MAPENZI KABURINI
MWANDISHI: SAID KAITA
MAWASILIANO: 0783372139
E-mail: Saidikaita7@gmail.com
Facebook Page: Saidikaitastories.com
Blog: Saidikaitastories
ONESHO LA KWANZA
(Ni mishale ya saa tano asubuhi. Durudu akiwa na marafiki zake kijiweni. Durudu anamuongelea msichana aliyerudi kutoka mjini siku si chache aitwaye Safi. Baadhi ya rafiki zake wanamvunja moyo kwamba hawezi kumpata Safi, mmojawapo ni Pajero. Baada ya rafiki zake kumpa maneno kuhusiana na Safi. Durudu anaamua kuondoka huku akiwa na mawazo mengi kwelikweli. Anapoelekea nyumbani anakutana na Safi njiani akiwa anaelekea nyumbani. Durudu anamsalimia kwa bashasha zote).
Durudu:(Anamsalimia kwa kumpa mkono).
Mambo vipi Safi?
Safi: (Safi anamjibu kwa mashauzi ).
Safi.
Durudu: Habari za mjini?
Safi: Nzuri tu.
Durudu: Huko Dar es salaam pazuri
kwelikweli. Kwasababu umerudi
ukiwa unang’ara sana.
Safi: Kawaida tu.
Durudu: Hasa unajua Safi… mara kwa
mara umeona nikikwambia sana
suala kuwa
mpenzi wangu. Lakini bado naona
kwako inakuwa kama mzigo
mkubwa sana.
Safi: “ anacheka kwa kumkebehi”
hahahaha!!!
Durudu: Unajua Safi nakupenda sana.
Safi: Asante sana.
Durudu: siyo hivyo ulivyochukulia.
Safi: Bali?
Durudu: Nataka uwe mpenzi wangu.
Safi: Mbona nina mchumba! Na
nilishakwambia tangu mwanzo
huelewi wewe Durudu?
Durudu: Hapana ila wewe nielewe bana
kwanza.
Safi: Wewe embu nielewe. Kwanza
wanipotezea muda mie. Mimi
siwezikuwa katika
mahusiano ya kimapenzi na
mvulana yeyote hapa mkurumuzi.
Siyo type yangu nyiye. Wewe
unaweza kuuhudumia huu mwili?
(Safi anaondoka na kumuacha
Durudu akiwa anamuangalia tu).
(Durudu akiwa anaelekea nyumbani kwa kweli anamuona rafiki yake anamuendea na kumsalimia. Durudu anamueleza Yule rafiki kuhusu Safi lakini rafiki yake anamwambia ajikaze tu atampata. Baada ya maongezi kuisha Durudu anaelekea nyumbani kwake huku akiwa anaongea peke yake kimoyomoyo akisema hivi).
"Huyu Safi ananiumiza kichwa hivi. kwanza si kuna Yule Maalim namsikia hapa Mkurumuzi atanifanyia mambo yote haya. Naenda kwanza hapa nina kama shilingi elfu tano hii inamtosha".
(mishale ya saa saba anaonekana Durudu akiwa na maongezi na Maalimu. Maalimu amevaa kanzu nyeupe na kofia ya kumuonyesha hadhi yake. Wote wamekaa chini ya mkeka.)
Durudu: Ahaa!!! Maalimu ni muda
mrefu sijakutembelea (Maalimu
anamkatisha maongezi
Durudu kwa kusema)
Maalimu: Kwa hilo ondoa shaka kabisa…
kwa hilo ondoa shaka kabisa
najua nyie ni moja ya
vijana hapa kijijini ambao mna
chacharika sana, Kwahiyo lazima mambo mengi yawepo.
Durudu: Ni kweli Maalimu (akanyamaza
kwa sekunde kasha akasema).
Maalimu Jambo kubwa
lililonileta hapa ahaa….. kuna ….
Kuna …. Mwanadada hivi.
Maalimu: Mwanadada?
Durudu: Ndiyo… ndiyo Maalimu
Maalimu: Mwanadada yupi huyo?
Durudu: Ahaa…. Wanamuita… Safi.
Maalimu: Anaitwa Safi?
Durudu: Ndiyo… ndiyo Maalimu.
Natumai utakuwa unamjua
nikikuelezea vizuri.
Maalimu: Embu nieleze vizuri,
Durudu: Mwanadada hivi… si mrefu
sana , si mfupi sana, ni majani
ya kunde, si mweupe
kwa ujumla, ana umbo Fulani hivi
zuri sana. Ametokea mjini Dar es
salaam juzi juzi tu hapa.
Kwahiyo vijana wa Uburungeni
wameshaanza
kumfatilia sana na
mimi namuelewa kweli kweli.
Maalimu: Ahaaa … kwaiyo unasubiri
nini angali u kijana mzima?
Durudu: Mimi nishamtongoza mara ya
kwanza, ya pili akakataa…. Sasa
kwa mara ya
tatu nikaona ngoja nije kwako.
Kwasababu najua wewe ndo kila
kitu na utanipatia kilainishi ili
nimpate huyu mwana dada.
Maalimu: Kwaiyo ndiyo lengo lako kuu
kabisa?
Durudu: Ndiyo Maalimu nataka
nikimtongoza tu anikubalie na
baadae jioni lazima aje geto
kwangu.
Maalimu: Basi hilo ni jambo rahisi tu
kama kilio cha samaki machozi
kuishia baharini tu na bahari
kuzidi kujaa.
Durudu: Fanya kweli Maalimu.
Maalimu: Ondoa shaka kwa hilo hapa
umefika. (anaonekana akiwa
anachukua kalamu ya mti na kisha
anachukua zaharani kidogo na kuikorogea katika kikombe kilichokuwa na maji kidogo kisha anaweka chini kikombe kile tayari akiwa ameshayakoroga maji. Anachukua kalamu yake ya mti na karatasi jeupe pee kisha akachovya kalamu yake kwenye maji yale yaliyo changanywa zaharani na kuwa rangi nyekundu. Baada ya kuchovya anaonekana anaanza kuandika maneno ya kiarabu katika karatasi lile jeupe. Baada ya dakika tatu akawa ameshamaliza kazi kisha akamkabiakiangalia karatasi iliyokuwa imefungiwa dawa ndani yake)
Durudu: (akipokea huku akiangalia
dawa ile kwa makini) Maalimu,
nipe maelekezo.
Maalimu: Hilo ondoa shaka ndicho
kinachofuatia.
Durudu: Ahaa… hapo sawa
Maalimu: hii dawa utakuwa nayo tu
jaribu kuitunza lakini kuna
maneno nimeshayaandika
hapa ya kuweza kumvuta nyota
na leo leo hatimaye
utatimiza haja yako.
Durudu: Kweli Maalimu ?
Maalimu: Haswaaa kwa hilo ondoa shaka
kabisa, ni kitu kidogo tu hicho na
lazima leo leo utampata.
Durudu: Basi nashukuru sana Maalimu
kwa msaada wako (anaingiza
mkono kwenye mfuko wa mbele
wa kulia kwenye suruali yake na
kutoa shilingi elfu tano
kisha anamkabidhi Maalimu).
Maalimu: (Anapokea hela huku akisema)
nashukuru kwa kutambua
mchango wangu kwako.
Durudu: Sawa Maalimu. Basi …..Maalimu
acha mimi nigeuze.
Maalimu: Sawa utanipa taarifa.
(Durudu anapotoka kwa Maalim huku akiwa anafurahia kwelikweli akijua lazima tu atampata Safi kwa urahisi tu. Ghafla kwa mbele anamuona Safi akiwa anaelekea dukani, anamuendea anamfuata na kumsalimia).
Durudu: (Anamsalimia kwa kumpa mkono).
Tumekutana tena.
Safi: (Akiwa anafurahia kwelikweli).
Yaani hadi nashangaa.
Durudu: Usishangae… mambo ya kawaida
haya bana. Kwanza watoka wapi?
Safi: Natokea hapo nyumbani kuelekea
dukani.
Durud: Aaaa… aaaa …. Unajua …. Unajua
Safi mimi bado na shida kwako.
Safi: Yanini?
Durudu: Uwe mpenzi wangu.
Safi: Unajua Durudu hata mi
nakupenda sana ni kwa vile tu
muda ule hukuja na style
nzuri tu.
Durudu: Kweli kabisaa?
Safi: Kwanini nikufiche?... Huo ndiyo
ukweli.
Durudu: Sawa basi. Vipi unaweza kupata
nafasi ukaja leo pale kwangu?
Safi: Ndiyo nitatumia njia yoyote hadi
nije tu. Ila si pale pale ulipokuwa
unaishi?
Durudu: Ndiyo… ndiyo ni pale pale.
Nihamie wapi tena tofauti na hapo.
Safi: Haya basi.
Durudu: Kwahiyo utakuja saa ngapi?
Safi: Kuanzia saa moja hivi wewe
nisubirie tu hapo nyumbani kwako
ukijua leo una mgeni.
Durudu: Sawa.
Safi: Haya basi acha mimi nielekee hapo
dukani kwanza.
Durudu: Sawa.
(wanaagana kwa kukumbatiana. Safi anaondoka na kumuacha Durudu akiwa anamuungalia tu namna alivyojaaliwa umbile lake. Durudu anafikiria usiku wake wa leo utakuwa ni usiku mzuri sana kwa ugeni alioupata. Basi anaelekea hadi nyumbani kwake. Chumba anachoishi ni chumba kimoja tu. Kwahiyo akaingia na kuanza kupanga vizuri na kupafanyia usafi.Saa moja jioni giza limeshaanza kuingia.Durudu anaonekana amekaa hapo nje ya mlango wake akiwa anamsubiri huyo Safi. Tochi ikiwa imewaka kuleta mwanga kidogo.Ghafla anamuona Safi anakuja, anamkimbilia na kumkumbatia na kusema hivi).
