambo yaani napagawa kinyama.
“Hamna shida brother ndiyo maana nakwambia fanyafanya ukweli kwa yule mdada uweze kujiachia pale. Chukua chako pale mapema akija kukuzingua wewe pita hivi.
“Yaani wewe acha ndiyo hivyo.Yaani hadi yule jamaa wa Nura kanichana yaani kaniambia ukweli kabisa kuhusiana na Nura alivyo.
Kabisa. Acha wewe
“Yaani alafu yule jamaa nahisi kama na yeye ni mhunimhuni tu wa huku Arusha
Yaani kakulia Arusha siyo?
“Ndiyo maana yake. Kakulia hapo Ungalimited”
Haaaaaa. Kambi alishangaa sana baada ya kuambiwa kuwa Mpundu ni mzaliwa wa Arusha maeneo ya Ungalimited kisha akasema. Nura ushaibiwa tayari huko uliko. Chalii wangu unawajua watoto wa Ungalimi wewe?.
“Nawajua. Kwasababu hata yeye mwenyewe siku hiyo aliniambia kabisa kwamba nifanye juu chini niachane na huyo Nura mapema sana kabla miezi sita haijaisha.
“Duuu vipi tena brother hapo kutakuwa na jambo nyuma ya pazia nini?. Kwa namna alivyokuwa akikuambia ni kwamba alikuwa na hali gani hivi?.
“Aaaaaa ni hali ya kawaida tu. Lakini kwa namna nilivyomsoma ana maana kubwa sana aliponiambia na kunishauri mimi kuwezakujitoa pale haraka sana.
“Fanya hivyo ili na wewe uweze kung'ang'ania kule kwako.
“Sasa hapa inabidi nitafute namna ya kuweza kumkasirisha hapo ili aweze kuchukia mazima na kunifukuza pale kwake asinitumie mimi kwenye shughuli zake zozote zile. Kwasababu ameshanizoea vibaya sana.
Tafuta namna yoyote ile brother
“Sawa.Tuko pamoja kabisa hapo.
Kwakweli kwa siku ile Mpundu na Nuru waliweza kuzungumza mengi sana yakiwa ni ya kimaisha kama ilivyo kwao wakiwa katika maongezi kwa kweli ni vigumu maongezi yao kuisha.















SURA YA SABA
Miezi na siku nazo zilizidi kwenda kama upepo wa Hurricane huku nazo tarehe za kurudisha mkopo ambao Mpundu alikuwa ameuchukua kutoka katika Taasisi ya Utoaji Mikopo ya Kibiashara (TUMIKI) hapo jijini Arusha. Lakini kwa Mpundu hakuwa na hata muda wa kusema atarudisha fedha ile. Japokuwa Mpundu alichukua mkopo ule hakuna chochote alichofanya cha kusema atafaidika na kisha akalipe deni lile zaidi tu ni kwamba alienda kununua jumba la kifahari moja huko Marekani katika jimbo la Calfonia ambako pia kuna ndugu zake walikuwa wakiishi huko. Kwahiyo ndiyo maana ikawa ni rahisi kwa yeye kuweza kununua jumba hilo la kifahari huko Marekani katika jimbo la Calfonia. Kisha akawa ameanzisha baadhi ya vitega uchumi vyake huko huko Marekani bila Nura kujua. Jumba hilo alilinunua baada ya kumaliza masomo yake ya elimu ya juu katika chuo Kikuu cha Dar es salaam akiwa na Shahada ya awali ya Sheria. Lakini hadi muda huo Nura haelewi chochote kabisa kinachoendelea kuhusiana na mipangilio mipya ya Mpundu ya mara kwa mara tu kwenda huko Marekani. Kwahiyo safari za kwenda Marekani kwa Mpundu zikawa za mara kwa mara kwake. Mpundu alimjuza Nura kuwa hatoweza hata kuhudhuria katika mahafali yao kwasababu anaona ni kama itammalizia ada tu bila hata faida yoyote. Jambo la msingi aliloliona kwake si kusherekea bali ni aweze kufaulu tu.
Siku zote jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza kabisa tena giza totoro. Kwasababu vitega uchumi vya Nura vingi ambavyo alivyokuwa akivianzisha viliweza kusainishwa kwa jina la Mpundu. Kwa kuwa Nura anajua fika kwamba Mpundu ni mpenzi wake wa maisha na mke wake wa maisha. Mpundu alizidi kumuibia fedha Bibiye Nura na bila hata Bibiye Nura kuweza kutambua chochote kile kinachoendelea kuhusiana na mali zake.
Basi siku hiyo ikiwa ni siku ya jumamosi Nuru aliamua kumchukua Kambi na kumpeleka hadi sehemu ambayo Nuru amejenga nyumba yake. Maeneo ambayo amejenga ni maeneo ya Moshono karibia na maeneo alipofungua zile chegani za kike pamoja na maduka ya urembo na ya nguo kwa wanawake.
Kwa muda huo na Nuru naye alikuwa ameshafanikisha kununua gari moja hivi ambalo ni aina ya Rava 4. Kwahiyo katika eneo hilo inaonekana nyumba ya Nuru iliyojengwa vizuri kabisa. Basi Nuru na Kambi wakiwa wanazunguka katika kila kona za nyumba ile wakiwa wanaendelea na mazungumzo kama ifuatavyo.
“Daaaa!! Eee bwana kijana umeamua kabisa kuutoa umasikini.
“Ohooo!! Wewe Kambi unafikiri haya mambo ukiyafanyia utani utajikuta hadi unafikia kuoa bado tu umepangisha tu. Alafu unajikuta unafuga ndevu tu. Mwisho wa siku inakuwa ni aibu tu.
“Ndiyo maana yake. Yaani mimi nafurahi sana kwamba umesikiliza maneno yangu kweli na kuyafanyia kazi. Nilipokuwa nakwambia kwamba mng'ang'anie Nura hivyo hivyo tu nilikuwa na maana kubwa sana.
“Kweli kabisa Kambi. Daaa unajua kuna kipindi nilitamani kukurupuka kabisa na kuanza kumshushia matusi machafu bali nikaja nikakaa kitako na kufikiria kwamba hapa mtaka cha uvunguni sharti ainame na siyo kubinua kitanda. Kwasbabu ukibinua kitanda lazima watu wengine nao watamani.
“Ndiyo maana yake. Wewe unafikiri nyumba kama hii wewe leo ungeijenga kama ungeongozwa na hisia pamoja na hasira zako?.
Hapana kabisa. Muda huo wanaonekana wakizunguka ndani mle mwa nyumba ile ikiwa inaonesha kabisa upya wake. Chini ikiwa imetandazwa tiles zenye kupendezesha nyumba kweli kweli. Kisha muda huo Kambi akawa anasema hivi.
“Alafu pia na ile nyumba ya kule Njiro inabidi uikamilishe mapema.
“Ile ya kule kwaajili ya familia siyo?
Ndiyo ndiyo.
“Sawa. Ile chapu tu itamalizika. Kwasababu wale mafundi nimewawekea conditions ngumu kweli kweli ambazo zitawafanya wamalize mapema na kwa uhakika.
“Basi vizuri. Kwa hapo Nuru nakupa hongera. Maisha ndivyo yalivyo hivi. Hakuna maisha mengine zaidi ya hapa duniani tu. Kwahiyo kwa hapa duniani inabidi uishi kwa raha mstarehe kabisa japokuwa ni kwa muda mchache.
“Hahahaaa. Alicheka kisha akasema. Haya bana nimekubali nadharia yako.
Ndiyo maana yake.
“OK… basi twende zetu turudi natumai umeshajionea nyumba ya bwana Nuru.
Walitoka kupitia geti kubwa ambako kulikuwa na mageti mawili yaani dogo na kubwa. Ambapo hilo kubwa ni kwa ajili ya kupitia gari na hilo dogo ni kwa ajili ya watu kuweza kupita. Jumba hilo nalo lilikuwa na ukuta mrefu sana hadi kufikia hata mita nne kabisa. Ndipo wakawa wamerudi kwenye gari na kuelekea huko mjini huku geti likiwa linafungwa kwa kitenzambali.
Siku hiyo Nura akiwa yuko maeneo ya Kariakoo. Ambapo na yeye kwa kipindi hicho tayari ameshamaliza masomo yake ya elimu ya juu katika chuo Kikuu cha Dar es salaam. Kwahiyo muda huo anaonekana yuko ndani ya gari pamoja na Mpundu. Siku hiyo ikiwa ni mwishoni mwa wiki mishale ya saa kumi hivi. Nura wakiwa ndani ya gari katika mtaa fulani wa hapo Kariakoo. Nura alikuwa na dhumuni la kumpigia simu Nuru. Nuru alisikia simu ikiwa inaita kisha akainuka na kwenda kuichukua ambapo muda huo Nuru yuko ndani ya jumba la kifahari la marehemu mzee Kerima ambalo kwasasa linamilikiwa na Bibye Nura. Nuru alipokea simu ile na maongezi yakawa yameenda kama ifuatavyo.
Wewe Nuru mbona umekuwa mzito wa kupokea simu?.
Simu ilikuwa kwenye chaji.
SawaSasa dhumuni la kukupigia simu ni kwamba siku si chache tunakuja huko Arusha.
Karibuni sana nimewamiss sana
Hata kama usipotumiss
“Duuu yashakuwa hayo
“Wewe bwana eeee sasa wewe Nuru nasema hivi hadi siku hiyo tunakuja hapo nyumbani sitaki nikukute hapo.
“Bali unataka unikute dukani siyo?.
“Wewe usinifanye mimi mtoto eee wewe una duka?. Nakwambia chukua kila kilicho chako hapo ondoka zako.Yaani sitaki nione sura yako hapo.
Nura
“Ndiyo maana yake au huelewi nachokwambia Nuru. Nimekwambia sisi tunakuja huko Arusha siku si chache kwahiyo nachotaka ondoka hapo. Chukua kila kilichochako nenda kwenu.
Sasa Nura mimi nitaenda kulala wapi?. Alijifanya hana chochote kabisa. Yaani mtu ambaye hajiwezi kabisa.
Kalale hata sitendi.
“Ntaanzaje anzaje kabisa kulala stendi jamani?
Mimi nahisi ni kama hunielewi kabisa wewe. Nakwambia nikikukuta hapo nakuitia polisi kwamba wewe ni mwizi.
Kabisa mimi ni mwizi.
Sasa wewe baki hapo
Amakweli shukurani ya punda mateke.
“Sasa nakwambia wewe ng'ang'ania kukaa hapo kwenye hiyo nyumba ndiyo utajua kweli shukurani ya punda ni mateke au laa.
Nura aliendelea kumshushia maneno machafu hadi alipoona Nura amezidi kulalamika tu aliamua kukata simu na Nura akawa amejua kabisa kuwa ameshamkomesha Nuru. Lakini Nuru kwake aliona ni kama amepata ruhusa nzuri ya kuondoka kwa amani katika himaya ya Nura.
Kama kawaida ilivyo kwa Nuru hupenda kila jambo ambalo litamtokea au atakalolifanya na kuwa ni kama jipya hupenda sana amshirikishe rafiki yake wa karibu sana ambaye ni Kambi. Kwahiyo muda huo huo Nuru alimpigia simu Kambi. Kwa wakati huo Kambi anaonekana akiwa katika uwanja wa ndege wa KIA akiwa katika maandalizi ya kwenda kupanda ndege inayoelekea jijini Dar es salaam. Muda huo tayari ni kama mishale ya saa kumi na moja kasoro ya jioni. Pembeni panaonekana pia kuna wasafiri wengine wanasuburi muda wa kuruhusiwa kwa ajili ya kwenda kupanda ndege ya kuelekea Dar es salaam. Kambi alipokea simu na wakawa wameanza maongezi yao. Kambi aliweza kumsikiliza vizuri Nura kisha akamwambia kwamba ni vizuri sana boss kamfukuza siyo kwamba mfanyakazi kakimbia. Kambi alimueleza kuwa Nuru kuwa ndiyo yuko katika haraati za kupanda ndege sababu safari hii alikuwa na mpango wa kwenda hadi ujerumani kwa masuala yake ya kibiashara. Basi waliongea hadi ikawa tayari muda maalum kabisa ulikuwa umewadia kwaajili ya kuweza kupanda ndege.
Basi ilipofika mishale ya saa moja jioni hivi Mpundu alimpigia simu Nuru. Muda huo Mpundu anaonekana yuko maeneo ya ndani. Inavyoonekana ndani hapo Nura hayupo kabisa. Nuru muda huo Nuru alikuwa akiendesha gari akiwa anatoka Njiro kuelekea maeneo ya Moshono ambapo kwa muda huo alikuwa amefika Mnara wa saa. Kwahiyo baada ya kuona simu kutoka kwa Mpundu akawa amejua fika hapa kuna taarifa mpya kutoka kwa jambazi asiyejulijakana. Basi Nuru alipaki gari na kisha akawa amepokea simu. Maongezi yao yalikuwa kama ifuatavyo.
Oya Nuru vipi?.
Poa nambie brother.
Fresh kabisa.
Mmmmh nipe habari.
“Ohooooo nimekupigia hapa ili kukuuliza vipi umeshajipanga?.
“Ndiyo maana yake. Mimi nilikuwa nasubiri tamko kutoka kwa Nura tu.
Ahaaaa nimi ndiyo kama nilivyokwambia kuhusiana na ile issue miezi imeshakaribia kuisha.
Duuu Hivi imebaki miezi mingapi?.
“Ahaaaa miezi tena. Nikwambie kitu yaani umebaki mwezi mmoja tu hadi muda huu tunavyoongea hapa. Kesho si ndiyo tarehe ya moja au siyo?.
“Ndiyo maana yake kesho tarehe ya moja.
“Sasa kesho kuna gari litatangulizwa kuletwa huko Arusha.
Kupitia nini?.
“Kupitia haya magari yanayosafirisha magari kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Aaaaaaa haina shida
“Kwahiyo kesho kutwa au mtondo goo tunaweza kuwasili hapo.
Mnakuja kwa ndege siyo?
“Ndiyo maana yake. Demu ana hela chafu huyu. Sasa nakwambia tulia ndani ya mwezi huu tu utaona kwamba huyu demu atakavyojuta katika maisha yake kunifahamu mimi mtoto wa Ungalimited.
Kwa nini tena?
“Wewe tulia usipende kuhadithiwa mara kwa mara subiri ujionee live live.
“Haya bana nasubiri.
“Poa ila wewe fanya huo mpango wa kuchukua vitu vyako hapo ili baadae nikija kuharibu mambo asije akakulaumu wewe wakati hata hujui A wala B.
Unajua unanitisha sana Mpundu.
Kwanini?.
Kwa namna ulivyompania yaani. Daaaa.
“Huyu demu mjinga sana hawezi akawa anazalilisha wanaume kila siku hivi.Yeye anajifanya kununua wanaume sasa tulia tumenunulika na lazima tumuibie.
“Kumuibia?. Nuru
“Na kumfilisi kabisa ukiachana na kumuibiya kidogo tu.
Duuuu kwelikweli una hasira naye sana.
“Huyu ni mtoto mdogo sana kwangu.Yaani kwanza kipindi hicho tukiwa chuo alikuwa akinilipia hata ada na pia kuna madume wengi tu walikuwa wanalipiwa ada na Nura. Sema mimi tu ndiyo alikuwa amepagawa kwangu ndiyo maana akatulia tu hapa.
Kabisa kuwalipia. Nuru aliuliza huku akiwa ameshtuka.
“Ndiyo maana yake. Lakini wote hao alikuwa anatembea nao kwa kila aliyekuwa amemlipia.
“Brother bana kama hatari hiyo. Hilo gonjwa la kisasa vipi lisije likakukuta brother. Utakuja kujiona mabega juu kuwa makini sana brother.
“Hapana huwa naenda kupima mara kwa mara. Kwahiyo hata sina hofu kwa hilo.
Hapana brother usijiamini kwa asilimia zote. Wewe cha msingi ni kuwa makini tu.
“Sawasawa. Ila brother kuwa makini na wewe huko. Kwasababu kitu kinachoenda kutokea siku si chache huko ni shida sana. Kinaweza kikafanya hadi huyu Nura hata kuwa kichaa kabisa. Yaani kwanza kwasasa yaani ndiyo kajichanganya kabisa kabisa.
Kwanini unasema hivyo?.
Yaani huwezikuamini nakwambia kwasasa ni mwendo wa kuhifadhi fedha Barclay's Bank.
Acha utani wewe. Benki ya matajiri tu hiyo.
“Ndiyo maana yake hata mimi tajiri sema mdogo.
“Haya bana. Shukurani kwa kunisanua mapema?.
“Hamna noma. Nakusubiri tu wewe huko usije ukaniangusha huko.
Sitokuangusha.
“Sawa
“Kwasababu wewe ukishakamilisha mambo yako wewe nijulishe hata kwa SMS tu. Kwasababu mimi hapa ndiyo naweza kumuamuru tuje huko au vipi.
 Hamna noma.
“Ndiyo maana nimeamua aje huko ili aje kujionea kinachotaka kutokea siku za usoni.
“Duuuuuu wewe ni silent killer. KwaKweli nimeamini kikulacho kinguoni mwako. Walipeana mipango ya hapa na pale yote hiyo ni kutokana kila mtu kwa Nura yuko kwa ajili ya maslahi tu na vinginevyo.


