SARA- Hadithi ya watoto

MWANDISHI: SAID KAITA HADITHI: SARA NAMBA: +255783372139 E-MAIL: saidikaita7@gmail.com Fb Page: Saidikaitastories.com Blog: Saidikaitastories.blogspot.com Sara ni mtoto mwenye miaka mitano. Anampenda sana mama yake, hupenda kukaa nyumbani na kujishughulisha na michezo mbalimbali kama vile kupika kwa kutumia matope. Ambapo, huchota maji, kisha hutafuta mahali ambapo pana mchanga mzuri na kujipikilisha mwenyewe. Ila, michezo yote hiyo hupenda kufanyia nyumbani kwao tu. Huwa hapendi kabisa kwenda kucheza kwa majirani, kwani huhofia sana mama yake akirejea asijemgombeza. Pia, huogopa kupigwa na wenzake kwa kuwa yeye ni mpole sana. Aonapo amechoka hutafuta sehemu nzuri na kutandika kwa vipande vya kanga ambavyo mama yake amempatia kama vya kuchezea. Michezo hiyo hufanya baada ya kumaliza shughuli zake ndogo ndogo ambazo mama yake humuachia pale nyumbani kama vile kufagia uwanja wao, kuosha vyombo kama vile sahani, bakuli na vijiko. Kabla mama yake hajatoka huwa amemwandalia vizuri vitu vyote hivyo na kumuacha sasa yeye apange muda wake wa kuviosha vyombo hivyo. Ifikapo muda wa kula huchukua jiko la mafuta ya taa na kuwasha kwa kiberiti ambacho mama yake alimuonesha atakitumia. Mara nyingi mchana hula wali, kwa hiyo humpasa Sara achukue wali ule na kwenda kuupasha kwa makini kisha hula. Mama wa Sara hupenda kurudi mapema sana baada ya mishughuliko yake ya siku. Siku moja mama Sara alichelewa sana kurudi. Sara alijiuliza sana maswali mengi. Kwa kuwa haikuwa kawaida ya mama kuchelewa hivyo. Kwa vile anampenda sana mama yake, Sara aliijiwa na mawazo ya kwenda kumtafuta mama yake popote alipo. “Lazima nimfuate mama alipo”. Sara alijisemesha mwenyewe kwa sauti ambayo ilionesha ina kiu ya kumuona Mama. Basi kwa ujasiri wake, alivaa koti lake vizuri ambalo aliwekewa na mama wake sehemu ya jikoni. Pindi asikiapo baridi ndipo huvaa. Baada ya kuvaa koti lile na kuhakikisha viatu alivyovaa kamwe havitamuumiza katika safari yake, ilibidi aanze safari. Hakutaka hata kwenda kuwaambia majirani zake huko anakoenda. Alianza safari polepole huku akifuata njia ambayo mama yake huitumia kila siku wakati anarejea kutoka mishughulikoni. Kwa muda huo tayari ilikuwa imeshatimia saa moja kasoro jioni. Tayari jua lilikuwa limeshalala na kuacha sasa anga ikiwa imenuna kwelikweli kama imepigwa na jua. Alitembea kama dakika kumi na tano lakini hakupata kukutana na mtu yeyote huko njiani. Jambo hili lilimshangaza hadi kujiuliza. “Leo kuna nini?” Ila, kutokuwa kwa watu vile hakukuweza kumkatisha tamaa. Bali aliendelea na safari hadi alipofika sehemu ambayo ina eneo kubwa sana la mchanga. Sehemu hiyo ilikuwa na kelele ambazo zilileta utofauti kidogo. Alipozidi kukikacha kichanga kilichopo katika eneo lile alishangaa tu kitu kimepita, “Mvuu” Ni sauti tu ya kitu alisikia kama kimepita japo hakuona chochote. Hakujali chochote juu ya hali iliyokuwa ikitokea. Alianza kuzunguka kuanzia sokoni ambapo mama yake ndipo hufanya kazi huko za upishi. Hapo hakuweza kumkuta, marafiki wa na mama Sara nao walikuwa wameshaondoka muda mrefu sana. Kwa hiyo, hakupata hata mtu wa kumuuliza. Baada ya pale kushindikana alienda hadi bwawani ambapo mama yake huenda kuchukua samaki huko lakini hakufanikisha kuona sura ya mama yake kabisa. Moyo ulimuuma sana kila anapoenda anamkosa mama yake. Ndipo alipoona bora aende katika duka la mchele ambapo mama yake hununua mchele wa jumla. Hapo nako alikuta pamefungwa kabisa. Sura yake ilimjaa huzuni sana. Alijua kabisa mama yake kuna jambo limemsibu, si bure kabisa. Ilibidi arejee nyumbani tu, alipokuwa akirejea nyumban alikutana na jirani yake aitwaye Roja alikuwa na baiskeli. Ilibi Roja ampatie lifti Sara. Roja alimuuliza maswali Sara "Mbona upo pekee yako? Ulikuwa wapi?" lakini Sara muda wote huo alikuwa amekaa kimya kama maji ya mtungini yakitafakari nani anakuja kunichota? Roja alijua kabisa Sara hataki kuongea. Roja alikanyaga pedeli hadi kufikia nyumbani kwa akina Sara. Walipofika hapo walimkuta mama Sara amesharudi na alikuwa ameshaanza kufikiri namna ya kwenda kumtafuta Sara. Sara alifurahi sana kumuona mama yake, pia mama Sara naye alifurahi sana. Mwisho FACEBOOK: Saidi Kaita Twitter: @SaKaitahadithi TiKtok: sakaitasimulizi

Comments

  1. Ndugu msomaji wa hadithi zangu, ninapenda kukukaribisha katika hadithi hii yenye mafunzo mengi sana. Ni hadithi yenye kuburudisha, kuelimisha, kuonya na kumpa ujasiri mtoto. Pia, kama una maoni usisite kuniandikia. Karibu sana!

    ReplyDelete
  2. Hadithi hii inalenga watoto kuanzia miaka mitano na kuendelea. Pia, ni hadithi inayofaa kusomwa na watu wote. Watajifunza mengi

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WIMBO WA AFRIKA MASHARIKI (EAC)

SIRI

PESA ILIVYO