Durudu: (akiwa amemshika Safi kiuno).
Daaaa… unajua siamini kama ni
wewe umekuja hapa.
Safi: Ndiyo uamini. Jamani mi
n'taanzaje kukudanganya sasa.
Durudu: Haya karibu ndani basi.Au
unataka tukae nje kwanza.
Safi: Hapana sijaja kwa ajili ya kukaa
nje.
Durudu: Haya basi twende ndani mpenzi
wangu.
(Wanaingia ndani tayari wala hataki kusubiri kwa sasababu haamini kama ni kweli yuko na Safi muda ule. Tayari wakaanza kutomasana Durudu akiwa na matarajio kweli ya kumfikisha kileleni ili afanye lake jambo kwa urahisi. Tayari Safi anajikuta kitandani kalegea Safi anasikika akisema hivi).
Aaaaaaa…
******************************************
. ONESH0 LA PILI
(Asubuhi kumepambazuka Safi ndiyo anaamka yuko kavaa vinguo vya kumuonesha tu viungo vyake vyote vya ndani. Durudu naye yuko pembeni hapo akiwa ana furaha kwelikweli kwa mtomasano wa usiku mzima. Durudu anasikika akisema hivi ).
Durudu: Mpenzi wangu…
Safi: “Anaitika kwa sauti ya chini tena
ya puani” yes honey.
Durudu: Usiku wa leo ulikuwa mzuri
sana. Yaani nilikuwa natamani
kabisa hata pasikuche kwa utamu
huo. Amakweli wewe mtoto ni
mtamu sana.
Safi: Asante Duru…. Yaani hata mimi
mwenyewe hata sikuwa nataka
pakuche Kabisa.
Durudu: Safi nakuomba tu usiniache.
Kwasababu ulivyoniachia utamu
wa leo hii halafu Kesho nije
kusikia uko kwa mwingine kwa
kweli roho itaniuma sana.
Safi: Hapana sitokuacha. Kuwa huru
kabisa hapa ndiyo kwako na hii ni
mali yako. Mwenye dhamana ni
wewe tu.
Durudu: Haya sina la kusema.
Safi: Basi sawa Duru acha mimi nirudi
nyumbani.
Durudu:Hawatokusumbua huko
nyumbani?
Safi: Waanzie wapi. Mimi mtoto wa
mjini bana lazima niwe huru…
angali mama yangu anayajua
haya vyema tu.
Durudu:Haya bana. “Anamchumu Safi na
tayari wanainuka na kutoka nje”
“Ni hapo hapo katika kijiji cha Mkurumuzi kwa muda unaonekana ni asubuhi hivi. Durudu na Pajero wakiwa na maongezi ya hapa na pale. Wamekaa kwenye gogo”.
Durudu: Unajua Pajero leo mimi kama
nakuona hauko fresh vile… au
vipi?
Pajero: Aaaa…. Unajua bana haya mambo
gwaride…. Amakweli gwaride
halina adabu.
Durudu: unamaanisha nini Pajero?
Pajero: si juzi juzi tu hapa wewe ulikuwa
unalalamika kuhusu huyo Safi.
Durudu: ndiyo… kwani inaingilianaje na
mambo ya gwaride sasa?!
Pajero: ulikuwa msemo tu. … aaa kwa
ujumla ni kwamba kuna yule wa
kuitwa Sofi. Yaani hata kama ni
mke wa rafiki yangu kwakweli
hapa mambo ya ushemeji
nimeyashindwa…. Eeee bwana
namtamani Yule mtoto kwelikweli.
Nashanga juzi tu hapa Yule Rojo
katokea Dar eti tayari kammiliki.
Sasa sijui nitampataje?
Durudu: sasa Pajero ya nini ukwamwe na
tonge wakati mlenda upo?!!!.
Mbona jambo rahisi Sana hilo.
Kwani mimi mbona ilikuwa rahisi
tu kumpata Safi. Huoni sasa hivi
Safi analala pale geto anaamkia
pale mageto na
anashinda pale mageto. Yote hii ni Kwasababu tu ya Maalim, mzee wa
kuunganisha nyota na namna yoyote tu utakavyo ili umpate huyo
unayemtaka.
Pajero: kwani shilingi ngapi vile alikufanyia?
Durudu: mbona hilo buku tano tu yaani chapu siku hiyo hiyo mambo mtelezo.
Pajero: basi sichelewi umeshanifungua tulia nijipange kwa hako kabuku tano hata
niuze kuku tu hapa ili nimpate Sofi.
(mazingira yanayoonekana ni nyumbani kwa maalim ambapo amevaa kishekhe Huku Pajero akiwa amekaa kitako kwenye kirago kakunja nne)
Maalim: Nhaam kijana embu jieleze….
Pajero: Daaaa…. Maalim mimi kuna mwanadada namhitaji niwe naye kimapenzi ila ndiyo
Hivyo kuna mtu ameshamuwahi.
Maalim: hilo ondoa shaka kabisa. Wewe cha msingi unachotaka ni kwamba huyo
Mwanadada awe nawe kimapenzi au sivyo?
Pajero: Ndiyo Maalim.
Maalim: Mwanadada anaitwa nani?
Pajero: Anaitwa Sofi.
Maalim: Ahaaa…. Unataka tumfanyaje huyo mume wake?
Pajero: Hata kumlaza uume kama ikiwezekana.
Maalum: Ni maamuzi yako tu. Ndiyo maana nimekuuliza kwanza wala
sijakulazimisha mimi. Ndiyo Maalim hapa Mkurumuzi hashiki mtu hapo.
Yaani mimi mchana kweupe . Naweza kukubadilisha wewe mwanaume
kuwa mwanamke. Mbona wananijua Wengi tu. “anachukua karatasi akiwa
anaandika kupitia kalamu ya mti iliyotiwa
Katika maji yaliyochanganyiwa dhaharani na kuwa ya rangi nyekundu.
Anamkabidhi kikaratasi hicho kilichoandikwa maandishi ya kiarabu kisha
anamwambia hivi” sasa hii karatasi ishike na uishike vizuri kabisa. Nenda
nayo kwa hapa mambo tayari.
Pajero: Kwahiyo lini mambo yatakuwa yamenyooka?
Maalim: Leo hii hii…wewe nenda kaandae kitanda chako tu.
Pajero: Shukrani sana Maalim. “anaingiza mfukoni na kutoa shilingi elfu tano na
Anampatia Maalim kisha Maalim akasema hivi”.
Maalim: Ahsante. Karibuni tena.
(Ni siku hiyo hiyo. Pajero na Durudu wako maeneo yao ya kupigia hadithi).
Durudu: Vipi Pajero ushaweka mambo sawa?
Pajero: Ndiyo nimetoka muda si mrefu huko kwa Maalim.
Durudu: Ahaaa hapo tayari yaani leo leo hii Sofi anakuja hapo mageto kwako. Hiyo lazima.
Pajero: Duuuuu siamini mpaka aje. Kwasababau yaani ungejuwa kitambo sana yaani
Nilikuwa nikimtamani sana Sofi. Yaani kama kweli leo nitamfanikisha daaaa
ntakuwa sijui kama nimesafiri hadi Uchina kwa miguu.
Durudu: Acha mambo yako bana hawa watoto kuwapata ni kiurahisi tu. Yaani Mzee wa
kulainisha yuko pale halafu tushindwe kuwapata. Yaani sasa mimi hapa kijijini
ndiyo nataka nipitie visichana vyote vinavyojifanya mida saa sita kifuani. Kila
siku kumeza mate tu hadi koo linakauka sitaki.
Pajero: Ndiyo maana yake.
(Ndani kwa Pajero. Panaonekana kuna taa ya solar imewaka. Kitandani wako
Sofi na Pajero. Sofi akiwa amevaa dera).
Pajero: “Anaongea kwa kujifanya kama hajui chochote kabisa kuhusu Sofi kuja
muda huo Kwa kuwa Sofi na Rojo tayari pameshatokea mtafaruku” Unajua
mimi nimeshangaa sana kwa wewe kuwa muda huu hapa.
Sofi: Hapana Pajero haina haja ya kushangaa. Kwasababu kuna haja gani ya
mimi Kulala na mwanamume ambaye jogoo hawiki?
Pajero: Jogoo hawiki?!!!
Sofi: Ndiyo.
Pajero: Kwahiyo rafiki yangu Rojo jogoo hawiki kabisa?
Sofi: Ndiyo. Wewe unafikiri mimi
kuja usiku huu kwako ni kirahisi tu. Mimi ni
msichana na si msichana tu wa kukaa ndani usiku kazi yangu inajulikana. Sasa
ninapolala na mwanaume ambaye lifti haipandi si bora nije kwako tu.
Pajero: Haya bana. Kwahiyo kwasasa
nikuite shemu au nani?
Sofi: Niite mke. Embu tupeane
utamu bana. “Na taa inazimwa”
******************************************
ONESHO LA TATU
(Ni mishale ya asubuhi inaonekana kumeshapambazuka. Kijiji kimechachama watu wanapita huku kule wakiwa kila mtu na yake. Huyu anaenda shambani, mwingine mtoni na sehemu nyingine nyinginezo. Rojo akiwa na hasira kwelikweli anaonekana akiwa anaelekea kwa rafiki yake wa karibu ambaye ni Pajero. Rojo anaonekana amevaa suruali ya jinsi ya rangi nyeusi na tisheti nyeusi. Anafika kwa Pajero anakuta mlango uko wazi anaanza kuita huku akiwa anagonga mlango kwa nguvu).