      Ni siku iliyofuatia mishale ya saa nne asubuhi tayari Nuru alikuwa ameshahamisha vitu vyake vyote ambavyo vilikuwa katika jumba la kifahari la marehemu mzee Kerima na kuvileta katika nyumba yake mpya iliyoko maeneo ya moshono. Muda huo Nuru akiwa anaonekana yuko maeneo ya kibarazani akiwa amesimama huku akiwa anaangalia mizigo yake iliyoletwa na gari lililoondoka muda si mrefu kama iko kamili. Kwasababu mizigo yake ile ililetwa kwa gari la kubebea mizigo. Muda huo Nuru akiwa hapo kibarazani na kama hatua zake zikionekana kama anataka kutembea na kuanza kuangalia sehemu nyingine. Muda huo alikuwa amevaa suruali ya jinsi ya rangi nyeusi na tisheti ya bluu na mkononi pia amevaa saa nzuri sana yenye kujulisha hadhi ya tajiri mpya mjini ambaye ni Nuru. Akiwa anatembeatembea huku akiwa anazungumza kimoyomoyo.
“Yaani kwakweli mwanamke sijui nimfananishe na kitu gani tu jamaniau ni kwa huyu Nura tu ndiye ambaye anatabia kama hizi?. Mmhhahaahhah yaani eti kabisa anafikia hadi anaandika majina ya mwanamme katika kila mradi atakaouanzisha. Yaani utafikiri anajua kwamba yeye ndiye atafariki wa kwanza ndipo afuatie Mpundu. Hajui dunia ya leo ni dunia ya kizazi cha nyoka?. Nura huko uliko kama ndiyo uko moshi au bado uko Dar mungu akujaalie tu. Kwasababu kwa miaka michache tu hii nimejikuta nimebadilisha maisha yangu na pia na familia yetu. Lakini hii ni baada ya mimi kuzidi kujifanya mjinga sana na kujifanya kama vile umenipiga limbwata. Hapana wewe nilikuwa najielewa kabisa tena kabisa. Sema ndiyo hivyo kuna baadhi ya maeneo ukifika wewe jifanye kama mjinga tu yaani kama huelewi elewa tu. Ila eee mwenyezimungu najua baadhi ninayoyafanya ni kama makosa kwako ila ndiyo hivyo mimi sina namna. Kwasababu huyu mwanamke yeye ndiye aliyeanzisha timbwili lote hili. Mungu nisamehe tu kama nimekosea kubwa. Hii dunia ya leo ndiyo hivyo muda mwingine ukizidisha usamaria mwema utashia kupata shukurani kwa watu tu na ndiyo itakuwa faida kwako kila siku na wewe unabaki kulala njaa tu.
Muda huo kashuka kutoka hapo kibarazani akawa anazunguka nyumba nzima huku akiwa anaendelea kuongea tu. Ila ilikuwa ni halali yako mimi kukufanyia hivi. Kwasababu wewe mshenzi ungejua ni namna gani nilivyokuwa nakupenda. Yaani ndiyo maana nasema mungu angeweza kufanya kwamba moyo wa mtu fulani unaompenda mtu fulani uwe unaonekana kwa mtu fulani aaaaa kwakweli watu wengi sana wasingeolewa na kuoa na watu wengi wangeolewa na kuoa. Ila ndiyo hivyo mipango ya mungu haina makosa. Siku zote malipo ni hapa hapa duniani na akhera huko ni mahesabu tu. Nimekuja kuamini kweli uvumilivu katika michakato ya kuweza kuyajenga maisha ni kitu ambacho hakiepukiki. Muda huo anaonekana ameingia ndani akiwa anazunguka ndani ya nyumba yake akiwa huku anaendelea kuongea. Kweli mali hii niliyotumia kujengea nyumba hii kwa upande mmoja inaweza kuwa ni kama mali ya kushoto hivi na pia kwa upande mwingine ni kama mali ya kulia. Ila hali kuyafikiria yote hayo ya kulia na kushoto ni imani tu wala si chochote. Sina budi kusema Nura Shukurani sana kwakuishi na wewe miaka yote hiyo na kuweza kunifunika akili yangu kutoweza kuwaza haswaa masuala ya kuwa na mchumba mwingine. Kwasababu nilijua tu nikianza kuwa na mawazo ya kuwa na mchumba mwingine naye huyo mwingine nahisi angeanza kuniumiza kichwa ile mbaya. Pia hata hatua ya kimaendeleo sidhani kama ningepiga hatua kama nilivyofikia kwasasa. Hadi muda huu yaani sina hata mawazo ya kusema niwe na mpenzi. Kwa kweli kuna muda nilikuwa najihisi kwamba siko vizuri kiafya kabisa. Lakini haina shida siwezijua namna mungu alivyonipangia. Mungu nibariki katika maisha yangu. Inshaallah.
Baada ya kupita wiki moja ambapo tayari Nura na Mpundu walikuwa wameshawasili Arusha. Muda huo ikiwa ni mishale ya saa mbili za usiku wakiwa wanaonekana wako katika ukumbi wa jumba la kifahari la marehemu mzee Kerima. Hapo nje kuna taa zimewaka kweli kweli zenye kumuwezesha mtu hata kuweza kuona hata sindano iliyoanguka. Basi hapo nje walipokuwa wamekaa ni sehemu ya kupumzikia na kuna viti maalum kabisa viko hapo. Ndani huko palikuwepo wafanyakazi wakiwa wanaanda chakula cha usiku ili wakubwa waweze kupata chakula. Kwa pale nje walihadhithiana hadithi za hapa na pale. Walikuwa wakifananisha mandhari ya Dar es Salaam na Arusha yanavyotofautiana. Hali ya hewa ya Dar es laam na Arusha inavyotofautiana. Walipanga mengi wakiwa hapo nje. Mpundu alimwambia Nura mipango mbalimbali ya kibiashara aliyokuwa akiifikiria. Lakini mipango mingi ilikuwa ni ya kiuongo tu ili kumfanya tu Nura aweze kuamini kuwa Mpundu naye ana kichwa cha biashara. Nura alifurahi sana kwa namna alivyofika pale nyumbani na kukuta Nuru hayupo kwahiyo Nuru ametii amri ya Nura. Ni kitu ambacho alijiona sana kuwa yeye ndiyo yeye anaweza kusikilizwa kwa kila neno lake atakalolinena. Liwe ni baya au zuri lazima tu lisikilizwe sababu tu ni hela alizonazo. Kwa asilimia kubwa Nura aliamini kuwa pesa ndiyo kila kitu katika dunia hii na wala si kitu kingine. Sababu aliona pesa inakufanya uheshimiwe ni kila rika. Mzee, kijana na hata viongozi wa juu wanaweza kukuheshimu sana kwa kuwa wao wanaona wewe ni mtu mkubwa sana kwako. Kwahiyo ndiyo maana wanakuwa wanakuheshimu. Hivyo ndivyo alivyokuwa akiamini Nura katika maisha yake. Basi kwa siku ile waliongea ya hapa na pale na wakawa wameamua hata chakula ni vyema wangepatia pale pale nje kwa kuwa waliona ni uvivu tena kuanza kuingia ndani kwa ajili ya kula tu ambapo kutafanya kukatika kwa maongezi yao. Hata kama watayaendeleza lakini hayatonoga kama hya mwanzoni kabisa. Wakiwa wanaendelea kupata chakula pale ambapo chakula hicho kilikuwa ni vibanzi kuku ambazo zinaonekana zilipikwa ustadi wa hali ya juu. Kwa harufu yake tu iliyokuwa ikinukia inaweza kumfanya mpishi ashibe kwa ile harufu tu ndiyo baadae aje aanze kuhisi njaa. Kila mtu alikuwa na sahani yake. Ambapo hapo kati kulikuwa na meza ndogo hivi na wenyewe wakiwa wamekaa kwenye viti maalumu vya kukalia nje. Kila mtu alikuwa na kimeza chake kidogo. Mpundu alijaribu kumdodosa Nura baadhi ya mambo kwa kumuuliza hivi.
“Hivi ni nini haswa ulifikiria kwamba hadi ukamwambia Nuru atoke hapa?.
Wala.
Bali ni nini?.
“Nilijikuta tu napanga nimuondoe tu hapa nyumbani. Kwasababu niliona kama atanizidishia makelele tu nikija huku. Acha akakae mbali huko ili tuwe huru.
“Sasa kwanini hata ungemuacha tu abaki kule dukani na siyo kumfukuza kotekote?.
Aaaaaa nimeamua hivyo ili ukaribu na yeye ukatike kabisaaa moja kwa moja. Mimi siwezikuchangiana mawazo na mtu kama yule kabisa. Masikini kama yule mimi nimpeleke wapi sasa. Acha akae huku nitatafuta mtu mwingine tu wa kumfix hapo na biashara zangu zitaenda tu. waliongea mengi sana ndipo Mpundu akasema sasa ni muda wa Nura kulia.
Ikiwa imebaki kama wiki moja hivi ili Mpundu kusafiri kwenda Markani aliweza kumjulisha kabisa Nuru kuhusu safari yake aliyokuwa ameipanga. Kisha akampa kabisa Nuru tahadhari kuhusu Nura.















SURA YA NANE
Mawazo kwa Nuru ya kusema kuwa na mpenzi kwake yalikuwa bado sana kwa kuwa kila mwanamke atakayemuona huwa anamfananisha na Nura ambaye aliweza kuushikilia moyo wake kwa siku nyingi sana lakini baadae anakuja kumwaga mboga. Yaani tangu wakiwa elimu ya upili na baadae Nura anakuja kuutupa moyo wa Nuru baada tu ya kumaliza kidato cha nne. Pia Nura ndiye mwanamke pekee ambaye alimfundisha mapenzi lakini baadae hakuweza kufaidika chochote kutoka kwa ukufunzi ambao aliupata wa mapenzi kutoka kwa Nura. Nuru akiwa maeneo ya nyumbani kwake akiwa amekaa kwenye sofa mbele panaonekana kuna meza ya kioo juu kuna Glass yenye juice iliyokuwa imejaa tele. Muda huo Nuru akawa anaongea peke yake kama.
“Nura kwasasa nimepata lakini sijapata hamu ya kupata mpenzi. Hali yote hii inatokana na sababu mbalimbali ambazo zimesababishwa na wewe huko. Ila haina haja ya kumlaumu marehemu angali ndiyo hivyo amekata kauli yaani hawezi kutoa chochote kutoka katika kinywa chake. Wewe ndiye uliyenifundisha mapenzi lakini ndiyo hivyo sijui kwamba cheti cha mapezi ni kusalitiwa au laa?. Kwa mimi ndivyo ninavyohisi hivyo. Basi hata mimi sina la kusema bali nashukuru kwa mabaya na mazuri uliyonitendea. Pesa sabuni ya roho. Tundamani aliimba kweli”. …………………………………………………………………………………………………………………………………………………

Kwakweli Nuru aliimba wimbo ule hadi machozi yalimbubujika mithili ya mtoto aliyenyimwa pipi ya ahadi. Kwasababu Nuru anaona ni namna gani kweli ule wimbo ulivyojaaliwa maudhui ya hali ya juu yenye uhalisia kabisa katika jamii yake.
Ikiwa ni mishale ya saa saba mchana siku ya jumapili. Muda huo Nura na Mpundu walikuwa wamekaa maeneo ya nyumbani pembezoni panaonekana kuna bustani iliyo nzuri kabisa yaani yenye kuvutia. Kwa ujumla sehemu waliyokuwa wamekaa ni sehemu maalum ya kupumzikia. Kuna viti maalumu vya kuweza kupumzikia hapo. Mandhari ya hapo kweli inaonesha ni ya kuvutia sana. Walikuwa katika maongezi marefu sana. Kwa muda huo jua lilikuwa likiwaka kwa mbali hivi. Kwahiyo si kwamba lilikwa limewaka sana bali ni kwa hali ya kati tu. Katika ukumbi ule panaonekana magari yaliyopaki huko ni mengi na yote yakiwa yamepakiwa kwenye mwamvuli maalumu wa kufunika kwajili ya kuepusha kukutana mwanga mkali wa jua. Muda huo walikuwa na maongezi yao ya hapa na pale. Mpundu aliweza kumkumbusha Nura kuwa safari yake ya kwenda Marekani kuwa tayari imeshakaribia. Nura alijiona kuwa atabaki mpweke sana sababu Mpundu anaenda Marekani na si kwamba atakaa wiki moja na kugeuza. Mpundu alimpa moyo wa matumaini kuwa lazima atarudi na watazidi kuwasiliana kwa kina zaidi ili kumuondoa katika hali upweke. Mpundu alimuuliza kuhusu mipango ya kumpata mtu mwingine wa kusimamia maduka na Nura akawa amesema kuwa ameshapata mtu amabye kwake aliona ni mwaminifu ni akikaa hapo anawza akasimamia vizuri tu maduka yake. Waliweza kila kitu vizuri ikiwa ni ya kibiashara.






Ni siku nyingine mpya kabisa yenye kuendeleza kuleta furaha kwa baadhi ya watu na baadhi ya wengine hudhuni kuja kuwatokea japokuwa hadi muda huu hawajajua kama wanaweza wakatokewa na hudhuni au laa. Bali wanalolijua ni moja tu ambalo ni la kufurahi tu.
 Ni mishale yaa saa moja asubuhi Mpundu tayari alikuwa ameshawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA. Muda huo Mpundu anaonekana amevaa mithili ya muamerika. Kwasababu kavaa suruali aina ya jinsi ya rangi nyeusi hivi shati la mikono mirefu lenye rangi ya bluu na likiwa na maua maua ya rangi nyeusi huku akiwa amenyonga tai yake ya kijerumani yenye mistari meupe na meusi na sehemu nyingine ya bluu liiyokuwa. Mkononi pia kavaa saa ambayo ilikuwa inaonesha hali ya ujanja wa Mpundu hadi kuweza kuishi maisha mazuri hivyo. Muda huo kuna ndege ilikuwa imepaki mahala pake kabisa ikiwa ndiyo inaonesha iko tayari kuanza kupakia abiria wake.
Ndege waliyokuwa wanatakiwa wapande ilikuwa tayari imeshaweka mabawa yake vizuri. Muda huo ndege yao ndiyo kama ilikuwa inaingia site ilikuweza kufanya abiria waanze kupanda. Mpundu alimpigia simu bwana Nuru na kumjulisha kuwa safari ndiyo inaanza kunoga hivyo. Muda si mrefu anatoweka Tanzania na hapa Afrika kabisa. Nurua alimwambia tu huko aendako awe makini tu na azidi kumuomba mungu wake. Pia Mpundu aliweza kumwambia ukweli dhahiri kwanini haswa anaenda Marekani. Kwasababu tangu mwanzo alikuwa akimuambia kijuujuu tu bila hata kufikia majibu kamili ya kuhusu safari yake. Alimjulisha kuwa kabisa kurudi Tanzania kwake ni kitu hakitowezekana labda sijui itokee nini kabisa. Bali Nura si wa kumfanya arudi Tanzania kabisa. Walipomaliza maongezi basi ikawa ndiyo muda basi wa wao kuanza kupanda ndege.
Ikiwa ni mishale ya saa mbili na nusu asubuhi kwa majira ya Afrika mashariki. Kwa maeneo ya Arusha muda huo bado baridi inayoyoma kweli kweli. Linaonekana jopo la watumishi wa Taasisi ya Utoaji Mikopo ya Kibiashara (TUMIKI) likiwa limekaa katika ukumbi maalumu wa kuweza kufanyia mikutano. Wanaoonekana hapo na kujulikana mojawapo ni muhudumu ambaye aliweza kusikiliza taarifa za Mpundu alipokuwa akijieleza kwaajili ya kuweza kupatiwa mkopo na shahidi wake kwa siku hiyo alikuwa na Jeshi Mkwasi Msophe. Muhudumu ambaye alisikiliza maelezo ya Mpundu anaitwa Ruhya Max ambaye cheo chake katika taasisi hiyo yeye ndiyo kama msikilizaji mkuu wa maelezo kwa watu wote wanaokuja katika taasisi hiyo na kuomba mkopo. Basi kikao hicho kilianza ambapo aliyekuwa muongozaji wa kikao kile alisimama na kutoa salamu kwa watu wote. Alitoa amri ya kufungua kikao kama ilivyo ada. Baada ya kuongea mengi yaliyokuwa yakihusiana na kikao kile basi aliweza kumruhusu Ruhya Max asimame aseme yake. Kwahiyo alimkaribisha Ruhya Max kama msikilizaji mkuu katika taasisi ya TUMIKI. Alisimama Ruhya akiwa amevaa vizuri na umbile lake la kuonesha kwamba si mrefu sana na si mfupi sana bali ya kiasi cha kati. Akiwa wamevaa kiislamu zaidi. Alianza kusema hivi.
“Kwaujumla tu niweze kusema habarini za asubuhi?.
Nzuri. Waliitikia kwa pamoja.
“Natumai wote tu bukheri wa afya. Aaaa mimi kama msikilizaji mkuu kwa watu wanaokuja kuomba mkopo katika taasisi yetu ninapenda kutoa ufumbuzi mdogo utakaotoa mwanga kwa baadhi ya wanajopo ambao hawajajua vizuri nini dhumuni la kikao hiki kwa undani zaidi. Kikao hiki kina lengo la kuwataarifu na kutoa maamuzi kutoka kwa muamzi mkuu wa TUMIKI katika tawi la Arusha. Baada ya kuongea vile ndipo akaanza kuelezea muhtasari  mzima wa wao kukaa pale. “Aaaaaaa ilikuwa ni tarehe ya 14 ya mwezi wa kwanza mnamo mwaka huu. Muombaji mkopo aliyekuwa amejitambulisha kwangu kwa jina la Mpundu Ahmed Omar akiwa na shahidi wake kama mtetezi wake ili sisi kuweza kumpatia mkopo kwa namna taratibu na sheria zilivyo katika katiba ya TUMIKI shahidi huyo aliyekuwa akiitwa Jeshi Mkwasi Msophe. Bwana Mpundu Ahmed Omar alihitaji apatiwe shilingi millioni mia moja na ndugu. Mpundu Ahmed Omar alipatiwa mkopo huo wa shilingi millioni mia moja kutokana na maelezo yake yaliyokuwa yamenyooka. Fedha hiyo aliamua ihifadhiwe katika akaunti yake mpya ya kibiashara aliyokuwa ameifungua kwaajili ya mradi wake.
 Ndugu Mpundu Ahmed Omar aliahidi mbele ya shahidi wake ambaye ni Jeshi Mkwasi Msophe kwamba fedha hii atakayopewa alikuwa na mpango wa kuanzisha mradi wa kilimo cha ufuta na ufugaji wa kuku wa kienyeji na kisasa. Ndugu Mpundu Ahmed Omar pindi nilipomuuliza kwamba je fedha hii unayopatiwa ukishindwa kuirudisha nini kitakuwa kifaidishi kwetu?. Majibu aliyonipatia ndugu Mpundu Ahmed Omar alijibu bila wasiwasi kabisa yaani bila kusukumwa na mtu yeyote mbele ya shahidi wake ambaye ni Jeshi Mkwasi Msophe. Ndugu Mpundu Ahmed Omar alisema kwamba. Ninanukuu. Alisema. Kitakachokuwa kifaidishi kwenu ni nyumba ambayo inaghorofa mbili yenye ukubwa wa nusu heka. Alimaliza nukuu ile kisha akasema. Alitoa vithibitisho dhahiri vya kuweza kuonesha nyumba hiyo. Ambapo alionesha picha ambazo alikuwa amepiga sehemu mbalimbali za nyumba hiyo. Nilimuuliza kwamba je nyumba hiyo ni ya kwake pekee au laaa?. Ndugu Mpundu Ahmed Omar alinijibu kwa urahisi kabisa mbele ya shahidi wake bwana Jeshi Mkwasi Msophe kwa kusema kwamba nyumba hiyo ni yao yaani mke na mme. Baada ya ndugu Mpundu Ahmed Omar kusema hivyo na kukiri kabisa mbele ya shahidi wake ndugu Jeshi Mkwasi Msophe nilimpatia fomu ambayo aliweza kujaza taarifa zake zote na kuweza kuandika saini yake kama fomu hii ikiwa ndiyo kama mkataba inavyoonekana. Baada ya kumaliza taarifa zote nikawa nimezikubali na kuzipitisha kupelekwa fomu ile kupigwa muhuri na mtu anayegawa mikopo ndugu Hilarry Kikuyu kwa tarehe tajwa hapo juu. Baada ya hapo ndugu Mpundu Ahmed Omar alipatiwa mkopo wake wa shilingi milioni mia moja na kuwekewa katika akaunti yake aliyofungulia jina na kuiita Mradi Mixture. Riba yake ilikuwa ni asilimia thelathini ambapo alitakiwa alipe ndani ya miezi sita ikiwa ni fedha tathilimu. Lakini kufikia leo na muda huu hakuna marejesho yoyote yaliyofanyika kupitia mkopaji huyu. Mpaka hapo nitakuwa nimeshafikia mwisho wa maelezo yangu kuhusiana na suala hili. Shukuranini sana kwa kuweza kunisikiliza kwa umakini. Nimkaribishe muongozaji aweze kumkaribisha muamzi mkuu wa TUMIKI. Alisimama na kusema hivi.
Shukurani sana dada Ruhya Max kwa maelezo uliyoyatoa kabisa yanajitosheleza kabisa. Basi nisiongee sana kwasababu sina budi ya kumkaribisha muamzi mkuu wa taasisi yetu. Ndugu Hillary Kikuyu ambaye ndiye muamuzi mkuu wa TUMIKI tawi la Arusha. Alisimama na kusema.
“Aaaa nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwa maelezo yaliyotolewa kwa umakini kabisa na msikilizaji mkuu kwa watu wanaokuja kuomba mkopo hapa TUMIKI katika tawi letu la Arusha. Pia nipende kumshukuru sana kwa maelezo mazuri sana ambayo msikilizaji mkuu Bibiye Ruhya Max ameweza kuyatoa kwa ufasaha kabisa na kuweza kunipa mimi utafakuri mzuri wenye amuzi moja tu. Nisiwe na maongezi mengi sana katika jambo hili bali niseme tu kuanzia tarehe ya kumi na tano ya mwezi huu nyumba hiyo iliyowekwa rehani iliyokuwa ikimilikiwa na ndugu Mpundu Ahmed Omar pamoja na mke wake Nura Kerima itaanza kupigwa mnada. Kwasababu nyumba hii inavyoonekana ni ya zaidi ya shilingi milioni mia moja. Kwahiyo kinachohitajika hapa ni gari letu la matangazo liwe standby muda wowote tu kwa tarehe hizo kazi ianzwe. Shukurani sana sote tuliowasili katika kikao huko. Alimaliza maongezi yake. Mwenyekiti wa kikao kile alisimama ambaye ndiyo alikuwa muongozaji kisha akawa amelishukuru jopo lile lililokuwa ni jopo la watu kumi. Baada ya hapo basi mwenyekiti aliweza kuruhusu watu wakaendelee na shughuli nyingine za kiofisi.


Ikiwa ni mishale ya saa kumi usiku paliweza kutokea janga kubwa sana katika moja ya nyumba ambazo walikuwa wakiishi wapangaji wa Nura. Katika eneo hilo kulikuwa na vyumba kumi ambapo ni huko huko maeneo ya Njiro. Nyumba hizo zilikuwa zimejengwa vizuri sana hata kodi walizokuwa wakilipia ilikuwa ni ya bei ya juu kidogo. Nyumba zote hizo Nura ndiye aliyeachiwa za urithi kama namna wazazi wake walivyokuwa wameongea kipindi cha uhai wao. Lakini mwisho wa siku nyumba hizo zilikuwa ni kama balaa kwa Nura. Kwasababu kwa muda huo ikiwa ni mishale ya saa kumi usiku nyumba iliyokuwa yenye vyumba kumi paliwezakutokea mlipuko wa moto katika eneo hilo na inavyoonekana moto huo ni watu kabisa ndiyo waliweza kuwasha. Kwahiyo baadhi ya wapangaji ambao walikuwa ndani hapo na ambao walifanikiwa kuokoka katika janga hilo la moto ndipo ikabidi wampigie simu huyo Nura. Wapangaji waliofanikiwa kutoka wengine wakiwa wamejifunika mashuka tu wengine wamevaa nguo za kulalia tu huko na wengine wamevaa bukta tu kwa wale wavulana na hata baadhi wa wanawake na wasichana ambao walikuwa ni moja ya wapangaji wa nyumba hizo. Watu walipiga ukunga sana ili tu kutaka kupatiwa msaada.
Muda huo huko katika kaya za watu wengine yaani za majirani ni wachache sana hadi muda huo ni wachache sana walikuwa wakielewa nini kabisa kinachoendelea huko. Kuna mpangaji anaonekana anampigia simu Nura. Mpangaji huyo yeye amevaa suruali yake kwa namna anavyoonekana ana mke na watoto kabisa. Kwasababu kuna watoto wawili yuko nao hapo wa kike na wa kiume pamoja na mke wake. Basi Nura anaonekana yuko kitandani tena anaonekana yuko na mwanaume katika kitanda hicho. Mwanaume huyo ndiye ambaye alisikia simu hiyo. Basi mwanaume huyo ilibidi amuamshe Nura na kumwambia hivi.
Nura.
“Yuko kimya tu.
Nura amka.
“Yuko kimya tu.
Nura inuka simu yako inaita
Nura alivurumbuka huku akiwa amejifunika shuka kubwa kisha akasemakwa. Ninga nani anapiga usiku huu?. Alitaja jina la mwanaume yule aliyekuwa amelala naye ambaye anaitwa Ninga.
Sielewi ni namba mpya tu
“Sasa kama ni namba mpya kuna haja gani ya kupokea usiku huu?. Hujui inaweza ikawa hata ni jinni!. Embu lala bana. Alijifunika shuka.
Pokea bana Nura huwezijua huyu mtu ana malengo gani. Si kila namba mpya ni mbaya kwako.
Eeee bwana eeeee embu niache mimi nilale. Mimi siwezikupokea simu ambayo ni namba mpya kwangu.
Nura si kirahisi rahisi tu hivyo.
Wewe Ninga mimi hii namba mpya alafu usiku wote huu embu niache.
Kwahiyo nipokee mimi au?.
Unapokea kwani simu yako hiyo?.
“Hapana. Lakini wewe si unaogopa kupokea?.
“Ndiyo maana nakwambia hivi simu si ya kwako Ninga jamani hunielewi kabisa?.
Sawasawa
Nura alijifunika gubigubi na kisha akalala na simu ikawa imekata. Mpangaji yule akawa analalamika kwanini Nura hapokei simu lakini hakuwa na majibu yoyote. Sauti za ukunga zilizidi kuongezeka eneo lile kisha mpangaji yule akawa amempigia tena simu Nura. Kwa muda huo ikabidi Nura apokee simu huku akiwa na hasira kwelikweli japokuwaa hakuwa anajua simu ile ilikuwa ikihusu nini. Alipopokea tu alikutana na makelele yaliyokuwa yakitokana na kunga zilizokuwa zikiendelea pale. Alishtuka sana kwa sauti zile kisha akawa anasubiria taarifa gani anapewa kutoka kwa mtu huyo. Taarifa ambayo alipewa ilikuwa ni taarifa ya moja kwa moja ya nyumba iliyo na wapangaji pale Njiro imeungua. Kwakweli aliweza kushtuka sana na kuanza kuamka harakaharaka huku akiwa amevaa nguo ya kwanza kuvaliwa na ya mwisho kuvuliwa huku kifuani nako pakiwa pamebanwa vizuri. Pengine pote palionekana hapajasitiriwa kabisa. Alivaa nguo harakaharaka huku akiwa anamuambia Ninga kuwa ainuke na watoke nje sababu nyumba yao imeungua. Ninga alimwambia kwamba apige simu kwenye kitengo cha zima moto lije bali Nura kwa muda huo hakuwa hata anamsikiliza mtu alikuwa tayari ameshachanganyikiwa kabisa. Alishuka haraharaka huku akiwa amevaa suruali na tisheti nyeusi na kwenda haraka haraka huku akiwa anamwambia kuwa mlinzi afungue geti harakaharaka. Nura wala hakuwa na muda wa kutafuta kitenzambali kabisa. Nura akiwa na haraka zake aliwasha gari aina ya NOAH na kuanza safari. Alipita pale getini hadi mlinzi mwenyewe akawa ameshangaa nini kabisa kimemkuta Nura. Hakuelewa kabisa kilichomkuta Nura. Ninga alipotoka na kuanza kumuita Nura na mlinzi akawa amemwambia kuwa Nura ameshatoka yuko nje huku. Ninga alisimama hapo nje kisha akawa anasema.
Yaani huyu demu ameshachanganyikiwa kabisa mbona ameniacha sasa hapa?. Ila   mimi naye ni fala unajua. Huu ni kama msala kabisa huyu demu hapa ataanza kunibebesha mzigo. Mimi hapa japokuwa nilikuwa sina mpango wa kwenda Dar es salaam leo acha mimi muda huu huu nijiandae niondoke zangu japokuwa nilitaka kusafiri wiki ijayo hapa sitaki msala hapa. Huu utakuwa ni undugu lawama kabisa. Nikishamaliza tu naenda stendi nasuburi gari la saa kumi na mbili la kwenda Dar. Maana hili janga naona kwangu litakuja kuwa gumu sana. Ninga alirudi ndani na kwenda kujiandaa. Alipokuwa akijiandaa alikuta fedha nyingi sehemu ambapo ndiyo Nura huweka fedha zake. Alipoangalia vizuri fedha zile zilizokuwa zimefungwa kwa mafungu mafungu zilikuwa ni kiasi cha shilingi lake saba. Akawa anasema haachi hata mia anaondoka nazo.







SURA YA TISA
Basi huko kwenye nyumba za Nura moto ulizidi kushika kasi kwa kaweli msaada ulikuwa ni mgumu sana hata wa majirani. Kwasababu hamna hata maji ya kuweza kusema uzime moto. Kwasababu kwanza eneo hilo lina vyumba vingi sana. Hivyo basi ikawa inawafanya watu washindwe hata ni wapi pa kuanzia na hata wapi pa kusimamia tu. Hapo nje zikawa zinasikika sauti tu za wale wapangaji pale wakiwa wanalia tu. Kuna mpangaji alikuwa ni wa kiume ni kama kijana tu hivi. Aliuliza swali kwakusema.
Hivi kwanza hao fire wamepigiwa simu kweli au tunasubiri tu nyumba imalizike kuwaka natuchukue screpa zetu?. Kuna mpangaji alikuwa pembeni ya kijana aliyeuliza swali. Mpangaji huyo alikuwa ni wa kike akawa anasema. Yaani wewe kaka usiende mbali sana huko kwenye mambo ya fire. Haya kwanza huyo mwenye nyumba kwani amepigiwa simu hadi muda huu?. Huku akiwa amejifunika na shuka aliloliokota wakati akikimbia. Kijana yule alijibu kwa kusema. Kuna mtu nilisikia anaongea naye hapa mida mida hivi.
Akaambiwaje?.
Sikujua kilichokuwa kimeendelea.
“Kwahiyo tuseme huna uhakika kabisa?.
Ndiyo. Kuna mpangaji mwingine alikuwa wa kiume akawa anasema hivi. Sasa nyiye hata tukimsubiria huyo mwenye nyumba atatusaidia nini?. Mpangaji mwingine wa kike akasema hivi. Chochote kile. Kwasababu yeye ndiye mwenye nyumba.
Lakini ujue sisi ndiyo wapangaji kwenye hizi nyumba.
Sasa tufanyaje kwa mfano?.
“Ni bora kuwapigia simu hao fire tu hapa waje. Hapa hatuna namna kama ni maji ndiyo kama hayo yako huko ndani. Ndoo zimeungua zote huko ndani. Wewe unafikiri utazima na nini?.
Una namba zao?.
Sina hapa.
“Wewe hata ungekuwa nayo usingeweza kuwapigia na kujieleza vizuri hadi wakuelewe vizuri. Ohooooo haya. Mpangaji mmoja hivi alikuwa ni mwanamama anavyoonekana amekula chumvi kidogo. Hapo alikuwa yuko na watoto wake. Mwanamama huyo kavaa dera na huku watoto wake wakiwa wote ni wa kike walikuwa wamejifunika kanga tu. Alikuwa analia sana huku akipiga ukunga na kusema hivi. Uwiiiiiiii… wanangu Eeeee tutaenda wapi leo hii uwiiiiiii eeeee mungu eeeeee tusaidie. Kuna kijana ambaye na yeye ni mpangaji wa nyumba hiyo akasema hivi. Sasa mama unavyomuomba mungu na tumesimama huku mbali hivi tunaangalia tu nyumba zinavyowaka moto kweli hapo kuna mafanikio kabisa?. Mama yule alimjibu kijana yule kwa kumkaripia kwelikweli kwakusema. Kwahiyo wewe ulikuwa unatakaje wewe kijana?  au wewe ndiye uliyewasha moto hapa nini?.
“Weeeeee mama tuheshimiane kabisaaa tena shika adabu yako. Yaani mimi na akili yangu nichome vitu vyangu kabisa sinitakuwa na kichaa kabisa.
“Kwanza hapo inavyoonekana hapo ni kama una kichaa kabisa.
Mama embu tuheshimiane. Tulia kwanza niondoke hili eneo tu hapa usijeukaniletea balaa bure. Mpangaji mwingine ambaye alikuwa ni kijana hivi yuko na jamaa yake naye alikuwa wa kiume alimuuliza. Kwani station ya Fire ni mbali sana?.
Ndiyo iko mbali si kule mjini ila mimi nimeshawapigia simu fire wanasema wanakuja sasa. Watu waliendelea kujipa moyo wakiwa wanangojea gari la zima moto lile.
Baada ya muda kupita kabisa ndipo gari la zima moto likawa limeshawasili kwenye tukio hilo la moto. Basi walifika hapo gari lao likiwa bado ving'ora vikiwa vinapiga makelele. Wafanyakazi wake walishuka na kwenda kuangalia namna kweli nyumba ile ilivyoungua. Baada ya kushuka wale wapangaji wakawa wanajua wamepata hata ahueni kidogo ya kuweza kuokoa vitu vyao ambavyo viko huko ndani. Lakini cha kushangaza askari wale wa zima moto walisema kwamba gari halina maji hata kidogo kwahiyo inawaladhimu wao waende sehemu ambayo ina maji ndipo wajaze maji ndipo waje kuzima. Kwakweli wapangaji wale waliingiwa na hasira sana vichwani mwao. Kwahiyo hadi tena wale wapangaji wakaanzisha varangati la kuwapiga wale askari wa gari la zima moto. Askari wale walipoona wamezidiwa haraka haraka walirukia gari lao na kuweza kugeuza na kuwaacha wapangaji wale wakiwa wameduwaa tu.
Nura alijitahidi kuendesha gari kwa kasi sana ili kuweza kuwahi huko lakini akiwa hajui kama gari la zima moto limefanya mambo yasiyo ya kufanywa kabisa. Huku njiani simu yake ilikuwa ikiita kila sekunde. Yaani ikate hii na iingie hii ndivyo ilivyokuwa na hakuwa ana uwezo wa kupokea simu kabisa kwa wakati ule. Basi gari lile alilikimbiza kama vile ni mchana. Alipokaribia na maeneo ambayo nyumba zake na kuona ni kweli kabisa nyumba zinawaka moto hapo alizidisha mwendo mkali sana. Alifika sehemu fulani hivi ambapo kuna kona hivi na upande unaofuatia huko palikuwa na gogo kubwa hivi la mti ambalo kwa mishale ya mchana watu hupumzika maeneo hayo yaani hupafanya eneo hilo kama kijiwe chao cha kunywea kahawa na kupiga zoga. Nura alikunja kona akiwa katika mwendo kasi zaidi kwa mwendo kasi ambao alikuwa nao na namna alivyokunja tu kona aligonga gogo hilo na gari lile likawa limepinduka vibaya na kuanza kubiringita na kubiringita takribani mara nne kutoka lilipoangukia. Ilisikia sauti ya Nura akiwa ndani ya gari sauti ikisika kwa mbali akisema. Uwiiiii Nuruuuu nisaidie nakufa kama kifo cha wazazi wanguuuuuu!”.
Kwakweli siku hiyo nafasi ya Nuru kwa Nura ndipo ilipoonekana. Kwa sababu inavyoonesha ni kwamba Nura humpenda Nuru sana kwa wakati wa shida tu. Ila kwa wakati ambao si wa shida Nura humuona Nuru kama msalani panavyonuka wakati tukianza kuendesha. Alimkumbuka Nuru baada ya kuingia katika majanga ya kupata ajali ile.
Sauti ile ya gari kuanguka iliweza kusikika hata na majirani na pia hata kwa wale wapangaji walisikia mshituko ule wa gari. Muda huo tayari mishale ya kuelekea saa kumi na moja alfajir ilikuwa imeshakaribia. Kwa sauti ya muanguko ule walijiua kabisa huyo dereva hatokuwa amepona kabisa. Mwingine anasikika akisema hivi. Mbona ile gari ni kama vile gari ya mwenye nyumba!. Mpangaji ambaye ndiye aliyekuwa amempigia Nura anamjua vizuri. Kwahiyo alipoangalia gari lile akajua kabisa ni gari la Nura. Muda huo taa zimewaka katika kona za nyumba za majirani. Pia wanakaya wa nyumba ambapo Nura kaangukia hapo walianza kutoka nje baada ya kusikia mshituko ule na pia kusikia watu wamejaa hapo nje. Mtu yule ambaye alimpigia simu Nura muda huo ameshafika hapo kwenye tukio akawa anasema kuwa.
“Jamani hii ndiyo gari ya mwenye nyumba. Jamani eeeee tufanyeni mpango tunyanyue bana hili gari. Ili tujue huyu mtu hapo ndani yuko hai au vipi jamani. Muda huo kuna mpangaji akajitokeza akisema. Unajua wewe mzee unazingua kweli kweli.
Nazingua nini tena.
“Kwahiyo tuache nyumba zinawaka moto kule na vitu vyetu vinaungua alafu tunahangaika hapa.
Siyo hivyo jamani umoja ni mshikamano na utengano ni udhaifu. Embu fufanyeni kweli bana. Kwa sababu kule ndiyo hivyo tumeshindwa.
Ila unazingua kweli kweli
“Jamani eeee tunyanyueni bana hili gari. Wengine huku na wengine kule jamani tuinueeee. Watu walilizunguka gari lile huku na kule ndipo wakaanza kuinua wakisema.
Umoja eeeeeeeee
Nguvu eeeee.
“Twendeeee”. Kweli waliweza kuonesha umoja na mshikamano wa kunyenyua.
 Walinyanyua gari lile kwa umoja na mshikamano hadi wakawa wamelisimamisha. Baada  ya kulisimamisha tu gari lile wakawa wanalazimisha sasa namna ya kufanya ili kuweza kufungua vioo na kuweza kisha wakataka pia kumjua aliyepo ndani atakuwa ni nani?. Hekaheka za kufungua mlango ule zilifanyika hadi wakawa wamefanikisha kufungua kioo na kuweza kumtoa mtu aliyekuwa ndani ambaye ni Nura. Walimkuta tayari akiwa amezimia kwa namna tu jinsi mshtuko wa gari ule ulivyokuwa. Ni bahati sana alikuwa amejifunga mkanda vizuri ndiyo maana hata hakuweza kuumia bali tu ni alipoteza fahamu. Aliumia sana sehemu za usoni na mpangaji wa kwanza akasema hivi.
Mbona ni kweli ni ndiye mwenye nyumba huyu. Basi watu walifanya juu chini na kuweza kubaini kuwa alikuwa ni Nura. Ndipo walipofanya namna ya kuanza sasa kumpeleka Nura hospitali. Kwasababu japokuwa lile gari lilianguka sana lakini si kwamba lilishindikana kuwaka. Baadhi ya wanamama waliweza kupanda lakini kwa wengine waliona ni bora washuke tu sababu kazi ya kukaa na mgonjwa mahututi vile inahitaji moyo sana.
Wapangaji waliweza kuchanganyikiwa sana kwa kutojielewa je waanze wapi, waende wapi na wamalizie wapi?. Nyumba zile zilizidi kuungua sana japokuwa watu walikuwa wameshawasili wengi sana. Lakini hamna chochote walichofanikisha kuokoa. Nyumba kama ni kuwaka moto ziliwaka sana na kutokubakiza chochote kabisa pale. Wapangaji wengi walibaki wakiwa wanazunguka tu hapo nje ya nyumba zile zilizoungua huku vichwani mwao pakiwa kila mtu mawazo yakiwa yamemjaa kwamba itakuwaje tena katika kwenda kuanza maisha?.  Kwasababu watu nguo zao, vitanda vyao, runinga zao na vitu vingine kadhalika viliweza kuungua vyote. Kwahiyo hawakuwa na namna yoyote ndipo akawa amejitokeza mwenyekiti wa eneo hilo na kuanza kuongea na wapangaji hao pia na watu wengine waliokuweko pale. Muda huo mwenyekiti anaonekana akiwa amesimama mbele ya wananchi wake huku akisema hivi.
“Nichukue nafasi hii kukupeni pole kwa jambo ambalo limewakumba kwa namna ambavyo hamkuwa mnafikiria kama kweli hili jambo linaweza kujitokeza. Mimi kama mwenyekiti roho imeniuma sana kwa namna wananchi wa mtaa wangu katika nyumba hizi kwa janga lililowakuta. Ni kitu kinachoendelea kunisononesha sana kwamba ni namna gani mtaanza kwenda kuyaanza maisha. Kwasababu unakuta tayari mwingine alikuwa ameshaanza kabisa hata kujipanga ili ajenge nyumba yake kabisa alikuwa ameshaandaa vitanda na makochi kabisa. Roho inazidi kuniuma sana kwa wale ambao wana watoto wanaohitajika kwenda shule sijui sare zao za shule zitakuwa kama zimebaki. Ni jambo la kumshukuru mungu kwamba hadi muda huu hatujapata taarifa yoyote ya kusema kwamba kuna mtu amefarifiki. Basi tusibaki katika kuweza kusononesha roho zetu sana cha msingi kwa sasa kwa wananchi wengine. Jamani tunakuombeni tufanye mpango wa kuweza kuwasaidia hawa wenzetu waliokumbwa na janga hili. Tufanyeni juu chini hadi tuweze kuwafanya angalau nao hata warudishe furaha zao. Kwahiyo ninachokuombeni jamani cha kufanya kuanzia sasa ninakuombeni kama una chochote kilete hapo nyumbani kwangu mimi kama mwenyekiti ndipo nitaanza kufanya ni namna gani hawa watu wataweza angalau hata kula na kuvaa kwa siku ya leo. Niseme pia katika imani wanasema kwamba kazi ya mungu haina makosa au mipango ya mungu haina makosa. Lakini mimi kama mwenyekiti wa mtaa huu nitafanya juu chini pia ili kuweza kubaini chanzo cha moto huu kuweza kuunguza vyumba vyote hivi. Kwa watakaoshikwa naapa lazima sheria ifuate mkondo wake. Kwahiyo mimi kama mwenyekiti wa mtaa huu nitakuwa nanyi bega kwa bega katika jukumu hili. Nimalizie kwa kusema kuwa mungu akutangulieni katika mahitaji yenu.
Baada ya mwenyekiti kuongea vile kwa kweli kwa wahanga wa janga lile walifarijika sana kwa kiongozi wao kuweza kuwapa ule moyo wa matumaini. Basi wananchi wengine walirudi majumbani kwao na wengine wakawa wanawaangalia marafiki zao waliokutwa na janga hilo ili kuweza kutafuta namna ya kuwasaidia hata kuwachukua wakaishi wote tu.
Ninga aliweza kufanya michakato haraka haraka na kuweza kuondoka pale pia huku akiwa ameondoka na kiasi kikubwa tu cha fedha ambayo aliikuta pale mezani. Kwa ujumla tangu Mpundu kuondoka Nura ndiyo aliamua kumtafuta Ninga ambaye alikuwa rafiki yake hivi ndipo akawa naye pale nyumbani. Ninga kwa Arusha alikuja tu kwa shughuli zake binafsi ndipo alipowasiliana na Nura kisha Nura akamuambia aje kwake akae hata siku chache tu hivi ndipo aondoke. Lakini Ninga alichokishanga ni kwamba Nura alikuwa akitaka sana Ninga abaki pale. Kwahiyo akawa amemlewesha kwa kumwambia kuwa atampatia fedha kama akiwa anaishi naye cha msingi aweze kumfurahisha kimapenzi tu.