Rojo: Pajero…
Pajero: “kimya”
Rojo: Pajero…
Pajero: “Anaitikia huku akiwa amelala”
Oya nani wewe?
Rojo: Eeee bwana embu toka huku nje.
Mimi Rojo hapa…
Pajero: “Pajero anainuka na kulitupa
shuka lake anaangalia kwa
dirishaani kumeshapambazuka
kabisa. Anaanza kuongea
kimoyomoyo akisema hivi ”. Huyu
Rojo asubuhi yote hii ndiyo
amenijia kwasababu ya huyo mke
wake. Mhhh… embu
nikamsikilize anasema nini.
Rojo: Pajero embu toka haraka haraka.
Pajero: Kwani kuna nini Rojo? “ Tayari
Pajero muda huo ametoka akiwa
amejifunika shuka tu”
Rojo: Hivi Pajero rafiki yangu wa karibu
kabisa ndiyo umeamua kunifanyia
kabisa hivi?
Pajero: Kukufanyia nini?
Rojo: Unataka ujifanye hujui chochote
angali hii movie umeicheza wewe
kabisa. Yaaani kabisa Pajero
unaamua kunichukulia mke wangu
kabisa na kuja kulala naye usiku
mzima na asubuhi ndiyo anakuja
kama mfanyakazi wa ndani alalaye nyumbani kwao.
Pajero: Yaani ndiyo hicho kilichokufanya
ukadamka asubuhi yote hapa na
kuja kunipigia makelele asubuhi
hii. Wakati huyo mke wako ndiyo
amekuja mwenyewe hapa na
kanihadithia story nzima ikabidi
nimkaribishe kwangu hapa.
Rojo: Hongera sana kwa kuwa na ujasiri
wa kuongea hivyo. Ila jua tu siku
zote malipo ni hapa hapa duniani.
Namshukuru Mungu na mimi
nimeshampata mwanamme
mwenzangu mwenye UKIMWI kwa
hapa mkurumuzi na ninajua kuna
zaidi ya wewe ambao
wameshamparamia huyo Sofi.
Unanunua embe kwa kuangalia
ganda lake tu. Kuwa makini. (Kisha
akaondoka na kumuacha Pajero
akiwa ameduwaa tu kwa
maneno ya mwisho aliyoyasikia)
(Ni mchana wa saa nane wanaonekana Maalim na Durudu wakiwa katika mazungumzo. Sehemu waliyokuwa wamekaa ni kwenye kirago. Maalim kama kawaida yake mzee wa kanzu muda wote kofia nyeupe kanzu ikiwa ni nyekundu).
Durudu: Unajua Maalim yaani leo
dhumuni kubwa la kuja mimi
hapa… laaa kwamba ni kuja
kukushukuru tu kwa msaada
mkubwa ambao unakuwa
unanifanyia kwa kweli.
Maalim: Hilo ondoa shaka kabisa Durudu. Unajua kama umejaaliwa kuwa na
msaada fulani basi usikatae
kuwapatia watu. Ni vyema
kuwasaidia watu ili wasiendelee
kuteseka na mambo
yanayowakumba.
Durudu: Yaani si kwa hao wadada tu yaani hata kwenye kesi mbalimbali za
mashamba hapa kijijini
umenisaidia sana. Yaani kwasasa
hao wadada kwanza mbona
wananikoma sana.
Maalim: Lazima wakukome kwasababu
tayari ushapitia kwa simba hapa
lazima msitu usinyae.
Durudu: Hivi Maalim si huwa unawapata
sana? Kwasababu kama sisi tu
unatufanyia hivi, je vipi kwa wewe
mwenye mauwezo kabisa?
Maalim: Unajua mimi huwa nawashangaa
sana hao wanaosema eti oooh...
mganga hajigangi waseme tu
kwamba daktari hajigangi.
Durudu: Kwanini Maalim?
Maalim: Yaani mimi nimuone msichana
Yule pale tayari ameshaanza
kutunisha kifua kama njiwa
manga halafu nimuache. Kwa
ujinga upi huo nilionao. Yaani
mimi nachinja juu
kwa juu.
Durudu: Kweli lazima uwanyooshe.
Maalim: Yaani hutoamini kuna msichana
nilikutana nae huko Mwanza
tukawa tumejuana chapu chapu
halafu nikaondoka zangu.
Nilipofika tu nyumbani nikamkalia . kwenye kirago hapo nikayafanya
mambo yangu hapo mbona
nakwambia kesho yake ananipigia
simu anataka kuja kwangu.
Durudu: Kwahiyo ikawaje?
Maalim: Heee…. Kuja hapa kwangu vigumu wewe nilichomfanya nikumpeleka
guest house hapo galapo. Nilikaa
nae wiki nzima tu nakwambia
nilipiga kavu kavu.
Durudu: Hukumleta hapa?
Maalim: Hapana weee aliishia kule kule
asubuhi nikampandisha Noah za
kwenda Babati nikaona
hapana ni bora nimpeleke mpaka
Babati tu. Saa ngapi vile ilipofika
tayari magari yanayotokea Moshi
hayo hapo akapanda ndiyo moja
kwa moja hadi leo. Kwanza
nikamzimisha kabisa kumbukumbu
kwangu.
Durudu: Duuuu Maalim wewe hatari sana
unajua.
Maalim: Vitengo vyetu hivi.
Durudu: Basi sawa Maalim acha mimi
nigeuze hivi.
Maalim: Inshaallh.
“Ni mazingira ya nyumbani kwa Maalim. Maalim anaonekana yuko kitandani akiwa analia tu kwa pembeni anaonekana mdogo wake akiwa amesimama hapo akimsikiliza kaka yake anavyolalamika. Kitanda alicholalia ni kitanda cha kamba ambacho ni cha tandika tukaze huku akiwa amejifunika shuka la kiarusha. Ndani hapo panaonekana kuna kibatari tu kimewaka kinatoa moshi kwelikweli kama vile gari moshi. Haruna anamwambia Maalim hivi”
Haruna: Hivi kaka embu niambie ni
ugonjwa gani huwa
unanisumbua? Kwasababu
wewe naona kama unanificha
hivi kwa vile mimi ni mdogo. Ila
tu kumbuka hata kama mimi
ni mdogo vipi mimi ndiye
ninayekuhudumia kila siku
halafu unataka kunificha, haya
leo hii imefikia mahali unahemea
juu juu tu hata sielewi nianzie
wapi. Embu nakuomba kaka
usinifiche.
Maalim: “Akiwa anaongea huku anaonesha kabisa sauti yake haimfikishi
mahali popote” mdogo wangu hii
hadithi ni ndefu sana.
Haruna: Hapana kaka najua kweli hadithi
ni ndefu ila unaweza kuongea hata
kwa kufupisha tu ila nijue ni
namna gani ya mimi kuelewa.
Maalimu: Haruna hii dunia iko duara.
Kwahiyo ni mzunguko yaani kuna
vitu vingi sana utakutana navyo
wakati wa mzunguko wako ila ni
wewe tu kuamua kuvikwepa au la.
Haruna: Mbona kama bado wanificha
kaka embu ingia kwenye mada
husika kaka. Huoni na hata hii
sauti yako haiwezi kukufikisha
mahali!...Wewe unataka treni iishe
mafuta msituni na msafara bado
kilometa mia?!. Embu jieleze kaka
nijue zaidi. Usizunguke mbuyu
sana. Kwasababu naona kama
unajing’atanga’ata sana Kaka.
Maalim: Unajua mdogo wangu hii kazi
yangu niliyokuwa nikiifanya ndiyo
iliyonifikisha hadi mimi kuwa
hivi!!!...Haruna ni kwamba kwanza
mimi nina huo ugonjwa wa
UKIMWI.
Haruna: UKIMWI kabisa kaka? Mbona
ulikuwa unanificha, kwanini?
Maalim: Ndiyo Haru… Haruna siyo muda
wa kulalamika huu.
Haruna: Sasa mbona muda mrefu sana
ulikuwa ukinificha sana . Haya
uliupataje kaka huo UKIMWI?
Maalim: Mdogo wangu nimeupata kijinga
sana huu ugonjwa. Yaani ni
kwasababu ya matamanio tu ya
wasichana. Haruna yaani hakuna
msichana mzuri aliyepita machoni
mwangu nikamtamani halafu
nikamuacha salama kabisa. Pia hii
kuparalaizi unayoiona hapa kwa
huu upande wa kushoto ni hayo
hayo mambo ndiyo yamenifanya
hivi. “kimya kwa sekunde chache
kisha akaendelea kuongea” kuna
shekhe nilimtumia talasimu….
nilikuwa namjaribu kama
nitamuweza kumbe yuko ngangari
lile kombora likanirudia mimi na
mwisho wa siku ndiyo maana
waniona hapa upande huu wa
kushoto wote umeparalaizi kabisa.
Haruna: Kaka yangu pole sana ila ndiyo
hivyo mipango ya Mungu tu.
Maalim: Niseme tu mdogo wangu hii kazi
niliyokuwa nikiifanya usije hata
siku moja ukasikia kuna mahali
wanafundisha halafu na wewe
ukaende kusomea haifai kabisa hii.