Ni siku nyingine kabisa ambayo ndiyo iliweza kuharibu kabisa maisha ya Nura. Kwakweli siku hiyo ilikuwa ni kama siku ya hukumu kwake. Siku hiyo ikiwa ni mishale ya saa mbili asubuhi tayari barabarani panasikika mtu akiwa kwenye gari na kipaza sauti. Sauti hiyo ilikuwa ikisikika hivi.
MNADA MNADA MNADA
Tunawakaribisha katika mnada wetu. Mnada huo ni mnada wa nyumba iliyopo maeneo ya Njiro kwa msola. Nyumba hiyo ina ghorofa mbili zenye kila aina ya maurembo huko ndani. Kila kitu ni ndani kwa ndani. Mnada huo utaanza kufanyika leo leo hii kuanzia mishale ya saa nne asubuhi. Bei ni kuanzia shilingi milioni mia tano. Kwahiyo changamkia nafasi hii.
Nura alizidiwa sana kwa ajali ile ambayo aliipata hadi akafanyiwa uhamisho wa kimatibabu kutoka katika hospitali ya Mount Meru ya Jijini Arusha na kupelekwa hadi katika hospital ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro wilayani Moshi. Aliyekuwa anamsaidia kwa kuweza kufanya uhamisho ule ni yule yule mpangaji ambaye aliyekuwa amempigia simu Nura kwa kumjuza kuhusiana na nyumba kuwaka moto. Kwasababu walipofika Mount Meru hospital kwa namna alivyokuwa ameumia alionekana kabisa kuwa hatoweza kufanyiwa matibabu labda kupatiwa huduma ya kwanza. Ndipo AMBULACE ilipoletwa na kupakizwa ndani ya pale na msafara wa kwenda KCMC ukawa umeaanza bila kutegemea.
Ni mishale ya saa nne asubuhi hivi tayari jumba hilo la kifahari lilikuwa limeshazungushiwa mikanda ya makatazo kwenye ukuta paliandikwa kwa maandishi ya makubwa yaliyokuwa yakisomeka hivi.
N
YUMBA HII INAUZWA NA TAASISI YA UTOAJI MIKOPO YA KIBIASHARA (TUMIKI) KUTOKANA NA MKOPAJI AMESHINDWA KULIPA DENI LA FEDHA ALIZOKOPA NA TAYARI MUDA UMESHAKWISHA. KWA MAWASILIANO ZAIDI TUPIGIE SIMU NAMBARI. 0783372139.
Kwa muda huo kila mtu anayepita hapo na kusoma maandishi yale kwakweli alikuwa akisononeshwa sana rohoni mwake bali pia kuna wengine ndiyo walikuwa wakifurahi kabisa hapo kwa namna nyumba hiyo inavyopigwa mnada. Hadi inafika mishale hiyo ya saa tano asubuhi tayari matajiri walikuwa wameshajaa katika eneo hilo la kwenye jumba hilo la kifahari la Nura ambalo aliachiwa kama urithi na wazazi wake. Hadi muda huo kwa kweli Nura bado yuko katika hospital ya KCMC huko Moshi na bado hajitambui kabisa. Muda huo panaonekana mtangazaji wa bei pale akiwa ameshika maiki akisema hivi.
“Jamani! Mabibi na mabwana huu ndiyo ule muda ambao tulikuwa tukiusubiri kwa hamu sana. Nyumba hii tunayoiona hapo ndiyo ambayo mkopaji aliahidi kwamba itakuwa kama kifaidishi kwetu. Kwahiyo nitaanza kupanda na kushuka dau hadi mwisho wa siku ni mtu mmoja tu ndiye atakayefanikiwa kuchukua nyumba hii. Haya wale wa million mia tano wako wapi?.
(Kimya).
Basi kama kimya kimetawala inamaanisha tushuke au siyo?. Walipokelea kwa sauti kubwa kwa kusema. Ndiyoooooooooooo. Zilikuwa ni sauti za kitajiri.
“Sawasawa. Haya wale wa milioni mia nne hadi mia tatu wakooo?. Alijitokeza mmoja wa milioni mia nne akasema hivi. “Wa milioni mia nne niko hapa.
“Haya jitokeze mbele.
Sawasawa. Alijitokeza mbele pale akionekana kweli kama ni pesa anayo kabisa. Kwa sababu hata sura za matajiri kwa ujumla huo zinaonekana kwa namna hata mtu alivyo. Tajiri aliyejitokeza pale mbele alikuwa na kitambi kama msanii mmoja hivi wa HipHop na weusi wake ule ndiyo walifanana moja kwa moja kasoro yule tajiri hakuwa na ndevu.
“Jamani wanaTUMIKI mpigieni makofi na vigelegele huyoooooo wa milioni mia nne. Kweli wanaTUMIKI walimpigia makofi yule jamaa kwa kuwa tayari wamesharudisha fedha yao ya kutosha hadi hapo. Basi mnada ule kuisha kwake ni pale pindi tu yule jamaa wa milioni mia nne alipojitokeza. Kwasababu hakujitokeza mwingine juu ya hapo ili washindane. Walimchukua na kisha wakampeleka sehemu maalumu kwaajili ya kufanya mazungumzo ni namna gani ya kufanya malipo na kupatiwa vitu vingine vinavyohitajika.
Ni siku hiyo hiyo mishale ya saa mbili usiku duka la Nura lililopo makao mapya ambalo Nuru alikuwa akiuza nalo lilichomwa moto na kikosi ambacho kilikuwa kimeshapangwa na Mpundu kabla hajasafiri kwenda Marekani. Muda huo hapo katika duka hilo panaonekana watu wamejaa sana na moto umewaka kila kona. Japokuwa watu wamejaa lakini ndiyo hivyo hawana nyenzo yoyote ya kuweza kuuzima moto ule. Kikubwa walichokuwa wakisubiri ilikuwa ni gari la zima moto walilolipigia simu. Inasikika sauti ya gari la zima moto likiwa katika mwendo kasi kweli kweli ving'ora vikiwa vimetawala maeneo hayo. Zima moto lile likiwa katika mwendo mkali sana lilipofika maeneo ya posta wakati wa kukunja kona lilianguka na kubiringita kabisa na kusababisha tena ajali kwa magari mengine. Kwa kweli ajali ile iliweza kuleta maafa makubwa sana kwa daladala ambazo zilikuwa na abiria. Pia waliokuwa maeneo ya sheli nao waliweza kukutana na majanga makubwa sana. Kwahiyo ikawa ni ajali juu ya ajali.
Watu waliweza kusubiria sana kuwa zima moto lije lakini wala hawakuona mafanikio yoyote bali walizidi kusikia tu sauti ya kingora ikiwa imekata. Ndipo watu walipoanza kutafuta namna tena ya kuanza kuokoa majeruhi na watu waliokuwa wamefariki kutokana na ajali ile. Kwakweli ajali ile ilisababisha vifo vya watu wengi sana kuliko majeruhi. Abiria na madereva waliokuwa kwenye daladala waliaga dunia na wengine ikawa hata ni vigumu kuwatoa huo ndani kwa namna gari lao lilivyoumia.





Huko dukani kwa Nura watu waliendelea kutafuta namna ya kuweza kuuzima moto. Kwakweli akili za mwanadamu hufanya kazi panapotokea tatizo fulani lakini ni hadi mtu huyo aamue. Kilichotokea pale katika harakati za kuzima moto watu walifanya kila njia hadi moto ukawa umezima. Walijaribu maji na hata walipoona mahali kuna mchanga walichukua na kwenda kupamwagia na moto kuanza kupungua hadi mwisho wa siku ukawa umeisha. Kwa sababu wananchi wasingefikiria njia ya kuutoa moto ule ungeweza kuwaka hata katika maeneo ya majirani ya duka lile na ingeletea madhara makubwa sana.
Muda huo huo kwa maeneo ya Shule ya sekondari ya Sinoni maeneo ya uwanjani panasikika mtu anaongea na simu. Mtu huyo sura yake kwa keli ni vigumu sana kuweza kumuona na kuweza kumtambua je ni mvulana au msichana bali kinachojulisha kuwa ni mvulana ni ile sauti yake tu. Kwa sababu eneo alilokuwa amesimama kuna giza kali sana. Mtu huyo alikuwa amevalia koti jeusi likiwa linamfika kwenye miguu chini kabisa huku akiwa amevaa buti iliyokuwa ikionesha kabisa ilikuwa ni ya kazi. Akiwa anatembeatembea alipigiwa simu na baada ya kuangalia alikuta aliyempigia simu lilikuja jina lililohifadhiwa kama Mpundu. Mtu yule aliangalia kushoto kulia nyuma na mbele kisha akapokea simu. Walifanya maongezi ya hapa na pale na maongezi yao yakawa yameonesha dhahiri kuwa Mapunda ndiye aliyekuwa amepanga njama ya kuchoma moto duka la Nura. Njama hizo alikuwa ameshapanga kabla hajaondoka yaani kuelekea huko Marekani. Mpundu alifurahi sana alipomsikia jamaa yule akiwa anamwambia kuwa misheni zote alizokuwa amezipangilia zimefanikiwa kwa asilimia zote. Yule jamaa alimtaarifu Mpundu kuwa yamebaki maduka yaliyoko pale Njiro kwa Msola na maduka mawili yaliyoko maeneo ya USA RIVER. Ambapo alimuahidi haitopita wiki moja maduka hayo lazima yatakuwa yamechomwa na mtu huyo akiwa yeye ndiyo kiongozi wa kikundi hicho. Pia Mpundu alimueleza jamaa huyo madhumuni yake ni kuwa anataka kumfilisi kabisa Nura yaani Mpundu anataka kumaliza kabisa kizazi cha Nura kiuchumi. Pia Mpundu aliweza kumuahidi jamaa yule kuwa kwa kazi kubwa waliyokuwa wameifanya na kikundi chake basi ataweza kuwapatia kiasi kikubwa cha fedha. Mpundu alimuasa sana jamaa yule kuwa akija kumpatia fedha yule jamaa na kweli awapatie wana kikunbdi wenzake fedha bila kuwapunja. Kwa sababu alisisitiza hivyo akijua kuwa wakipunjana tu lazima mmoja wao atakuwa na kiroho mwisho wa siku mikakati yote itavujishwa na tayari wataingia matatani. Basi baada ya kumaliza mazungumzo yao Mpundu alikata simu na kisha mtu yule akawa anaangali pande zote kama kulikuwa na mtu yeyote anamsikiliza. Alipojua kuwa hakuna aliyekuwa akimsikiliza aliweza kuondoka akiwa anaelekea maeneo ya mjini.


Ni siku iliyofuatia asubuhi na mapema habari magazetini ni kuhusu kuwaka moto maduka na nyumba za Nura. Magazeti mengi kwa mbele yalikuwa yametandaza habari hiyo ikiwa na picha za nyumba na duka kubwa la Nura. Pia habari ikiwa imekolezwa kabisa ikiwa imeambatanishwa na picha ikisema kuwa.
SIMANZI!
JUMBA LA KIFAHARI LA BILIONEA KERIMA LAPIGWA MNADA. Uk wa 5
Kwa siku ile wauza magazeti waliuza sana magazeti kwa kuwa watu walikuwa na viroho sana vya kusoma habari hiyo. Watu walijaa sana katika maeneo hayo hadi wauza magazeti wakawa wanachanganyikiwa ni yupi kachukua na katoa shilingi ngapi.
Ilipowadia mishale ya saa tano asubuhi tayari Nura alikuwa ndiyo anawasilishwa hapo maeneo ya nyumbani kwake. Muda huo hawakuwa na gari ambayo alipata nayo ajali bali ni dereva tax tu ndiye aliyekuwa amemleta akiwa na yule jamaa ambaye alimpigia simu Nura kumpeleka. Kwa sababu siku ambayo Nura alifikisha katika hospitali ya Mount Meru baada ya kuonekana anatakiwa asafirishwa mpangaji aliyekuwa naye aliweza kumpigia rafiki yake aje kuchukua gari lile na kulipeleka gereji na malipo yatafanywa wakirudi.
Kwa ujumla hadi muda huo simu karibia zote za Nura zilikuwa zimezimwa na aliyekuwa amemshikia simu zake ni huyo huyo aliyempeleka hadi hospitali ya KCMC huko Moshi. Mpangaji huyo ana familia kabisa ya watoto wa nne lakini hadi muda huo kwa yeye naye alikuwa bado hajaelewa watoto wake wanaendeleaje na mama yao huko waliko tangu siku hiyo janga la moto lilipowakuta. Mara nyingi sana huitwa Baba Filipo. Lakini kilichomshangaza kabisa Nura ni baada ya kuona maandishi yale ambayo yalikuwa yameandikwa ukutani pale. Nura akiwa bado kama ana mawenge kidogo hivi katika macho yake akawa amemuita Baba Filipo kwakumwambia hivi.
Baba Filipo mbona kama naota. Muda huo wamesimama hapo baada ya tax kuondoka kisha baba Filipo akawa amesema hivi. Vipi tena Nura mchana wote huu unaota tena?. Alimjibu akiwa anamuangalia Nura kisha Nura akasema. Utakuwa hujapaona vizuri wewe kabisa.
“Hapana…Umeona nini?.
“Wewe huoni haya maandishi yaliyoandikwa hapo makubwa kabisa?.
Heeeeee nini tena. Alishangaa na kuanza kuyasoma.
N
YUMBA HII INAUZWA NA TAASISI YA UTOAJI MIKOPO YA KIBIASHARA (TUMIKI) KUTOKANA NA MKOPAJI AMESHINDWA KULIPA DENI LA FEDHA ALIZOKOPA. KWA MAWASILIANO ZAIDI TUPIGIGIE SIMI NAMBARI. 0783372139.
“Mbona kama sielewi hapa. Muda huo tena Nura akawa yuko hatarini kwakweli. Wakiwa wanaendelea kuongea pale tayari wanaona watu wanakuja baadhi yao wakiwa wamevaa nguo za kupaka rangi na baadhi ya wafanyakazi wa TUMIKI nao walikuwepo hapo wakiwa pamoja na walinzi na moja ya walinzi ni yule mlinzi wa Nura ambaye kwasasa amepata tenda kutoka TUMIKI. Alijifanya hamjui kabisa Nura na kusimamia kidete katika kazi yake. Walipofika pale na kuwakuta Nura na Baba Filipo wakiwa wamesimama hapo nje wakiwa wanasoma maandishi yale. Tajiri aliyenunua nyumba ile akawa anasema hivi.
“Nyiye mnasoma hilo tangazo sasa mmeshachelewa sana nyiye. Embu tokeni hapo tufute. Nura akawa anasema hivi. Unamaanisha nini unavyosema hivyo.
Tuseme hujaelewa tu siyo.
Ndiyo maana nimekuuliza.
Haya soma maandishi.
“Nimeshayasoma haina haja ya kurudia.
“Ahaaaa basi sawa aliyenunua nyumba hii ni mimi na niko hapa na wajumbe wa TUMIKI na tunataka kufuta haya maandishi.
Wewe Baba unasemaje?. Akiwa anaongea kwa hasira.
Kwani wewe umesikiaje wewe?.
Unamjua mwenye nyumba?. Anaongea huku akimuangalia mtu huyo aliyenunua nyumba.
Mwenye nyumba hayupo. Tajiri yule alijibu kirahisi tu.
“Hayupo kivipi nyiye
“Embu wewe dada wa mikopo mueleweshe huyu nahisi anajifanya kama vile haelewi. Hajui watu tunaishi hapa kwakufuata Sheria na kanuni za eneo husika. Embu mueleweshe huyu. Nyiye vijana saa za kazi njooni muanze kufuta haya maandishi hapa. Nakweli muda huo msaidizi wa msikilizaji mkuu wa TUMIKI alijitokeza pale mbele na kusema hivi.
Dada mimi naitwa Mwashabani ni msikilizaji msaidizi kutoka katika Taasisi ya Utoaji wa Mikopo ya Kibiashara (TUMIKI) tawi la Arusha. Alijitambulisha kwa makini kisha Nura akasema. Mhhh nimekusikia niambie kwanini mmeandika nyumba yangu hivi?.
Ahsante kwa swali lako zuri sana. Aaaa nanukuu alichokisema msikilizaji mkuu katika taasisi yetu ya TUMIKI na nukuu nyingine za kutoka kwa mdaiwa. Akiongea hivyo siku hiyo ilikuwa ndiyo siku ya kikao cha kuweza kutoa hukumu. Kikao hicho kilikaliwa na jopo la watu kumi. Mimi kama msikilizaji msaidizi ninanukuu. Akawa anasoma katika kijitabu fulani hivi cha rangi ya bluu. Alimsomea maelezo yote ambayo yalikuwa ni nukuu ya kilichosemwa na Mpundu siku ile akiwa anachukua mkopo. Maelezo hayo pia yalisomwa siku hiyo na Ruhya katika kikako kilichokaliwa kwa ajili ya kuelezea mashtaka ya Mpundu katika jopo la TUMIKI ambalo lilikaa ili kutoa maamuzi ya moja kwa moja. Kwa kweli hapo ndipo Nura alianza kuchanganyikiwa kabisa baada ya msikilizaji msaidizi wa Taasisi ile ya utoaji mikopo ya kibiashara kunena yote. Nura aliongea huku akiwa analia sana.
Hivi kweli kabisa ni Mpundu ndiye aliyenifanyia hivi?. Uwiiiiiiiiii siamini Mpundu kumbe ulinidanganya ukaniambia umesafiri kumbe ni kwa sababu hii kabisa. Mpundu nasema hivi ulaaniwe huko uliko. Yule tajiri aliyenunua nyumba akawa anasema hivi. Eeee bwana eee kalilie mbali kule usilete balaa hapa kwangu.
Nura akawa anasema hivi. Yaani nyumba yangu ya urithi imeuzwa kwa bei ya kijinga hivi.  Uwiiiiiiiiii nitaficha wapi uso wangu jamani eeee.
“Wewe kumbe ulikuwa unaringia mali za urithi. Sasa hapo ndiyo utajua hata kuuza maparachichi nayo ni kazi nzuri tu. Yule tajiri alimjibu kwa hasira. Kwakweli Nura alipoambiwa taarifa zile alizidi kuchanganyikiwa tu. Tena akiwa pale kuna mtu alimpigia na kumjulisha kuwa duka lake limechomwa. Hapo ndipo alipozidi kuchanganykiwa kabisa. Dakika chache baada ya kupewa taarifa zile alijikuta ameanguka na kuzimia hapo hapo. Baba Filipo akawa amejikuta kuwa amebeba tena ule mzigo. Baba Filipo akawa hana namna na akawa ameamua kuanza kumpepea Nura ili aweze kupata fahamu. Kwa sababu kwanza hadi muda huo hata fedha iliyobaki ni ndogo sana ambayo haitoweza hata kumfikisha hospitali kabisa kwa ajili ya matibabu tena. Yule tajiri wala hakujali kuzimia kwa Nura kwa sababu ya majanga yanayomkuta bali ndiyo aliendelea kuwasimamia vijana wa kupaka rangi wafanye haraka haraka ili tu tangazo lifutwe kabisa. Baada ya muda kidogo ambapo ilichukua kama nusu saa kabisa ndipo Nura akawa amezinduka. Japokuwa alikuwa amezinduka lakini bado tu hajatengamaa vizuri. Kwa sababu kila alipokuwa akifikiria hayo majanga hujikuta anazidi kuchanganyikiwa tu. Ndipo Baba Filipo akawa ameamua kumkokota hadi wakaenda kupanda Haice za kuelekea mjini na pia ndipo wakapande Haice za kwenda majengo huko kwa Babu yake Mama Filipo. Kwahiyo ikambidi tu Nura akaishi huko kwa Baba Filipo japokuwa ni kwa kujibana tu. Kwasababu hadi muda wanaondoka pale Nura alikuwa bado hajatengamaa kabisa nab ado hana nguvu za kuanza kupambana na Nura.
Ikiwa imeshapita kama wiki moja hivi kijana Mpundu alimpigia simu mkuu wa kikosi chake ambacho alikipanga kwa ajili ya kuweza kuchoma kila mali ya Nura. Muda huo ilikuwa ni mishale ya saa kumi na mbili jioni. Kijana huyo alikuwa akiitwa Mnaa anaonekana yuko maeneo ya Ungalimited akiwa na rafiki zake. Baada ya kuona simu ile Mnaa aliondoka pale na kisha akawa amesogea mahali hivi kuweza kumsikiliza Mpundu vizuri kabisa. Mpundu alianza kumuuliza Mnaa kama eneo alilokaa linafaa kufanya mazungumzo yao ndipo Mnaa alipomjibu kuwa inawezekana kabisa. Walifanya mazungumzo kama dakika tano hivi ambapo muda huo Mnaa alimjulisha maduka waliyoyachoma na kusema kuwa maduka yote yamechomwa na kubaki mali nyingine tu. Mpundu alifurahi sana kwa kupata taarifa ile na akasema kuwa kila kitu kimeshafulu ambacho alikipangilia akiwa Arusha baada ya kuhakikisha vizuri tabia ya Nura. Baada ya Mpundu kumaliza maongezi na Mnaa aliweza kumpigia simu Nuru ili kuweza kumjuza taarifa za matukio yote ambayo Mpundu alikuwa ameyapanga na hadi muda huu tayari yameshakamilika yote.




















SURA YA KUMI
Ni penzi jipya tena mtaani kutoka kwa kijana anayeanza kutanuka kwa utajiri naye si mwingine ni Nuru. Ni baada ya kupita mwezi mmoja na siku kadhaa hivi. Muda huo inaonesha saa ya mshale iliyokuwa imewekwa juu ya ukuta katika nyumba ya Nuru ikiwa ni saa nane mchana juu ya alama. Muda huo Nuru anaonekana yuko kwenye sofa akiwa na msichana ambaye naye alikuwa amejaaliwa kwa uzuri. Wamekaa kwa namna wanavyoonekana kuna uhusiano wa karibu sana kati ya Nuru na msichana huyo. Mwanadada huyo kwa jina anaitwa Hanifa. Muonekano wa Hanifa namna ulivyo tu natumai ni jambo lililomfanya Nuru kuweza kuyasahau mabaya yote ambayo alitendewa na Nura. Hanifa kwa muonekano wake usoni kwa kweli shavu ni la kuteleza tu lililokuwa jeupee peee kama jua la utosini. Sura yake iliyokuwa ni ya kuvutia aongeapo huwa anaonesha tabasamu zuri sana lililoambatana na kubonyea kwa mashavu yake na kumfanya Nuru azidi kupagawa na huyo Hanifa. Hanifa kwa mdomo kajaaliwa sana kwa ajili ya kufanya shughuli nzuri ya mama na Baba kwa muda unaotakikana.
Kwa siku hiyo ndiyo kama mara ya kwanza kwa Nuru kuweza kumleta Hanifa hapo nyumbani. Siku hiyo Nuru kwanza ilibidi amueleze Hanifa kwa undani mambo yaliyokuwa yakimsibu tangu zamani haswahaswa katika mapenzi. Kwa muda huo ilikuwa ni mishale ya saa nane mchana. Wakiwa wanafanya mazungumzo huku Nuru ndiye aliyekuwa muongeaji mkuu huku wakiwa wameshikana mikono na wakiwa wamekaribiaana sana. Nuru aliweza kumueleza Hanifa mambo mengi sana juu yake hadi Hanifa alitoa machozi kwa kuwa alijua kabisa Nuru alikuwa ana mapenzi ya dhati kwa Nura lakini ndiyo Nura wala hakujali hicho bali aliona pesa ndiyo kila kitu katika maisha yake.  Baada ya maelezo yaliyokuwa yamemwingia Hanifa tayari wote walijikuta wakiwa wanaangaliana tu macho kwa macho tayari sumaku zikaanza tayari naye Nuru hakusubiri kwa hali ambayo Hanifa aliionesha kwa Nura. Nura alipitisha mikono yake huku na kule mwilini mwa Hanifa na kujikuta wanaanzisha mchezo pale pale kwenye sofa.
Kwa Hanifa alikuwa bado akiwa anaishi nyumbani kwao na wazazi wake wawili kabisa. Ambapo kwa yeye kwao ndiye wa kwanza na kufuatiwa na wadogo zake wa kiume wawili. Nyumbani kwao ni hapo hapo Arusha maeneo ya Mbauda Sokoni. Hanifa katika elimu naye alisoma hadi kidato cha nne katika shule ya Arusha secondari iliyopo mkoani Arusha na baada ya hapo alipata alama ambazo hazikuweza kumruhusu kuendelee na kidato cha tano na sita. Baba yake aliweza kumshauri Hanifa akajifunze kozi ya Ngamizi kwa muda wa miezi sita katika eneo lililokuwa likiitwa JENGO LA MOLLEL hapo hapo jijini Arusha lililopo maeneo ya Makao Mapya. Baada ya Hanifa kuweza kumaliza kozi yake alipatiwa cheti cha Ngamizi kilichokuwa kimeonesha programu mbalimbali alizozisomea. Kwahiyo baada ya kumaliza hapo Hanifa aliweza kufunguliwa kitega uchumi kizuri sana na Baba yake ambacho kilikuwa ni Stationar. Ambapo Stationar hiyo iliweza kumsaidia kuendeleza ufanisi wa kozi yake ambayo alikuwa amejifunza kwa muda huo wa miezi sita na pia katika kuweza kujipatia fedha ndogondogo za kuweza kujikimu kimaisha na kuacha kuwategemea wazazi wake kwa kila jambo. Kwahiyo hadi Hanifa anaingia katika uhusiano wa kimapenzi na Nuru yeye alikuwa bado yuko katika kitega uchumi chake kilekile cha Stationar.


Taarifa ya kuchomwa nyumba za Nura zilisambaa sana kwa vile Baba yake pamoja na  mama yake walikuwa wakijulikana sana kutokana pia na shughuli zao za kibiashara walizokuwa wakizifanya kipindi cha uhai wao na vitu vingine walivyokuwa wakimiliki. Kwahiyo habari hiyo ilisambaa sana hadi kwenye magazeti mbalimbali. Habari ile iliandikiwa kwa namna mbalimbali kwa namna tu mwandishi alivyoona ili tu watu wazidi kununua gazeti hilo. Hadi wengine walianza kutoa Makala zilizokuwa zikielezea kupanda na kushuka kwa ukoo wa Kerima na Makala hizo zikawa zinanunuliwa sana. Kwahiyo watu taarifa hizo waliweza kuzipata kwa kirahisi sana kupitia magazeti mengi ambayo yalikuwa ni kama magazeti ya udaku.
Baada ya kupita kama miezi minne hivi tayari bwana Kambi alikuwa amesharejea kutoka huko katika matembezi yake ya nchi za nje ambayo yalikuwa ni ya kibiashara zaidi. Basi siku hiyo Kambi alienda kumtembelea Nuru nyumbani kwake huko moshono. Muda huo ikiwa ni mishale ya saa tano asubuhi wanaoonekana hapo kila mtu amekaa kwenye kochi lake wakiwa wanaangalia runinga. Walipeana habari kemkemu za tangu kuondoka hadi muda ule. Nuru aliweza kumjulisha kuhusiana na Hanifa ambaye ndiyo mpenzi wake mpya.





Baada ya kupita miezi kama miwili hivi na siku kadhaa. Siku hiyo katika soko la Kilombero la jijini Arusha maeneo ya Ngarenaro. Muda huo ikiwa ni mishale ya saa tano asubuhi inaonekana sura ya Nura karibu na geti la kutokea. Sehemu hiyo Nura anaonekana kwa mbele kuna beseni lililokuwa na mbogamboga na pia kuna meza ndogo hivi inaonekana ina bamia, karoti na vinginevyo. Pia eneo hilo kwa pembeni kuna wanamama wengine wakiwa wanauza mboga mbalimbali. Jua limewaka kweli kweli lakini hakuna mtu aliyekuwa akijali bali kila mtu alijuwa kuwa mchumia juani hulia kimvulini. Nura anaonekana amevaa dera lililokuwa limechafuka kwelikweli na sehemu nyingine ikiwa limechanika huku kichwani akiwa amejifunga na kanga nayo iliyokuwa imechafuka sana. Baadhi ya watu wanaomjua Nura walikuwa wakishangaa sana kuwa Nura akiwa katika eneo hilo la sokoni tena akiwa anauza mboga mboga. Kuna baadhi ya wateja wakiwa wanapita maeneo hayo wakiwa wanaangalia vyao wanavyovitaka. Wateja wengine walikuwa wakishanunua mboga zao pale wanaanza kumteta huko wakiwa wanajiuliza kuwa ndiye yule tajiri wanayemjua au laa. Kila aliyepita pale alipokutanisha tu na sura ya Nura aliweza kushangaa sana lakini Nura wala hakuwa anajali bali alijali kazi yake kuwa inaendaje sababu yeye ndiyo anayejua chanzo cha yeye kuwa pale kwa muda ule. Ushauri wa yeye kuja sokoni ni baba Filipo ndiye aliyempa. Kwa sababu Nura hakuwa na namna yoyote ya kusema kwamba angeweza kujikwamua hata kidogo. Kwa sababu kwenye akaunti yake ya benki fedha zilichukuliwa na Mpundu na kubakiza fedha chache sana katika akaunti hiyo.
Zikiwa zimebaki siku chache ili Nuru na Hanifa kukaribia kufunga kifungo chao cha maisha. Ambapo kifungo hicho wakiishi vizuri wanaweza kufanikisha maendeleo yao katika nyanja mbalimbali tu za kimaisha. Nuru alikuwa nyumbani kwa Kambi ambapo kwa siku hiyo walikuwa wana mawili matatu wakizungumza wakiwa wanajiandaa na siku chache zilizobaki za arusi. Basi muda huo ikiwa inaonekana ni mishale ya saa nane mchana. Mazingira yakiwa ni ya sebuleni kwa Kambi.
Aaaaaaa Nuru unajua nimekuita hapa ili kuweza kukueleza jambo ambalo litakuwa kwamba ni la msingi sana kwako katika kuanzia siki hiyo ya arusi na hadi ndoa yenu. Maneno haya natumai yatakuwa ni kama mshumaa kwenu utakaokuwa unawalinda nyiye. Aliongea huku akiwa anamuangalia Nuru.
“Ni jambo gani hilo ndugu yangu unalotaka kuniambia lenye baraka hivyo?. Alimuuliza kwa ujasiri akitaka kujua kwa undani nini haswaa.
“Aaaaaaa Nuru kwanza unajua kwamba mimi nimeoa?.
Ndiyo nalijua hilo suala kabisa.
Basi kama ndiyo hivyo mimi ni mhenga kwako kabisa. Alifurahi.
Kwanini unasema hivyo?. Nuru alimuuliza swali Kambi. Nayajua mengi ya kwenye ndoa na pia wewe kama rafiki yangu ni vyema sana nikaweza kukueleza jambo ambalo ni la msingi sana na litaweza kukusaidia katika maisha yako ya ndoa na ukazidi kuyafurahia maisha hayo. Aliongea kwa hisia kisha Nuru akasema. Ni kweli wewe ni mhenga ni vyema ukaniambia. Kwa sababu siku zote wanasema maneno ya mwanadamu siku zote yakishaongewa mbele za watu kwa kweli hubaki kama tangazo kuu katika kichwa cha mtu. Kisha Kambi akasema. Natumai Nuru mejionea maisha yangu ya ndoa ambayo nimeanza kuyaishi na pia hadi leo nayaishi japokuwa hata kama kuna mabadiliko yatakuwa ni kidogo sana. Kambi aliongea kwa ujasiri kisha Nuru akasema. Ni kweli Kambi. Ni mara nyingi sana huwa nasafiri kuelekea nchi za nje na nikakuwa nakaa siku nyingi sana huko ulaya. Lakini hata siku moja sikuwahi kukuletea changamoto za mke wangu kwamba eti mke wangu ananifanyia vitimbi hivi na vile Noooo haijawahi tokea kabisa. Alijielezea Kambi kisha Nuru akasema. Ni kweli brother hadi kuna muda nilikuwa nikijiuliza hivi huyu Kambi mbona huwa anachukua hata muda wa miezi hata minne hivi na kumuacha mke wake swalemba tu Lakini hamna chokochoko zozote nilizowahi kuzisikia kutoka kwako kuhusiana na mke wako kabisaaaaa. Embu niambie Kambi nini siri ya urembo hapo?. Kwa sababu nahisi ndiyo maana mwanzoni mwa mazungumzo yetu ulijiita kwamba wewe ni mhenga. Kwasababu mimi kufunga arusi natumai ndiyo kama mtoto amezaliwa. Hivyo basi nahitaji kupewa muongozo vizuri ili makuzi yangu yaweze kwenda katika mstari mnyoofu na mwandani wangu ambaye ni Hanifa. Basi Kambi akiwa kama mhenga alkiweza kumueleza yote Nura na Nuru akaonekana kwa ameelewa vyema kabisa. Lakini Kambi kuna swali alimuuliza Nuru akisema.
Sasa Nuru Nura naye vipi umeshampatia kadi ya arusi?. Alimuuliza Nuru huku akiwa anafurahi. Aaaaaaa kwakweli nilitamani sana nimpatie kadi lakini nimefikiria mambo mawili makubwa. Alionesha kwa mkono kisha Kambi akamuuliza Nura akisema. Mambo gani hayo?. Aaaaaaa jambo la kwanza kabisa ni kuhusiana na kwamba hadi muda huu sijui ni sehemu gani aliko huyo Nura. Nuru alijielezea vyema kisha Kambi akasema. Mmmmh hilo ni jambo la kwanza mmmmh vipi kuhusiana na jambo la pili na la mwisho?. Kambi alimuuliza Nuru na Nuru akawa amejibu kiurahisi tu kwa kusema. Aaaaaaa kwa kweli naona kama vile atanitoa kwenye mood kwa siku hiyo ya arusi. Sawasawa brother nimekuelewaila kwa mimi nahitaji tufanye juu chini hadi na Nura apewe kadi ya mwaliko wa arusi. Daaaa sasa brother hapo tutafanyaje na ni kwanini unalazimisha?. Nuru alimuuliza Kambi kisha Kambia akasema. Katika kufanya tutatumia hata watu kwa namna mbalimbali na pia nina sababu kubwa sana ya kusema apatiwe kadi hiyo. Sababu yangu kubwa aaaa… nahitaji ajue kwamba dunia hii kila mtu ana kitabu chake na katika kila kitabu kina kurasa tofautitofauti na kila kurasa kuna matukio mbalimbali na matukio hayo lazima uyapitie tu. Kwahiyo sasa yeye alikuwa akisoma kitabu chako katika ukurasa wa matatizo tu na yeye akiwa katika ukurasa wenye furaha kila alipokuwa akifunua. Kwahiyo natamani sana aje kukuona ndipo ajue kwamba utomvu wa embe huchukiwa sana lakini wajisahau kwamba lile embe likija kuiva tu utaanza kulipiga tu na watu wengi hulipigania na kila mtu udenda ukimuanguka na unaenda kula utomvu ule ule ambao uliukataa. Sijui kama umenielewa ndugu yangu?. Kwakweli Nuru alikuwa akimsikiliza sana kwa makini Kambi lakini maneno yale kwa kweli katika kuweza kutaka kuyaelewa ilikuwa ni vigumu kweli. Nuru akasema. Duuu unajua Kambi wewe ungeamua kusoma kabisa kabisa hadi sasa ungekuwa mtu mkubwa sana katika kuisaidia nchi yetu kuipatia wataalamu wazuri sana wa fasihi. Natumai wewe ungekuwa hata profesa sema ndiyo hivyo kila mlima una malengo yake. Unajua maneno uliyoniongelea hapo ni machache sana nimeyaelewa. Japokuwa wewe si mwanafasihi. Nuru alimuelezea Kambi upeo wake kisha Kambi akasema. Aaaaaaa nikwambie kitu brother Nuru. Kuna malenga mmoja hivi anaitwa Haji Gora Haji ambaye alikuwa ni mshairi mzuri sana lakini hakuwa amesoma kabisa. Ameandika mambo makubwa sana ambayo yanafanya wasomi wafikirie sana wakiwa katika mitihani. Ni katika diwani yake ya Kimbunga. Lakini natumai tumeelewana kwa machache basi itabidi tufanye mambo yaende kama tulivyopanga. Japokuwa waswahili wanasema kwamba mipango si matumizi. Nuru akasema. Kweli ila natumai tutayafanikisha tu. Mazungumzo yao yaani kati ya Nuru na Kambi yalikuchukua muda mrefu sana hadi kuja kumalizika. Baada ya hapo Nuru aliweza kurudi nyumbani kwake huko Moshono.