Yaani kumbuka sisi wanadamu
tumeumbwa na tamaa. Mwisiho wa
siku ukishasomea tu hii kumvuta
nyota msichana yeyote na kufanya
lolote lile ni uamuzi wako tu. Haya
mambo achana nayo kabisa kaa nayo
mbali…
Haruna: Pole sana kaka. “kanyamaza pale
na baada ya dakika chache tayari
Maalim anaaga dunia. Mdogo wake
muda huu akawa
amechanganyikiwa kwelikweli.
Ikabidi atoke kwenda nje na kuanza
kuwaita majirani”.
(Ni kijiweni wamekaa Pajero na Durudu kwa pembeni pia kuna vijana wengine wakiwa wanacheza bao hapo pamoja na wazee. Ndiyo maeneo yao mazuri ya kuja kupumzika baada ya kupata chakula cha mchana. Hapo basi kukawa na soga kati ya Durudu na Pajero. Sehemu waliyokaa ni kwenye kivuli cha mti uliokuwa umetandaza kivuli kizuri sana katika eneo hilo na maeneo mengine kukiwa na jua kali limewaka. Pajero anaonekana amevaa suruali ya jinsi ya bluu yenye kupauka tu hivi na shati jeusi likiwa limepauka sana akiwa amevaa yebo. Durudu kavaa shati la mikono mirefu la rangi nyeupe la kitambaa lakini limechanika begani na suruali ya kitambaa na chini kavaa katambuga)
Durudu: Daaa eeeh bwana Pajero ndiyo
hivyo mtaalamu wetu ameaga
dunia.
Pajero: Daaa kwa kweli hili jambo
limenishtua sana unajua.
Durudu: Yaani nilikuwa bado na uhitaji
naye sana. Kwasababu kuna
mavitu mengi sana nilitaka
nimtumie.
Pajero: Ila ndiyo hivyo mipango ya
Mungu haina makosa.
Durudu: Ni kweli ila ndiyo hivyo. Yaani
kuna kesi fulani hivi ya shamba
ndiyo nilitaka nimtumie ili
nishinde hiyo kesi sema ndiyo
hivyo sina namna.
Pajero: Nasikia pia UKIMWI ndiyo
umemchukua haraka hivi!
Durudu: Inaweza ikawa ni kweli. Kwa
sababu na yule Maalim naye kwa
kurukia visichana na wamama wa
watu alikuwa hajambo.
Pajero: Ila ndiyo hivyo huyu ashakuwa
marehemu kwahiyo wala hata
tusimkalie kikao kabisa kwa sasa.
Yeye Mungu ndiye atajua nini cha
kumfanya.
Durudu: Duuu ni kweli ila kwasasa
kuwapata wasichana itakuwa ni
ngumu sana labda tupate fununu
za mtu mwingine ambaye
hujishughulisha na haya mambo. Ila
kama yeye amefariki kwa huo
ugonjwa sijui sisi tutafariki kwa
ugonjwa gani. Gonjwa linatisha hili
na sisi ndiyo watu wenyewe wala
hatutumii mipira tunajifanya
uwanjani tuko vizuri tunacheza
pekupeku tu hapa mwisho wa siku
ndiyo hivyo tunakuja kuchomwa na
mbigiri. Matokeo yake ndiyo hivyo
kuhudhuria hospitali kutaanza kama
vile mama mjamzito. Oya tuwe
makini kijiji cha mkurumuzi
kimeshawaka moto.
******************************************
ONESHO LA NNE.
( Jukwaani, nyuma ya jukwaa anaonekana Durudu na Daktari. Daktaria amevaa koti lake jeupe akiwa amekaa kwenye kiti huku akiwa amevaa miwani na nywele zake zikiwa ndefu kidogo na ukutani panaonekana kuna kalenda imebandikwa ya 2011. Durudu yuko hapo amekaa kwenye kiti akiwa amevaa suruali ya jinsi na shati jeupe. Basi kulikuwa na mahojiano kati ya Daktari na Durudu kuhusu vipimo alivyofanya vya UKIMWI).
Daktari: Aaaa kijana… umesema unaitwa
Durudu?
Durudu: Ndiyo dokta.
Daktari: Ahaa… sawa. Unajua Durudu ni
vijana wachache sana katika kijiji
hiki ambao wanaamua kweli kuja
kuangalia afya zao kama wewe
hivi ulivyokuja mwenyewe
asubuhi na mapema.
Durudu: Kweli dokta…!!!!
Daktari: Hutoamini leo hii ni tarehe ya
20/01/2011 tangu mwaka uanze
hamna hata mtu mmoja
aliyejitokeza kuja kupima afya
hapa. Si vijana wala si watu wa
aina gani. Na ukumbuke watu,
mwaka mpya wamefurahia sana
hapo Kikore usiku kucha. Watu
wanajamiiana tu bila hata
kutumia kondomu. Yaani
nikupe hongera tu kwa kuja
kupima. Kwahiyo kwa muda huu
unaosubiria majibu yako hapa ni
bora nikupe somo kidogo.
Kwasababu haya mambo ni
mambo ambayo yako tu sana.
Durudu: Ila lakini dokta ndiyo hivyo kweli
unakuta mtu anatambua kabisa
kwamba ana UKIMWI lakini
anaogopa hata kuja kuchukua
dawa. Kwahiyo nayo
changamoto kubwa sana hii.
Daktari: Unajua Durudu kuna watu
wanasumbuliwa na magonjwa
makubwa sana kama vile kansa
na kadhalika katika dunia hii na
hadi kuna muda mwingine
wanamuomba Mungu kwa kusema
kwamba ni bora hata mungu
angewapatia hata huo UKIMWI tu. Kwahiyo ukisema uoga yaani hiyo
ni dhana potofu kabisa unajua.
Inabidi iondolewe akilini
Durudu: Kwahiyo dokta unaniambia ni
bora kujua afya yako mapema.
Daktari: Ni sawa ila si kujua tu afya yako
mapema tu. Bali pia ukishajua
mambo yameenda vibaya ni
vyema mapema ukaanza kutumia
dawa za kukufanya hata kuweza
kupunguza makali yake.
Durudu: Ahaa hapo umenifungua sana
akili.
Daktari: Tatizo kubwa katika hiki kijiji cha
mkurumuzi ni kwamba watu
wanajua kwamba mtu ukishapata
tu UKIMWI tayari wewe kufa
kwako kuko karibu Lahasha…
siku zote kama tatizo hujalitafutia
suluhisho lazima tu tatizo lile
likumalize. Mbona kuna baadhi ya
watu huwa wanakuja kuchukua
dawa hivi hapa kwa kila siku zao
walizoandikiwa na ndiyo wanaishi
vizuri tu na miili yao ukiiangalia
hutoamini kama ukiambiwa huyu
ana UKIMWI.
Durudu: Kwahiyo unataka kuniambia
kwamba kuna wasichana huwa
wanakuja kuchukua dawa hapa
hizo za kutuliza makali?
Daktari: Ndiyo. Huwa wanakuja hapa
wanachukua na miili yao naiona
inanawiri tu kila siku. Ninawajua
kabisa tena na huko huko kwenu
ulikonieleza unaishi. Kuna mdada
rangi ya majani kunde hivi mrefu
wa size ya kati hivi anasema
alikuwa akiishi mjini huko.
Durudu: “ Akawa ameshamtambua ni nani
anaongelewa. Akaongea
kimoyomoyo akisema hivi” Huyo
ni Safi wala si mwingine. “ kisha
akamwambia daktari hivi” Hapo
nimekuelewa.
Daktari: Unajua usiwe na uoga kwa kitu
ambacho kama ni kutokea
kikiamua kutokea kinaweza tu
kutokea. Kwahiyo wewe hapo
hata kama ukikutwa una huo
UKIMWI si jambo la kukufanya
wewe kujinyonga. Hiyo itakuwa ni
siri yako na wewe utakuwa
unakuja kuchukua dawa tu hapa
na siku zinaenda. Usifanye maisha
yako kuwa magumu. ( kwa nje
kunasikika kuna sauti ya
muhudumu inaita majina ya watu
kuja kuchukua vipimo vyao. Jina la
Durudu linasikika anatoka nje kwa
kwafungua mlango kwa haraka na
kusema hivi)
Durudu: Kama ni Durudu niko hapa.
Muhudumu: Ahaaa …. Kumbe ndiyo
wewe chukua karatasi yako hii
hapa.
Durudu: “ Anapokea karatasi yake ya
majibu na kuangalia ikiwa
imeandikwa Positive lakini
haelewi inamaanisha nini.
Anaamua kuingia kwa daktari
akiwa na karatasi yake ya
majibu na kumpa daktari
karatasi ile”. Daktari embu
sijaelewa vizuri inamanisha
nini hii kama umeandikiwa
Positive?
Daktari: Yaani kwanza huyu
muhudumu amefanya vibaya
sana kwa kugawa karatasi
kiholela holela tu. Mjinga kweli huyu tulia nitaongea nae baadae.
Durudu: Sawa dokta… ila wewe
niambie hii inamaanisha nini?
Daktari: Unajua Durudu kama
nilivyoongea na wewe tangu
mwanzo na nikakwambia kwamba
hata kama hautakutwa na UKIMWI
wewe hiyo itakuwa ni siri yako tu.
Si kwamba ndiyo unatoka hapo
nje na kuanza kutangaza huko.
Hapana si vyema, natumai
umenielwa vizuri?.
Durudu: nimekuelewa dokta.
Daktari: pia kinyume chake yaani kama
umegundulika unao ni vyema iwe
siri yako. Kwa ujumla ni mimi na
wewe ndiyo tunajua tu.
Durudu:sawa dokta… kwahiyo majibu
yangu vipi?
Daktari: Aaaaa…. Durudu kwa ujumla…
umeathirika.
Durudu: (kwa sekunde kama tano akiwa
kimya) nimeathirika…!!!!
Daktari: Ndiyo Durudu… cha msingi tu
umenielewa tangu mwanzoni.
Kwahiyo wala usiwaze sana.
Nitakuandikia dawa tu hapa na
pia siku ambazo utakazokuwa
unakuja kuchukua. Usije
ukakata tamaa kabisa katika kuja
kuchukua dawa.
Durudu: Sawa dokta.
Daktari: Sasa hii karatasi ichukue na
itunze vizuri kama nilivyokuambia
ni siri yako. Pia chukua hizi dawa
kazihifadhi sehemu nzuri na
uzitumie kama nilivyokuandikia
hapo.
Durudu: “ Anapokea dawa na kuinuka
huku akimshukuru daktari. Tayari anatoka nje huku akiwa
anawasalimia wagonjwa walioko
katika foleni. Hapo anakutana
na bango limeandikwa kwa
maandishi ya rangi nyekundu
yakisomeka hivi”.
KONDOMU KINGA MADHUBUTI. TUMIA MARA KWA MARA KAMA KWELI UNAMPENDA MWENZA WAKO. TUMIA KWA MAKINI ILI UEPUKE KUUPATA UKIMWI NA HATA MIMBA ZISIZOKUWA NA MATARAJIO.
“ Anaondoka na kusema hivi” kweli hii ndiyo raha ya kuja hospitali sema ndiyo hivyo nimekumbuka shuka kumekucha. Mbu wamening’ata hadi basi.
(Ni jioni kwa jua la saa kumi hivi. Pajero amekuja kumtembelea Durudu na kumkuta Durudu akiwa amekaa nje kwenye kigoda huku akiwa anasikiliza redio. Pajero naye anakaa kwenye kigoda. Nguo alizovaa ni shati la mikono mirefu na suruali nyeusi ya jinsi. Pajero amevaa kanzu nyeupe na kofia nyeupe na miguuni amevaa ndala za batabata).
Durudu: Ahaaa kijana umekuja
kunitembelea leo…
Pajero: Aaa nikasema embu tulia kwanza
nikamtembelee jamaa yangu…
kwasababu tangia uoe hata
sijawahi kuja tena hapa. Kwahiyo
nikasema isiwe mbaya sana acha
leo niirushe miguu yangu hapo
kwa rafiki yangu na bahati
nimekukuta.
Durudu: Ahaaa sawa bana kijana. Karibu
sana si unajua tena kwa sasa hii ni
kaya. Unajua Pajero maamuzi ya
kuoa kwakweli niliyafikiria sana.
Nikasema hapa unaweza hata
ukafa kesho hujaacha hata
mbegu yako hapa duniani
Kwahiyo nikaona ni bora tu nioe.
Pajero: Ni kweli.
Durudu: Wewe ndiyo tayari Sofi umeamua
kumshikilia moja kwa moja.
Pajero: Ndiyo hivyo ilibidi tu ipigwe tu
ndoa ya mkeka tu hapa na ndiyo
tayari mke wangu hivi na tayari
kwasasa nishamuweka mimba.
Durudu: Hujataka kuchelewa kabisa!
Pajero: Nani achelewe. Hizi siyo karne za
kina Ibrahim wewe kuzaa mtoto
ukiwa na miaka karibia na mia
huko. Siyo karne hii yaani
mapema tu.
Durudu: Ni kheri kufanya hivyo. Unajua
pia Pajero hapa kijijini kuna huu
ugonjwa yaani nakwambia
unasambaa kwelikweli kama
kuharisha ukiwa safarini.
Pajero: Upi?
Durudu: UKIMWI…
Pajero: Duuuu yaani afadhali Durudu
umeanzisha hiyo mada.
Kwasababu nakumbuka siku ile
ya kwanza tu Sofi alivyokuja
kulala kwangu nakwambia
asubuhi yake Sofi si alirudi
nyumbani kwa Rojo na kumwambia
kwamba alikuwa kwangu. Kwahiyo
jamaa asubuhi asubuhi katimba
kwa muhuni.
Durudu: Kijana ikawaje? Kwasababu
hujawahi kuniambia kabisa hilo.
Pajero: Nakwambia kuna maneno ya
mwisho aliniambia yaani hadi
nikawa nimebaki nimeduwaa tu
sielewi hata niongeee nini hasa.
Durudu: Alikuambiaje?
Pajero: Kwamba ameshapata kijana
mwingine mwenye UKIMWI hapa
kijijini mkurumuzi.
Durudu: Hiyo nayo si ya utani Pajero.
Kwahiyo alikuwa anamaanisha
ameshamuambukiza Sofi na Sofi
atakuwa amekuambukiza wewe au sio?
Pajero: Inaweza ikawa…
Durudu: tusiandikie mate kwanza
ulishawahi kwenda kupima?
Pajero: Yaani kwenda kupima hospitali
kabisa?....
Durudu: Ndiyo kwani watu huwa
wanapima wapi Pajero? Huu
ugonjwa hauangaliwi kwa macho
tu hivi. Wewe nenda kapime tu
ujue nini haswaa Hatima Yake.
Kwasababu kila mtu afanyapo
jambo fulani Hatima Yake hutokea
baada ya kufanya jambo hilo.
Hiyo hatima inaweza kuwa nzuri
au laa. Kwahiyo ni vyema kujua
afya yako. Tena ikiwezekana
muende wote na huyo mke wako.
Kwasababu inawezekana yeye
huyo Sofi akawa anao lakini wewe
huna. Kwahiyo nendeni tu
mkahakikishe.
Pajero: Atakubali kweli.
Durudu: Hapana usiwe na mawazo
hayo. Wewe jaribu kuwa na
maneno ya ushawishi tu mwisho
wake anaweza kukubali tu.
Pajero: Haya bana nitaenda kumjaribu na
ndipo nitajua Hatima Yake. Embu
nambie kwanza shemu vipi
anaendeleaje?. Kwasababu hata
sikumjulia hali.
Durudu:Yuko vizuri kwasasa naye ni mama
kijacho unajua...
Pajero: Duuuu ulimuoa tayari
umeshamuweka nini?
Durudu: Ndiyo hivyo utawashaje kibatari
kabla hujaweka mafuta wewe.
Pajero: “ Anacheka na kusema” haya bana
Durudu umenishinda.
Durudu: Ndivyo inavyotakiwa.
Pajero: Haya bana. Basi acha mimi nifanye kurudi hapo nyumbani kwanza.
Kwasababu nilikuwa na mpango
wa kwenda mashineni hapo
Kikore.
Durudu: Haina shida ndiyo majukumu
hayo Pajero.
Pajero: Haya bana. Shemeji akija wewe
msalimie tu. Asije akasema
nimemsusa sana. Kwasababu
Madeva naye ana vituko sana. “ anainuka na kumpa mkono
Durudu huku msafara ukianza”.
Durudu: Kwa hilo ondoa shaka.
(Ni Mwaka mmoja na miezi kadhaa tayari umepita. Kitandani anaonekana mke wake Durudu ambaye ni Madeva akiwa amelala kifudifudi. Ni usiku panaonekana taa ya nguvu za jua imewaka hapo ikiwa imewekwa kwenye ndoo ya maji. Mwili wake unaonekana umeisha kwelikweli ikiwa inaashiria afya yake ina mgogoro kabisa. Kwa pembeni hapa Durudu yuko hapo yuko kajifunika shuka kwa juu tu huku akiwa amempakata mwanaye wa miezi kadhaa tu aitwaye Ijojo pia na mdogo wake Durudu aitwaye Ilali mwenye kama umri wa miaka kumi na saba ambaye naye huwa anaishi hapo hapo nyumbani kwa Durudu. Ilali akiwa amesimama. Madeva analalamika kuhusu afya yake)
Madeva: Baba Ijojo yaani hali yangu hapa
ni mbaya sana kwakweli sijui kama
asubuhi nitaiona.
Durudu: mke wangu wala usizungumze
hivyo. Sasa usiku huu unafikiri
tutaanzaje hata hiyo safari ya
kusema upelekwe hadi Galapo.
Pikipiki yenyewe tu ndiyo hiyo
sijui elfu tano kwanza ni shida
kuipata na usiku huu lazima
atupige bei ya juu.
Madeva: Ni sawa Baba Ijojo ila tu ujue….
Hali yangu ndiyo hiyo haifai. Si
bora hata tungeenda huu usiku
hata hapo hospitali tu…. Hapo hata
na baiskeli tunaweza kwenda
huyu Ilali hapa akabaki na mtoto
hapa.
Durudu: Ni sawa mke wangu. Ila ndiyo
hivyo huu ni usiku sana. Na
isitoshe pia hela yenyewe ndiyo
hivyo. Tukifika pale lazima
atatupiga bei ya juu sana na hela
mimi sina kabisa hapa. Ni bora
pakuche ndipo tukajua nini
Hatima Yake.
Madeva: Haya… umenishinda kwa maneno na siyo kwa hoja. Sina la kuongea
kabisa … acha mimi nife pole pole
huku najionea tu.
Ilali: Kweli kaka kama mambo
yameshindikana na hali hii ya
shemeji unavyoiona hapa itabidi. asubuhi uumize sana kichwa ili
shemeji afikishwe hospitali. La
sivyo hapa… nahisi dalili hii
umejionea mwenyewe na unajua
Hatima yake.