Jitihada zilifanyika ili kuweza kumpata Nura lakini Nuru na Kambi hawakuweza kufanikiwa kamwe katika kuweza kumpatia Nura kadi ya Arusi. Walizunguka kona mbalimbali za Arusi huko Sinoni, Njiro, Mbauda, Banda Mbili, Majengo yote, Shamsi, Ngarenaro nzima, Ungalimited, Matejo, Kisongo, Kwa Mrombo, Moshono, Sanawari hadi huko kijenge juu kabisa wala hawakufanikiwa kabisa bali walichofanikisha ni kamliza tu mafuta ya gari na kujikuta wameingia hasara sana.
Lakini suala la kutompata Nura si suala ambalo lingekwamisha arusi kufanyika kamwe bali ilikuwa ni kama kuonesha ule utu tu. Basi siku ya arusi nayo iliwadia ambapo arusi hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Naura hapo jijini Arusha. Kwa siku hiyo uzuri wa Hanifa ulizidi kuliko hata ule wa siku zote kutokana na jitihada za mrembaji tu namna alizozitumia. Hiyo ilikuwa ikionesha dhahiri shahiri kwamba warembaji wamefanya kazi kubwa sana na yenye umahiri mkubwa na wakionesha kuwa ni wabobeaji wazuri kabisa. Pia kwa siku hiyo wazazi wa Nuru nao walikuwa wamependeza sana wakiwa wanaonesha tabasamu tukufu kwa mwanao kuweza kupata jiko zuri na yeye aanzishe familia nyingine ambayo itazidi kuleta udugu. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa Nuru kuweza kutimiza jambo ambalo kama ni kukata tamaa alishalikatia tamaa ila leo hii limetimia. Arusi ile ilifanyika kwa furaha kubwa kabisa na pamoja na rafiki zake Nuru pia wakiwemo hapo. Kambi alikuwa kama msimamizi mkuu wa arusi ile kwahiyo hakutaka kabisa kumuangusha rafiki yake na kweli alilikazia ngita hadi arusi ile ilipomaliza kwa amani na furaha. Watu walikula na kusaza na hadi wakasema kweli mtoto wa maskini anajua kuhudumia.
Kwa usiku huo Nuru akiwa anashereheka sherehe yake ya arusi. Lakini kwa upande mwingine usiku huo huo Nura akiwa anaonekana yuko amelala jikoni akiwa amelala juu ya kigodoro kidogo kisichokuwa na hadhi yoyote ile. Kwa upande wake wa kushoto kuna mafiga yanaonekana hapo. Muda huo kuna taa ya kutumia nguvu ya jua ikiwa inaonekana imeweka. Taa hiyo ilikuwa karibu naye muda huo Nura alikuwa ameingia katika bahari ya mawazo akiwa anawaza na kuwazua huku na kule. Karibu na mlangoni panaonekana mende wanarukaruka. Nura alijikuta akiwa anaongea pekee yake tu akiwa anajiuliza maswali ambayo mengine yalikosa majibu. Kwa sababu hakuna wa kumsaidia katika kuweza kujibu maswali yale. Hapo ndipo utaweza kuamini msemo usemao kwamba kila mtu atabeba mzigo wake na mzigo wenyewe ndiyo huo.  Nura akawa anasema.
“Eeee mungu Baba sijielewi hadi muda huu mimi hapa ni nani na nitakuwa nani kabisa katika dunia hii. Sina mtoto hata wa kusema kwamba ataniangalia ninavyohangaika ninavyoteseka ninavyodhalilika yaani ninavyopita katika msitu wa changamoto kubwa hivi. Eeeee mungu wangu eeeee au ni kwa vile nilimtesa sana yule mkaka wa watu au ni nini?... Huyo niliyempenda naye ndiyo hivyo hadi muda huu simuoni aliko. Aliniahidi kuwa atarudi naye amekuwa kama yesu ambaye wakristo humsubiri na hawajui ni lini atakuja. Kama ni laana kweli mimi nastahili kulaaniwa kabisa. Tena nilaaniwe saba mara sabini acha nijinyonge kwa maneno tu huku nikiwa nasubiri siku ya hukumu yangu ya mwisho. Ni mengi sana mazuri Nuru amenifanyia lakini mimi niliona ni kama ananiletea kiherehere tu kwangu na nikaamua kumfukuzia mbali ili niburudike na Mpundu ambaye hadi kwa sasa nahisi atakuwa bado yuko huko Marekani. Nuru naye nahisi ni kama vile ameoteshwa kwamba mimi nimefilisika na ninahisi ndiyo maana yake huyu Mpundu harudi. Mpundu nimefanya naye starehe na kumuamini kwa kila kitu atakachoamua kukifanya juu yangu. Siamini kama kweli ni yeye atakuwa amenikombea fedha zangu zote zilizopo kwenye akaunti zangu za Benki. Amakweli usimuamini binadamu mwenzako kwa kuwa ninyi nyote mmeumbwa kwa udongo tu. Kwahiyo ni watu ambao hatuna Shukurani. Eeeeee mungu wangu eeeee ndiyo maisha yameniendea kombo kabisa. Sielewi niyaanzie wapi na niyapeleke wapi hadi kuishia wapi. Jamani Baba na mama huko mliko niangalieni kama ni laana mmenipa jaribuni kuzipunguza. Maisha yangu yamekuwa kama muongoza ngalawa ambaye wimbi dogo tu atashindwa kulikwepa na kujikuta alishatupwa mbali. Sijiamini na siamini kabisa kama kweli mimi leo hii eti nauza mboga pale Kilombero tena nje ya geti kabisa. Kwa kweli nimeamini kabisaaaa maisha ni kitendawili ambacho kukitegua kwake yahitaji akili. Kweli hakuna ajuae kesho. Aliongea hadi usingizi alipopitiwa na usingizi.
Basi miezi na siku zikiwa zimeenda siku hiyo maeneo ya huko majengo anapoishi Nura kwa Babu yake mama Filipo nako huko walianza kumchoka huyo Nura. Kwasababu Nura ameshakuwa ni kama akili zimemruka kabisa. Kila kitu anategemea kutoka kwa Babu yake mama Filipo. Muda huo ikiwa ni mishale ya saa nane mchana ni baada ya kumaliza kupata chakula cha mchana. Muda huo Babu yake mama Filipo aliitisha kikao cha ghafla palepale nyumbani. Ambapo kwa siku hiyo ilikuwa ni siku ya jumapili. Waliokuweko katika kikao kile moja wapo alikuwa ni Nura ambaye anaonekana amevaa dera ambalo linaonekana haliko kama hadhi ya kipindi hicho akijulikana Nura the boss lady. Nywele zake hazieleweki kabisa yaani ni muda mrefu sana nywele hizo hazijapitiwa na mkono wa msusi. Sura yake inaonekana imefubaa mithili ya shati lilikuwa limevaliwa na mtoto mdogo kwa namna tu lilivyochafuka. Pia Baba Filipo naye yuko hapo amevaa shati jeusi na refu kweli kweli akiwa na mama Filipo hapo pembeni na John naye alikuwepo hapo katika kikao hicho. Ambapo John ni mjukuu wa babu na ndiye anayeishi na babu hapo nyumbani. Ambapo katika masuala ya mapishi na usafi anayefanya yote hayo ni huyo John. Nyumba inavyoonekana ni nyumba fulani hivi ambayo kwa kweli ni ndogo sana ukiangalia na watu wanaoishi hapo ndani. Basi muda huo Babu yake mama Filipo alifungua kikao kwa kuanza na kuwashukuru wanafamilia kuwa katika kikao kile. Baba alieleza kuhusu familia mpya iliyokuja katika kaya yake. Aliona kuwa familia ile tayari imeshakuwa ni mzigo mkubwa sana katika kaya yake. Alifikia mahali na kusema kuwa.
Sasa kuna huyu mwanadada mliyemleta hapa mnasema ndiyo alikuwa mwenye nyumba pia amekuwa ni mzigo mkubwa kabisa hapa nyumbani kwangu. Yaani kama ni msaada nimeshawapatia vya kutosha na kwa sasa ni muda wa nyiye kuweza kusaka yenu. Siongei vibaya na sina hasira bali ni kwa sababu huu msaada ninaoupata mimi hapa huko najulikana kwamba mimi niko hapa na mjukuu wangu huyu John tangu Bibi yake afariki. Natumai hadi hapo tumeelewana vyema kabisa Baba Filipo na mama Filipo na wengineo wenye Masikio walioko hapa. Maneno yale ya Babu kwakweli yaliwezakumuingia sana Baba Filipo na kuweza kutambua kweli pale walipo hadi muda walipo kwamba wanamnyonya babu kutokana na msaada ambao anapatiwa. Kwahiyo Baba Filipo alijibu kwa huruma akisema hivi.
Ni kweli tangu tuje hapa tumekuwa ni watu wa kulialia tu.Vitu vingi vyetu viliungua na moto. Pia niseme tu kwamba wewe umekuwa ni msaada wetu mkubwa sana tangu tukumbwe na janga hili. Ni kweli na ni uwazi kabisa kwamba ni wakati wetu na sisi tukajihangaikie kwa namna nyingine. Kwasababu ni tayari imeshapita nahisi kama vile miezi mitano na sita na kuendelea kabisa. Kwahiyo siwezikukulaumu kwa wewe kusema hivi.
Mmmmh kwa wewe mama Filipo na wewe unasemaje?. Baba alitoa ruhusa kwa mama Filipo naye anene uneni wowote.
“Ni kweli Babu kama tu vile Baba Filipo alivyotangulia kusema kama mume wangu maneno yake sina budi kuyafuata kabisa. Pia niseme ni shukurani kubwa sana ya wewe kuweza kutupokea hapa. Nakumbuka siku hiyo nilikuja tu hapa tena kwa kukurupuka ndipo nikaanza kukujuza nini haswaa kilichokuwa kimetusibu hadi tukaja hapa. Kwahiyo sitoweza yapinga maneno yako kwa kuwa kuyapinga tu maneno yako itakuwa inaonesha fika mimi au sisi ni watu tusio wa kutosheka au kuridhika kabisa. Aliongea Mama Filipo.
Sawasawa basi nahisi kwa zamu mlivyoenda wakati wa majibu yenu mkiwa mnanijbu hapa nimeipenda. Nahisi kwa sasa itakuwa ni zamu ya Nura kuweza naye kunipatia mrejesho wa nilichokiitia hapa. Nura karibu. Alimkaribisha Nura huku akiwa anamuangalia kwa jicho la machale. Nura aliitikia karibu ile kwa upole kweli akiwa anasema hivi. Ahsante Babu. Yaani kwakweli mimi hata sijui nianzie wapi kabisa. Nura aliongea kwa sauti ya huruma kisha baba akasema hivi.
Hapana unajua kabisa unaweza kuanzia mwanzo na kuendelea ili nikuelewe vizuri. Kwa sababu wewe haswaa ndiye kabisa uliyenifanya nikaitisha kikao hiki. Kwa sababu wewe nimekupokea hapa sikujui na wala hunijui na huyu Baba Filipo naye ni kama alijitolea msaada tu ndipo nae msaada ukawa umemshindwa. Basi ninalo la kusema hapa kutoka moyoni mwangu. Nasema hivi kuanzia kesho kutwa sitaki kuona mtu hapa zaidi ya mimi na mjukuu wangu John basi. Nahisi hata kikao chetu ndiyo kimeshafungwa hivyo. Baada ya kumaliza kuzungumza vile ndipo babu akawa ameamua kuinuka na kuingia zake ndani akiwa anamaanaisha kabisa kuwa kikao kimeishakwisha na hakuna maongezi mengine baada ya kikao hicho. Kikubwa kilichobaki ni wao kujipanga ili waweze kuondoka na kumuacha baba akiwa huru. Kwa sababu msaada alioutoa unamtosha.
Ni baada ya miezi sita tangu arusi ya Nuru na Bi Hanifa kufanyika. Ambapo kwa kipindi hicho hata mazoea ya ndoa tayari wameshakuwa nayo. Ikiwa ni siku ya jumapili mishale ya saa nane mchana.Wanaonekana Nuru na Kambi wako nyumbani kwa Nuru huko Moshono. Sehemu walipokuwa wamekaa ni kwenye sofa hivi. Kwa mbele hivi kuna meza inayongaa kwelikweli ikionesha dhahiri shahiri ufahari wa huyo Nuru. Juu ya meza kuna glass mbili zenye juice. Pia kwa mbele kidogo kuna runinga kubwa iko pale wakiwa wanaangalia. Kwa upande wa pili hivi yaani kwenye kochi hivi na mke wake Nuru yaani Hanifa yuko hapo ametulia. Kwa yeye yuko naye anafuatilia zaidi tamthiliya iliyokuwa ikioneshwa na channel hiyo maalumu. Nuru anaonekana amevaa tisheti nyeusi iliyokuwa imeandikwa kwa maandishi ya rangi nyekundu yakiwa yanasomeka NO BACKDATE 2 ME na suruali iliyokuwa ya jeans ya rangi ya bluu. Kwa Kambi alikuwa amevaa tisheti ya jezi ya Barcelona na huku suruali akiwa amevaa jeans ya rangi nyeusi. Kwa Hanifa alikuwa amevaa dera la rangi ya bluu na kichwani akiwa amejifunga kitambaa cha bluu.
Basi kwa maongezi yalianza pale na Hanifa akawa ameona si vizuri kuwasikiliza watu wakiwa wanapanga mipangilio yao ya kibiashara. Kwahiyo akawa ametoka pale na kuelekea chumbani kama ilivyo maadili ya mwanamke ndani ya nyumba ajapo mgeni nini anatakiwa afanye mume wake awapo katika maongezi na mgeni. Ili kuweza kuwaachia Nuru na Kambi uwanja mpana wa majadiliano. Waliyapanga mambo mengi yakiwa ni ya kibiashara pamoja na hata mambo ya kifamilia. Pia katika suala biashara Kambi aliamua kumwambia Nuru kuwa ana mpango waingiae wote katika biashara ya madini. Yaani kununua na kuuza nchi za nje. Jambo hilo Nuru aliweza kulipokea kwa furaha kabisa na kuona ni jambo ambalo litamsaidia sana katika yeye kukua kiakili na kibiashara zaidi. Basi baada ya kumaliza mazungumzo yale waliweza kumwita Hanifa na Kambi akawa amemshukuru sana Hanifa kwa juice iliyokuwa nzuri ambayo aliwapatia. Basi baada ya kumaliza mazungumzo yao kwa ujumla ndipo Kambi alipoamua kuondoka na kurudi nyumbani kwakwe huko Njiro.
Nura kama kuwa na mawazo yalizidi kumjaa kichwani mwake na kuanza kukua kama bahari ya Hindi. Alitafuta namna mbalimbali za kuweza kumuangamiza Mpundu lakini kikwazo kilikuwa ni kwamba pesa. Basi Nura tayari kwa kipindi hicho ameshatoka pale kwa Babu na kwenda maeneo ya Kitopeni huko ambako nyumba zilivyo kwa ujumla ni za mbavu ya mbwa. Kwenda juu fupi lakini ukiingia ndani ni kama handaki la wanajeshi. Kwahiyo huko ndiko kukawa ndiyo makazi yake makuu ya Nura. Nura aliona maisha yalizidi kumwendea kombo hadi mwisho wa siku akaamua kupiga mawazo ya kwenda kwa mganga ili aweze kumsaidia tu mambo yake.
Basi muda huo ikiwa ni saa moja za jioni kabisa hapo chumbani kwa huyo mganga pamejaa kila aina ya vikorokocho vya kiganga. Kijumba hicho alichokuwa ameingia ni kibanda ambacho kilikuwa ni kifupi sana na hakikuwa na nguvu sana ambapo hata upepo mkali ungetokea pale ingekuwa ni hatari sana. Kwa juu palikuwa pamefunikwa kwa matambara tu. Mganga huyo ni wa jinsia ya kiume kwa mwonekane wako ni mweusi na mnene kidogo. Hapo alipo amekalia ngozi hivi na kajifunga kaniki. Kichwani amejifunika na kipande cha ngozi ambacho kwa kweli kilikuwa kinatisha sana. Pia kwa pembeni panaonekana kuna paka kama saba wakiwa wanalia na sauti zao wanavyozitoa kwakweli zinatisha sana na kumfanya Nura akae pale kwa uwoga. Basi mganga akaaza kusema hivi.
Huhuhuhuh Mimi naitwa Mganga Mafimbo. Nura alishtuka kwa hilo jina tu na namna alivyokuwa akiongea kisha akasema hivi. Mafimbo?. Ndiyo unashanga mimi ndiyo mganga maarufu hapa mtaani kwetunaweza kurudisha vilivyopotea, naweza kuunganisha vilivyotengana na vinginevyo zaidi ya hivi nilivyosema. Mmmmh Huhuhhuhuh haya ongea. Mganga alikuwa akiongea huku akiwa anatingisha kichwa kisha Nura akawa anasema hivi. Nimeelekezwa hapa kwako. Aliongea Nura na mganga akasema. Sawandiyo mimi hapa. Mhhh huhuuh endelea na maelezo. Nimekuja hapa kwako kwa sababu kuna mtu amechukua mali zangu zotenataka umuue. Muda huo mganga Mafimbo anavyoongea huku anatikisa kichwa chake akamuuliza Nura hivi. Nimuue kabisa?.... ahahahaaaa shiiiiiiiiiii. Alimuuliza kwa sauti kali iliyotoka hadi ikatingisha kibanda chake na Nura akawa amekubali kwa haraka mganga akasema. “Umeridhia kabisa kutoka moyoni?. Nura naye hakuchelewa kujibu na mganga akwa amemwambia kwamba. Majibu yako yana hasira na hayana maana yoyote kabisa kwa huyo mtu unayetaka kumfanyia hivyo. Mizimu yangu inasema kwamba wewe mwanadada wewe una roho ya korosho sana wewe.ndiyo maana hadi muda huu upo hapa. Nura alikasirika sana kwa kuambiwa vile kisha akasema hivi. Heeeee wewe Mganga hiyo siyo kazi niliyokupa uifanye. Nura aliongea kwa hasira kisha mganga akacheka kwa nguvu tena kisha akasema kuwa. Laiti ugejua kwa mimi bila hawa hamna chochote kitakachofanikisha hapa hata kidogo. Nikisema kuua ni hadi wazimu wangu waniruhusu si kirahisi rahisi tu. Kwanza najua hujaolewa si ndiyo maana yake. Alimuuliza swali lile kwa sauti isiyo ya kiuganga kisha Nura akasema hivi. Ndiyo sijaolewa. Nura alijibu kwa ujasiri kisha mganga akasema. Na huyo ndiyo uliyekuwa ukitaraji atakuoa au siyo?. Ndiyo. Nura alijibu. Hahahahaaaa wahenga walisema chumvi hailambwi bali huonjwa tu. Kwahiyo yule aliyeonja hana shida kwamba akiondoka kwa sababu ameshajua kwamba hii chumvi mbaya. Muda huo mganga yule kuna dawa ya unga kaichota kutoka kwenye kikopo hivi. Alichota kwa kutumia kijiko kidogo na akawa amefunga kwenye kamfuko kadogo hivi cha rangi nyeusi kisha mganga akamwambia kuwa Nura ailambe dawa ile iliyokuwa kama ugoro hivi kwa uzito wake. Mganga alipomuona Nura anaogopa dawa ile kisha mganga akawa amemwambi Nura hivi. Hahahahaaaa mtaka cha uvunguni shariti ainame. Nura aliipokea dawa ile na akawa ameilamba bila kujua na kuuliza ni dawa ya nini ya nini. Baada ya kunywa dawa ile ndipo mganga akawa amemwambia Nura kuwa aweze kwenda na dawa ile pamoja na nyingine ya mafuta aliyopatia kisha aje siku inayofuatia ili wajue ni namna gani ya kumalizia shughuli yake.
Na kweli siku iliyofuatia mishale ya saa mbili usiku tayari Nura alikuwa ameshawasili pale kwa mganga mafimbo. Muda huo Nura anaonekana amevaa nguo zile zile kama za mara ya kwanza ambazo alikuwa amekuja nayo siku iliyopita. Basi muda huo Mganga Mafimbo naye hakuchelewesha mipangilio yake aliyokuwa ameipanga katika namna ya kumuhudumia Nura. Alichukua dawa na kisha akamwambia Nura anyooshe mikono ndipo mganga akawa amempaka mafuta fulani hivi kwenye kiganja. Mafuta yale yalikuwa na harufu kali sana ambayo yalimfanya pale pale Nura kuweza kupoteza fahamu ambalo ndiyo lilikuwa lengo lake kabisa ili aweze kufanikisha kulala nae. Kwahiyo kwa hapo mganga ikawa ni rahisi tu kuweza kufanya mapenzi na mwanadada amabye ameshatikisa sana jiji la Arusha kwa pesa. Nura hadi anakuja kupata fahamu tayari na muda ulikuwa umeshaenda sana na muda huo mganga alikuwa ameshamvisha nguo vizuri Nura na kumfanya mwili wake usiwe ni wa kuhisi chochote yaani kama kuna lolote alilofanyiwa. Mganga alimfanya Nura awe ni wa kukubali tu kila alichokipanga. Mwisho wa siku mganga alimuahidi Nura kuwa watakuwa wanaishi wote kama wachumba. Nura aliweza kukubaliana na suala hilo kwasababu hakuwa na namna. Baada ya kuinuka mganga aliweza kumtoa Nura pale na kumruhusu aweze kuondoka zake.


Mwaka mmoja umeisha tangu Nuru na Hanifa kuoana na Hanifa alikuwa ameshajifungua mapacha wawili waliokuwa wa kiume na wa kike. Kwa majina wakawa wanaitwa Said na Saida. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya jumapili ikiwa ni mishale ya saa nane mchana hivi. Muda huo Hanifa na Nuru wanaonekana wamekaa kwenye sofa. Nuru anaonekana amevaa bukta nyeusi na tisheti nyekundu akiwa anaonekana muda huo amempakata Saida ambaye ndiye huyo mwanae wa kike na kwa Hanifa anaonekana amevaa dera la bluu akiwa amempakata Said. Kwa mapacha hao yaani kati ya Said na Saida mkubwa ni Saida. Ambapo kwa kipindi hicho imeshapita kama miezi minne hivi tangu Hanifa kujifungua. Walikuwa wakiyapanga yao ya maisha ya hapa na pale. Walipanga kuhusu familia na mambo mengine kemkemu.


Ikiwa ni siku nyingine kabisa ambapo tangu Nura kuanza mapenzi na mganga Mafimbo ambapo waliishi katika uhusiano kwa muda wa miezi kama sita tu. Kuna mtu anaoneka katika mandhari inayoonekana hapo ni mandhari ya jalalani hivi. Kuna mwanamke anaonekana hapo akiwa anachezea mauchafu ya jalalani pale. Kwa ujumla ni kama kichaa vile. Nywele zake zikiwa zinaonekana zimefumukafumuka sana. Nguo zake hazifai kabisa kama ndiyo hizo nywele ziko rafurafu kweli kweli hadi zimeficha sura ya mtu huyo. Lakini kwa sauti inayosikika hapo ni kama sauti ya Nura akiwa anajitapa kuwa yeye ni tajiri mkubwa sana na hakuna kama yeye. Nura anapiga makelele kweli Kweli hapo jalalani ambapo jalala alilokuwepo lilikuwa ni jalala lililopo katika soko la Mbauda karibu na msikiti wa Mbauda. Pia kuna watu wanaonekana pia wako hapo wakiwa wanamshangaa huyo Nura mambo anayoyafanya hapo jalalani. Ambapo watu waliokuwepo pale walikuwa ni wanamama. Baadhi ya wanamama waliopo hapo wanamjua fika Nura. Kwahiyo walikuwa wakimshangaa sana mambo anayoyafanya huyo Nura. Wanamama wale baadhi yao walikuwa wakimjua kabisa ndipo walipanza kujiuliza kuwa mbona yule ni kama mtoto wa marehemu mzee Kerima.
Basi ikiwa ni siku nyingine kabisa kwa siku hiyo wakiwa wamekaa Kambi na Nuru kule kule nyumbani kwa Nuru huko Moshono. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya jumamosi mishale ya saa nane mchana. Kwa hali ya hewa ya siku hiyo ilikuwa ni ya kawaida sana. Muda huo Nuru na Hanifa wanaonekana wamekaa kwenye kochi moja na Hanifa. Nuru akiwa amevaa suruali nyeusi na tisheti nyeusi na kwa Hanifa akiwa amevaa gauni lililokuwa la rangi nyekundu iliyokuwa imechanganyikana na rangi ya kijani. Kitambaa alichokuwa amejifunga kichwani kilikuwa ni cha rangi ya njano. Kwa Kambi alikuwa amekaa kwenye kochi lingine. Kambi alikuwa amevaa suruali ya bluu na tisheti nyekundu. Muda huo kwa mezani hapo panaonekana kuna vinywaji vya watu watatu.Vinywaji hivyo vikiwa vimewekwa kwenye glass zilizokuwa ni za kupendeza kwelikweli. Pia kwenye runinga kulikuwa na kipindi kilikuwa kikioneshwa hapo. Kwa siku hiyo walikuwa wana mazungumzo maalumu sana. Kambi akiwa anaonekana ndiyo anaweka glass ya sharubati aliyokuwa akinywa ili kutaka kunena Jambo lililowafanya Wakawa pale kwa mda ule.
Aaaaaaa...Kambi ...jambo lililonileta hapa aaaaa natumai linafahamika?. Nuru muda huo alikuwa ameegemea kochi. Basi aliinuka na kisha akawa amekaa kitako vizuri akiwa anataka kumjibu Kambi kama ifuatavyo. Aaaaaaaaa....Ni kweli ila si kwa undani sana. Nuru aliongea kisha Kambi akasema. Ni Kweli kwasababu najua fika jambo hili nilikukanyagia tu nilipokuwa nakuelezea. Kwahiyo itakuwa ni vizuri sana kulikweka mezani na kuanza kulijadili na ili hata shemeji yangu hapa aweze kuelewa nini kinachoendelea na hata kama itahitajika ushauri basi anaweza kutoainawezeka kwamba yeye ndiye akawa kama msuluhishi mzuri sana katika suala tunalotaka kulizungumzia na kama atakuwa amelielewa vizuri. Kambi alijielezea vizuri kisha Nuru akasema. Sawasawa. Karibu. Aaaaa unajua Nuru na Hanifa katika hii dunia hakuna ajuae kuhusiana na kesho. Unajua Aaaaaa shemeji nakuomba uninuie radhi kwanza kwa jambo ambalo nataka kwenda kuliwakilisha. Hanifa akiwa anamjibu Kambi sura yake akiwa ameiweka katika hali ya kutabasamu na tabasamu lake likamwingia moyoni mwa Kambi na Kambi akiwa anajua kwamba lazima tu Hanifa atakubali. Hanifa alisema. Haina shida shem wala usihofu kuwa huru kabisa kwenye hilo. Alimkaribisha kwa sauti ya heshima kisha Kambi akasema. Ahsante sana kwa kunipa ruksa Aaaaa niseme tu bana unajua Nuru kabla hujaanza mapenzi na Hanifa ulishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanadada mwingine ambaye ni Nura. Natumai hilo hata shemu hapa ulishawahi kumueleza. Nuru alijibu kisha Kambi akaendelea na maongezi. Kambi akamuuliza Hanifa kwakusema hivi. Ni kweli shemu bwana Nuru alishawahi kukueleza jambo hili?. Alimuuliza kwa kumuangalia Hanifa na Hanifa akajibu kwamba. Ndiyo alinipa huu ukweli mapema sana wakati wa penzi langu na yeye lilipokuwa limeanza. Ahaaaa vizuri aaaaa ni vizuri tu kuwa na ule uwazi. Kwasababu hakuna lisilojulikana chini ya jua. Kwahiyo sasa jamani yule mwanadada ni kweli alishawahi kukuumiza sana Nuru. Kwahiyo ni kwamba hakuwa anajua kesho au hata baada ya masaa mawili tu mbeleni ni jambo gani litamkumba. Natumai kila mmoja wetu hapa anajua kwamba ni tayari imeshapita kama mwaka mmoja na kitu kabisa tangu Nura kuchomewa nyumba zake zote na mpenzi ambaye aliyetokea kumuamini katika kila Nyanja. Walijibu kwa pamoja. Ndiyo. Kisha Kambi akasema. Kwasasa Nura ni kama kichaa na kama ulivyokutana nae kwa mara chache huko mtaani hadi unamuonea huruma kabisa. Sawa kwa mambo aliyokufanyia si wa kumuonea huruma kabisa yule Mwanadada. Ila inabidi ukae na ufikiri je ni vizuri kuishi kwa hisia?. Kambi aliyanena yale kisha Nuru akamkatisha maongezi na kusema.
Unajua Kambi mimi kuna muda kwa kweli nashindwa kabisa hata kujijibu. Kwa sababu jambo hili linaniumiza sana kichwa. Yaani nashindwa kabisa kujipa maamuzi ya kusema ni kweli nimsaidie mtu ambaye alinitesa mimi nikayaona mapenzi kama vile nimekalia misumari ya nchi kumi. Kwa kweli hapo utata wanijia sana nashindwa kuuachia kabisa moyo wangu na kuulainisha kabisa kwamba mimi leo nimsaidie huyu mwanakulaaniwa. Yaani nahisi pia ni vigumu sana hata kuweza kujibu kabisa hata swali lako. Nuru aliyanena yale kwa hisia kali. Hanifa akaamua kujibu badala ya Nuru. Hanifa alimshika Nuru mkono wake wa kulia kwa mkono wake wa kulia na jambo lile likamfanya hata Nuru kupunguza hasira kidogo kisha Hanifa akawa anasema hivi. Aaaaaaa mume wangu. Najua hasira ulizonazo ni hasira ambazo hata kama zikiwekwa kwenye chujio ni vigumu sana kuweza kuchujika na kuweza kujulikana ni chembe ngapi kabisa hata zinaonesha moyo wa huruma kwa Nura. Basi niseme tu embu jaribu kufanya tu hivi kwamba jifanye hii dunia ni kama vile usiku ambao ukilala hujui je asubuhi naweza kuamka au laaa. Kwasababu unaweza ukalala na ndiyo ukalala mazima kabisa. Nahisi umenielewa kwa hapo. Tuwe na moyo kama machozi ambapo mtu atokwapo na machozi humbubuja na machozi yale kuanguka bila hata kurudi tena katika jicho la mtu huyo. Lakini muda mwingine mtu huyo akilia na machozi mengine yanatoka tu japokuwa yanajua kuwa hayatorudi. Naomba unielewe.  Maneno yale alikuwa akiyaongea kwa sauti iliyomfanya Nuru aweze kumwelewa mke wake kisha Hanifa akaendelea kuongea. Aaaaaa asante. Nuru na Hanifa tukiwa tumeungana na mimi napenda kutoa wazo la kwamba yule mwanadada inabidi tumpeleke kwenye matibabu. Nuru akajibu kwakusema. Wapi?. Aaaaa nilikuwa nafikiria kwamba tumpeleke huko mirembe kule Dodoma. Natumai huwa unapasikia. Kambi alitoa ushauri kisha Hanifa na Nuru nao wakakubali. Hanifa pia naye akawa anajibu kwakusema hivi. Sawa Shemu hilo ndilo suluhisho zuri kabisa. Kwasababu tukisema na sisi kuweka kinyongo aaaaaaa kwakweli itakuwa hatujamfanyia ubinadamu kabisa. Tukumbuke na nikumbuke kabisa Nuru ulishawahi kuniambia kwamba huyo Nura hana wazazi. Kwahivyo basi unamaanisha kwamba Nura hadi muda huu yeye ni yatima. Ndiyo maana yake. Nuru alijibu. Je unaonaje ukayasahau ya zamani na kuweza kuleta kabisa roho ya utu kwa mwanadamu mwenzako ambaye hana hata mzazi mmoja?. Kambi alimuomba Nuru kisha Nuru akawa amekubali kisha Kambi akaendele kusema. Kwasababu unajua shemu utajiri mlio nao kwasasa natumai ndiyo kama unakaribia kwa yule mwanadada. Pia kama ni utajiri wa Nuru umeanzia kwa huyo Nura. Kisha Hanifa akasema. Kwahiyo embu tu nakuomba mume wangu shusha roho ya chuki na kabisa uyafute mawazo mabaya Kwa yule mwanadada. Yule anahitajika kusaidika kumsaidia Nura huo ndiyo ubinadamu ulivyo mume wangu. Ukisema kabisa uishi kwa visasi kwa kweli katika hii dunia hautafanikisha chochote kabisa. Kumbuka maisha yako kwa ujumla yako katika jamii ambayo imekuzunguka. Katika jamii hii ndiyo hao wazuri na wabaya wapo hapo. Kwahiyo haina haja ya kusema kwamba eti oooo kwa vile huyu alishawahi kunitendea hivi na vile basi na mimi nimfanyie hivi na hivi. Hapana haifai usilipe ubaya kwa ubaya hapana haifai kabisa. Wewe lipa tu wema hata kama mtu amekufanyia ubaya na ndiyo dunia ya sasa ilivyo. Natumai tumekubaliana katika hilo.
Kwa maongezi yale hadi kukamilika waliweza kukubaliana ni namna gai ya kwenda kumsaidia Nura kwa hali na mali na kuweza kuyasahau ya zamani. Baada ya kumaliza maongezi yale basi kambi aliweza kurejea nyumbani kwake.