Durudu: Nimekuelewa mdogo wangu.
Pakikucha tu lazima nitafanya
hivyo sina namna hapa. Itabidi tu
huyu kesho apelekwe hospitali.
“ Ni nyumbani kwa Durudu wote wakiwa wamekaa kwenye mkeka Durudu akiwa amekaa na mwanaye ambaye ni Ijojo tayari ameshakuwa na umri miaka sita. Durudu amevaa suruali nyeusi ya kitambaa na shati jeupe la mikono mirefu. Ilali ni muongeaji kama baba yake weupe wake kama mama yake. Ilali amevaa kanzu nyeusi na kofia nyeusi. Pia Ilali yupo hapo pembeni ameshakuwa ni mkubwa tu. Ambapo ni mishale ya saa kumi jioni”.
Durudu: Unajua Ilali ni muda kama wa
miaka mitano tangu afariki mke
waangu, Mama Ijojo ambapo
kwako ni shemeji yako. Natumai
hilo unalitambua.
Ilali: Ndiyo nalitambua sana kaka.
Durudu: Aaa jambo la msingi hapa si
kwamba nataka kukukumbusheeni
machungu… lahasha...
Ilali: Nakuelewa kaka.
Durudu: Aaaa lengo kubwa ni kuhusu
tangu mwanzoni nilikuwa
nakwambia kwamba mwanangu
akija kufika umri wa kujielewa
hivi itanibidi nikuachieni nyumba
hii na mimi niende Arusha
kutafuta maisha. Kwasababu
unajua sisi ndiyo tumebaki hapa
kama familia. Ndiyo hivyo mama
na baba yetu wamefariki zamani
sana. Sasa jambo hilo lisitufanye
kukata tama katika kutaka
kuyajenga maisha yetu. Najua
kwasasa umeshakuwa na akili za
kujua hili ni baya na hili zuri.
Ilali: Nimeshakuelewa kaka.
Durudu: Kwahiyo mimi ninachokuomba ni
wewe kuwa makini tu na watoto
wa hapa mtaani. Yaani si vijana
wa kike wala kina nani. Wewe ishi
kama wewe na haya mashamba
hapa nyumbani usije ukayauza
kabisa. Haya mashamba mdogo
wangu ukiyauza tayari hata hii
kaya tayari itakuwa imeshavunjika. Kwahiyo nakuomba sana usije
ukaniangusha. Hapa Mkurumuzi
kuna ugonjwa huu wanauitwa
ugonjwa wa kisasa ambao ni
UKIMWI ogopa sana hiki kitu. kuwa
makini sana na visichana vya hapa
kijijini, najua umeshakuwa nani
wakati wa wewe mwili wako kuwa
wa moto ila cha msingi tumia kinga usifurahie kusema tu haina ladha.
Ilali: Sawa kaka siwezi kuuza kabisa.
Durudu: Pia huyu Ijojo nataka aendelee
kwenda shule. Asubuhi ukiamka
mwambie ajiandae na kwenda
shule. Najua hapa nyumbani na
shule ya msingi Kikore siyo mbali
kabisa. Kwahiyo nakuomba tu
usije ukanifanyia makidamakida tu
mdogo wangu. Mimi nakuaminia
wewe ndiyo mdogo wangu wa
kiume wa nguvu. Nakutegemea
katika Nyanja nyingi sana. Huko
mjini mimi maisha yakishakaa
vizuri nitakuja kuwachukueni ili
niende nanyi Arusha.
Ilali: Sawa kaka. Ila sasa huko unaenda
kukaa kwa nani?
Durudu: Naenda kukaa kwa rafiki yangu
utu nilisomaga nae kipindi hicho.
Yeye aliondoka hapa kijijini
kitambo sana. Kama miaka mitano
ilikuwa imepita kabla sijaoa.
Ilali: Haina shida kaka mimi nakutakia
maandalizi mema tu.
Durudu: Shukurani Ilali. Unasikia Ijojo
uende shule eee…
Ijojo: Sawa baba.
Durudu: Haya basi embu nendeni hapo
matindigani mkalete mboga mbili
tatu hivi tufanye usiku kuwa
mzuri.
“Ilali na Ijojo wanainuka na kuelekea huko walikotumwa. Durudu anabaki peke yake huku akiwa anaogelea katika bahari ya mawazo. Anaongea kimoyo moyo akiwa anasema hivi”.
Daaa hiki kijiji embu kwanza nikikimbie kwa sababu ya watu
wanakufa kila kukicha na huu UKIMWI. Duuuu Safi aliyeniambukiza huu ugonjwa naye amefariki, huyo Pajero na mke wake pia wamefariki kwa huu huu ugonjwa, Rojo naye kafariki muda tu kwa huu UKIMWI. Nimebaki mimi tu kabisa hivi Mungu hanioni kabisa. Maalim ndiyo Yule alifariki kitambo tu naye yaani karibia marafiki zangu wamekufa. Angalia visichana vingi ambavyo nimepita navyo nao wamekufa kwelikweli. Hivi mimi kifo changu kitakuwaje? Kweli Mungu ndiyo anajua hatima yangu. Ama kweli haya ni Mapenzi Kaburini yaani kila niliyefanya naye mapenzi bila kutumia mpira yuko kaburini kwa sasa. Ooooh… Mungu zilaze roho hizo mahali upapendako kwa sababu mimi siwezi kukuchagulia. Na mimi utaamua utakavyoamu nini cha kunifanyia. Kwa sababu nashangaa shetani ndiye anabakizwa. Ooooh jamani uliyefikiria kusema mapenzi Kaburini hongera sana. Kwa sababu nilitamani sana kujua ni namna gani watu wanafanya mapenzi huko Kaburini kumbe ndiyo hivyo watu wanavyoenda kaburini kwa hayo mapenzi. Jamani ndugu zangu hata kama hamnisikii nakwambieni tu kuweni makini. Duu embu nijishughulishe na mambo mengine tu hapa haya mawazo yatanifanya nianze kukonda tena hapa…
ONESHO LA TANO
(Mandhari ya nje ya soko la kilombero. Durudu amevaa boshori, shati la mikono mirefu na suruali nyeusi ya jinsi. Ameweka matunda yake kwenye meza iliyoegeshwa tu miti. Matuda yakiwa ni mapapai, matikiti, mananasi, na maembe na matunda mengi mengineyo. Anaongea na mteja ambaye ni wa jinsia ya kike. Mteja amevaa dera na kujifunga kishekhati. Durudu anamwambia hivi)
Durudu: Karibu dada matunda bei rahisi tu
ni kama bure kabisa rafiki jina
nani vile?. Kwasababu huwa
unakuja hapa ila sijawahi
kukuuliza jina lako wakati wewe
ni mteja wangu sana.
Mteja: “ anamjibu huku akitabasamu”
Wewe niite mteja tu.
Durudu: Haya bana mteja. “anatabasamu”
Mteja: Kweli mimi mteja wako. Kwahiyo
niite tu hivyo.
Durudu: Ahaaa Mteja wangu unataka nini
na nini mteja nikufungue?
Mteja: Leo nataka maembe ya elfu
mbili, matikiti mawili, matango
manne, na nanasi moja.
Durudu: Vipi nikuwekee maembe ya juice
au ya nini?
Mteja: Hapana. Fanya mchanganyiko tu
ila sitaki yaliyoiva sana.
Durudu: Ahaa sawa. Hapo sawa. “ anachagua matunda
aliyoelekezwa na kumfungia
kwenye mfuko mweusi. mteja
anampatia fedha ya matunda yale
na Durudu anamrudishia chenji
na mteja wake anasema hivi”.
Mteja: Asante sana.
Durudu: Na mimi nikushuru sana kwa
kuniungisha mzigo wote huu.
Karibu sana. Kweli
Mtejani ni Mfalme.
Mteja: Ahsante… “ huku akitabasamu”
Kwaheri.
“ Mteja anaondoka huku Durudu akiwa anaongea pekee yake kimoyomoyo akisema hivi”. Afadhali huyu mtoto leo hata katia Baraka tena hapa. Kwa sababu hii ni kama awamu ya tatu anakuja hapa. Ila mteja mzuri kwelikweli. Kama vile ananivutia.sss
“ Mandhari ni ya nyumbani wanapoishi Durudu na huyo jamaa yake ambaye anaitwa Kijukuu. Wamepangisha chumba kimoja huko majengo. Wamekaa nje na maongezi kidogo yakiwa yamewatawala. Huyo kijukuu kavaa kisuruali kimembana kwelikweli na boshori lake la rangi ya bluu na kavalia na sweta juu. Durudu naye amevaa jinsi na tisheti nyeusi. Jua limewaka ni kivulini wamekaa ”.
Kijukuu: Oya chalii yangu eeee naona
kama vile unapaogopa ogopa sana
hapa mageto. Sijui kama vile
hujapazoea au vipi?
Durudu: Kwanini Kijukuu?
Kijukuu: Naona unaishia na mademu huko
mbali tu. Kama unataka kupiga
demu kuwa huru wewe
unaniambia tu tayari mimi
nakuachia nanja najua kabisa
chalii anapiga kitu.
Durudu: Haina shida unajua kuku mgeni hakosi kamba mguuni. Kwahiyo
wala usihofu.
Kijukuu: Hamna imenibidi tu nikuambie
mapema ili usije ukaanza
kuogopa na kuanza
kuwapeleka mademu huko guest
na unamaliza hela bure wakati
geto la muhuni ambalo kwasasa
ni la wahuni liko hapa.
Durudu: Hamna noma.
Kijukuu: Kwahiyo embu hiyo kamba
iondoe mguuni mapema sana.
Hapa mjini usikae kiwakiwaki tu
chalii yangu. Watoto wazuri
wanakuja kila siku kununua
matunda halafu unabaki kuumia
tu wakati uwezekano upo kabisa.
Wewe ukiona tu vipi
umeshajinyakulia huko tayari
wewe nijulishe tu ili nisije
nikaingilia mechi yako hapa.
Durudu: Hamna noma.
Kijukuu: Siku za jumapili ndiyo huwa hapa hawa wapangaji wenzangu huwa
wanakuweko sana hapa
nyumbani ila ndiyo hivyo ukileta
demu wako unawawekea
wambuzi tu. Hakuna kucheka
na kima hapa. Una demu wako
umewakuta hapa ni salamu ndani inatosha.
Durudu: Hapo nimekupata Kijukuu.
Kijukuu: Hamna noma bablai mbona
wananimanya sana
hapa.Wanamjua kabisa
Kijukuu ni nani.
“ Ni mazingira ya ndani wanapoishi Kijukuu na Durudu. Durudu anaonekana yuko na msichana aitwae Mwatabu. Wako kitandani wamejifunika shuka hapo wanaonekana wameshamaliza shughuli. Mwatabu kwa sura tu amejaaliwa, mdomo uliokaa vizuri kwa ajili ya kazi maalum ya tukio lililotokea kwa muda si mrefu kati ya Durudu na Mwatabu”.
Durudu: Sasa Mwatabu tutakuwa
tunatumia kondomu hadi lini
hivi?
Mwatabu: Hadi tukapime kwanza ndiyo
hapo nitaprove.
Durudu: Unajua ni kama haina ladha
kabisa.
Mwatabu: Wewe ndiyo unafanya isiwe
na ladha kabisa.
Durudu: Kwanini?
Mwatabu: Kwani tungepima tukajua afya
zetu mbona hata hiyo ladha
ungeipata vizuri tu.
Durudu: Ila Mwatabu kwa kweli wewe
tambua tu mimi sina malengo ya
kukuchezea tu mimi nataka
nikuoe kabisa.
Mwatabu: Mimi mwenyewe na malengo na
wewe kwamba niolewe na wewe. Wewe ukafikiri mimi siyatamani mambo uliyonipa hapa muda si
mrefu? Nayatamani sana Ila
kama ndiyo hivyo hutaki kupima tutaishije hapo? Mimi siwezi
kuishi na mwanaume ambaye
sijapima nae kabisa hivi
nikahakikisha. Kwasasa Durudu
kuna magonjwa mengi tu, kuna
huu UKIMWI ambao watu
wanaondoka kama vile vivuli
bila hata kujijua. Kweli mimi
niko tayari kuolewa na wewe ila
kama tu ukikubali tukapime.
Durudu: Haya haina shida. Tulia
nitakujulisha.
Mwatabu: Mimi tayari muda wowote tu.
Durudu: Haya. “ wanainuka pale na kila
mtu anavaa nguo na tayari
wanatoka nje na wanaagana
tayari Mwatabu anaondoka na
kumuacha Durudu akiwa
amesimama tu kama msitimu
usiounganishwa nyaya.kisha
Durudu akawa anaongea pekee
yake akisema hivi” Yaani hawa
watoto wa mjini sijui wakoje.
Huyu Mwatabu sijui amejua
mimi nina UKIMWI ndiyo maana
ameng’ang’ania kwelikweli.
Huyu mjinga kweli, mimi cha
msingi nimeshamlamba basi
apite hivi. Wangapi hapa mtaani
nimewalamba kavu tu. Kwanza
tangu nizaliwe leo ndiyo
nimetumia kondomu. Yaani
utafikiri msumeno siwezi
kufanya upumbavu huu.
Ingekuwa kisu kinachinja na
hala yake hapo sawa. Sifanyi huo
ujinga. Nimeshawapitia wengi tu
kavu na nitaendelea kuwapita
kavu. Ila mtamu
kwelikweli kama sura yake ilivyo.
“ Ni muda wa miaka miwili na miezi kadhaa. Durudu ameshaanza kuishi pekee yake. Biashara zinaenda vizuri sana. Alipopangisha ni sehemu yenye vyumba viwili maeneo ya hapo hapo majengo ya chini. Lakini muda huo anaonekana yuko chumbani kwake na msichana hapo wakiwa tayari wameshapeana utamu. Kitandani wakiwa wamejifunika shuka. Durudu anamwambia huyo mwanadada hivi”
Durudu: Daaaa unajua Doli wewe mtamu
sana. Daaa kweli Mungu
amekujaalia kabisa.
Doli: Wala mbona kawaida tu.
Durudu: Kweli. Daaa kweli Tanga
mmejaaliwa na ndiyo maana
wakasema ndiko yalikozaliwa
huko. Siwezi kupinga kwa
nilichokiona leo.
Doli: Wewe nisifie tu halafu uje
kuniacha hapa. Kwa sababu nyiye wanaume bana sijui mkoje?
Durudu: Hapana Doli mimi siwezi
kukuacha kabisa. Mimi na wewe
namuomba Mungu tudumu
milele. Mimi matarajio yangu ni
kukuoa kabisa.
Doli: Haya mimi niko tayari.
Durudu: Unajua Doli kwasasa
nimeshakuwa umri unaenda.
Nikisema nimrukie mwanamke
huyu kesho Yule sasa kweli
mwisho wa siku hata Mungu
atanilaani nikajikuta nahangaika
tu na hao wasichana tu badala ya kutafuta maisha. Yaani mimi leo
hii ingekuwa nahangaika tu na
hao wasichana leo hii
nisingekuwa naishi kwenye hiki
chumba pekee yangu. Sasa hivi ni
mwaka wa pili hivi nahisi
unakaribia kukata kabisa
nimekuja hapa nikiwa nakaa
mageto kwa rafiki yangu tu.
Kwahiyo kwasasa ni muda wa
mimi kuweza kupata mwenza wa
kuniburudisha na hadi tuoane
kabisa. Doli nina malengo na
wewe embu niamini.
Doli: Sawa nitakuamini kama na wewe
utakuwa kweli na hayo malengo.
Durudu: Sawa. Ila unajua Doli kuna jambo
nataka nikujulishe sijui
utalipokeaje!
Doli: Niambie ndipo nijue nitalipokeaje.
Durudu: Yaani hadi naogopa kukwambia.
Doli: Niambie na mimi nijue nitaogopa
au laaa.
Durudu: Aaaaaaa Doli kwamba….
Unajua… Doli…
Doli: Mbona kigugumizi cha ghafla tu?
Kimetokea wapi? Embu ongea bana.
Wewe hujui mimi hapa mimi ni
mfanyakazi wa ndani nanimetoroka tu kwa vile nimeaga naenda
kusalimia marafiki zangu. Embu
niambie bana Durudu mimi
niwahi zangu.
Durudu: Isiwe tabu sana. Aaaa… Doli mimi
… nime… nimeathi…athirika.
Doli: “ haamini alichokisikia kutoka
kwa Durudu. Doli anasema”.
Durudu ati unasemaje?
Durudu: Nina UKIMWI.
Doli: UKIMWI… UKIMWI kabisa huu
ninaoujua. Yaani kabisa Durudu
umeamua kunichinjia baharini
kabisa. Durudu sasa mimi
nitamueleza nani haya majanga
kabisa. Durudu mimi Yule bosi
wangu hatanielewa kabisa. Hivi
eeeee Mungu wangu weeee kweli
kuna watu hampendi kabisa
maendeleo ya wenzenu. Ooooooh!!! jamani kuna watu ni chui. Durudu
kabisa na hatujatumia hata cha
kondomu.
Durudu: Doli usikasirike ndiyo
imeshatokea hivi.
Doli: Imetokea hivi… yaani unaongea
kirahisi kabisa. “ anaongea huku
machozi yakimbubujika
kwelikweli”
Durudu:Ndiyo maana nimeahidi nitakuoa
Doli siwezi kukuacha kama
ukikubaliana na mimi. Hiyo ndiyo
imeshatokea tayari.
“ Doli anainuka kwa hasira anavaa nguo na pia Durudu naye anainuka na kuanza kuvaa nguo haraka haraka ili amsindikize Doli. Anampa maneno ya kumtia moyo. Wanatoka nje wanatembea wote hadi sehemu yenye boda boda na wanapakia kwenye piki piki moja. Doli anapoishi ni huko kwa Morombo”.
“ Mandhari ya nyumbani kabisa kwa Durudu. Ambapo Durudu alijitahidi hadi kufikia kujenga nyumba yake kabisa yenye vyumba vinne hapo ni baada ya kama ya miaka mitano kabisa. Wanaonekana wamekaa Doli na Durudu wakiwa wana maongezi ya hapa na pale. Doli amevaa dera na kichwani kajifunga kitambaa chekundu huku Durudu akiwa amevaa suruali ya kitambaa na shati jeupe.walipokaa ni kwenye makochi. Nyumba yake kwa huko juu bado haijakamilika vizuri yaani haina silingiboard. Wanaangalia runinga”.
Durudu: Doli mke wangu. Kwasasa ni muda tayari umeshapita tangu tuingie
kwenye ndoa yetu. Majanga mengi
tumeyapata hadi muda huu na
moja wapo ni hilo la wewe
kuharibika kwa mimba yako.
Niseme tu nikushukuru kwa
uvumilivu wako.
Doli: Sawa.