Basi msako wa kuanza kumsaka Nura ulianza ili waweze kumpeleka huko kwenye hospitali ya vichaa huko Dodoma (Mirembe). Kumfanyia vile Nura litakuwa ni jambo kubwa la kiubinadamu tu. Kwa sababu hana namna ni nani wa kumsaidia kama ni wazazi wake tayari walishatangulia huko katika makazi ya milele na kwa ndugu zake ndiyo hivyo kwa ujumla Nura hakuwa anaishi nao vizuri. Kwasababu yeye aliona hela kwamba ni kama roho au kimbola cha kupata marafiki wakati hela ni roho ya kupata marafiki wa muda ule ukiwa na fedha za kutosha. Sasa wewe fanya kufilisika ndipo uje uanze kujiuliza maswali kwamba kwanini wazungu wanasema kwamba the friend indeed is the friend in need. Sasa ndicho kipindi alichokuwa nacho Nura.
Basi nakweli siku ya kwanza ya pili na ya tatu ndipo wakaja wakafanikiwa kumpata Nura. Aliyempata Nura ni Nuru kabisa. Kwahiyo baada kumpata ilibidi wamfungie kwenye chumba chake maalumu na atakuwa anapatiwa huduma kwenye chumba hicho. Kwa siku hiyo walivyokuwa wamemuweka ndani wakiwa wanasuburi kufanya mipango ya namna gani ya kumpeleka Nura wala Nura hakuwa analeta fujo yoyote ile. Nuru kama ni nguo alimpatia tena nzuri sana chakula nacho ilibidi ampatie chakula kizuri sana na ili hata afya yake iweze kurejea.
Kwa ujumla katika dunia hii haina haja ya kuwekeana kinyongo wakati hata aliyetuumba tu hajatutaarifu kwamba bwana mtu fulani utakuwa hivi na mtu fulani utakuwa vile. Kwa ujumla waswahili wasemapo kabla hujafa hujaumbika wana maana kubwa sana. Leo hii Nura ni mtu ambaye hawezi tena kusema kwamba hata kupangisha nyumba au wala kujiendeleza na jambo fulani la kiuchumi. Nura alikuwa ni mtoto wa tajiri mkubwa sana katika jiji la Arusha hata ikumbukwe kabisa katika mazishi ya wazazi wake Nura watu waliokuja katika msiba ule walikuwa ni wengi sana. Lakini ndiyo hivyo kwa namna wazazi walivyokuwa wamemuachia mali zote na tayari Nura akajiona yeye ndiyo kioo ambacho hupendwa na mtu wakati akiwa tayari ni mzuri. Katika hii dunia ni vizuri sana hata kama ukifa leo ni vyema sana ukaacha kitu ambacho watu milele daima watakuwa wanakukumbuka. Mawazo yako yatazidi kuwaimarisha uliowaacha. Kwahiyo si vyema kupita katika hii dunia kama vile kivuli. Mathalani kwa Nura hata kama akifariki leo ndiyo tayari ameshakata jina la Mzee Kerima. Ukoo wa mzee Kerima ndiyo tayari hautoweza kusikika hata kidogo. Enyi mabibi na mabwana kuweni makini sana katika masuala haya ya kimapenzi. Kuwa na hela na kubaki kuhongana tu mwisho wa siku inakuwa imebaki story tu si vyema. Ni vizuri sana kuutumia uhai ulionao, uwezo ulionao vizuri, ishi na marafiki vizuri. Kwa sababu hujui leo na kesho ni nani haswaa atakayekuja kukuokoa kwenye janga fulani utakalokuwa umepata. Siku zote kuwa mtu wa heshima, busara na utu.
Siku hiyo wakiwa hapo ndani yaani huyo Nuru na Hanifa. Ilikuwa ni mishale ya saa tisa mchana sehemu waliyokuwa wamekaa inaonekana hapo mbele kuna runinga iko pia wote wakiwa wamekaa kwenye sofa wakiwa wamekaribiana kabisa. Kwa namna walivyokuwa wamekaa wanaonesha dhahiri shahiri kwamba mazungumzo yaliyopo pale ni mazuri ya hekima na busara.Yaliyokuwa yamejaa heshima na utu ndani yake. Basi kwa muonekano kwa Nuru anaonekana amevaa suruali ya jeans ambayo ilikuwa ni ya rangi nyeusi na tisheti ya bluu na huku kwa Hanifa alikuwa amevaa dera lake la rangi ya bluu. Kichwani akiwa ameegesha tu kanga. Mazungumzo yao kwa asilimia kubwa yalikuwa yamejikita katika maandalizi ya safari ya kumpeleka Nura huko Mirembe. Waliweza kukubaliana kuwa Hanifa atabaki pale pale nyumbani ili kuweza kuendeleza majukumu ya pale nyumbani kama vile kulea watoto na mengineyo. Pia waliweza kukubaliana kuwa suala hilo hawatawataarifu wazazi wake kwa kuwa waliogopa kuwa wazazi wake wanaweza wakaleta sana kipingimazi juu ya jambo hilo. Kwasababu ano wazazi wa Nuru wana hasira sana kwa namna mwanao alivyokuwa akionewa na Nura.
Basi ikiwa tayari ni mishale ya asubuhi na mapema sana na ikiwa tayari imepita siku moja tangu kumpata Nura. Muda huo inavyoonekana hapo nyumbani kwa Nuru gari ilikuwa nzuri kweli kweli aina ya Rava 4 ikiwa inaunguruma. Kwa pembeni pia anaonekana yuko Nuru ambaye alikuwa amevaa suruali ya jeans ya rangi nyeusi na akiwa amevaa pia sweta jeusi na zito na kichwani akiwa amevaa boshori la rangi nyeusi. Kambi alikuwepo hapo ambapo alikuwa amevaa kama huyo Nuru tu kasoro ilikuwa ni kwenye rangi ya mavazi aliyokuwa amevaa huyo Kambi ambayo yote yalikuwa ni ya rangi ta bluu. Pia na Hanifa naye alikuwepo hapo pamoja na Nura wakiwa tayari katika maandalizi ya kuanza msafara. Ambapo muda huo wanaonekana pia ndiyo wanamuingiza Nura ndani ya gari. Hapo anaonekana Nura akiwa ni mpole sana. Alikuwa amevalishwa suruali nyekundu na sweta jeusi. Kwa kweli ukimuangalia vizuri kabisa na ukimfananisha na yule Nura wa enzi za Mpundu hutoamini unachokiona hapo bali utaamini kwamba maisha ni kama gwaride ambapo ukisikia nyuma geuka wa Kwanza anakuwa wa mwisho na wa mwisho anakuwa wa Kwanza. Walimfungulia mlango huku Kambi akionekana ndiyo yuko karibu naye zaidi. Kwahiyo wakawa wameingia ndani na tayari Nuru akawa anamuaga Hanifa ili waweze kwenda safari njema iliyojawa na baraka kutoka kwa kwa mungu na kwa  mke wake pia. Nuru aliwaaga hadi wanawe ndipo akawa ameingia ndani ya gari. Hanifa alifungua geti kisha safari ikaanza. Kambi alikuwa amekaa nyuma akiwa na Nura ili tu kuimarisha ulinzi kwa Nura. Baada ya kutoka pale tu nyumbani ujumbe uliingia kwenye simu ya Nuru. Simu yake iliyokuwa ndogo hivi iliyokuwa imeandikwa ALCATEL. Alichukua simu ile na kusoma ujumbe uliokuwa ukisema kuwa.
Nuru vipi? Pole na mishughuliko. Ni mimi Mpundu. Usishtuke mimi kukutumia sms kwa namba ya Tz. Now niko Tz huku Dodoma. Lakini nina mpango wa kuja Arusha. Nitakuja kwa usafiri wa ndege. Kuna mambo kidogo yamejitokeza.
Nuru alishtushwa sana na ujumbe ule na akawa makini sana ili Nuru asione. Aliamua kumjibu kwa kusema kuwa.
Sawa nakuja na mm nakuja Dodoma. Nitakujulisha nikifika.
Ilibidi Nuru apige moyo konde na hakumwambia kabisa Nura wala Kambi kuhusu jambo lile.
Basi msafara wa kuelekea huko Dodoma kwaajili ya matibabu ya huyo Nura yaliendelea na hadi wakawa wamefanikiwa kufika salama salimini kabisa. Michakato ya kuanza kufuatilia sasa ni namna gani Nura ataanza kutibiwa nayo ilianza. Baada ya Nura kupelekwa katika chumba maalum kwaajili ya matibabu ambapo muda huo ilikuwa ni mishale ya saa nane mchana.
Basi Nura akiwa anaendelea na matibabu ilibidi Nuru aangalie ni namna gani ya kuweza kumpata Mpundu ili waweze kufanya naye mazungumzo. Nuru alimueleza Mpundu jambo lililokuwa limewaleta Dodoma na kumwambi kuwa kuna mambo ya kibiashara tu na mambo mengine ya kifamilia wala hakumwambia kuhusu Nura kabisa. Pia Mpundu naye alisema kuwa lengo la kuja Tanzania ni kuwa kuna msiba wa ndugu yake mama Mpundu. Hivyo alikuja ili kusimamia suala hilo. Kwa sababu kwa akina mama Mpundu yeye ndiye wa kike tu kwahiyo ndipo Mpundu akaona kuwa ni vyema basi akaja kumsaidia mama yake katika suala hilo la mirathi. Mpundu alimwambia Nuru kuwa kwa ujumla ni kama amekuja moja kwa moja Tanzania kwa sababu amekuja hadi na mchumba wake kabisa. Mpundu alimwambia Nuru kuwa akiwa anarudi Arusha amjulishe kama ikiwezekana wawe katika msafara mmoja. Walipomaliza maongezi basi Nuru alikata simu na kumficha Mpundu kabisa juu ya Nura.
Ilichukua siku kadhaa ndipo Nura akawa amesharuhusiwa kutoka kule hospitali na wakawa wamerudi pamoja nyumbani. Ambapo pia alipewa madawa ambayo alihitajika kuyameza ili pia yamsaidie kumuondolea matatizo hayo.
Basi baada ya kukaa pale nyumbani kama mwenzi mmoja hivi ndipo siku hiyo Nuru alipoenda kumchukua Mpundu na kisha wakaelekea nyumbani kwa Nuru na ili wakaweze pia kujadili mambo mbalimbali kama vile suala la bwana Mpundu kutaka kuoa na pia suala la kusuluhishana lifanyike kabisa. Basi siku hiyo ikiwa ni mishale ya saa tano asubuhi ikiwa ni siku ya jumapili honi ilisikika ikilia huko nje ndipo mke wake Nuru Yaani akawa ameenda kufungua geti. Basi Nuru aliingiza gari hapo kwenye ukumbi wake wa kuegesha magari na ndipo wakawa wameshuka. Hanifa alimkaribisha Mpundu vizuri japokuwa hakuwa anamjua. Ni tabia iliyo njema kwa Hanifa. Basi waliweza kuingia hadi ndani na walipofika sebuleni hapo Nura yeye alikuwa amekaa akiwa anaangalia Runinga hapo. Basi muda huo mke wake Nuru akawa amesharudishia mlango vizuri huku Nura alitaka kujua ni mgeni gani amekuja. Ile Kabla Nura hajageuka inasikika sauti ya Nuru ikisema. Mpundu karibu unaweza kuketi hapa.