Durudu: Pia ndiyo hivyo hata sasa afya
yako si nzuri sana. Ila bado nasema nitaendelea kuwa na wewe. Kwa
sababu haya yote ni mimi kama
msababishaji ila kwasasa si muda
wa kuanza tena kulaumiana au
kulalamika bali ni muda wa sisi
kujipanga ipasavyo tujue ni namna
gani ya kujiendeleza zaidi ya
tulipofikia muda huu.
Doli: Sawa mume wangu nimekuelewa.
Durudu: Aaaah ni kwamba unakumbuka
kuhusu mwanangu na mdogo
wangu wako nyumbani kule
niliwaacha.
Doli: Ndiyo uliniambia vipi kwani kuna
nini huko?
Durudu: Aaaaah… hamna ila nilitaka tu
nikujulishe kwamba nataka
nikawachukue niwalete huku
mjini wafanye kazi nao na Yule
mwanangu aje aendelee na
masomo huku. Kwasababu
kwasasa Yule Ilali ambaye ndiyo
mdogo wangu ameshakuwa ni mtu
mkubwa kabisa hata ukimwambia
simamia sehemu fulani anaweza
kufanya hivyo kabisa.
Doli: Haina shida itakuwa ni vyema
ukifanya hivyo. Kwasababu ndiyo
hivyo hata afya yangu ndiyo kama
unavyojionea hapa. Hiyo kansa ya
koo niliyonayo hapa hii ni muda
wowote tu natumai itanichukua.
Ukichanganya na huo UKIMWI
ndiyo kwaheri kabisa.
Durudu: Embu bana usiongelee kuhusu hilo
jambo kabisa.
Doli: Ndiyo ukweli huo. Ila sawa.
“ Ni nyumbani kwa Durudu tunaona Doli akiwa amelala kitandani. Durudu akiwa amesimama hapo pamoja na Ilali na Ijojo. Doli anaonekana hali yake si nzuri kabisa sauti anayoitoa ni sauti ya chini sana. Anaongea kama vile sauti inakata kata. Ilali anaonekana kabisa ameshakuwa ni mrefu kabisa na hata Ijojo naye ameshakuwa kabisa si kama wa kipindi kile. Muda huo ni mishale ya saa kumi alasiri. Durudu anamuongelesha Doli”
Durudu: Mke wangu unajisikiaje?
Doli: “ Anaongea kwa shida lakini hata
hasikiki kabisa. Anaongea kwa
ishara akiwa anauonyooshea
mkono wake shingoni”.
Durudu: Sasa Ilali embu angalia kwenye
simu yangu hapo angalia kuna
namba imeandikwa Tax embu
mpigie halafu mwambie aje hapa
nyumbani kwangu muda huu.
Ilali: Sawa kaka. “ Ilali anaenda
kuchukua simu ikiwa kwenye
kochi. Simu ni aina ya TECNO
ndogo tu. Anaingia kwenye orodha
ya majina na kutafuta TAX anapiga
simu”.
Durudu: Embu Ijojo chukua baadhi ya
nguo za mama yako na uweke
kwenye mkoba ili TAX ikija tu
isiwe shida tena.
Ijojo: Sawa baba.
Durudu: Sasa Ijojo itabidi ubaki hapa
nyumbani kwa ulinzi zaidi. Sisi
tutaenda hospitali pamoja na Ilali.
Ijojo: Sawa baba.
“TAX inasikika huko nje ikiwa inaliza honi. Tayari Doli anainuliwa. Durudu, Ilali, na Dereva ndiyo wamembeba na kumpeleka kwenye gari. Wote wanaingia ndani ya gari na dereva anakanyaga gia kueleka MOUNT MERU HOSPITAL”.
“ Inaonekana ndiyo panapambazuka. Daktari pamoja na rafiki wa Doli ambaye ndiye aliyekuwa amelala na Doli wodini wana maongezi huku wakiwa wanatembea. Wanakutana na Durudu akiwa ameshikilia kikapu chenye chupa na vitu vingine vikiwa vimefunikwa. Daktari anakatisha mazungumzo baada ya kumuona Durudu na pia rafiki yake Doli naye anaonekana yuko kimya Durudu anasema”.
Durudu: “ Akiongea akiwa na hamasa ya
kujua hali ya Doli” Dokta vipi hali
ya mke wangu?
Daktari: Aaaaah …. Kuwa huru kwanza za
nyumbani?. Uko swalama kabisa?.
Shemeji: “ anaonekana anampokea
Durudu kikapu.”
Durudu: Huko hawajambo kabisa. “ Ilali
pia naye anaonekana anakuja
anawakuta wakiwa katika
mazungumzo” vipi mke wangu?
Daktari: Aaaaa?…. Durudu hali ya Mama
si nzuri sana….
Durudu: Si nzuri ni sawa tangu jana hali si
nzuri embu nielezenivizuri.i
Daktari: Aaaa… kwa ujumla… ame…
amefariki alfajiri…
Durudu: “ Baada ya kuambiwa tu anabaki
ameduwaa tu hana hata la
kuongea. Daktari anamwambia
hivi.”
Daktari: Unajua mipango ya Mungu haina
makosa.
Durudu: Naruhusiwa kwenda kumuangalia
muda huu.
Daktari: Embu tulia kwanza kwasasa hivi
embu tuende kwanza sehemu ya
Mapumziko. Kwasababu tayari
tumeshampeleka mwochari…
kwahiyo embu ungetulia kwanza.
“ Ni siku ya nne baada ya maziko kufanyika. Mandhari inayoonekana ni nyumbani kwa Durudu panaonekana watu wakiwa wamekaa makundi makundi wakiwa na mazungumzo ya hapa na pale. Ilali na Ijojo wakiwa nao wako kibarazani hapo, baadhi ya ndugu wa Durudu wako pale katika kikao hicho kilichokuwa kinahusu ugawaji wa mirathi. Muda huo ilikuwa ni mishale ya saa nne asubuhi. Panaonekana kuna meza pia juu ya meza kuna matunda yamewekwa ili watu wajipatie kula. Pia kuna kisu cha kukatia matunda kipo hapo kinaonekana. Shemeji zake Durudu nao wako hapo na binamu zake pia wako hapo pamoja na Kijukuu katika kikao hicho. Durudu anasema hivi”.
Durudu: Habarini ndugu, jamaa na
marafiki.
Wote: Salama.
Durudu: Mkusanyiko huu unamaanisha
kuna mazungumzo maalum.
Baadhi ya watu natumai
hawakuwa wanawajua wadogo
zangu na mwanangu. Huyu hapa
ni Ijojo (Ananyoosha kidole kwa
Ijojo ) ndiyo mwanangu wa kwanza na huyu hapa (Ananyoosha kidole
kwa Ilali) ni Ilali ni mdogo wangu
na katika familia yetu tumezaliwa
wawili tu yaani mimi na huyu Ilali.
Pia ndiyo huwa naishi nao wote
hawa hapa nyumbani. Pia tangu
mwanzoni tu hawa ndiyo kama
warithi wa vitu mbalimbali
ambavyo ni vyangu. Kama nyumba hii tayari ilikuwa imeshaandikwa
hii ni yao yaani kwa wote.
Nimependa kusema tu hivi
kwasababu hakuna ajuae badae
wala kesho. Nyumbani kule nako
panajulikana baadhi ya maeneo
ambayo ni ya kwao ya ushikirika
yaani kati ya Ilali na Ijojo.
Embu Ilali na Ijojo wasalimuni
ndugu zenu hapa.
Ilali: (Anasimama ili kutaka kuwasalimia ndugu. Durudu anaonekana
anachukua tunda hapo mezani.
Anachukua na kisu, analikata
chungwa huku akiwa anawaza
sana ni watu wengi ameshawaua
sana kwa huo ugonjwa wa UKIMWI.
Anamfikiria aliyempa UKIMWI
ambaye ni Safi, baadhi ya wasichana wake wote aliyowapitia na
kuwapatia UKIMWI hadi
anamkumbuka mke wake ni yeye
ndiye kamuambukiza UKIMWI na
kafariki. Pale pale anaamua
kujichoma kisu kifuani na
anaanguka chini watu wanashangaa
tu mtu yuko chini. Wanaanza
kumnyenyua ili kumpeleka hospitali
tayari anafariki hapo hapo).
TAMATI

Habari ndugu. Napenda kukukaribisha tena katika tamthiliya iitwayo MAPENZI KABURINI. Ni tamthiliya inayosisimua, elimisha, kuonya na kuburudisha.
ReplyDeleteMaoni yako ni muhimu sana
Habari ndugu. Napenda kukukaribisha tena katika tamthiliya iitwayo MAPENZI KABURINI. Ni tamthiliya inayosisimua, elimisha, kuonya na kuburudisha.
ReplyDeleteMaoni yako ni muhimu sana
Kijana unamaono Mazuri. Ila ili kumake money, somo nature ya Soko lako kwanza. Lipoje, linataka nini?
ReplyDeleteMfano, Watz wengi hawapendi kusoma kwanini usifungue Youtube Chanell na Kuziweka inform of motion Picture?
Nashukuru sana. Pia maoni yako lazima niyafanyie kazi ndugu yangu. Nikushukuru sana kwa ushauri wako.
DeleteNashukuru sana. Pia maoni yako lazima niyafanyie kazi ndugu yangu. Nikushukuru sana kwa ushauri wako.
DeleteKeep up nice job
ReplyDeleteThanks
DeleteNimependa sana hadithi zako kwa kweli unaweza
DeleteShukran sana... Karibu tena.
Delete