SURA YA KUMI NA MOJA
Baada ya Nura kusikia Nuru ametaja jina la Mpundu pale pale mwili ulimsisimka na kisha Nura akawa amegeuka vizuri na kusema kwa sauti iliyokuwa imejawa na hasira kali akisema. Wewe mwanaharamu umetokea wapi wewe?.
Kwa kweli baada tu ya Nura kusimama na kusema hivyo ikabidi watu wote pale ndani nao wasimame na kuwa makini. Pia Mpundu kwa kweli alijikuta ni kama vile amechanganyikiwa kabisa. Mwili mzima wa Mpundu ulilegea kabisa. Hana hata neno lolote lile la kuongea zaidi ni kwamba tu alikuwa ameduwaa tu.Yote hiyo ni kwa sababu Nuru hakuwa amemtaarifu kabisa Mpundu juu ya suala hilo. Kwahiyo hapo ndani mambo yakawa ni vurumai. Mpundu akawa amemkodolea macho huyo Nuru kisha akawa anasema hivi.
“Nuru rafiki yangu mbona tena umenileta Jehanamu huku kabisa aaaaa?. Yaani Nuru umenileta hapa kumbe ni kuja kunifunga mimi kabisa. Yaani daaa siamini uwiiiiiiiiii maisha yangu nahisi yako matatani kabisa. Mpundu aliongea kwa kulalamika hadi machozi yakawa yanamlenga kisha Nuru akasema. Wewe tulia kwanza bana. Hapana. Yaani unanileta kwa Nura kabisaaaa wakati unajua nini nilimfanyia Daaaa hii ni hatari kabisaaaa. Eeeeee Mungu Eeeeeeeeee nifiche uso wangu wapi?. Aliendelea kuongea huku machozi yakimtoka kisha Nuru akasema. Siyo lengo langu bana wewe hauko kichwani mwangu. Mimi ndiyo najua fika kwamba ni nini nimewaza hadi nikakuleta hapa na kukukutanisheni hapa. Kisha Mpundu akahema kihemo kikubwa kwelikweli. Muda huo Nura akiwa ameshasimama na huku akiwa amevalia dera la rangi nyekundu iliyokuwa imechanganyikana na rangi ya bluu. Muda huo anavyoongea akiwa anamtusi huyo Mpundu huku akiwa amejishika kiuno maneno akiwa anayatoa akisema hivi. Huyu mwanaharamu katokea wapi?. Eti tena kabisa anajaribu kuanza kuongea fyokofyoko hapa.Weeeeeeeeee mwanakulaaniwa wewe uliyekosa wajukuu wa kuchukua urithi wako wa kulaaniwa.Yaaani embu mcheki limwanaume lizima linajifanya ni bonge la mtanashati kumbe unaishi kwa mali za kiwiziwizi tu hapa. Bilalifakini wewe huna adabu kama mbwa wa uswahilini. Yaani watu wewe unaweza ukapewa cheo cha ushetani kabisaaaa ambaye atakuwa kama kijinga kikuu kwa siku hiyo ya kiama. Mpundu huna hata aibu unaamua kunitakatishia kabisaa mali zangu nilizoachiwa na marehemu mzee Kerima. Wallah Watallah wewe mwanadamu ulaaniwe na ulaaniwe kabisaaaa kama Farao. Hata kama sina jukumu la kukulaani lakini namuomba mungu tu ulaaniwe. Embu mcheki sura yake. Ndiyo maana yake umekosa mafunzo ya maadili kabisaaaa Mpundu.Yaaani nilipoteza ndugu zangu wengi na marafiki zangu wengi sana kwa sababu ya wewe tu. Alafu sijui wapi tu hayo mawazo yalikuijia na ukaamua kufanya hivyo. Aliongea kwa hasira sana ndipo Nuru akawa ameingilia maongezi yale na kuomba kuwa embu kwanza wakae na kuyasuluhuisha mambo hayo. Kambi alianza kwa kusema.
Nyote hapa yaani Nura na Mpundu mnaweza kutulaumu sisi kwa sababu nyote nyiye hamjui ni nini haswaa tulichokuwa tumewakusudieni kabisa kukukutanisheni ana kwa ana na kuweza kukalishana pamoja na kuyaongea baadhi ya mauchafu yaliyofanyika na yafutike. Mauchafu hayo ni ya kutendeana yaani huyu kamtendea yule na yule kamtendea huyu. Basi madhumuni makubwa ya Nuru kwa Mpundu kuweza kukuleta hapa kwa kukushitukiza na kumkuta Nura hapa ni kwamba tulikuwa na madhumuni yetu. Hatukutaka kuwaleteni hapa ili eti kwamba muanze kupigana, kutukanana na kuanza kuchambana hapa kama waswahili fulani. Hapana marufuku kwa hilo kabisaaaa. Hatukuwa na madhumuni hayo kabisaaaa. Sidhani kama Kati ya moja wetu kama alikuwa na chembechembe za namna hiyo na hata kama anazo namuomba azifute. Kwahiyo hiki kikao kinachotakiwa kufunguliwa muda si mrefu kitakuwa kama vile kikao cha kuleta amani kati ya Nura na Mpundu kama vile amani ilivyoletwa na kati ya Nuru na Nura. Basi hatuna budi na hawa pia tukawafanyia jambo hilo. Haina haja makesi kama haya ya kuanza kufikishana hadi huko mahakani. Hapana tutakuwa tunaanza kujengeana chuki nyingine ambazo nazo hizo zitakuwa ni chuki za milele kabisa. Hatuna maana mbaya kabisa juu ya jambo hili. Tukumbuke sisi ni wanadamu na kama ni wanadamu basi ni kwamba tumezaliwa tunaishi na mwisho wa siku tutakufa tu. Sasa swali ni je tutakufaje? yaani tutakufa kwa migogoro migogoro hivi au tutakufa kwa njaanjaaa hivi?. Kwa ujumla si vyema kufa ukiwa na kinyongo na mtu fulani. Si vyema sana katika uso huu wa dunia hii mfano tukimuangalia huyu Nura mambo ambayo alimfanyia Nuru kwa kweli kama Nuru angekuwa na roho kama ya panya kunusa sumu sijui kama hata angemsaidia Nura. Nura ulikuwa ni wa kufa kabisa lakini nikamkalisha rafiki yangu tulikutana hapa hapa tukiwa pamoja na Hanifa hapa na yeye akawa ametoa mchango wa kimawazo katika suala hili. Tena Hanifa alitoa mchango mkubwa sana. Hapo sasa ndipo tukaamua kukupeleka hadi huko mirembe kwaajili ya matibabu zaidi. Kwa ujumla tu niseme kwamba jambo kubwa lililotuleta hapa ni kutatua tu matatizo na si kuongeza matatizo. Tukiongeza matatizo mwisho wa siku hatutakuwa tumejenga chochote kabisa kama kweli tukifanya hivyo. Kwahiyo embu tu nipende kumkaribisha Nuru aweze kuongea naye lake jambo na hatuna budi kumsikiliza kwa makini. Kwa sababu uelewaji wake kutokana na usikivu wetu ndivyo tutakavyokuwa tumetambua nini haswaa Nuru anaongelea. Karibu sana Nuru. Maneno yale yaliwaingia watu wote waliokuwa wamekaa pale na wakawa wametulia kimya kisha Nuru akasema.
Aaaaaa Asante Kambi kwa kunipa nafasi hii takatifu na kama kweli ni takatifu itabidi niitendee haki kama ipasavyo. Aaaaa nitapenda kwenda kwa matukio na matukio hayo nitayaelezea kwa kina yaani kwa undani zaidi na undani huo ukiwa unaongozwa zaidi na ukweli kutokana na uimara nitakaokuwa nao wakati naelezea matukio haya. Nimependa niende kwa matukio kwa sababu najua hadi hata sisi kufikia kukaa hapa kwa muda huu ni kutokana na matukio mbalimbali ambayo tayari yameshafanyika ndipo yakawa yameleta tukio la Leo. Hivyo basi mtiririko wa matukio nitakaokuwa nikienda nao natumai na utaweza kulainisha nyoyo za watu walioko hapa. Kwanza kabisa nianze na mimi ni moja ya muhanga na ambaye aliyenifanya hadi nikawa katika uhanga huo ni Nura. Jambo hilo na mke wangu natumai analijua fika yaani in and out. Ohooooo kama basi unajua basi itakuwa ni hongera kwangu. Aaaaa niendelee tu kusema kwamba Nura wewe nakumbuka ulikuwa ni kama mpenzi wangu. Embu naomba tusikilizane kwa makini hapo. Kwamba nasema Nura ulikuwa kama mpenzi wangu.Yaani kwa sasa nikiwa namaanisha imebaki story tu. Lakini mwisho wa siku tuliishi kama wapenzi lakini ndiyo hivyo baada ya kwenda zako chuo ndipo ukakutana na wajanja wa mjini ambao tayari wanalijua jiji kabla yako. Mwisho wa siku mimi ukawa umenifanya kama vile kibaraka katika moja ya duka lako ambalo nilikuwa nikiuza hapo. Kwa siku zilivyozidi kwenda ndipo nikawa nazidi kuona na migogoro kati ya mimi na wewe inazidi tu. Lakini mwisho wa siku rafiki yangu wa karibu huyu Kambi alikuwa akinipa ushauri mzuri sana tena kuhusiana na wewe Nura. Mwisho wa siku ndivyo hivyo unakuja kutoka Dar es salaam ukiwa na Mpundu. Mimi huku ukiwa waniona kama vile choo kilichochafuka kwa mida ya mchana angali mida ya asubuhi na wewe ulienda kujisaidia katika choo hicho hicho. Basi ikanibdi tu nifuate maneno ya Kambi tu hapa kwamba acha tu nikubaliane na matokeo. Mwisho wa siku ndiyo hivyo nakuja kusikia Nura kwenye vyombo vya habari na magazeti vikisema kwamba mtoto wa tajiri kuangukia jehanamu. Nilishangaa sana baada ya kuona hivyo na kwa mda huo nakumbuka kabisa Mpundu uliniambia kwamba uko Marekani. Mpundu aliitikia kwa kichwa kisha Nuru akaendelea kuelezea. Lakini baada ya saa, siku, wiki, mwezi na miezi ndiyo hivyo tunakuja kuanza kukutana na Nura ukiwa kwenye majalala huko Mbauda-Sokoni na maeneo mengine. Mwisho wa siku tukaja na tukakaa mezani na kutafuta njia za kukushika wewe Nura ili tukupeleke huko mirembe. Kwa kweli roho yangu ilikuwa ikisitasita sana kuhusiana na mimi kabisa kushiriki katika suala la kukupeleka wewe Nura huko Hospitali. Lakini kupitia nguvu ya mke wangu pamoja na rafiki yangu wa karibu bwana Kambi ndiyo walioweza kunikalisha hapahapa katika sebule hii na tukaweza kuongea na wakanishawishi hadi nikawa nimekubali tu. Nikasema kwamba japokuwa kweli Nura amenitendea mabaya ya kiasi gani na ninajua hakuna na baya alilonifanyia eti kwamba litakuwa limejichora katika sehemu ya mwili wangu yaani iwe usoni na kadhalika. Ndipo sasa nikawa nimeamua kwamba ni gari yangu kabisa ndiyo itakayompeleka Nura na kumrudisha. Kila kitu nilihudumia na pia nikiwa nimeungana vizuri na Kambi. Siku hiyo na ndiyo siku Mpundu uliponitumia sms asubuhi ndipo nikakujuza kwamba nakuja Dodoma na tulikutana kabisa huko. Lakini sikutaka kukuambia chochote kuhusiana na huyo Nura. Kwahiyo Nura sina mengi sana ya kuongea bali tu ninachokiomba kwa nyiye watu wawili haswahaswa wewe Nura ambaye unaonekana kwamba una hasira sana.Yaani ni kwamba na mimi ningesema kwamba niendelee kuishi kichukichuki tu na wewe je hadi muda huu ungekuwa ni Nura wa miezi michache iliyopita?. Kisha Nura akajibu hivi. Hapana. Pia leo Nura ungekuwa hata mzima kweli?. Nuru alimuuliza Nura na Nura akasema. Hapana. Je sikuwa na utu?. Hapana. Ahaaaa basi Sawa kama Nilikuwa na utu nikiwa kama mwanadamu na wewe ukiwa kama mwanadamu huwezikuwa na huo utu?. Nura alinyamaza kwa sekunde chache kidogo ndipo akawa amemjibu Nuru kwa kusema hivi. Naweza kuwa nao. Kwahiyo kwamba unamaanisha umemsamehe Mpundu?. Hapo napo palikuwa pagumu kwa Nura kuweza kumjibu Nuru. Baada ya sekunde chache kupita hivi ndipo Nura akasema hivi. Sawa. Nimemsamehe Mpundu ila.... niseme tu malipo ni hapa hapa duniani. Kusema vile Nuru akamuuliza Nura. Ukimaanisha nini?. Waliosema msemo huo wenyewe hawakutoa maana yake bali tu ni watu wameamua kujitolea maana zao. Sawa, tusiende mbali sana ila nachotaka na kukuuliza wewe hapa ni kwamba umeshamsamehe Mpundu kama nilivyokusamehe wewe. Natumai kwa hapo imeisha. Walipomaliza masuluhisho ndipo Nuru akawa amemruhusu mke wake naye apate kutoa neno lolote.
Aaaaa asante sana mume wangu kwa nafasi hii uliyonipa kwa muda huu. Sina budi kukupa hongera pia kwa kazi kubwa uliyoifanya ya kuweza kumshusha hasira Nura. Sababu mgogoro huu ni kama ule wa Kenya 2008 hadi Jakaya kwenda kusuluhisha na akapewa shahada ya heshima basi kwa wewe nakupa pia shahada hiyo. Ni kazi kubwa sana umefanya. Aaaaa… Nura napenda kushukuru sana kwa ukubali wako kwamba umemsamehe Mpundu japokuwa kwamba kila mtu huwa ana moyo wake. Yaani siwezi kuhisi hata siku moja kwamba nini unawaza japokuwa umekubali tu suala hili. Kwa ujumla ni vigumu kuweza kuelewa kabisa. Sina maana mbaya bali nina maana ya kumpa hongera mungu ambaye ndiye muweza wa yote aliyeamua kufanya kwamba utaona vitu vyote bali si kuona hisia za mwenzako. Hivyo basi Nura ukumbuke tu kwamba Nuru ni mume wangu. Kwa wewe alikuwa ni mpenzi wako japokuwa kwa akilini mwako ulimuweka kama vile kijakazi wako. Moja ya watu waliomuumiza Nuru katika suala la mapenzi ni wewe na hakuna mwingine. Lakini hayo yote ni Nuru ndiye ambaye alinieleza kwa undani na nikawa nimemuelewa mimi kama mke wake wa ndoa. Basi kwa utu niliokuwa nao nikaamua tu kumwambia ayasahau ya zamani na tuanze kuganga yajayo ndipo mwisho wa siku tunakuja kupata uhakika wa msemo usemao kwamba malipo ni hapa hapa duniani akhera ni mahesabu tu. Kwa sababu baada ya siku chache tu tulianza kukuona huko majalalani ndipo hapo roho ikatusuta na tukajikuta tumeona aibu ndipo tukaamua kukusaidia na huku tayari tukiwa tumeshasahau ya zamani kabisaaaa.  Lakini mimi sikutaka tena kukumbushia ya zamani nikiwa nasema kwamba aaaa mimi sitaki kumsaidia huyu Nura kwasababu alimtesa sana mume wangu lahasha sikutaka hivyo. Natumai huduma zote hapa ulizipata kwa asilimia mia kabisa. Kwahiyo dhamira yangu kuu kabisa ni kwamba nakuomba zidisha utu na ufanye kwamba yameisha tu na umsamehe. Baada ya Hanifa kunena vile ndipo Nura akasema. Sawa nimewaelewa. Basi baada ya Hanifa kumaliza maongezi pale juu ya Nura ndipo Kambi naye akaamua kuongea lake.
“Aaaaa Nura nikushukuru sana na pia kwa ujumla tukushukuru sana kwa kuweza kusikiliza maombi yetu kwako katika kuweza kumsamehe Mpundu. Yote hii ni kutokana tu na maana ya utu tuliyoweza kuielezea kwa namna zote na ukaweza kuielewa maana hiyo na kutuelewa sisi. Tukumbuke kwamba haya ni maisha tu. Hivyo basi jambo kama linaweza hata kumkumba tena mmoja wetu hapa. Kwahiyo si vizuri kuishi kwa chuki kabisa. Hivyo basi nisiwe muongeaji sana embu kwa nafasi hii kidogo pia tumpe Mpundu kama ana lolote jambo la kuweza kuongea. Muda huo Mpundu akiwa anaongea kwa sauti ya kuogopa ogopa hivi. Alikuwa anasema hivi.
“Sina kubwa la kusema zaidi ya kusema tu shukurani sana kwa Nuru, Kambi, pamoja na Shemeji hapa. Kwa sababu sikutarajia kabisa kama hali ingeweza kuwa nzuri kabisa hapa. Kwa namna nilivyokuwa nimekuja tu hapa nilijua kabisa kwamba Nuru ameshaniuza kabisa na ndiyo maana nikajikuta nimepaniki sana. Kumbe tena na huku Nura ndiyo amepaniki zaidi. Kwahiyo nipende kusema tu ni shukurani kubwa sana natakiwa kukupatieni. Kwa sababu masuluhisho mliyoyafanya hapa kwa kweli pangekuwa na mtu ambaye hawajui kabisa yaani ndiyo mara ya kwanza kukutana na nyinyi kwa namna mlivyofanya masuluhishi mtazani kwamba mmesomea kitivo hicho. Pia ni shukurani kubwa sana kwa Nura kuweza kulainika moyo wake. Niseme tu kipindi kile ni hisia ndiyo zilikuwa zikiniongeza bila kujua kutakuwa na matokeo hasi au chanya?. Kwahiyo nawashukuruni sana kwa kunisikiliza.
Basi maongezi yale waliweza kuyamaliza na wakawa wamepeana kabisa mikono ikiashiria kwamba uwepo wa amani katika eneo lile pia na amani ya wao kwa wao. Kama ni mikono kupeana ni jambo la kawaida tu hilo ambalo kwa mkono anaweza kupewa mtu bali moyoni mwake huwezijua kama kweli huo mkono ameutoa kwa moja kwa moja au kuna unusu wa amani utajitokeza. Yaani ni kwa shingo upande au vipi.


Nura aliendelea kuishi pale kwa Nuru kama muda wa mwezi mmoja hivi ndipo Nuru akawa amempatia mtaji Nura ambapo mtaji huo utaenda kumsaidia yeye kuanza maisha yake mapya. Aliamua kufanya hivyo ni baada ya kuona kuwa tayari Nura ameshatengamaa kiafya. Lakini mawasiliano yakawa yanaendelea vizuri sana yaani kati ya Nura na Nuru. Nuru alimtafutia Nura chumba cha kupangisha ikiwa ni maeneo ya Mbauda. Alimlipia chumba kile kwa muda wa miezi sita na kumpatia fedha tathilimu shilingi milioni moja kama ya kuanzia maisha na huku akiwa amempatia nyingine ya kuanzishia biashara yake.
Ilipopita miezi mitatu hivi ndipo kikao cha kujadili kuhusiana na arusi ya Mpundu itakuwajekuwaje kiliweza kufanyika. Kwa siku hiyo wanaonekana Nuru, Mpundu na Kambi wamekaa pembezoni mwa bustani ambapo wakiwa nyumbani kwa Nuru. Mezani hapo panaonekana kuna vinywaji vilaini vilikuwa vikionekana. Kwa Nuru akiwa na Fanta Passion, Kambi akiwa ma 7Up na Mpundu akiwa na Coca-cola. Kwa mishale ya muda huo ilikuwa ni mishale ya saa tano za asubuhi hivi. Kwa hali ya hewa ya siku hiyo kwa Arusha ilikuwa ni ya kawaida tu yaani si jua kali wala si baridi. Maongezi yale kwa kweli yalienda vizuri kabisa na hadi wakawa wamemaliza na kumaliza kwao kukawa kuna faida kubwa sana. Ambapo majadiliano yale yalichukua muda wa masaa matatu na nusu.

Ilipowadia siku ya arusi ya Mpundu kwa kweli kwa siku hiyo nyumbani kwa akina Mpundu huko Ngarenaro palikuwa ni furaha kubwa sana. Ndugu mbalimbali waliweza kuwasili katika arusi ile. Marafiki zake ambao alisoma nao shule ya msingi, upili na kidato cha tano na sita waliweza kuwasili na wakiwemo pia na wale wa chuo. Nura, Nuru, Hanifa na Kambi walipendeza sana kwa siku hiyo. Wote walifanya juu chini arusi ile iweze kwenda vizuri. Kwa sababu ni rafiki yao na ni moja ya familia yao katika urafiki. Hadi ilipowadia mishale ya saa kumi na moja jioni arusi ilikuwa imeshakamilika vizuri kabisa na watu wakiwa wamekula na kusaza. Waliohitaji kuchukua chakula waliweza kuweka kwenye Marliboro na kwenda kula cha usiku. Basi baada ya arusi kumalizika ziliandaliwa gari za kwenda kuwapeleka bibi arusi na bwana arusi kwenye fungate. Msafara wa kwenda huko ulianza ulikuwa wa kwenda katika hoteli moja hivi ya kifahari ikiwa inajulikana kwa jina la Ngurudoto Hotel kwaajili ya kwenda kufanya mapumziko huko.
Basi wakiwa katika msafara wa kuelekea huko kwa muda huo bibi na bwana arusi wakiwa wamepakizwa kwenye gari la kifahari. Msafara ulivyokuwa ukiendelea ambapo msafara ule ulikuwa na gari saba ambapo gari walilokuwa wamepakizwa Bibi na bwana arusi lilikuwa ni la tatu katika msafara ule na ikiwa ni Range Rover pekee. Yaani kwa wengine walikuwa na aina nyingine za magari. Ghafla tu kwa mbele walikutana na uzio wa msitari wa mawe yakiwa yamepangwa hapo njiani kwa mawe hayo yakiwa yameshiba kwelikweli. Baada ya kuona vile kwa kweli ikabidi msafara usimamishwe ili kuweza kujua ni nini haswaa kimejitokeza mbele hapo. Watu walishangaa sana kwa kukutana na janga hilo. Hawakuweza kusubiri ndipo wasindikizaji wakawa wametoka nje ya gari na kuja kuanza kutoa mawe yale. Walianza kutoa mawe yale huku wakiwa wamewaacha bibi arusi na bwana arusi pekee yao kabisa wakiwa kwenye gari huku dereva naye alishuka. Walijitahdi kuyasukuma mawe yale kwa sababu yalikuwa ni mazito sana. Huyu alishika huku na mwingine kushika kule ili tu kuweza kukamilisha kuyatoa mawe yale. Watu walitokwa na majasho hadi nguo walizokuwa wamevaa kwa ajili ya arusi kuchafuka na kuwa kama wakipanda mlima usiokuwa na baridi.





Wakiwa wanaendelea kusukuma mawe huku na kule risasi zilisikika zikiwa zinarindima kutoka msituni kwenda kwenye gari lililokuwa limewabeba bibi na bwana arusi. Kwa kweli kwa risasi zilizorindima pale si risasi za kusema kwamba kwa aliyepitiwa na risasi hizo kwamba atakuwa salama. Watu walishtushwa sana kwa tukio hilo na waliokuwa na presha hapo hapo walizimia na wengine kuanza kulia tu na kukimbia bila hata kujua wanakimbilia wapi. Hawakuwa wanajua je huku wanakokimbilia ndiyo pana usalama au laa. Kila mtu alianza kusali sala yake cha msingi tu aweze kupona. Wengine walibaki tu wakiangalia ni wapi risasi hizo zinatokea na hata hawakuwa wanaziona sura ambazo zinarusha risasi.
Baada ya risasi kusimama kurushwa ndipo wakawa wameenda kufungua mlango kwenye gari la bibi arusi na bwana arusi. Kwa kweli waliwakuta bibi arusi na bwana arusi wakiwa hawafai kabisa wameshakufa kwa risasi zilizomiminwa hapo kama njugu. Kwa kweli watu walichanganyikiwa sana wakawa wanahangaika sasa ni namna gani wafanye ili hata waweze kujua ni nani aliyesababisha vurumai yote hiyo. Eneo hilo lilitawala vilio na simanzi kama watu waliofiwa na muokozi wao. Anaonekana Nuru anachukua simu ili aweze kuwapigia askari waje kwa ajili ya msaada wa kiulinzi. Nuru alikata simu baada ya kuwapigia kituo kikuu cha polisi na akawa anahangaika tu kama amechanganyikiwa kabisa. Basi baada ya muda kidogo hivi ndipo anaonekana Nura amejitokeza nyuma ya msafara kutoka msituni huku akiwa ameshika bastola sura yake ikionekana ina hasira sana na kujikunja hadi uzuri aliokuwa nao kwa muda huo ulipotoea. Alianza kunena kwa sauti akiwa anasema.
“Mimi ndiyo Nura Kerima Isambe natumai Nuru unanijua vizuri. Samahani sana Nuru kwa jambo nililofanya nimeamua kufanya hivi ili kuweza kumaliza ukurasa wa chuki. Sina mtoto wala wazazi ndiyo maana sikusubiri kufanya jambo hili. Hili tukio ni mimi ndiyo nimelipanga na pia nimelifanya msije mkamhusisha mtu mwingine kabisa. Alikufa baba yangu, Mpundu na mke wake nimeamua kuwaua na sina hata mtoto wa kusingiziwa naye ningemuua basi acha tu na mimi nijiue. Baada ya kusema vile Nuru na Kambi walianza kumkimbilia ili kumuokoa Nura bali wakawa wameshachelewa. Sauti ya risasi ilisikika ikiwa ni Nura amejipiga kichwani mwake na kichwa kupasuka kama tairi la gairi. Nuru, Kambi, Hanifa na wengineo waliokuwa pale walibaki wakiwa wamesimama tu na kushindwa hata la kusema. Ndipo Nuru akanena kwa kusema.
“Hivyo ndivyo pesa ilivyo. Amakweli kuanzishwa kwa vita ni kwa ajili ya kumaliza vita.

Comments

  1. Habari ndugu. Napenda kukukaribisha katika hadithi yangu iitwayo PESA ILIVYO. Ni hadithi yenye kusisimua sana, kuelimisha, na kufanya.
    Maoni yako ni muhimu sana kwangu.
    Karibu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. This comment has been removed by a blog administrator.

      Delete
  2. 🔥🔥🔥🔥

    ReplyDelete
  3. Kazi ni nzuri sana, inasisimua.
    Inaburudisha, inaelimisha, inaonya, n.k
    Umejitahidi sana kwakweli.

    Kuna makosa madogo madogo kama kuna uwezekano utayarekebisha, mfano katika SURA YA KUMI umetumia neno "arusi" badala ya neno "harusi", lakini kuna mkanganyiko wa majina katika mfululizo wa matukio n.k
    Kwa yote, kazi ni nzuri sana.
    Je, nawezaje kupata kazi nyingine kama hii?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nashukuru sana ndugu kwa maoni yako. Natumai nitayafanyia kazi. Kazi nyingine zilizopo kweny blog yangu zipo. 1. SIRI 2.MSAMAHA WA KWELI ? 3. MAPENZI KABURINI hii iko katika mfumo wa tamthiliya.
      Chakufanya ww ingia Google alafu andika jina la hadithi yoyote hapo. Mfano SIRI-Saidikaitastories.

      Nashukuru
      Mawasiliano: 0783372139

      Delete
    2. Au andika tu Saidikaitastories kisha utaangalia mipangilio ya hadithi nilizokuorodheshea.

      Delete
    3. Au andika tu Saidikaitastories kisha utaangalia mipangilio ya hadithi nilizokuorodheshea.

      Delete
    4. Kazi nzuri sana kaka,,always literary work is not from vacuum

      Delete
  4. Hongera sana kuelimisha jamii

    ReplyDelete
  5. Hongera sana kaka nimenifunza kitu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WIMBO WA AFRIKA MASHARIKI (EAC)

SIRI